KWIYEYA: Ni kweli Bashe na Nape hawakupikwa vizuri

Shigganza

Senior Member
May 24, 2018
160
412
Kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM ndg. Dk. Bashiru Ally ktk kipindi cha mahojiano na Azam tv wakiwa na Mwandishi Tido Mhando Katibu wa CCM alieleza bayana kuhusu Hussein Bashe na Nape Mnauye juu ya Siasa wanazoendesha kwamba:-
"Nape Mnauye na Hussein Bashe ni miongoni mwa vijana waliopitia ktk Umoja wa Vijana wa CCM wakati mfumo wa kuwaandaa Viongozi ukiwa umekufa."

Kauli hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM sio ya kwanza, ni kauli iliyozungumzwa mara kwa mara na viongozi wastaafu, na wachambuzi mbalimbali mashuhuri ktk masuala ya uongozi, siasa na mengine mengi ya kijamii.
Mwaka jana nilieleza kuhusu suala la wanasiasa kuhama hama kutoka CCM wakienda Chadema, ACT na kurudi tena CCM, nilisema hiyo sio siasa wala si demokrasia bali demokrasia na siasa vinatumika kama njia ya watu hao kutimiza matakwa yao binafsi.
Ikiwa kijana mfano kijana wa CCM amepikwa sawa sawa, lazima awe na sifa walau zifuatazo:-
1. Kutunza siri kwa kina,
2. Awe na msimamo,
3. Awe mtii-fu, na mwadilifu,
4. Awe mvumilivu,
5. Awe mwenye itikadi kali, nk
Kijana wa CCM ni kijana aliyeandaliwa na kuwa tayali kujitoa, na aliye tayali kulinda na kutetea chama na viongozi wote.
Lakini pia aliye tayali kukipigania chama chake popote hata kama amebaki peke yake ktk vita wengine wote wakauawa, atakwenda popote na kukifufua chama chake.
Kuwa mpokeaji mzuri wa hoja ili kuzifanyia upembuzi na utafiti.
Hayo pamoja na mengine ndio hukamilisha ukada wa kuitwa kweli wewe ni Kada wa CCM.

Kinachowasumbua wanasiasa vijana aina ya Bashe ni upungufu aliouelezea Dk. Bashiru, hawakuandaliwa kuwa viongozi bora.
Kwenye chama chochote huwa kuna vitengo na mojawapo kitengo cha propaganda, kitengo hichi hupendwa sana na vijana kwa sababu wsnakiona kama sehemu ya ujira wakati wa kampeni.
Ni kitengo cha uzushi, kuchanganya uongo na ukweli kwa kutumia matukio, historia ya mtu fulani mfano mkombea wa upande meingine.
Na wakati mwingine kuunda matukio ya uongo ilimradi mdanganyi awe na cha kupeleka kwa wahusika kama viongozi, wanasiasa au kupeleka kwa wananchi ili wamwamini.
Kwa hiyo Umoja wa Vijana wa kizazi cha wakati huo cha akina Bashe uliliacha jukumu lake na kujiingiza ktk kitengo hichi, kikawa kinaandaa wagombea, vijana waligawika na kuwa wafugwaji wa wanasiasa, kundi kubwa la UVCCM lilitekwa na Lowassa, wachache waliobaki wakawa kwa wanasiasa wengine kama Steven Wasira, Samwel Sitta, akina Pinda na Membe.


