Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Liverpool FC (The Reds) | Special Thread

Mechi na chelsea mane alicheleweshwa sub na mechi ilipoisha alionekana akimlaumu kocha, Jana kafunga hajashangilia, Alikua anatupa Ujumbe gan kwa kutokushangilia? Kuna kitu gan kinaendelea hapo?
 
Mechi na chelsea mane alicheleweshwa sub na mechi ilipoisha alionekana akimlaumu kocha, Jana kafunga hajashangilia, Alikua anatupa Ujumbe gan kwa kutokushangilia? Kuna kitu gan kinaendelea hapo?
The man is currently not happy because he sees/thinks the respect,appreciation,faith and value he was given earlier by the manager and to some extent by the fans,are no longer there.

As a human being i would have felt the same regarding Klopp's treatment towards him recently
 
Respect sana mkuu, unajua alikua na kaufalme kake, ilifikia hatua watu wakawa wanasema akiumia mane au kwenda afcon liver haifanyi vzr, kale kaufalme kamehamia kwa mo Salah, hilo litakua linamtesa sana na huenda ndio maana muda mwingine analazimisha kufunga hata Kama Kuna mtu yupo pazuri zaidi yake. Ni vizuri klopp akamtambua na kumpa matibabu ya kisaikolojia. Mpira ni kitu Cha ajabu Kuna siku atarudi kwenye fomu na loyalty watakua wanapokezana.
 
Ukwel huyu jamaa nampenda kuliko wote liverpool maana ni zaid ya fighter ila naumia pia nikiona furaha yake ikipungua anfield klopp anajisahaulisha tu umuhimu wa huyu jamaa
 
Kama Coutinho anaenda barca january hii atakuwa amejitoa ushiriki wa uefa champions league msimu huu.
 
The man is currently not happy because he sees/thinks the respect,appreciation,faith and value he was given earlier by the manager and to some extent by the fans,are no longer there.

As a human being i would have felt the same regarding Klopp's treatment towards him recently

Miongoni Mwa Wachezaji Waliokoseshwa Heshima Na Washabiki na Kutoaminika Mpaka Kwa Kocha Ni Mignolet, Moreno, Lovren na Henderson! Lakini mbona Hawana Bifu na ingawa uwezo wao Ni Mdogo lakini Wanapokuwa uwanjani Wanajituma kadri ya Kiasi cha uwezo wao na Wanakuwa na Furaha!!
Kwanini Kwa Sadio Mane iwe Tofauti wakati Bado anaaminiwa na Mashabiki pamona na Klopp??
Kilichopungua Kwa Mane Ni Hile Status Yake tu Yakuwa Ni "Main man" wa Livedpool lakini kafanya Kiburi...

Na Tabia Hii Kaianza Siku hile Ya Game na Chelsea!! Mimi Nahisi Kuna Sababu Nyengine Mbali inayomfanya Akose Furaha na si Kulilia Heshima.

Ninachodhani, Sababu Kubwa ya Mane Kuleta hizi sintofahamu Ni Kuwa Hakubaliani Na Kufanyiwa Rotation.

Kiukweli hili halibishiki Hakuna Mchezaji Hata Mmoja Duniani Anaekubali Kufanyiwa Rotation! Hata Hawa Kina Firmino na Coutinho huwa Hawapendi lakini Huyu Mane Yeye Kaamua Kuonesha waziwazi Kuwa Anachukia Kuekwa Bench Kwa Kisingizio Cha Rotation.

Kwani Rotation inaondosha Consistency ya Mchezaji!
Mtazame Gini uwezo wake ulivyishuka Kutokana Na Hii Rotation!!

By the way Sitegemei Tena Kutokea Kwa Hichi Kinachoitwa Rotation Kwani Kipindi Cha Mrundikano Wa Mechi Kimeshapita sasa tutaendelea Na Mechi Zetu za Kila Weekend.
 
Miongoni Mwa Wachezaji Waliokoseshwa Heshima Na Washabiki na Kutoaminika Mpaka Kwa Kocha Ni Mignolet, Moreno, Lovren na Henderson! Lakini mbona Hawana Bifu na ingawa uwezo wao Ni Mdogo lakini Wanapokuwa uwanjani Wanajituma kadri ya Kiasi cha uwezo wao na Wanakuwa na Furaha!!
Kwanini Kwa Sadio Mane iwe Tofauti wakati Bado anaaminiwa na Mashabiki pamona na Klopp??
Kilichopungua Kwa Mane Ni Hile Status Yake tu Yakuwa Ni "Main man" wa Livedpool lakini kafanya Kiburi...

Na Tabia Hii Kaianza Siku hile Ya Game na Chelsea!! Mimi Nahisi Kuna Sababu Nyengine Mbali inayomfanya Akose Furaha na si Kulilia Heshima.

Ninachodhani, Sababu Kubwa ya Mane Kuleta hizi sintofahamu Ni Kuwa Hakubaliani Na Kufanyiwa Rotation.

