Kigwangala,
Kama wewe kweli ni Mbunge wa Nzega, basi ningeliomba sanasana muanzishe tena ile mikutano ya watu wa Tabora ili kujadili nini kifanyike kusaidia mkoa wetu wa Tabora.
Wanyamwezi tunasema "Mmulika nyoka usiku, huanzia miguuni.........." Sisi Wanyamwezi tumegeuzwa kuwa Chambio la mafisadi kwa kuwapa kura na wanaondoka na pia CCM huwapa viongzi wanaotoka Tabora VISENTI kama mababu zetu walivyopewa Heleni, Bangili, shanga (wambo), Vioo, na vitakataka vingine.
Ulipotaka kuwasha moto wa Mgodi, wengi wetu tulikusifu ila kumbe sijui ilikuwa nguvu ya soda?
Mwenyewe unajua kuwa Watu wa Tabora walikandamizwa sana wakati wa Nyerere kwa kuwashughulikia vijana machachari enzi hizo ambao walikuwa wakimpinga sana Nyerere. Kutokana na kushughulikiwa kwa watu hao, Wanyamwezi wamekuwa waoga hata kumuogopa kunguru.
Hapa Sikonge, mtemi Lugusha alikuja kupewa kifungo cha nyumbani. Alipokuja kuruhusiwa, hata akili zake zikawa zimepitwa kwa mambo mengi na akaishia kuwa kituko tu bungeni. Kasanga Tumbo na yeye alikuwa kifungoni kwao Ipole. Chief Fundikira alikimbilia Kenya na aliporudi hakufahamu hata kinachoendelea Tanzania.
Kusoteshwa kwa hawa watu kuliwafanya Wanyamwezi wanywee na tangu hapo tumekosa kabisa sifa za WAJUKUU WA MIRAMBO.
Baadaye wamekuja kupandikizwa watu kadhaa ambao sijui hata wamekuwa wakifanya vitu kwa kuwasaidia Wanyamwezi au kama Usalama wa taifa ili kuonyesha jinsi Wanyamwezi tusivyo na akili.
1. Huwezi kusifia alichofanya Sitta kwa kujenga ofisi ya Spika Urambo kwa mahela mengi. Alikosa kitu cha maana cha kufanya na hizo hela ili kusaidia watu wa Urambo/Tabora?
2. Juma Kapuya na mtoto wake. Wewe Prof. mzima unakesha kwenye pekechapekecha na vijukuu vyako unakata viuno(mkimbili)? Mtoto wake Baraka ananyanyasa watu wa Kaliua utafikiri wamekuwa mali yake? Ila mtu kama huyu ndiyo anapewa kuwa Waziri ili kuwaziba wanyamwezi mdomo kuwa mbona tumewapa waziri.
3. Wewe mwenyewe huna meno ya kuuma kwa sababu inajulikana kabisa umesoma kwa kutumia jina la mtu mwingine. Ukiwaletea maneno mengi CCM, watakubeba na maji. Ila wewe ndiyo umeonekana unafaa zaidi kuwa mbunge maana WAMEKUSHIKA HATAMU.
4. Mbunge wa SIKONGE mwalimu wa darasa la pili, ovyo kabisa..............
5. Tatu Ntimizi miaka kibao alikuwa akibebwa, kisa tu awe karibu na Mzee wa Kigogo........... etc etc etc.....
-Hii ndiyo TABORA yetu Mami Kingwangalla. Tunawasindikiza wenzetu wanaopeleka kwao kila kitu na sisi kubaki na makombo. Mapipa ya Lami pale Tabora Airport, alikuja Prof. Mwandosya na kuyabeba kuyapeleka Mbeya na huko liuwanja la ndege limemshinda hata kumaliza. Sasa tumekosa wote na huyu Mwandosya bado ni Waziri.
-Kiwanda cha kuchambulia tumbaku, jinga moja lilipewa pesa na likaruhusu kijengwe Morogoro, sijui taahira gani hili.
-Kiwanda cha nyuzi, hoi. Kiwanda cha asali marehemu. Kiwanda cha ..................................
Hii ndiyo NTOVOLA yetu Mami, na sisi tupo hapa kushindania CCM VS CHADEMA.
Inabidi tupige hatua kadhaa mbele na kuacha kuangalia hadi mwisho wa PUA zetu. Wakiwa mikoa mingine, acha watukanane ila wakija TABORA, lazima tupime mabaya na mazuri na kuanza kuangalia je sisi Wanyamwezi tunafaidika vipi na CCM au chadema au CUF au .....
Kama hatufaidiki, basi sina hamu na chama chochote. Kama kuna chama kinanipigania, hata kama ni cha Mrema, basi ntakichagua. Wenzetu Wasukuma, Wachaga na Wanyakyusa kidogo wako mbali sana na hao ndiyo wapinzani wakubwa wa CCM. Kwao kuna lami hadi vijijini. Kama huamini basi angalia miji kama Kyela, kuna lami hadi Ziwani na huku barabara nyingine ikienda hadi mpakani ya LAMI. Damn, lami hadi Wilayani na Tabora, hata barabara ya kutoka Dar kupitia hapo kwako NZEGA, ije iingine Tabora, hakuna LAMI. Umeme wa kuokoteza na leo tunakaa na kuangalia Chadema ina sura gani au Ufisadi wa CCM................
Narudia tena, sisi Wanyamwezi tuamke na tuanze KUMULIKA NYOKA MIGUUNI KWETU KWANZA.