Bashe na akina Nchimbi walikuwa mawakala na wapambe wa kundi la Lowassa, wakati Nape na Makonda wakiwa chini ya akina Samwel Sitta na Kikwete, vijana wengine wakachukuliwa na wanasiasa vijana wenzao kama akina January Makamba nk.
Matokeo ya kuwa ktk makundi ya wanasiasa vijana walikosa kujifunza na kuiishi misingi, maadili ya CCM bali wakawa na maadili ya viongozi na kujikuta wakiambulia misimamo.
Ukimwangalia Nape, Makonda na Bashe utaona jinsi walivyo na misimamo mikali, na msimamo ni msimamo tu, unaweza kuwa ni msimamo ya kusimamia mambo ya kijinga au msimamo wa kusimamia mambo ya maana.
Awali Nape na Makonda wote hao walikuwa na msimamo wa kusimamia mambo ya maana, kinyume na wenzao akina Bashe na Nchimbi, wao walikubali kubeba aibu, kashfa na kushiriki ufisadi wa Lowassa, maana yake walijiingiza ktk ufisadi kwa ssbabu ya maslahi binafsi.

Vijana hawa Nchimbi na Bashe waliungwa mkono na vijana wengi wa CCM, kwa sababu ya fedha na vyeo ndani ya chama na serikalini, upambe ukashika kasi zaidi, vijana wakawa wanasmini ktk watu/wanasiasa kuliko chama, wakawa wabeba mabegi ya wanasiasa ili wapewe pesa au vyeo.
Kauli ya Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru vijana wengi wameichukulia kama imemaanisha kuwasifu akina Nape na Bashe, inawezekana kuwa amewapa sifa, lakini ni sifa nzuri au mbaya?, "Utukutu", "Hawajapitia ktk mfumo wa kuwaandaa viongozi"
Lakini bado vijana wanasifia, hayo ndio matokeo ya elimu nchini.Wanasiasa vijana wanatakiwa wajifunze kwa viongozi bora, na si kwa wanasiasa maarufu wakati hawajui umaaarufu huo waliupataje, je, kwa kuumiza wengine au kihalali.
Kuna wanasiasa ktk dunia hii wameua watu kwa sababu ya kuusaka umaarufu na ufisadi, cha ajabu hupachikwa majina ya utukufu kama ya ukombozi na ushujaa.
Katika mazingira hayo huwezi kutarajia siasa safi, haki, usawa na utu wa binadamu, ni lazima jamii itakumbwa na siasa za maji taka.
Hata hii hama hama tunayofikiri ndio demokrasia ni ujinga tu, ni ulaghaai, ni uongo na ni ufisadi zaidi.


Lawrence Kego Masha alikihama chama chetu CCM na kuhamia CHADEMA tukamponda, lakini baadae akakihama chama hicho cha Chadema baadhi yetu walimsifu Masha.Hawa kwangu mimi nawaita ni wanafiki na hawapaswi kuaminiwa hata kidogo.
Chama chetu kinapowaamini vijana kama hawa kinajifunga mdomo chenyewe mbele ya umma na kuwapa sintofahamu ya wananchi juu ya maadili ya CCM.
Fuatilia kambukumbu hii kwa ufupi kuhusu wanasiasa vijana waliopata kuaminiwa ndani ya CCM ambao wamewahi kupata wadhifa na wakatuangusha.


Hatua ya Rais John Magufuli kumvua uwaziri Nape Mnauye ilihitimisha miaka kumi michungu kwa wanasiasa vijana waliopewa wadhifa mzito wa uwaziri na Marais wetu.
Kuanzia utawala wa Rais Jakaya Kikwete na huu wa Rais Dk John Magufuli vijana wamekuwa wakipewa uwaziri lakini wengi wameondolewa kwa makosa yao ya kiutendaji.Wakati wa utawala wa Mwalimu Julius Nyerere wengi wa wanasiasa vijana walipewa kwanza nyadhifa za unaibu uwaziri kwa kipindi kirefu kabla hawajapewa uwaziri kamili.Nape na Masha ni kati ya hao vijana niliowataja uwaziri wao kuwalipua, William Ngeleja, Lazaro Nyarandu, Adam Malima, Ezekiel Maige, Stephen Masele, Emmanuel Nchimbi.Lawrence Kego Masha baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 alikuwa akitajwa kama mmoja wa wanasiasa vijana wa CCM ambao wangekuja kuwa viongozi wakubwa ndani ya chama chetu.