Kiukweli hili halibishiki Hakuna Mchezaji Hata Mmoja Duniani Anaekubali Kufanyiwa Rotation! Hata Hawa Kina Firmino na Coutinho huwa Hawapendi lakini Huyu Mane Yeye Kaamua Kuonesha waziwazi Kuwa Anachukia Kuekwa Bench Kwa Kisingizio Cha Rotation.

Kwani Rotation inaondosha Consistency ya Mchezaji!
Mtazame Gini uwezo wake ulivyishuka Kutokana Na Hii Rotation!!

By the way Sitegemei Tena Kurokea Kwa Hichi Kinachoitwa Rotation Kwani Kipindi Cha Mrundikano Wa Mechi Kimeshapita sasa tutaendelea Na Mechi Zetu za Kila Weekend.
Rotation haikwepeki

Hawa Ni watu sio mbwa mwitu

Mane is fine, na form imedip... Klopp kasema mane was sick, mane kasema he was sick

Tuache drama
 
Best progress:
Liverpool imeshinda
Michezo 5 Kati Ya 6 iliyopita ya Ugenini Kwenye Premier League.

4-1 v West Ham
3-0 v Stoke
5-1 v Brighton
4-0 v Bournemouth
3-3 v Arsenal
2-1 v Burnley

Tumevuna Points 16 kati ya 18 tulizopaswa.

"Tatizo Lipo Kwenye Uwanja Wetu Wa Anfield"
 
Mashabiki Wa Liverpool Walichokipendekeza Kupitia Mitandao Mbali mbali Ya Kijamii!

1) Coutinho Asiuzwe

2) Liverpool iishtaki Nike & Barcelona kwa FIFA Kwa Kumvuruga Mchezaji Kinyume na Taratibu.
√ Hapo Barcelona itakumbana na Transfer Ban.

3) Hapo imuadhibu Coutinho Kwa Kumpokonya Namba Kikosi Cha
Kwanza na Aishie Kusota Benchi.

4) Coutinho acheze Kama Mchezaji Wa Hakiba (Reserved) Kwa Kipindi Chote Cha Miaka 4 ya iliyobakia Ya Mkataba Wake.

5) Hapo Tayari Liverpool Wameshamharibia Ndoto Zake Za Kucheza Kombe LA Dunia Kwani Brazil Haichukui Wachezaji Wa Hakiba.

HILI LITAKUWA NI FUNZO KWA BARCELONA DHIDI YA LIVERPOOL KUVURUGA WACHEZAJI
WETU! NA VILEVILE NI FUNDISHO KWA WAAMERIKA WA KUSINI KUTOHESHIMU MIKATABA YAO NA KUTAKA KUVURUGA TIMU

Inaonekana huwajui FSG alichofanya Coutinho sio kitu kipya hapo Liverpool Sterling na Suarez walifanya the same na still wakauzwa ndio policy ya hao wamarekani na wamempata kocha anayefit kwenye policy zao .Kununua mchezaji kwa below £10m then kumuuza kwa £130 ni faida kubwa kwao
 
Man City tunatakiwa tumfunge, zile goli tano alizotupiga bado zinaniuma sana!
 
Ni opinions tu so sio lazima tuwaze sawa.Suala la Mane bado naliona vilevile kama nilivyoandika hapo juu.Hardhishwi na jinsi ambavyo anakuwa treated kwa sasa.Ni kama vile thamani yake imeshuka na kocha kwakuwa anapata anachokitaka kwa Salah basi ameamua kumuignore Mane.

Kwa mawazo yangu Klopp anapaswa kuonyesha kuwa bado anamuamini Mane ili mentality yake irudi normal.Kwa mawazo yangu with Salah and mentally fit Mane together we can get the accelerated striking force ambayo ni advantage kwa timu.

Still wote ni wachezaji wazuri sana
 
Baada ya michezo 22 msimu uliopta na msimu huu.
season 2016/17

Win 13
draw 06
loose 03
goals 51
concede 27
GD 24
position 4
pts 45

season 17/18
win 12
draw 08
loose 02
goals 50
concede 25
GD 25
position 04
pts 44
 
Baada ya michezo 22 msimu uliopta na msimu huu.
season 2016/17

Win 13
draw 06
loose 03
goals 51
concede 27
GD 24
position 4
pts 45

season 17/18
win 12
draw 08
loose 02
goals 50
concede 25
GD 25
position 04
pts 44

Dah! Hakuna Mabadiliki Yoyote Ya Kuboreka!! Bali Tumeshuka Kama asilimia 0.9% hivi!!!!
 
Accra, Ghana. Kiungo wa pembeni wa Liverpool, Mohamed Salah anapewa nafasi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, katika hafla itakayofanyika nchini Ghana.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri anapewa nafasi, baada ya kucheza kwa kiwango bora katika kikosi cha Liverpool.
Salah anachuana vikali na nyota wengine wawili akiwemo mshambuliaji wa Gabon, Pierre Erick Aubameyang aliyeshinda mwaka 2015 anayecheza Borussia Dortmund.

