Najua umeilewa point yangu kwa nilichokuquote ,regardless wachezaji ,makocha na vitu vingine timu yenye ukubwa wa Liverpool haitakiwi kukaaa hata miaka 5 tu bila kuchukua kombe la EPL , yaani huo ni mwiko..lakini for some reason hilo limeitokea Liverpool imefikia hatua sasa hata sio habari tena Liverpool kumaliza msimu bila kikombe.Inaanza kujenga tamaduni mbaya , makocha wanakuwa hawana presha tena . Kwa ubora wa kikosi chenu cha sasa sio tu mnatakiwa kushinda EPL tu bali mnatakiwa kushinda back to back EPL na kufika tena fainal ya champions league kama sio kuchukua kabisa.
Kilichotokea msimu wa 13/14 kwa kiasi kingine mshabiki walichangia ,yaani ile kushinda mechi nyingi mfululizo kuliwafanya mashabiki waamini Liverpool inaweza kushinda kila mechi , kimahesabu mechi vs Chelsea Liverpool ilitakiwa kupata draw tu, hakukuwa na sababu ya kwenda all out attacking ,kocha kwa hype za washabiki na yeye akacheza timu as if it was a must win match ,we all know what happened when Gerald alipoteleza, he was the last man yaani kikosi kizima kilishapanda mbele.
EPL ni marathon ni lazima kocha awe na hesabu sana katika kila mechi bila kujali ubora wa kikosi, last season mlimaliza 25 points nyuma ya man city maana yake hamkuwa hata na dalili ya kuchukua kombe.This season mmefanya maboresho kwenye timu Ila pia lazima kocha abadili approach kwenye baadhi ya mechi ,sio lazima ushinde mechi zote ili ushinde EPL, asipoliona hili mtakuwa tena na exciting season lakini bila kombe