Kitaaluma Masha ni wakili aliyesomea Marekani aliyeonekana mwenye akili, mwonekano mzuri na mzungumzaji mzuri;
Lakini nilieleze suala la mfumo huu wa hovyo kabisa kuwa wanasiasa kama Lowassa huathiliwa na mifumo ya umagharibi, weka akilini nia ya wamarekani kupitia IMF na Bank Kuu ya Dunia kupitia masharti yao na mlengo wao wa elimu juu ya kulihujumu bara letu la Afrika - Masha kasomea Marekani!.
Masha aliteuliwa kuwa naibu waziri wa Nishati na Madini mwaka 2006 baadaye akahamishiwa ktk wizara ya Mambo ya Ndani na hatimaye akateuliwa kuwa Waziri kamili ktk wizara hiyohiyo ya Mambo ya Ndani.


Kwa hiyo, tunapozungumzia suala la akina Bashe tunazungumzia mifumo ya kimagharibi, maana UVCCM misingi yake ni ya Kijamaa, ukomunist, kijana yeyote ambaye hajaipitia msingi ya Ujamaa hawezi kuwa mwaadilifu, hawezi kuwa viongozi bora na ni lazima atende ufisadi tu.Ndiyomaana huwa nasema nafasi ya uongozi haimfanyi mtu kuwa kiongozi, ni hapo ndipo ilidhihilika wazi kiwango cha upeo wa Masha, na ndivyo ilivyojidhihilisha kiwango cha upeo wa akina Nape na Bashe kutokana na walivyotengenezwa na maadili ya viongozi badala ya maadili ya uongozi ya CCM, maadili yasiyo ya CCM ni maadili ya kimagharibi, Marekani wasiokuwa na adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu bali maslahi ya kudumu.
Masha tangu hapo ateuliwe uwaziri hakuwa tena mtu wa watu, akawa mtu wa kujigamba na kujitapa na kuropoka ropoka hovyo, wenye idara walipogundua wakamtosa.


Masuala ya usalama wa taifa si yakuwapa watu waliotengenezwa na wamarekani, hao walishatengenezwa kuwa vibaraka wao kupitia hizi shule zao, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi, ni afadhali ya mtu aliyesomea Mashariki ya mbali ukomunist-ni.
Mambo ya Usalama yanawahusu wazalendo na wenye itikadi ya nchi yao na si vinginevyo, limekuwa jambo la kawaida leo hii unaonyeshwa na watu kwamba "yule ni usalama wa taifa, au mtu anakwambia "Mimi ni usalama wa taifa", Hii nini sasa?.
Ni jambo la aibu kumtambua afisa wa usalama ktk taifa lako nje na anayetakiwa kufahamika kwa kuwa tu u ofisini umemkuta.

Hichi ndicho kilimfanya Masha adumu kwenye nafasi hiyo kwa mhula mmoja tu na kutoswa kwenye Baraza na Mawaziri na baadaye akashindwa kwenye ubunge mwaka 2010.Mwaka 2015 Masha akahamia upinzani kupitia Chama cha CHADEMA, ni kwa sababu ya tamaa ya madaraka na vitu, huyo si muumini wa CCM.
Mwaka wa 2017 aligombea ubunge wa Afrika Mashariki, nimeyachambua haya ili vijana wenzangu wa Chama Cha Mapinduzi ambao mnashabikia kila kitu bila tafukuri mjitathimini na muone ni jinsi gani mnavyokiaibisha Chama chetu Cha Mapinduzi, na mtafakari kama mnao uhalali wa kuendeleza ushabiki huo.
Nataka tu kusema kwamba hatuko tayari kuiona CCM MPYA ikiwa na vijana wa namna hiyo na tukawavumilia.

