Hekaheka Uzeeni

JBourne59

JF-Expert Member
Jan 17, 2020
941
8,547
UPDATE

Simulizi hii ina misimu mitatu (three seasons) na zote zitakuwepo kwenye uzi huu huu.

1st season ina episodes 4 tu japo ndefu ndefu kiasi.

2nd season ipo post #90 na episodes zake ni fupi fupi...

3rd season #237

UTANGULIZI

Maisha baada ya kustaafu huwa yana ‘stress’ nyingi. Kujaribu kupunguza stress hizo nilifungua ‘account’ hii JF ili kujiburudisha na kuburudishwa. Account zangu nyingine JF zina ‘personality’ tofauti kabisa.

Michengesho (decoys) zipo kama kawaida ili kulinda nukta kuunganishwa.

HEKAHEKA UZEENI

Sehemu ya kwanza – KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA SI JAMBO LA GHAFLA.

Katika kazi za utumishi wa umma, wapo wanao staafu wakiwa na miaka arobaini na mitano na kuendelea, mimi nilibahatika kufanya kazi hadi miaka sitini na kustaafu kwa mujibu wa sheria. Kujifunza ‘hakwishi’, kuna karaha zake baada ya kustaafu hususani wakati wa kufuatilia stahiki zako. Angalau siku hizi utaratibu ni mzuri sana usumbufu umepunguwa kwa kiasi kikubwa.

Kwakuwa kustaafu ‘hakukuji’ ghafla, yampasa mtumishi yeyote aliyeajiriwa kuajiandaa na maisha baada ya kustaafu. Tumeshuhudia wengi baada ya kustaafu kuendelea Kwenda eneo la kazi na kukaa kupiga soga nk, hii hutokana na ama kufuatilia mambo yake ama kukosa sehemu muafaka ya Kwenda kwakuwa labda hakujiandaa na mahali ya Kwenda baada ya kustaafu.

Miaka 45 ni mtu mwenye nguvu bado, hivyo anaweza kufanya Maisha yaendelee kwa mtindo mwingine bila kuathirika na kazi alizozioea kazini, vivyo hivyo kwa miaka 50 ama 55 ama 60 na hata 65 bado mtu anaweza kujishughulisha na mambo ambayo yatamfanya asiwe ‘bored’

Mara nyingi kwa watumishi wengi maisha yao baada ya kustaafu huwa ni ya upweke, ‘kupigwa mizinga’ kutoka kwa ndugu na jamaa na usipokuwa makini utajikuta unapata magonjwa ya kisukari na moyo pasipo kutarajia kutokana na mtindo wa maisha utakao kuwa nao.

“…hela ya mafao ya kustaau siyo ya kujengea kaka…!” aliwahi kuniambia mzee mwenzangu mmoja aliyetangulia kustaafu.

“…hiyo hela ni ya kukutunza wewe, ni ya kufurahia maisha yako ya uzeeni hadi siku Mwenyezi Mungu atakapo kuchukuwa…”

“…ndugu na jamaa wengi watakuletea shida zao, sisemi usiwasaidie, lakini saidia kwa kiasi tu ili usiharibu fungu lako wala uhusiano wako na ndugu na jamaa, ikiwezekana tangaza hali mbaya ya uchumi kabisa ili wasiweke dhana kwamba una hela, singizia chochote kuepusha usumbufu, mwenzako yamenikuta sana…” Ni maneno yamzee mwenzangu mwingine ambaye yeye alitangulia kustaafu pia.

Sentesi ya ‘hela ya kustaafu ni ya kufurahia maisha..’ ndiyo iliyonifanya nianze kuandika simulizi hii.

Kama nilivyoserma awali, kwakuwa kustaafu ‘hakukuji’ ghafla yapaswa kujiandaa kwa kuwa na miradi midogo midogo wakati ukiwa bado katika utumishi. Hii ni kwa wote, watumishi wa umma na wa sekta binafsi. Anzisha mradi wowote wenye kukuingizia kipato hata kama ni kidogo ili mradi kiweze kukidhi mshahara wa anayesimamia, kutunza mtaji, kukuza mtaji na kujipatia faida kidogo. Hapa nazungumzia wale ambao kima chao cha mshahara ni cha chini. Kwa wale wenye vima vya juu nawashauri wafikirie kufanya miradi mikubwa yenye kuleta ajira kwa vijana na kutopeleka hela nje ya nchi, wekezeni humu humu nchini hiyo miradi yenu mikubwa kwa maana mzunguko wa fedha hizo zitabaki ndani. Sisemi msiwekeze nje ya nchi lakini nasema msisahau kuwekeza ndani kuwasaidia hawa vijana wetu wanaomaliza masomo yao kila mwaka.

