Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Acha ubishi mshikaji kakueleza ukweli,msikalie kujificha kwenye kivuli cha kuumia Salah na goli kipa wenu.Liverpool sio timu ya kuifunga Madrid kwa vyovyote vile na pale mmefika kibahati tu.
sasa wewe uliona madrid walikua na mpira gani pale?yaani timu kubwa inaingia uwanjani na option ya kuhakikisha wanamuumiza key player ndio ishinde?hata watford hawanaga hizo mbinu za kijinga.mapaka mlikua wengi sana,timu zenu zilishatolewa siku mingi nyie mnabaki kushadadia
 
Punguza jasba,mechi ilishaisha hata kabla ya 26052018
 
nimebahatika kuangalia mechi nane za liverpool msimu huu na mechi nne kati ya hizo ni pale walipokutana na timu zinazotoka jiji la manchester.
niwe mkweli mimi ni mshabiki wa manchester united na katika maisha yangu sijawahi kuipenda liverpool lakini napaswa niwapongeze kutokana na jitihada zao walizozionyesha msimu huu na kututoa kimaso maso timu za uingereza kama tunavyofahamu kwa miaka 5 hakuna timu ya uingereza iliofika fainal kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.
ujio wa jurgen klopp kama mwalimu wa liverpool umeleta mageuzi makubwa sana kwa klabu hiyo hususan aina ya soka wanalocheza la kumiliki mpira na kutokumpa adui nafasi ya kukaa na mpira kwa muda mrefu lakini udhaifu mkubwa alionao jurgen klopp ni kwamba inaonekana bado anaamini uwezo wa kifedha wa liverpool ni sawa sawa na uwezo wa kifedha wa timu yake ya zamani ya dortmund kwenye soko la usajili.
alipokuwa dortmund alijenga timu nzuri sana lakini tatizo ni kwamba dortmund walikosa back up ya wachezaji wenye uwezo wa kuleta mabadiliko pindi wanapopata nafasi ya kikosi cha kwanza, ukivuta kumbukumbu mpaka msimu wa 2012/2013 ambao dortmund walifika final na hata msimu uliofuata utagundua ya kwamba kilichowarudisha nyuma dortmund ni kutokuwa na wachezaji wa kutosha ambao wana ubora ukilinganisha na wapinzani wao kama bayern munich.
kwenye wachezaji 25 borussia walitegemea zaidi miujiza ya wachezaji 11 ambao ni lewandowski, marco reus, gundogan, gotze, subotic, hummels, weidenfeller, bender, kehl, blaszczykowski, schieber na groskreutz.
inamaana wachezaji 12 waliobakia walikuwa na viwango vya kawaida sana jambo ambalo lilipelekea dortmund kukosa mipango B pindi wanapokutana na timu zenye wachezaji wa viwango vya juu.
nampenda klopp kwa tabia yake ya kutokuacha kumpa nafsi mchezaji mwenye uwezo haijalishi ana umri mdogo, nimekua nikiwaonea wivu liverpool pindi ninapowaona vijana wawili alexander arnold na robertson wanapopata nafasi kwenye kikosi cha kwanza na wakicheza soka la kiwango cha juu sana kuliko hata walinzi wa pembeni wa timu ninayoishabikia, nawashauri liverpool wawape vijana hawa maslahi mazuri ili waondokane na tamaa ya kutaka kuondoka kwenye timu hiyo na hatimae yakatokezea kama ya rahem sterling, ashley cole na kyle walker. kiukweli huyu andrew robertson amenishangaza sana aina yake ya soka analocheza na kunifanya nitafakari hivi huyu beki wetu ashley young anacheza mpira wa aina gani?
andrew robertson hakupaswa kuzaliwa kwenye visiwa vya uingereza.
nimeona andiko la King Ngwaba akilalamika kuhusiana na liverpool kuwa na wachezaji wengi wenye viwango vya chini ukilinganisha na wapinzani wao real madrid, mimi nadhani ugonjwa wa kuwa na average player wengi kwenye kikosi si la liverpool peke yake kwa sababu hata manchester united, chelsea na arsenal pia ugonjwa huu upo na ndio maana msimu huu manchester city akabeba ubingwa kwa tofauti ya pointi 20 dhidi ya wapinzani wake.
liverpool wanahitaji wachezaji watano wenye kuendana na soka la kasi na kumiliki mpira ndipo wataweza kusimama na timu kama real madrid.
  • mlinzi wa kati ambaye atasaidiana van drjik ambaye ndiye usajili bora wa mwaka huu.
  • kiungo wa pembeni ambaye ataongeza ushindani dhidi ya sadio mane, jaribu kufikiria timu ya real madrid wana uwezo wa kumuanzisha bale, isco au asensio na wakapata matokeo mazuri.
  • mshambuliaji mwenye uwezo wa kufunga magoli 20 kwa msimu nadhani edin dzeko bado ana uwezo wa kucheza liverpool.
  • kiungo mshambuliaji ambaye hajazaliwa uingereza, nakusudia asicheze mpira wa kiingereza ambao ni wa kutokupenda kumiliki mpira.
  • nafasi ya goal keeper pia iangaliwe kwa umakini.
pia klabu inapaswa ipunguze wachezaji ambao ni liability ili kuwapa nafasi young player kutoka reserves team.
ni imani yangu ya kwamba liverpool wamepoteza pambano lakini hawajapoteza vita.
kama kweli tunataka kupambana na real madrid basi makocha wa timu zetu wawe na uono wa kusajili wachezaji mahodari na kuacha kusikiliza porojo za vyombo vya habari vya uingereza za kuwasifikia average player kutoka taifa lao.
aigoooooooo nimeota manchester united tumemsajili andrew robertson
GMW5_SJM_400x400.jpg
[HASHTAG]#ynwa[/HASHTAG]

Thumb up! What a good analysis from a real football fan.....
 
