Rita Mlaki, millioni 300 nje?
Good news kutoka huko ni uamuzi wa rais kuteua kamati maalum itakayo jumuisha mawakili, wabunge wa upinzani, wakuu wa dini zote mbili, na wabunge wa CCM, kulifuatilia suala zima la madini,
Magazeti yote leo yamekubali kuwa kwenye hili Muungwana, makes a sense, the bad news ni mkuu Luwassa, kutoka huko akiwa mnyonge sana!
Yaani Sumaye anapitwa na Makongoro Mahanga? ama kweli ukifia mwituni vidudu vyote vitakutambaa....
Miongoni mwa hotuba ambazo ziliwakuna wengi, ni ile iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John Malecela, ambapo wakati akimshukuru Marais Wastaafu, Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi ukumbi mzima ulitulia.
Wakati Malecela akihutubia, Mkapa alionekana mwenye huzuni na kuna wakati alikuwa anatafuta kimbaa kwa ajili ya kufuta machozi.
Kwa upande wa Makamba tokea kuanza kwa mkutano hakuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake na hata juzi usiku aliomba CCM isimuacha kwa kuwa wapinzani watamcheka.
?Naomba CCM isinigaragaze ndugu Mwenyekiti, kwani wapinzani watanicheka,? alisema kwa utani
Kiongozi mmoja ambaye anafanya kazi kwa karibu na Makamba, aliiambia Mwananchi kwamba wana wasiwasi kwamba bosi wao ataondolewa katika kiti hicho.
?Mpaka sasa tunahisi katibu anaondolewa katika nafasi, hivyo hata sisi hatujui hatma yetu,? alisema kada huyo.
Wachambuzi wa masuala ya siasa walioko hapa Dodoma, wanasema kuna uwezekano mkubwa wa Makamba kuondolewa katika wadhifa huo hasa ikizingatiwa Makamu Mwenyekiti Mpya, Pius Msekwa ni mtu anayefanya kazi kwa taratibu, kanuni na sheria, wakati Makamba staili yake ya kufanya kazi ni tofauti naye.
Mkuu Bubu na Mwafrika wa Kike,
Kamati itakuwa na wajumbe toka upinzani na wakuu wa dini na mawakili, sasa hviv unaamini hawa watakubali kuvutwa kama wajinga? Watakapoona tu kuna unazi watachomoa na kusema wazi WHy?
I mean mnyonge mnyongeni, lakini na haki kidogo tumpe!
Mkuu Bubu na Mwafrika wa Kike,
Kamati itakuwa na wajumbe toka upinzani na wakuu wa dini na mawakili, sasa hviv unaamini hawa watakubali kuvutwa kama wajinga? Watakapoona tu kuna unazi watachomoa na kusema wazi WHy?
I mean mnyonge mnyongeni, lakini na haki kidogo tumpe!
waziri mkuu wake awe Matayo David wote hawa licha ya kuwa wanamtandao maslahi ni close allies wa JK wa JK..what a crap....nafikiri wana CCM wamefanya nilokuwa nalitamani.......(majina kwenye mabano) washindwe pia U- NEC
kazi kweli kweli
Mkuu Dua,
Heshima mbele,
Uchaguzi bado, kesho mwenyekiti atawasilisha majina ya wajumbe anowataka wa skretariati, jina la katibu mkuu, na wajumbe wa kamati kuu pia watapigiwa kura kesho, kwa hiyo bado mkuu mchezo haujaisha!
Mzee ES, Karamagi alitamka Bungeni kuwa madai ya Zitto kuwa mikataba bado inaendelea kudusuriliwa hayakuwa ya kweli na kuwa mazungumzo yamekamilika. Sasa huku kwingine kwa nini? Tayari kuna Kamati ya Mabadiliko ya Sheria ambayo imekuwa ikifanya kazi zake je ni kamati hiyo hiyo inaongezwa wajumbe tu, au ni kamati mpya specifically kwa ajili ya madini?
Kama kweli kuna tatizo kubwa katika sekta ya madini na sheria iliyopo haimnufaishi Mtanzania kama inavyostahili, kwanini asisitishe utoaji wa leseni za uchunguzi na uchimbaji hadi sheria mpya itakapopatikana kama walivyofanya Uganda?
Napenda nimpatie haki yake lakini siyo kwa mazingaombwe namna hii? kwanini asiache Bunge ndiyo liunde kamati hiyo?
Did you have a good weekend?
siyo kukiri kuwa anasumbuliwa na "kelele" za wapinzani?