Hebu niache haya mambo ya ushauri-nasihi usio rasmi maana kila mtu anajipangia mambo yake mwenyewe, lakini usisahau pia kuishi na mkeo / mmeo vizuri maana ukitangulia kustaafu kabla ya mwenza wako na haukuwa unaishi naye katika mahaba tarajia ‘stress’ za vijimambo vidogovidogo tu ambapo sasa vitakusanyika na kuwa kero.

nijikite sasa kwenye hii sentesi …”..hela baada ya kustaafu ni za kufurahia Maisha…”

Wakati na mbwela-mbwela kusubiria ‘fuba’ la mkupuo si nikapata mkataba fulani hivi kusaidia mambo fulani nchini DRC!. Ulikuwa ni mchongo wa miezi mitatu. Namshukuru sana yule jamaa aliyeniunganisha maana alikuwa anajuwa uwezo wangu katika fani ile kuhusiana na mchongo huo.

‘Paapu’, nikaambiwa niripoti Goma – Kivu ya kaskazini DRC tarehe fulani. Nikajiangalia mfukoni nikaona kuchukuwa flight hakunifai.

“…bora nipande basi kwa kuwahi wiki moja kabla ya tarehe husika…” nilijisemea moyoni.

Wakati huo Stendi ya Mbezi, “Magufuli Bus Terminal” ilikuwa bado haijaanza kutumika, hivyo nikatinga Ubungo bus terminal kuangalia usafiri maridhawa. Nilikuta kuna basi mbili za kampuni moja ambayo niliambiwa ni wazuri kwenye huduma ambazo zote zilikuwa zinaenda Kigali. Nikakata tiketi ya basi kubwa kama walivyokuwa wakiita wenyewe.

Kwakuwa huwa napenda kuona mbele ya basi kwenye lami, nilichaguwa siti ya nyuma ya dereva siyo upande wa dirishani lakini ingawaje palikuwa bado hapajachukuliwa. Sababu nyingine iliyonifanya kuchukuwa nafasi hiyo nili ile nafasi kati ya dereva na siti nyuma yake ni kubwa pa kuweza kunyoosha miguu na pia kuna kama meza fulani hivi mbele (fridge) hivyo kufanya paonekane ni sehemu muafaka kwangu kwa safari ndefu kama ile.

Siku ya safari nikafika mapema sana Ubungo bus terminal, moja kwa moja kwenye eneo ambalo basi husika lilikuwa linapakilia abiria, nilikuta baadhi ya abiria wakiwa tayari ndani ya basi ingawaje nilifika takribani nusu saa hivi kabla ya safari. Sikuwa na mizigo bali backpack Fulani hivi kubwa kiasi ambayo iliweza kubeba laptop yangu pamoja na nguo zangu chache ambazo nilidhani kwa kazi ya siku 90 ningeweza ‘kupiganisha’ bila kuhisi sina nguo za kubadilisha.

Kampuni ya basi ilikuwa inaitwa ‘utatu mtakatifu’, kwa kweli basi nililopanda walijitahidi sana kufanya liwe na hadhi yake mle ndani, viti vyenye vitambaa vya ngozi (synthentic leather), nafasi kubwa kati ya siti na siti, ila kwenye lugha za kuhudumia wateja walikuwa wanafeli sana, sijui ni kwa sababu ya kutojuwa Kiswahili vizuri ama nini. Hakika kwenye hili walikuwa wanafeli, siku hiyo kulikuwa na madereva wawili, mmoja Mtanzania na wa pili ni Mnyarwanda, na mhudumu tuliye safiri naye mmoja mwanume na mwingine ambaye alishukia njiani alikuwa ni wakala wao, akisindikiza gari.

