Live: Kizota Dodoma

Live: Kizota Dodoma

  • Thread starter Thread starter MegaPyne
  • Start date Start date
Katibu Taarafa,

JK hakuzungumzia mkataba wa UMEME, ameongelea ya Madini. Kwa sasa tume ipo (mnajua Maria Kejo ni mmoja wapo wa wana tume hiyo?🙂 inazunguka duniani kote kucheck best practices za kwenye madini, Ikimaliza kazi yake JK ndipo atafanya mambo. Hiyo tume IMESHAANZA KAZI ZAKE.

ENDELEENI KUULIZA, ila ikumbukwe bado hata mimi natazama pande zote za shilingi.
 
FD,
Kwanza kabisa ahsante kwa mchango wako hapa jamvini. Najua unapenda kuongelea "upande wa pili wa hiyo shilingi" yetu.

Kwa kuwa umetuomba kukuuliza maswali, miye swali langu ni kuwa; Kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais na M/kiti wa CCM, je ameongelea vipi kuhusu swala la Mh. Balali kuendelea kuwa Gavana wakati serikali imeamuru uchunguzi ufanyike kwa kukubali hitilafu kadhaa zilizoonyeshwa na ripoti ya CAG, na madukuduku ya wadhamini wa Bajeti yetu, hali wakati Dr. Slaa anatoa hoja Bungeni walisema hayo ni mambo ya mtandaoni (internet) na si ya kuamini. Natanguliza shukrani zangu.

Ooh, BTW, naomba uache kuwaita wote wanaohoji kuhusu CCM kuwa ni Chadema. Kwani wengine hatuna vyama ndugu yangu. Ni hilo tu.

SteveD.
 
Shukran,
Msekwa mzee wangu nampa tano.. ila sidhani kama ataweza kazi ya Malecela kwani heshima yake ndani ya CCM na hasa vijana wapya (Mtandao) sio kubwa. Aliposimamishwa Uspika mzee wangu alikuwa mnyonge sijapata kuona na hata huko UK kwenyewe watu walimng'ong'a kwa sababu mzee huyu ana jeuri kama Mkapa. He did nothing for them kama inavyosemekana Mama Mongela ambaye leo kazikwa akiwa hai (hasikiki kabisa).
Haya tupe kinachoendelea!...
 
Mfwatiliaji,

Hakuongea specific kuhusu BOT, ila amesema (nadhani) ni DR Slaa kuwapotosha wafadhili, amesema wafadhili walipotoshwa as if hakuna serikali inafanya kuhusu hizo tuhuma. Amesema wakawaambia kuwa BOT inafanyiwa kazi..(OF coz tunajua inafanyiwa kazi si ndio)

Ila aliwaonya viongozi wa vyama vya ushirika, kwa kuoneana aibu na kutowajibishana. Akasema kwa sasa serikali inaboresha soko la mazao mbalimbali iliwemo korosho, na serikali inapump hela ktk hivyo vyama kwa hiyo ita vi monitor.

Man 1 Arsenal 1, mpira unaendela, Man kazidiwa kiaina.
 
FD,
Nakumbuka unaweka sahihi yako ya "Mtazama pande zote za shilingi " imeishia wapi mjomba?

Hivi kweli wewe unaamini kuwa Dr. Slaa amewachochea wafadhli ama ndio ukweli wenyewe?... Hivi maneno haya yangesemwa na Prof. Shivji ingesemwa nini ama ndio siasa sio kazi yake?.. maanake nashiondwa kuelewa ni nani hasa anatakiwa ku raise issue inayotukabiri nchini.
 
Mkandara!
Upo kwenye wazo Langu nafikiri tumepishana sekunde ktk kujibu hoja ya FD.
Swala si kuongelea mazuri bali ni kuyatekeleza na mafanikio kuonekana.Kuongea tu hakusaidii na wala hakuleti tija ya aina yeyote na Faida kwa Wananchi.