Acha ubishi mshikaji kakueleza ukweli,msikalie kujificha kwenye kivuli cha kuumia Salah na goli kipa wenu.Liverpool sio timu ya kuifunga Madrid kwa vyovyote vile na pale mmefika kibahati tu.

Mpaka Hapo Nimejiridhisha Kuwa Wewe Ni Mshabiki Maandazi.

Kwanini Hawa (ROMA, BARCA, CHELSEA, MAN CITY, MAN UNITED, SPURS, JUVE, PSG, BAYERN) wasiitumie Bahati Wakafika Tulipofika?

Niwazi Kuwa Mimi Ni ANTONY JOSHUA ninabishana Na MADA MAUGO.
 
Acha ubishi mshikaji kakueleza ukweli,msikalie kujificha kwenye kivuli cha kuumia Salah na goli kipa wenu.Liverpool sio timu ya kuifunga Madrid kwa vyovyote vile na pale mmefika kibahati tu.

Kwanza Onesha Discipline basi Japo Kidogo! Mimi Mawazo Yangu Yanajitegemea, Huwezi Chukua Mawazo Ya Wengine Ukayafanya Yananihusu!

Wako Wanaofanya Kuumia Kwa Salah Ndiyo Excuse Ya Kupoteza Mchezo! Lakini Mimi Sijawahi Kuongelea Kitu Hicho jaribu Kupitia Comments Zangu.

Halafu Nilishaacha Kuongelea Mechi Ya Fainali so, usijaribu Kuniprovoke Kuwa Lazima niijadili Kwani Hatuwezi Ku-Undo Kilichokwisha Kumaliza.
 
hao madrid hawana mpira wowote,wanaojua mpira wanajua hilo nyie wajinga wajinga msiojua lolote ndio mnabaki kupiga makelele,huyo ronaldo wenu alifichwa na mtoto mdogo sana Anorld,alikua anaruka ruka tu.

Hahaha, hii inaitwa bishana mpaka ufe.
 
hao madrid hawana mpira wowote,wanaojua mpira wanajua hilo nyie wajinga wajinga msiojua lolote ndio mnabaki kupiga makelele,huyo ronaldo wenu alifichwa na mtoto mdogo sana Anorld,alikua anaruka ruka tu.
Povuuuuuu ila TAA bado sana kuweza kumficha CR7 kilichotokea wale jamaa waliweka nguvu nyingi kumlinda CR7 kwa kumfata wengiwengi matokeo yake wengine ndo wanamaliza mchezo hahahahaha. Poleni [HASHTAG]#LOSERFOOLish[/HASHTAG]
 
Goli la Benzema linafungwa na washambuliaji wanaoijua kazi yao tu. Mwenyewe kasema, he knew what Karius was going to do. Ni akili ya kimpira imetumika pale, wakati beki zilikuwa busy kumkaba CR7.
 
feeling so sad!!!!

always we together

[HASHTAG]#WeAreLiverpool[/HASHTAG]
 
Kipa kafanya makosa kwasababu presha ya game ilikuwa kubwa. Without to underestimate players like Mane and Fermino, Real Madrid were better side than Liverpool, I don't understand why they couldn't score more goals !
Si kweli
Wkt Salah yupo ndani Liverpool walikuwa wazuri zaidi
Hata bila Salah tulistahili tuongoze kabla ya huyu mwehu kumpa bao Benzema
 
At least Kwanza Tuanze Na Fekir Na Alison ili tusijerudi alikotuacha Benitez.
Makipa wawili wapya LZM wala sio ombi tena!
Karius hawezi rudi hata kucheza team yyt Uingereza,watamuua aisee!
Hata yy anajua kuchezea Liverpool is OVER
 
Klopp aliwatayarisha vijana wake kwa final hii vizuri sana
lkn Karius kam let sana down
CD Lovren na VVD walikuwa bora mno uwanjani
Pembeni ndiyo balaa zaidi hadi CR7 akawa ana mbwela mbwela tu
Klopp nimemkubali sana
 
Jifariji tu but huna timu ya kumfunga madrid hasa katka finali
 
Si kweli
Wkt Salah yupo ndani Liverpool walikuwa wazuri zaidi
Hata bila Salah tulistahili tuongoze kabla ya huyu mwehu kumpa bao Benzema

Wewe Malafyale hujui mpira. Benzema ni genius, lile bao hakupewa. Mpira ulikuwa half way kipa akautokea akauwahi, alijua hawezi kurudi nao kwenye box, lazima aanze na beki. Pale ni akili imetumika. Mtakaa kulialia mpaka lini?
 
sasa wewe uliona madrid walikua na mpira gani pale?yaani timu kubwa inaingia uwanjani na option ya kuhakikisha wanamuumiza key player ndio ishinde?hata watford hawanaga hizo mbinu za kijinga.mapaka mlikua wengi sana,timu zenu zilishatolewa siku mingi nyie mnabaki kushadadia
Hata hatujapigwa thana...........
IMG_20170820_200352.jpg
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom