Live: Kizota Dodoma

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
POLENI WAJUMBE BAADA YA KUANGALIA NA KUSIKILIZA ONYESHO LA KWANZA LA MSANII KINGWENGU NGWENDULILE....kwa sasa burudikeni na muziki na misosi laini wakati msanii wa pili MANYWELE anapojiandaa kupanda....tupo pamoja hapo...dom.

Hapa ndipo credibility ya JF inapohojiwa, it's very sad!
 

Mkuu ES,
kuna kitu kimoja tu nilipokisoma haikuhitaji nimalizie kusoma ili kukupa thanks, hii habari imejaa ukweli kwa asilimia kubwa sana kwa kusema ukweli !
Nakupa hongera kwa hilo, naona sasa hivi UMEKUJA KAMILI !
Lakini kuna viongozi pia watatajwa nadhani watu watashangaa !
 

Kwa sisi ambao tuko mbali na nyumbani tunapenda kupata habari kamili na wala si mzaha-mzaha, ninakushukuru sana Mkuu.
 

Niko pamaoja na wewe FD, nadhani wale wasioripoti yanayoendelea Chimwaga kama yanavyojitokeza wanawanyima haki ya kimsingi kabisa watumiaji wengi wa JF. Kama Lunyungu anamchukia mtu au CCM hilo ni tatizo lake binafsi, asipotoshe umma wa JF. Akumbuke kuwa watu waliopo katika JF ni kutoka pamde zote za dunia ambao kwao habari kamili ndiyo siha yao.
Ahsante sana FD.
 

FD bado nasisitiza tupo pamoja, katika Mkutano Mkuu kama ule Mwenyekiti atategemewa zaidi kuongelea maendeleo / yatokanayo na ilani ya CCM, na hapo ndipo wakati wake wa kuelezea nini kimefanyika na wala sio jukwaa hasa la kupiga blah blah. Na kama asingefanya hivyo wa-CCM na wengine wetu tungemshangaa zaidi. JK knows exactly nini anachotakiwa kufanya.
 

Hii 'historical background' imetulia kiaina, ila tunasubiri zaidi uchunguzi wa ajali ya huyu waziri kwa hamu, kwa sababu hio conspiracy hapo juu inatutia shaka kidogo!
 
Nilitaka kuja na hoja yangu binafsi humu Jf. Lakini naiahirisha kwa muda nikisubiri matokeo/actions za hotuba ya leo. ninatoa hadi december mwishoni. nisipoona dalili yoyote nitatoa tamko rasmi kwamba JK is not the President tuliomchagua bali ni kanyaboya aidha CCM au wazungu/wawekezaji wametubadilishia.

Naomba niwe mvumilivu kwa mara nyingine.
 

babu dont worry speaking your opinion, unaweza ukasema time yoyote hiyo opinion yako !

nadhani watu walishasema pia before kwamba jk is the worst prezzo, so utakuwa unaendeleza libeneke !

great !
 

Katibu Tarafa,
Siri lazima ziwepo, huwezi kuzifuta katika ulimwengu huu. Si kila jambo linalofanywa ki-maamuzi na kiutendaji lianikwe haitakuwa ni practical.
Si unajua hatavyumba vyenye pesa huwekewa kijina-siri, kuingia pia kwenye mtandao wa JF lazima uwe na kijina-siri.
 

Heshima kwako,Mkuu.

Nadhani sikuwa peke yangu niliyekuwa nasubiri "za jikoni" kutoka kwako,na hujatuangusha tuliokuwa tukisubiri.

Hili la Sophia Simba limenishtua na kunisononesha kweli.Hivi hawa watu walio tayari kupoteza maisha ya wenzao kwa ajili tu ya madaraka,wanadhani wakifanikiwa katika azma hizo za kishetani hata hayo madaraka yatakuwa matamu?Muuaji yeyote anaendeshwa na tamaa na ubinafsi,na kwa maana hiyo muuaji akipata madaraka baada ya kutoa roho ya mtu mmoja hatoshindwa kuondoa roho nyingine,aidha kwa kurejea kuua mtu wingine physically au kuendekeza ufisadi utakaopelekea kupoteza maisha ya watanzania kadhaa kwa kukosa huduma muhimu kwa maisha yao.

