Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

We kichaa unataka kila kitu tukufunze sisi ulikuwa unatumia q badala ya k sasahivi unajidai mjuaji kila timu INA haki ya kusherehekea ushindi, nenda Europa huku si saizi yako
Sasa mbna matusi mzee ...hatushabiki mpira kwa kuitana vichaa ..tumia lugha nzuri tu mkuu utaeleweka.
 
Neville on Van Dijk

Gary Neville has admitted he was wrong about Virgil van Dijk.

The centre-back joined the Reds from Southampton in a £75m switch in January and has impressed massively at the heart of Jurgen Klopp’s defence.

“I thought Van Dijk was a good player at Southampton, but I didn’t think he was worth £75m, and I didn’t think he would have the impact on Liverpool’s defence that he’s had,” he told Sky Sports. “He’s a monster, and is looking a bit like Jaap Stam. It looks like he just throws people out of the way.”

Will Gary be eating his words on Xherdan Shaqiri soon?
Let’s hope so!
 
Breaking News
Screenshot_2018-08-14-10-19-49.jpg
 
hongereni liverpool kwa ushindi kwenye mechi dhidi ya West Ham United
niwe mkweli sijwahi kuishabikia liverpool lakini bahati nzuri juzi nilifanikiwa kuiangalia liverpool kwa dakika dakika 70. kwa mpira mulioendelea kucheza juzi liverpool wataendelea kuwa ndio timu pekee nchini uingereza yenye uwezo wa kuifunga manchester city kihalali.

maisha yangu yote nimekuwa nikiishabikia manchester united na tuna wachezaji bora zaidi ya liverpool lakini liverpool wanacheza vizuri zaidi kwa msimu wa tatu mfululizo kuliko manchester united na ndio maana nikasema wao pekee ndio wenye uwezo wa kuwafunga wababe wa etihad kihalali pasina kulinda ovyo kama umevamiwa na intarahamwe au boko haram mtaani kwenu, Ila kumfunga manchester city peke yake hakukukufanyi kuwa bingwa wa ligi kuu ya uingereza.

kwa mara ya kwanza nimebahatika kumuona naby keita akicheza mpira na amenishangaza sana uwezo aliouonyesha kwenye mechi ya juzi na nadhani kwa sasa liverpool muna kiungo bora na aliyekamilika zaidi ya ngolo kante wa chelsea, ushirikiano wake pamoja na widjnaldum ulikuwa ni wa kuvutia sana.

ila bado nimebaki nikijiuliza dhumuni kuu la liverpool msimu huu hasa ni lipi?
kuwania ubingwa wa uingereza na ligi ya mabingwa au kuwania nafasi nne za juu?

kama dhamira kuu ni kuwa na timu yenye ushindani kama real madrid, barcelona, juventus, psg na bayern munich kwa nini mumeshindwa kutafuta back up ya wachezaji kama mohammed salah, van djik, firmino na mlinzi mwengine mwenye uwezo wa kuleta ushindani dhidi ya lovren.

hivi bado kuna mashabiki humu ndani wanaoamini backup bora ya mohammed salah, van djik ni adam lallana, origi, matip na sturidge.
  1. misimu miwili ya ligi kuu kila klabu inacheza mechi 76 lakini cha ajabu zaidi ni kwamba joel matip tokea asajiliwe liverpool amecheza mechi 54 za mashindano yote lakini bado klopp hakuona umuhimu wa kuongeza mlinzi mwengine
  2. solanke tokea asajiliwe na liverpool amecheza mechi 21 na amefunga goli moja kwenye mechi za timu kubwa.
  3. msimu uliopita daniel sturridge alicheza mechi 6 tu msimu mzima.
  4. msimu uliopita adam lallana amecheza mechi 11 msimu mzima na hakufunga goli hata moja.
  5. msimu uliopita kupitia klabu ya wolfsburg origi alifunga magoli 6 kwenye mechi 31.
inamaana liverpool mumesahau kilichotokezea kwenye mechi dhidi ya real madrid?
ngoja tuone ila nilichojifunza ni kwamba timu zote za uingereza bado hazijawa tayari kupambana na timu kubwa za nchi nyengine.
kule kwetu sisi unafungwa na sevilla nyumbani kwako halafu bado unaingia sokoni kutafuta mchezaji mmoja ambaye ataleta ushindani kikosi cha kwanza wakati barcelona wana mwanadamu anayekupa uhakika wa kufunga magoli 40 kwa msimu na bado wameingia sokoni kutafuta viungo washambuliaji.
skysports-naby-keita-west-ham_4387955.jpg
 