K N K CU na Mkandara, naungana nanyi kwenye hii hoja. Nami kubwa ambalo hulichukulia mabango ni kuhusu utekelezaji na uwajibishwaji wa wale tuliowekeza matumaini yetu kutuongoza kutofanya hivyo. Shirika kama linazorota na kufirisika, lazima kuna walio husika, mifano ni mingi sana nchini mwetu hapa, lakini mifano ya walio wajibishwa ni michache au haipo kabisa.

CMB, Lunyungu na FD ahsante kwa kutuletea habari.

SteveD.
 
FD,
Tupe jibu la maswali hayo hapo juu
Ujenzi wa reli utaanza lini? 2. kiasi gani? na 3. lini inategemewa kwisha
Huo usambazaji wa Umeme unatarajiwa kufikia kiwango gani cha asilimia na mwaka gani?
hayo mengine yote ktk hotuba yaweke ktk maswali haya haya kisha tupe jibu kama hutabaki na ahadi mkononi!

Mkandara,

Ujenzi wa reli unafanyiwa tathmini na ma injinia kwa sasa. Unaanzia (nimesahau) sehemu moja kati (karibu na Tabora nadhani) mpaka Burundi na Rwanda, kisha baadaye watajenga mpaka Dar, sasa hii ya kuja Dar itakua ni Cheap, maana wataongeza Reli moja tu kati ya njia inayo exist, yaani reli itaweza kutumika na treni ya zamani na hiyo nyingine. Sikumbuki hela, lini nimesahau.

Usambazaji wa umeme kuongeza asilimia kwa kweli Mkandara nililiona ni la kisiasa zaidi, pale alikuwa anapiga blah blah.
Cha muhimu pale ilikuwa kile alichosema kila sehemu yenye nishati inayoweza kutoa umeme kama vile Gesi basi watapata umeme.

Lowasa ndie atakaye toa takwimu zaidi.
 
FD,
Kwa hiyo alichozungumza ni nadharia tu na hakuna kitu cha maana,unajua sisi watu wa hesabu tunajua 2+2=4.haya mambo ya tunafanya kwa siri ndio tusio yataka ktk ulimwengu wa sasa.basi yote ni utumbo tu hakuna jipya punda na masikio.manu 2,arsenal 1
 
FD,
Kwanza kabisa ahsante kwa mchango wako hapa jamvini. Najua unapenda kuongelea "upande wa pili wa hiyo shilingi" yetu.

Kwa kuwa umetuomba kukuuliza maswali, miye swali langu ni kuwa; Kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais na M/kiti wa CCM, je ameongelea vipi kuhusu swala la Mh. Balali kuendelea kuwa Gavana wakati serikali imeamuru uchunguzi ufanyike kwa kukubali hitilafu kadhaa zilizoonyeshwa na ripoti ya CAG, na madukuduku ya wadhamini wa Bajeti yetu, hali wakati Dr. Slaa anatoa hoja Bungeni walisema hayo ni mambo ya mtandaoni (internet) na si ya kuamini. Natanguliza shukrani zangu.

Ooh, BTW, naomba uache kuwaita wote wanaohoji kuhusu CCM kuwa ni Chadema. Kwani wengine hatuna vyama ndugu yangu. Ni hilo tu.

SteveD.

Steve, Ninaomba radhi kuwaita Chadema, Nilishaomba hata hivyo hapo juu, nikasema nilimaanisha Lunyungu na Phil.

OK kaka tuendelee. Hakuongelea hayo yote uliyouliza.

Ila mimi nitakujibu kuwa, unajua Gavana ni mgonjwa na yupoa Marekani muda mrefu?, unajua kwanini uchunguzi umeanza ndio na yeye anaugua na kwenda USA?, ukifikiri tena kidogo tu utagundua kua amepumzishwa kwanza mpaka uchunguzi uishe.