Hivi Sophia akiambulia patupu ktk uchaguzi huu atabaki na amani kweli?
 
babu dont worry speaking your opinion, unaweza ukasema time yoyote hiyo opinion yako !

nadhani watu walishasema pia before kwamba jk is the worst prezzo, so utakuwa unaendeleza libeneke !

great !


Kada,

Hii itakuwa ya kwangu binafsi na wala sitamshawishi mtu kuunga mkono. ndiyo maana nikasema, naomba kuwa mvumilivu kwa muda na wala sikukandia hotuba yake. nimetoa maoni kwamba hotuba ni nzuri kama Fd alivyotuabarisha na kwamba ita value only and only if atafanya kama alivyo yazungumza.
 

sawa babu !
 
Mimi nilidhani kwa kuwa waliwaalika Wapinzania basi ustaarabu ungalikuwa lukuki kumbe baadaye akina Cheyo waliona jengo dogo baada ya kuanza kustwa . Hata kama ujumbe ulikuwa unaenda kwenye vyama 4 pekee ambao walikuwa branded kama waroho wa madaraka kwa kuitwa paka mbele ya panya lakini Cheyo was heavily embarrased huku JK akitumia neno la mtaani na kuonyesha kutokuwa serious kwa kuwaita wapinzani watani wao wa jadi .Pale nilianza kuingiwa na maswali na again they laid their standing that they will never put their hands on rushwa nje ya Chama yaani serikalini.

Kweli mkutano huu una maajabu yaani wameamua kutojibu tuhuma na wamekimbilia kusema wao wana wajibika so mambo ya akina Karamagi ndiyo mwisho wake kwa CCM.JK he went far to suggest kwamba watoa tuhuma waende Mahakamani badala ya kutumia majukwaa ya kisiasa that was an indication kwamba kuna collective responsibilty na kuhitimisha maneno ambayo nimeyasikia hapa Dodoma kwamba Karamagi anasema JK hawezi kuthubutu kumuengua kwenye uwaziri kwa kuwa anamjua viilivyo na anaweza kumwanika.Baada ya jana sasa asubuhi nimekuwa natafakari na kuona kuna ka ukweli ndani ya haya madai .

Serikalo zote 2 za bara na visiwani walielezea jinsi wanavyo sifiwa na mataifa ya nje lakini ndani wanadharaulika . Hili lilikuwa ni jambo la kushangaza maana hao akina Bush hawajafika kijijini waone Mgambo, watendaji wa vijiji na kata anavyo wanyanyasa watu . Hawajafika waone watu wanavyo lala njaa , wanavyo kufa bila ya huduma za hospitali,hawana nguo wanavaa viraka, hawajui milo 3 wala shule za misingi haziko karibu na zikiwepo hakuna walimu wala nyumba za walimu.

Poleni sana kama mlitegemea kitu serious bali mliweza kupata presha hadi JK akayumba na kutumia maneno yale kubeza wapinzani. Nikabaki na maswali kibao nikijiuliza kwamba wale ni wana muziki wanaouza muziki wao na wakaanza kuwaponda wapinzani je wanunuzi wa muziki wao ni CCM pekee ?

Je na wale wasio kuwa na vyama wana nafasi gani katika muziki wa wana ccm wale ?

Mungu isaidie Tanzania tuko mbali .
 

Aise Lunyungu

Kura tano

Nyerere alisema kuwa ukiona watu wa nje wanakusifia ujue una kasoro.

Je JK alichaguliwa na Bushi au ndiyo kutapeli watanzania? Mbona ni huyo huyo aliomba majina ya wala rushwa? Nafikiri kafirisika kimawazo. Anahitaji msaada wa mawazo na wataalamu zaidi.
 
Lunyungu vipi mbona leo kimya? tupe update yanajiri huko Dom au mpaka aanze CMB na wewe ndio unaunganisha "ukiwa Dodoma"
 
Now I can see the original Mzee ES aka FMES. Mzee hongera sana, hayo maneno yako ni mazito giving an insightful picture of what is going on. Hivi ndivyo nilivyokujua mimi kule bcs na ndivyo heshima yako ilivyojengeka. Keep up the good work!
 
Bado nitaendelea kuhoji credibility ya JF?

Ukitaka kuona credibility ya JF ungeanza kwako kwanza. Hapa tupo watu wa mitazamo mbali mbali, mawazo yetu hayafanani kamwe! Hoji kwanza credibility ya hao waliomwalika huyo unayemtetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…