Pamoja na yote bado Liverpool hii haijafikia kiwango cha ile Liverpool ya akina Pepe Reina, Gerald, Kuit, Alonso na Torres. Na bado ilishindwa kubeba EPL
• Hata Intermilan Ya Kina
Christian Panucci, Javier Zanetti, Laurent Blanc, Ronaldo, Roberto Baggio, Vieri, Taribo West, Ivan Zamorano na Clarence Seedorf haikuwahi Kuchukua CL Na Kwenye Ligi Mwaka 1999/2000 imekamata Nafasi ya 4.
Lakini Intermilan Ya 2010 ya Kina Cambiaso, Sneida na Balotelli imefanikiwa Kubeba Champion League na Ligi Kuu.
• Hata Chelsea ya 2012 iliyochukuwa CL haijaifikia Chelsea Bora Kabisa Kuwahi Kutokea duniani ya 2004/2005 ambayo haikuwahi Kubeba CL.
• Hata Manchester ya 2011 iliyobeba Ubingwa Wa EPL yakina Carrick haijaifika hii Ya Mastaa Wa Bei mbaya Ya Kina Pogba, Sanchez, Lukaku, Fred, Martial, Matic na De Degea ambayo Haijabeba Ubingwa Wa EPL.
• Hata Real Madrid hii iliyobeba CL Mara 3 mfululizo haijaifikia Real Madrid ya Kina
Casillas, Hiero, Medieta, Morientes, Raul, MacCmanaman, Roberto Carlos, Figo, Ronaldo na Zidane ambayo imeshindwa Hata Kubeba CL mbili.
Kwahiyo Jifunze tena kupenda Mpira Mdogo wangu Mpira Hauchambuliwi Hivyo.
Mpira Ni Kitu Kinachehesabiwa Kwa Wakati Uliopo.
Kwataarifa Yako Liverpool hii ya Sasa Ni More Stable kulinganisha na Hiyo unayosema Wewe.