Pia Liverpool imemtoa mshambuaji nyota wa Senegal, Sadio Mane ambaye alikuwa nafasi ya tatu mwaka 2016.
Salah aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa BBC, alifunga mabao muhimu yaliyoiwesha Misri kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia nchini Russia mwaka huu.
Misri inashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990 ilipokata tiketi kucheza mashindano hayo nchini Italia.
 
Kuhusu Salah

WAPINZANI wana kazi mbili kubwa za kufanya siku hizi wanapokwenda Anfield. Kwanza ni kucheza dhidi ya Liverpool na pili ni namna ya kumzuia Mohammed Salah.

‘Ustadh Salah’ kama anavyoitwa katika vibandaumiza vingi nchini. Achana na mabao ya Harry Kane, achana pia na kasi ya Kevin de Bruyne, Mo Salah ndiye mchezaji hatari zaidi kwenye Premier League msimu huu. Namba zinazungumza!

Anawapa raha Liverpool. Anafunga na kutengeneza mabao kila siku. Haikushangaza sana mashabiki wa Majogoo hao wa Jiji la Liver, kumpachika jina la ‘Messi wa Anfield.’

Safari yake kutoka Misri hadi Ulaya ni kielelezo tosha cha ubora huu tunaoushuhudia leo hii. Salah alianza kuamini tangu utotoni.

Kabla ya kuwa Waziri Mkuu wa Misri, Ibrahim Mahlab, alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya El Mokawloon. Timu ya utotoni ya Mohammed Salah.

Taarifa zinaonyesha kuwa 2011 klabu kubwa za Misri, Zamalek na Al-Ahly zilituma ofa ya maana kwa ajili ya kuihitaji saini yake lakini Mahlab alizipiga chini akisisitiza kiwango cha Salah ni cha kucheza Ulaya.

Mahlab alikuwa na hisia kuwa Salah ameshafika kiwango cha kucheza Ulaya,” alisema Alaa Nabil aliyekuwa Mkurugenzi wa ufundi wa kikosi cha El Mokawloon na kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Misri. ‘Aliaminia angefanikiwa zaidi akiondoka Afrika.

‘Salah hakujua angeondoka vipi Misri wakati ule, lakini Mahlab aliendelea kumhakikishia kuwa iko njia ya kufanikisha hilo.
 
Liver waifukuzia saini yake kwa miaka minne

Hatimaye Salah alijiunga na FC Basel ya Uswisi na hapa ndio kwa mara ya kwanza mawakala wa Liverpool walipoanza kumfuatilia.

Katika mechi za Kombe la Uropa, Basel walipocheza dhidi ya Tottenham na Chelsea, wawakilishi wa Liverpool walisafiri kumfuatilia na mara kwa mara walikuwa wanakwenda pia mazoezini kumtazama.

Hapa Chelsea walipowapiga bao na kumsajili mwaka 2014, Liverpool hawakukata tamaa ya kuendelea kumfuatilia. Na alipojiunga na Fiorentina na Roma, skauti mkuu wa Liverpool, Barry Hunter na Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Michael Edwards, waliupasha uongozi kuwa wafanye kila linalowezekana kumnasa winga huyo.

“Kwa miaka minne, siku tano za kila wiki nilitoka nyumbani saa tatu asubuhi na kutembea kwa saa tano kufika mazoezini.

Kawaida mazoezi huanza saa tisa na nusu au saa kumi, hivyo nilijitahidi kuwahi mapema. Ningemaliza mazoezi saa 12 jioni kisha kuanza tena safari ya kurejea nyumbani.

“Saa nne na nusu usiku ningefika nyumbani kisha nakula, nalala na kujiandaa na safari nyingine siku inayofuata. Yalikuwa maisha yangu ya kila siku na nilishazoea,” maneno ya Mohammed Salah, alipofanya mahojiano na mtandao rasmi wa klabu ya Liverpool.

Ni stori inayokupa taswira ya magumu aliyopitia, lakini inakufunza pia jitihada mara zote hulipa.

Salah alizoea kutoka nyumbani saa tatu asubuni na kurejea saa nne na nusu usiku kwa ajili ya kufanya mazoezi. Angebadilisha zaidi ya mabasi matano kila siku njiani.

“Nilianza kufanya mazoezi katika kiwanja cha karibu na nyumbani. Ni umbali wa nusu saa tu kutoka katika kijiji chetu cha Basyoun,” aliongeza Salah, mwenye mabao 17 na asisti tano kwa dakika 1596 alizocheza kwenye Premier League msimu huu.

Baadaye nilipata timu katika mji wa Tanta, ni mwendo wa saa moja na nusu kutoka nyumbani. Sikukaa sana nikajiunga na timu Arab Contractors iliyokuwa Cairo. Hapo ndio nililazimika kutembea mwendo mrefu kutoka nyumbani kwa ajili ya kwenda kufanya mazoezi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom