Tena Kwa Sasahivi Ukitaka Ukose Mafanikio Basi Chukua Makocha Wanaotoka SCOTLAND, WALES au ENGLAND. Kwakweli Wabritish Kwa Soka la Sasa hivi Hawana Maana Tena na Baada Ya Kustaafu Sir Alex Fergurson Basi Makocha Wa Kibritish Watapotea Katika Ramani Ya Soka na Timu Za Kiiengereza Zitaendela Kufundishwa Na Wageni (Mourinho, Klopp, Guardiola, Pochetino, Conte na Emery).
Tatizo Kubwa la Wabritish Wanafeli Katika Usajili sijui Hata Kwanini!!!!
kwenye miaka yake 20 ya mafanikio umewahi kujiuliza kwa nini sir alex ferguson hakuwa na mafanikio makubwa kwenye ligi ya mabingwa.
jibu ni kwamba na yeye alijenga timu kwa kutegemea zaidi average player na ndio maana alijikuta akidhalilishwa mara kwa mara na wababe wa ulaya.
kwenye klabu kama real madrid, ac milan, inter milan, barcelona, bayern munich ulikuwa huwezi kumkuta mchezaji mwenye uwezo wa silvestre, brown, phil neville, fletcher, liam miller (RIP),quinton fortune, alan smith.
kwa emperor aliyoijenga pale old trafford alipaswa awe na jamii ya wachezaji kama gian franco zola,wesley sneijder, desailly, ronaldinho, modric na uwezo wa kuwasajili kwa kipindi tofauti alikuwa nao.
najua washabiki wenzangu wa manchester unite watanipinga.
miaka 20 ya mafanikio alipaswa awe na angalau makombe 5 ya UEFA kwa wastani wa miaka minne.
licha ya kuwa timu ilikuwa na uwezo wa kifedha lakini cha kushangaza AC MILAN walikuwa na kikosi bora kuliko united kwa zaidi ya miaka 6.