Unajua Tuhuma zinaweza kuwa za kweli au za uongo, sio vizuri kumharibia mtu CV yake bure. Hivyo hata hivyo jamaa hayupo .... si ndio inavyotakiwa na ndio ILIVYO.

Kwahiyo sikuona kama ni issue.
 
Hakuongelea mambo ya Dr Slaa.

Ila ameonya juu ya kuchafuliana majina, sijui mwka flani nani alifanya nini kwa kutumia majukwaa ya siasa na mtandao wa Kompyuta!
 
FD,
Kwa hiyo alichozungumza ni nadharia tu na hakuna kitu cha maana,unajua sisi watu wa hesabu tunajua 2+2=4.haya mambo ya tunafanya kwa siri ndio tusio yataka ktk ulimwengu wa sasa.basi yote ni utumbo tu hakuna jipya punda na masikio.manu 2,arsenal 1

Yeah, nimefurahi sana Man UTD 2 Arsenal 1 mpira unaendelea.

Steve, kweli kabisa ukisoma hotuba na mifano iliyotolewa utaelewa.
Ngoja kesho usikie.

Manu 2 Arsenal 2
 
Steve, Ninaomba radhi kuwaita Chadema, Nilishaomba hata hivyo hapo juu, nikasema nilimaanisha Lunyungu na Phil.

OK kaka tuendelee. Hakuongelea hayo yote uliyouliza.

Ila mimi nitakujibu kuwa, unajua Gavana ni mgonjwa na yupoa Marekani muda mrefu?, unajua kwanini uchunguzi umeanza ndio na yeye anaugua na kwenda USA?, ukifikiri tena kidogo tu utagundua kua amepumzishwa kwanza mpaka uchunguzi uishe.

Unajua Tuhuma zinaweza kuwa za kweli au za uongo, sio vizuri kumharibia mtu CV yake bure. Hivyo hata hivyo jamaa hayupo .... si ndio inavyotakiwa na ndio ILIVYO.

Kwahiyo sikuona kama ni issue.

FD, Ahsante kwa kunijibu.

Ila nina nyongeza; yaani kwa vile ni tuhuma tu na nituhuma zilizo trigger hata uchunguzi, nchini mwetu hatuwezi kutamka hadharani kuwa tumemsimamisha mtu fulani?! Uwazi tunaoupigia debe kila siku unaishia wapi....mbona kila kit kisiri siri tu jamani, si kama atakutwa hana hatia anaweza kusimikwa tena kwenye cheo chake au.., CV ya mtanzania mmoja na mambo ya transparance ya Taifa yanatupelekea huku... jamani nini tena..!!

SteveD.

Nami nachomekea...

Man U hureeeeee, niliweka 'bid' kule kwa michuziblogu..ushindi natumaini umewadia TENA!! Man U rules!!
 