Hivi karibu Bashe amesikika ktk vyombo vya habari akidai amefanya utafiti kuhusu mauaji na ukosekanaji wa haki za kiraia na kwamba anatarajia kupeleka hoja hiyo Bungeni.
Kitendo cha Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe kusema anaandaa hoja aipeleke bungeni, hoja ambayo ni ya kitaaluma na kitaasisi ni kituko kingine kinachodhilisha aliyoyasema Katibu wa CCM Dk. Bashiru cha wanasiasa hawa kutopikwa na CCM, ni matokeo ya ubebaji mabegi ya wanasiasa akina Edward Lowassa.


Ukiondoa mabo ya kitaaluma, hebu fikiria Mbunge wa Nzega Mjini anapeleka hoja Bungeni inayohusu Mauaji, ukosekanaji wa haki za wananchi, kukosa kwake ubunge au kupoteza maisha.Kazi za Mbunge ni kuwawakilisha wananchi waliomchagua na kuwakilisha mawazo yao Bungeni ili yapatiwe ufumbuzi.
Kutunga sheria na kuisimamia serikali nk, inashangaza Mbunge wa Nzega Mjini akawasemee wananchi wa Geita kuhusu kifo cha Mawazo ilihali kule Geita wapo wabunge walioaminiwa na wananchi wa majimbo hayo kama akina King Msukuma na Benard.


Hali kadhalika wananchi wa Igunga wanao wabunge wao, yupo Seif Gulamali na Dk. Dalali Kafumu, Arusha wapo kina Lema, Kibiti wapo kina Jafo nk.
Lakini wakati huo anafanya utafiti wa mauaji au ukosekanaji wa haki za raia na wananchi wa Geita, Arusha, Igunga, na Kibiti, hapa hapa Nzega wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kuna vijana wa CCM walipigwa na kuvunjwa miguu na watu waliosemekana ni vijana wa Chadema, na kuna kijana aliuawa hapa Mjini wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2014 aliyeonekana ni kada wa Chadema.
Kwenye mazungumzo na waandishi wa habari alitoyafanya Bashe kuhusu hoja hiyo sijasikia akitaja yaliyotokea ktk chaguzi hizo hapa Nzega, najiuliza ni Mbunge wa aina gani anaweza kuacha kuwasemea wananchi wa jimbo lake na kudania wajibu wa wabunge wenzake kama akina Msukuma na Kafumu!?
Na je, hayo ndiyo wanayostahili kusifiwa wabunge aina hii wanaorukia wajibu wa wengine na kuacha wajibu wao?


Wananchi mmeyaona matokeo ya ufuasi wa vijana wa CCM kwa wanasiasa?, ubebaji mabegi ya wanasiasa na matokeo ya ile kamati ya propaganda?
Hiyo ndiyo siasa tunayoipenda iendelee ktk jamii, siasa ya maneno kuliko vitendo?
Je, hatujui kuwa uongo ni sumu ya jamii unaoathili jamii nzima?
Nape sijamchambua ilivyo kwa sababu yeye anasumbuliwa na athari za kutenguliwa ktk nafasi ya uwaziri, ameathirika kisaikolojia pengine hakutegemea kabisa kuondoshwa kirahisi kiasi hicho.


Ni kwa sababu hiyo hiyo ya kutokupitia mafunzo ya UVCCM ya kuwaandaa viongozi na ndiyomaana alikalia kushindana na Makonda bila kujua amepotoshwa na mafisadi mauza unga na wapinzani aliokuwa akirushiana maneno mazito wakati akiwa Mwenezi.
Wakamsifu naye akalewa sifa na mwisho wa siku RC. Makonda akaonekana mshindi mbele ya Mkuu, akaonekana Jemedar mbele ya umma, sasa kiholo kinamsumbua Nape.
Mimi namweshimu sana Nape ktk misimamo yake wakati akiwa Mwenezi hasa ktk kushughulika na mafisadi, nilikuja kushangaa alipoungana nayo baada ya kuwa Waziri, kisa Makonda.


