Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,117
- 1,249,282
Apewa ruhusa na mkuu wa shule kukaa darasani masaa mawili tu
Nililazimika kuondoka shule mapema ili niwahi mazoezini. Nilikuwa na barua rasmi ya mkuu wa shule kwa ajili hiyo hivyo shule nilifika saa moja asubuhi na kutoka saa tatu.
Naikumbuka ile barua ya mkuu wa shule iliandikwa ‘Mo aruhusiwe kuondoka mapema ili awahi mazoezini.
Nilikaa shule kwa masaa mawili tu. Sijui maisha yangekuaje sasa kama ningefeli kwenye soka!
Sasa tunamzungumzia mchezaji bora wa Afrika, mchezaji bora wa mwezi Novemba, kwenye ligi kubwa ya England. Sasa tunamzungumzia Mo Salah, anayefunga anavyojisikia.
Hili halijatokea kwa bahati mbaya. Tangu utotoni Salah alikuwa na ndoto ya kuwa mchezaji bora duniani.
“Kama nilivyosema, ilikuwa ngumu nyakati zile lakini sikukata tamaa. Nilitamani kuwa mchezaji mkubwa siku moja, mchezaji wa kipekee kidogo,” alisema Salah.
Nawaambia ukweli, nilikuwa nikitamani kuwa mkubwa siku moja lakini sikufikiria kama ningekuwa hapa leo hii. Kila kitu kilikuwa ndoto kwangu nilipokuwa na miaka 14, lakini niliishi na imani kuwa nitafanikiwa. Namshukuru Mungu kwa yote.”
Hii ndio safari ya Mo Salah.