Shukran,
Mimi nadhani JK apunguze hizi ahadi za kiini macho kwani huo ujenzi wa reli toka tabora kwenda Burundi hauwezi kuanza na tathmini ya injini wakati reli ni sehemu ya taifa na injini ni sehemu ya utafiti wa kampuni itakayo endesha huduma hii. Yaani nashindwa kabisa kuunganisha uwezekano wa reli hii kuwepo. Gharama za ujenzi wa reli mpya toka Dar hadi Burundi ni mtaji wa taifa kwa miaka 50 ijayo..kwa mtaji gani ikiwa madini yenyewe yanaporwa.
I mean FD tujiulize maswali yenye kuleta maana vichwani mwetu. Ukatabati wa reli ya Dar - Dodoma tu umechukua mwaka na nusu kipande kidogo sana kilichokarabatiwa bado kuna sehemu kibao ambazo zinahitaji marekebisho makubwa sana kwa gharama kubwa sana. Hizi pekee sidhani kama tunaweza kuzimudu kwa mtaji wetu (baring in mind Uhujumu Uchumi).
Kutokana na taarifa nilizozipata treni linakwenda kama kilema. Hakuna huduma yoyote inayoweza kusifiwa ama tofauti kabla ya ajali ile ya Dodoma.. bado kabisa tunatumia ule msemo 'Msafiri kafir maadam Imefika... hii karne ya 21.
JK ametazamwa vibaya sana na watu wote sio nje ya chama wala ndani ya chama anahitaji kujirekebisha sana.
Mkapa on the other hand ktk miaka miwili ya mwanzo alijichotea sifa nyingi sana kwani kila kitu kiliwekwa kwa muda wake. Binafsi nilisema Tanzania imepata rais kwa mara ya kwanza hadi pale alipoingiza sheria za kulipisha wanafunzi wa shulke za msingi nikaanza kumshuku. Alipobinafsisha benki zetu kwa matapeli nikajua tumekwisha -Mtoto wa nyoka ni nyoka.
Kwa hiyo sote tuna matumaini na viongozi wetu na mara nyingi hatutazami chama chake ila kiongozi mwenyewe. Na kusema kweli nyota njema huonekana alfajir.. hivi sasa ni saa nne asubuhi na watoto hawajapata kifungua kinywa.. sijui mzee wangu kama kuna lunch ikiwa maandazi tu na chai ya rangi imekuwa hatuna uwezo.
 
Steve,

Gavana anaheshimika sana, hicho walichofanya ya kumpeleka USA ni stragtegy nzuri, bado haathiri uchunguzi, si ndio wote tunataka Au sio MKUU.

Nimeboreka, maswali yamekwisha, Man 2 Arsenal 2 Mpira umisha

Narudi Kizota, kuna unfinished business, nitakuwa ninawasoma kwenye simu ila sitojibu, bia za baadaye na kampeni za hapa na pale.

Kesho kazi ipo nzito zaidi. nitakua very busy.

Jumatatu wakuu, nimejitahidi sana, ila makombora yakija makubwa nitajimuvujisha na kujibu.

Asanteni

Nawasoma
 
Jamani tunaomba aliyekuwa kwenye huu mkutano bila unazi wa u-chama atupe yaliyojiri, akizingatia U-Tanzania. Mood ya walioshiriki n.k.
 
Mkandara,
Kutoka huko inakotoka (manyoni au isenya sijui) inayokuja Dar ni cheap kwasababu wanatumia infrastructure iliyopo. Yaani Reli ina two legs, wao wanaongeza third leg. So naona ni cheap, hiyo ya Rwanda na Burundi ndio tungoje, hii hata mimi inanipa wasiwassi.

Nishaaga nimekujibu kwa heshima yako tu BOB

Basi Jumatatu
 
Jamani tunaomba aliyekuwa kwenye huu mkutano bila unazi wa u-chama atupe yaliyojiri, akizingatia U-Tanzania. Mood ya walioshiriki n.k.


Duuh wakuu, DUA, nimeelezea Mood kama alivyouliza Mkandara na nimetoa sababu 2. Na nimekubali kuna matatizo. Sasa kipi tena cha kusema bila upendeleo au ..Utanzania?

Mtapata taarifa kutoka kwa wengine. Lunyungu sijamuona hapa Kizota, maana namjua.

Soma posts moja Mkandara kaniuliza na nimemjibu.

Jamani ninakimbia, jamaa wananingoja!
 
FD,

Asante sana na pumzika salama weekend. Umetufaa sana leo.
 
Mkuu FD,

Heshima mbele kwa kukata ishus na kutuhabarisha yanayojiri huko,
short, straight, strong, and very clear,

Mikutano ya vyama vya siasa sistusumbue wakuu, tujali taifa, amesema nini kuhusus taifa that is all, mengine tunashuka na kuwa level ya hao makada waliovaa manguo ya kijani wengi wao wakiwa wanauchapa usingizi tu!

At JF, We are better than them!
 
Back
Top Bottom