Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Gomez: You have to play each game like it's your last

1) Robertson alipata Nafasi Baada Ya Kuumia Moreno.

2) TAA alipata Nafasi Baada Ya Kuumia Clyne.

3) Ni wazi sasa Gomez anaitaka Nafasi Baada ya Kuumwa Kwa Lovren.


Kwasasa Liverpool Kuna Baadhi Ya Positions Ukiumia tu Ni Kosa manake Mara Hurudi Tena First XI.
hahaha....noma!!
 
Liverpool mpaka sasa imekaa Miaka imeshakaa Miaka 27 bila ya Kuchukua Kombe la Ligi (EPL) na si 19.

By the way! Chelsea ilikaa Miaka 50 bila ya Kubeba Kombe la Ligi (EPL) na hatimae ikabeba 2005! Lakini Kwenye Miaka 27 ya Liverpool ndiyo unaona mengi Kiasi ya Kwamba Haitowezekana tena Kubeba Kombe?

Sasa imewezekana vipi Kwenye 50 Hata ishindwe kuwezekana Kwenye 27?
Huyu ndezi wa kichaga eden kimario anaropoka tu anafikiri mpira ni mbege unatikisa tu na kupulizia
IMG-20180625-WA0023.jpg
 
Sio Kwamba Wamemchomea Mkuu!
Unajuwa iko hivi! Kulitokea Video ilisambaa Kwa Kasi (goes viral) Katika Mitandao Ya Kijamii kwa Muda mfupi ikimuonesha Mo Salah akiendesha gari huku akitumia Simu.
Sasa Kutokana Sheria Za Wenzetu Kuwa Ziko imara tofauti na Huku kwetu Kwani Huku tunapofanya Makosa Tunaikimbia Polisi, Lakini wenzetu Wanapofanya Makosa Wanakimbilia Polisi.
Ndiyo Kabla Ya Polisi Kuiona na Kutake Action dhidi ya Salah (ilikuwa Ni lazima waione).
Timu ikaamua Kuchukuwa hatua za tahadhari Mapema Hili swala Kuliripoti Polisi ili kuonesha ushirikiano na Kupisha uchunguzi (Pia Yawezekana Ni Editing tu) kama Hatua moja kumkinga Mo Salah na Kuja Kusumbuliwa na Polisi Kama Rooney msimu uliopita.
Asante king... kwa kunielewesha shukuran sana kwako
 
Nazani Tite ameshayaona Makosa Yake Kumchezesha Mchezaji Mechi (G. Jesus) Zote walizocheza World Cup Bila Ya Kufunga goli Hata Moja ambalo liwe japo la Offside wakati Mchezaji (Firmino) Mwenye Uwezo Wa Kufunga na Offer mambo mengi Zaidi Amemueka Benchi.

Sasa Ameamua Kumuacha Jesus Nje Kwenye Kikosi Chake Alichokitangaza na Kumfanya Firmino Kuwa Ndiye Striker wake Rasmi.


Goalkeepers: Allison (Liverpool), Neto (Valencia), Hugo (Flamengo).

Centre-backs: Dede (Cruzeiro), Marquinhos (PSG ), Thiago Silva (PSG), Felipe (Porto).

Full-backs: Alex Sandro (Juventus ), Flipe Luis (Atletico Madrid), Fabinho (Liverpool), Fagner (Corinthians).

Midfielders: Andreas Pereira (Manchester United), Fred (Manchester United), Arthur (Barcelona), Pilippe Coutinho (Barcelona), Renato Augusto (Beijing Guoan), Casemiro (Real Madrid), Lucas Paqueta (Flamengo).

Forwards: Douglas Costa (Juventus), Everton (Gremio), Roberto Firmino (Liverpool), Neymar (PSG), Pedro (Fluminense), Willian (Chelsea).
 
Sio Kwamba Sijiamimi Mkuu!
Mimi siamini Utabiri! Kwahiyo Si mtu Wa Kutangaza Kushinda Game kabla sijaicheza! Ninakiamini Mimi Ni Kile Kinachotokea Baada Ya Dakika 90 au 120.
Na ndiyomana Mimi Hata Siku moja Hunikuti Kutangaza Kuchukua Kombe Kabla Ya Ligi haijaanza.

Na Ninachoamini Mimi Ni Kwamba Mtu yeyote unayemsika anasema na Kujihakikishia Kuwa Msimu huu atabeba Kombe Kwenye Timu Yake basi Huyo Hajui Mpira. Kwasababu yeye Ni sawa na Mganga Wa Kienyeji tu na Ndiyomana haangalii Kuwa Mpira Ni Mchezo Wa Mahasebu, Makosa, Uimara Wa Timu, Mbinu, Fitness na Utayari. Factor moja tu Kati ya Hizo inaweza Kukunyima Ubingwa Hata Kama Una Kikosi Bora Kiasi gani.

Mtu anaejua Mpira Maranyingi Husema Msimu huu Nina matumaini Ya Kubeba Ubingwa... Na Sio Kujihakikishia Kuwa lazima Ataubeba kama wanavyosema baadhi ya Watu utafikiria Matokeo ya Mchezoni wanayapanga wao.

Mimi Ni Mshabiki Wa Liverpool lakini Kama Mshabiki Wa Mpira basi Msimu huu Naipa Nafasi Man City ya Kubeba Ubingwa Wa EPL... Lakini Sisemi Kuwa Lazima itabeba Bali naipa nafasi tu Kutokana na Uimara Wa Timu Yao. Kwani Kama Nilivyotaja Hapo juu zipo Factors ambazo zinaweza Kumkosesha Ubingwa.
Waloweka neno" Prediction" walifanya hivyo kuunogesha mchezo.
Hata wale wachambuzi hubashiri kunogesha.
Football ni zaidi ya burudani. Team ikifungwa magoli 20 dkk 45 za kwanza mashabiki wataondoka. Lakini basket ball hata vikapu 100 mashabiki watashangilia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom