Mshahara Hauongezwi Kama Wa Mfanyakazi Wa Serikali anapoongezewa na Raisi. Bali Huongezwa Pale Anapoongeza Mkataba Mpya tu...!
Kumbuka Mo Salah Aliponunuliwa Hakuwa hivi alivyo sasa! Kwahiyo alikubaliana Mshahara unaostahiki kulingana na Kiwango Cha Wakati huo.
Atakapoongeza Mkataba Mpya Ndiyo hapo Yeye Mwenyewe atadai new [HASHTAG]#salary[/HASHTAG] inayoendana na Kiwango Chake.
Kumbuka alipokuwa AS Roma alikuwa analipwa £50,000/= per week, Na Alipokuja Liverpool katika Negotiation alidai ili Asaini Mkataba na Liverpool ni Lazima alipwe £90,000/= kutokana na Kuwa ilikuwa ni hela ndefu kulingana na alikotokea na Liverpool wakamkubalia kumlipa hivyo.
Sasa Hapa hatuwezi ilaumu Timu wala kumlaumu Yeye..
Tusubiri Atakaposaini Mkataba mpya Ndiyo atadai hela Ndefu kama aliyodai VVD £180,000/= kwa week.
Kwahiyo Mo Salah kama atadumisha Kiwango hichi alichonacho basi Wanaweza kumzidi Hata VVD na akawa ni Mchezaji anaelipwa Zaidi Ndani ya Liverpool.