Kwa hiyo, kelele za akina Hussein Bashe ni za kifisadi, hazina maslahi yoyote ktk jamii bali wanazitumia changamoto hizo kama ngao ya kulinda maslahi yao binafsi; haitakaa itokee wakalinda maslahi ya wananchi.Ukitaka kujua hilo fuatilia historia yake uone kama kuna mahali aliweza kusimamia maslahi ya wananchi, migogoro mingi ya wananchi wa Nzega, changanya na migogoro ya ndani ya CCM ktk Wilaya ya Nzega chanzo kikubwa ni yeye, hapendi umoja, hapendi maslahi ya wengi wala haitakii mema Nzega yetu.
Sasa mtu wa namna hiyo, wewe na akili zako timamu unaanzia wapi kuuona uongozi bora, uanasiasa bora kutoka kwake?


Wahenga walisema Nyani hajui kilicho nyuma yake, wala fisi hajui harufu yake, kinyume chake, ni kwamba Mwenyekiti wa CCM Taifa ndg. Dk. John Pombe Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewafanya wanasiasa aina ya Hussein Bashe waujue ukweli wao kwamba Uchaguzi Mkuu ujao wa 2020 hawatatoboa, wanasiasa wa propaganda 2020 hawawezi kushinda uchaguzi.
Uchaguzi ujao unawahitaji watu wenye vision ya maendeleo ya kweli ktk jamii na sio maendeleo yakupikwa kwenye makaratasi, wasema kweli kwamba kama jambo fulani ni baya atasema ni baya na kama ni zuri atasema ni zuri, kama ni yeupe ayasema nyeupe, sio nyeusi, na wasio na kisilani, wasio wachochezi na kugawa watu kwa maslahi yao binafsi.
Watu hao tunao kwenye jamii zetu ila walifichwa na mafisadi kwa sababu ya fedha zao zisizo halali.
 
Katibu wa CCM ameongea ukweli mchungu hao vijana hawakupikwa na sio hao wako wengi kuanzia awamu ya nne mpaka hii ya tano wamebebwa tu kufikia hapo walipo sasa hivi wanaonekana mashujaa kwa sababu wanatoa kauli zinazokinzana na serikali lakini ukweli kauli zao zinatokana na kwamba hawana madaraka serikalini
 
Hata Padri Dr Kamongo nae hakupikwa vizuri kwenye siasa, bora hata ya Bahe na Nape wanajua siasa kidogo, japo siasa zao ni za majitaka
 
Hivi huko chadema hamna kuwajibishana kama mambo hayaendi sawa?

Haiwezekani tokea mwaka 2015 watu wanakimbia tu Chadema lakini viongozi wapo bila kuchukuliwa hatua yoyote.
 
Tatizo kubwa ktk siasa zetu ni kuwa na kile alichokiita Poff. Assad political entrepreneur kwa maana kwamba ukiona aliyoko nje anapiga kelele haina maana ni msafi ila ana njaa na akiingia ndio utajua kuwa hakua yeye kwenye kelele, hawa wanaoonekana mashujaa leo ni majuzi tu walikua wa hovyo na kila mmoja aliwazomea kwa kauli zao
 
Hivi huko chadema hamna kuwajibishana kama mambo hayaendi sawa?

Haiwezekani tokea mwaka 2015 watu wanakimbia tu Chadema lakini viongozi wapo bila kuchukuliwa hatua yoyote.
Kawajibike wewe
 
Hahaha ccm aliyepikwa vizuri ni msukuma na mlinga au kibajaji, think tank wa chama.
 
Ili Nape na Bashe "waive kisiasa", basi wahudhurie chuo cha mafunzo alikoivishwa huyo Katibu Mkuu wao!
 
Kupikwa na kutokupikwa kwa hawa wabunge ni hoja muhimu sana? Inamaana kesho tena atakuja mwingine kusema wamepikwa na kutoa sababu?
 
Back
Top Bottom