Kinyang’anyiro cha Ligi Kuu England, kimeanza tangu wikiendi iliyopita, timu zinazotabiriwa kumaliza ndani ya nne bora, mabingwa watetezi Manchester City, Liverpool, Tottenham na Manchester United zikianza kwa kishindo.
Tottenham iliyoziengua Chelsea na Arsenal katika ‘top four’ ikitamba kwa msimu wa tatu mfululizo licha ya kujadiliwa sana kutokana na kutosajili mchezaji yeyote katika dirisha la usajili wa kiangazi, lakini imethitisha kuwa haikuwa na sababu za kusajili kwani inacho kikosi bora baada ya kushinda ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United.

Ujio wa Kocha, Maurizio Sarri, unaweza kuwa suluhisho kwa Chelsea, kwani aliiwezesha kushinda mabao 3-0 dhidi ya timu ngeni katika Ligi hiyo, Huddersfield Town, lakini wikiendi hii ndipo atapaswa kuthibitisha kama anao ubavu wa kuchuana kuing’oa Tottenham ndani ya nne bora.
Sarri atathibitisha hilo, atakapoiongoza Chelsea kuikaribisha Arsenal kwenye Uwanja wa Stamfodge Bridge, iwapo itaondoka na ushindi wa kishindo kama ilioupata kwa Huddersfield ataanza kuwashawishi wengi kuipa nafasi ya kufanya vema msimu huu.
Arsenal jana Jumapili iliyopita ilicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani bila Arsene Wenger kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1996, licha ya kuwa nyumbani kocha Emery Unai hakuweza kuiepusha na adhabu kutoka kwa mabingwa watetezi City na kufungwa mabao 2-0.

Kocha wa kuwa huyo wikiendi ijayo pia atakuwa katika wakati mgumu kwani atasafiri kuifuata Chelsea moja ya timu ambazo zinaonekana zina vikosi bora vinavyoweza kupigania ubingwa.
Kwa upande wake Kocha City, Pep Guardiola alitamba kuwa kikosi chake kitazidi kutoa dozi kwa kila timu itakayocheza nayo akidai timu hiyo inamarika siku hadi siku.
Guardiola alisema kuwa anaamini katika mechi ijayo sio Bernardo Silva na Raheem Sterling pekee walioifungia mabao hayo, watakafunga tena wikiendi ijayo bali wafungaji wataongezeka watakapoikaribisha Huddersfield Jumapili hii.

Nayo Manchester United chini ya Jose Mourinho imeanza vema Ligi baada ya kuichapa timu bingwa ya Ligi hiyo msimu wa 2015/16, Leicester City kwa mabao 2-1 na wikiendi hii itaifuata timu isiyo na uzoefu ya Brighton.
Upande mwingine, Henrikh Mkhitaryan aliyehamia Arsenal akitokea United pamoja na washambuliaji mahiri Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette hawakuibeba Arsenal kama walivyofanya katika timu zao za zamani Aubameyang alikua tegemeo la mabao kwa Borussia Dortmund ya Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ na Lyon ya Ufaransa ‘Ligue 1’.
City ambayo iliilaza Chelsea mabao 2-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii inaonekana kuzidi kuimarika kila kukicha na sasa ni wazi kuwa inaweza kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza kutetea taji la Ligi Kuu.

City iliyomnunua Riyad Mahrez pekee katika dirisha la usajili wa kiangazi kwa Pauni 60 milioni kutoka Leicester City, alionyesha ana kitu amekiongeza kwa City.
Mitambo ya Liverpool inaonekana imeongezeka nguvu na imeonyesha dalili kuwa itaangamiza zaidi msimu huu baada ya Sadio Mane kufunga mawili, Mohamed Salah na Daniel Sturridge nao wakitupia, huku James Milner na Robeto Firmino, wakicheza soka la kiwango cha juu, hata hivyo Liverpool wikendi hii itakuwa ugenini ikiifuata Crystal Palace.
 
Premier League assists

√ James Milner - 79
√ David Silva - 75
√ Paul Scholes - 55
√ Mesut Ozil - 50
√ Juan Mata - 49

Of the current Premier League players only Cesc Fabregas (111) has more assists than James Milner in the Premier League.
 
Mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah anachunguzwa na Polisi wa Merseyside nchini Uingereza baada ya kuonekana kwenye video moja akiendesha gari huku akitumia simu, inadaiwa kuwa Club yake ndio iliyopiga simu Polisi kuwafahamisha kuhusu video hiyo ya Mchezaji wao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom