Kidowle
JF-Expert Member
- Oct 10, 2016
- 1,484
- 3,260
Bila shaka uwezo wako kisoka ni GPA ya 32
Bila shaka uwezo wako kisoka ni GPA ya 32
Salah asipozingua kwenye mechi VS Chelsea hapo September nina uhakika EPL title msimuu huu ni yetu
Toka msimu uliopita Liverpool ilikuwa na kikosi kizuri. Tatizo lilikuwa ni ufinyu wa kikosi na changamoto ya baadhi ya nafasi
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiangalia benchi letu uhai upo katikati kidogo, strikers hatuna bench, defense pia sidhani kama tuna bench la kuliamini.
Bado mapema sana mkuu, na game ya Chelsea siyo decider game, next week tuna Leicester.
Focus should be on Leicester, one game at a time.
Hahaha, una ugomvi na Ollachuga Oc.
Katika timu ambazo ninaona zinaweza kutufunga ni Chelsea na MUFC. Tukimpiga Chelsea tutakuwa tumebakiza threat moja tu ya MUFC which means tutakuwa Title kama Cityzens watakuwa na hali mbaya .
Leicester tunawapiga nje ndani maana niliwacheki kwenye opener yao vs MUFC kiukweli tunawapiga vizuri tu Home and away
Yule babu mvuta sigara nyota na mbwia ugoro ambae hajashinda kikombe cha aina yoyote wala mashindano yoyote yale katika maisha yake. Not even Ndondo cup
Mkuu tusiwe kama Mourinho kila akihojiwa anatutaja, tujikite kwenye kuijadili team yetu mkuu.
Tottenham jana wamenitisha jinsi team inavyocheza teamwork, kitu ambacho nimeona kama bado tuna hangaika nacho, tuna pasi nyingi za kiufundi ambazo zinapotea (turnovers), wachezaji ni kama bado hawajayaelewa majukumu yao hasa, positions nk.
Tunakutana na Tottenham in less than 3 weeks, na kuna international break hapo katikati, naiwaza sana hiyo game.
Wewe Kweli Kituko! Niwazi Kuwa umeibukia Hapo Chelsea 2015 ukaishia Kugoogle tu baadhi ya Matukio.
Hivi Benitez Hapo Chelsea Kapata Mafanikio Kuzidi Liverpool alikobeba CL?
Droo ya makundi UEFA ni hapo kesho.
Droo ya CARABAO pia ni hapo kesho.
Juu ya tutakuwa pot gani itajulikana hapo
baadae baada ya mechi ya wagiriki dhidi ya
Benfica kule Ugiriki.
kumbuka mechi ya kwanza PAOK alipata droo ya
1-1 kule Ureno.
Hapo jana pale Melwood kulifanyika mashindano
kidogo ndani ya mazoezi...
na timu zilikuwa kama hivi....
Timu A:
Mignolet, Robertson, Van Dijk, Keita, Jones,
Sturridge na fitness coach Conall Murtagh.
Timu B:
Grabara, Matip, Alexander-Arnold, Milner, Origi,
Shaqiri, Camacho.
Timu C:
Kelleher, Phillips, Moreno, Henderson, Lallana,
Salah, Mane.
Timu D:
Alisson, Gomez, Clyne, Fabinho, Wijnaldum,
Solanke, Firmino.
Timu D ya akina Alisson iliweza kuibuka washindi
huku Timu A ya akina Van Dijk wakiburuza mkia.
Sheyi Ojo anaweza kwenda Ufaransa.
Ama kweli pata pesa tujue tabia yakoUSUPASTAA gharama sana, asikwambie mtu. Ukitaka kulifahamu hilo, basi waulize maofisa wa Chama cha Soka cha Misri baada ya kuambiwa na Mohamed Salah wajiuzulu wote, la sivyo basi wahakikishe mchezaji huyo hasumbuliwi anapokwenda kwenye mechi za kimataifa.
Staa huyo wa Liverpool amedai mashabiki wa Misri walikuwa wakimsumbua sana, wakijazana hotelini kwake na kumgongea mlango nyakati za usiku kisha wanataka tu asaini vitabu na jezi zao au kupiga picha na mchezaji huyo jambo ambalo mwenyew amelitafsiri kuwa ni kero kwake.
Katika mfululizo wa barua kibao alizotuma kwenye chama hicho cha soka EFA, mwanasheria wa Mo Salah aliweka bayana baadhi ya masharti ambayo yanapaswa kufanywa ili kulinda usalama na hadhi ya mchezaji huyo anapokwenda kwenye majukumu yake ya kuitumikia timu ya taifa.
Katika barua iliyoandikwa Agosti 23 iliyotumwa kwa Rais wa EFA, Hany Abo Rida, mwanasheria huyo, Ramy Abbas Issa amewashutumu maofisa wa soka wa Misri kwa kumchukulia kawaida mchezaji huyo na kuwaruhusu mashabiki wafanye wanavyojisikia mbele yake.
Katika kuweka sawa jambo hilo, mwanasheria Issa ameweka bayana masharti sita ambayo yanapaswa kufuatwa wakati mchezaji huyo anapojiunga na timu ya taifa.
Kwanza, EFA ni lazima uzuie watu kuweka kambi nje ya chumba cha hoteli atakachofikia Salah, wasigonge mlango kutaka kupigwa picha na wala wasiende kumzongazonga anapokuwa mazoezini.
Pili, Salah lazima awe na walinzi wawili kila anapokwenda na walinzi hao wawepo nje ya hoteli atakayofikia Salah kumsubiri muda wote.
Tatu simu zote kwenye chumba cha Mo Salah ziwe zimefungiwa, asipigiwe na mashabiki na asijumuishwe kwenye ishu zozote za kimatangazo, mahojiano au kwenda kusalimia wadhamini wa EFA kwa namna yoyote ile.
Nyingine ni katika mechi za kimataifa, Salah ni lazima asafirishwe na ndege kutoka hotelini hadi atakapohitajika kwenda.
Kusiwepo na mtu yeyote mwenye ushirika na EFA awe na uwezo wa kuomba kupiga picha au asainiwe chochote na staa huyo.
EFA imedaiwa wamekasirishwa na mahitaji hayo ya Mo Salah, lakini mwenyewe amesisitiza: “Haya mambo yamewekwa na kupuuzwa ili tu nionekane mpuuzi, mimi sio mpuuzi.
“Tumewatumia barua nyingi na mimi nipo hapa sitaki matatizo.”
Madai ya Mo Salah ni amekuwa hajioni kuwa huru anapokwenda kuichezea timu yake ya taifa kutokana na kumfanya kama sehemu ya dili mbalimbali za kibiashara zinazowanufaisha mabosi wa EFA.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mwanasheria wake, staa huyo bado ana nia ya dhati ya kuendelea kuitumikia timu yake ya taifa.
Mo Salah kwa sasa amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu England msimu huu ambapo kikosi chake cha Liverpool kinaongoza baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza, ikikusanya pointi tisa na mabao saba, huku ikiwa haijafungwa bao lolote.
Liverpool imepania kuweka historia ya Ligi Kuu England ikiwemo kutwaa ubingwa kuipoka Manchester City.
Source:Mwanaspoti