Nilitulia kwenye kiti vizuri huku basi likiwa limekaribia kujaa kabisa abiria lakini kwenye kiti changu bado hapakuwa na abiria aliyekuja. Shingo nikiwa nimeinua juu kidogo kuangalia kwaya walizoweka kwenye runinga ya basi pale mbele mara nikasikia sauti ikiniambia…

“Excuse me, let me pass that is my seat..” alikuwa ni binti mrembo na kwa sura ile moja kwa moja nikajuwa huyu ni Mnyarwanda.

Nikampisha bila kusema neno, na alipokuwa ameketi sasa ikanibidi siti nibonyeze sehemu ili kuongeza nafasi ili tuenee vizuri maana si kwa ma ‘hips’ yale.

“Hujambo?” nilimsalimia na akaitikia kwa kichwa huku akiendelea na mambo yake mara kashika hiki mara kashika kile ili mradi alikuwa hatulii kama ana wasiwasi fulani hivi kama vile kuna jambo halijakamilika.

Macho nikarudisha kwenye runinga kuendelea kuburudika na kwaya za kisabato, ‘what a beautiful melody!’

Punde si punde mlango wa basi ukafungwa na tukawa kwenye foleni ya kutoka nje ya bus terminal. Ajabu ni kwamba vurugu za mabasi kugombania kutoka nje ya geti zilikuwepo licha ya utaratibu mzuri ambao uliwekwa na uongozi wa kituo na kusimamiwa na askari.

Baada ya chekecha chekecha ya hapa na pale hatimaye tukawa kwenye mstari ulionyooka sasa wa kutoka nje. Nikageuza shingo kuangalia nyuma, hakika basi lilikuwa limejaa na hakukuwa na mtu aliyesimama zaidi ya mhudumu mmoja na Yule msindikizaji ambao wote walisimama pale mlangoni, wakati huo tayari yule wakala msindikizaji alikuwa amesha maliza mambo ya ushuru wa getini nk.

===

Safari iliendelea hadi maeneo ya Mbezi Luis ambapo yule msindikizaji alikuwa ameshakamiliza zoezi lake la kukabidhi kila abiria tiketi ya mashine ingawaje tulikuwa na zile tiketi za karatasi. Tiketi hizi za mashine (POS) hazikuwa hizi zilizounganishwa na mifumo ya LATRA na TRA bali zilikuwa kwa ajili ya udhibiti wa kiofisi yao tu.

Niliangalia begi langu kwa mara nyingine, nikajiridhisha lipo salama haliwezi kumuangukia abiria wa jirani maana nililiweka kwenye kibebeo (carrier) cha upande wa kushoto wakati mimi nipo siti za upande wa kulia ili niweze kuliona muda wowote ninapotaka ingawaje watu wengine hupenda kuweka upande huo huo alipo kaa yeye tena juu sehemu aliyokaa.

Safari iliendelea, wakati huo video ilikuwa imezimwa na kufunguliwa radio (RFA) tukiendelea kupata habari. Kwenye hili la kelele za miziki, video za ndani ya basi walikuwa wamefanikiwa, maana hawakuwa wakifungulia kwa sauti za juu, ilikuwa sauti ya kadri tu ambapo hata ukiongea na simu kwa sauti ya chini bado mtasikilizana.

Basi lilitembea mwendo wa Serikali, ‘tatu bila, tano bila nane bila’ hadi tulivyofika Chalinze na misafara ya mabasi kuongozana na kukimbizana ikapungua na mabasi kuanza kumwaga moto. Kutoka Mbezi hadi Chalinze nadhani siku hiyo kulikuwa na fatiki kabambe ya ‘traffic police’ kwa maagizo ya kamanda wa wakati huo, maana kabla ya safari kulisikika tangazo pale Ubungo bus terminal kuwa madereva wote wakusanyike sehemu husika kwa ajili ya kuongea na Kamanda (alitajwa). Nadhani semina fupi ile iliwaingia hadi Chalinze tu, sijui madereva wa mabasi wana matatizo gani, kha!

Basi lilikuwa ni YUTONG, sijui namba ngapi ngapi lakini wenyewe wanasema ndio kubwa katika mfululizo wa wakati huo. Huko mbele ya safari ndio nikajuwa maana niliona ilivyokuwa inafunguka. Licha ya kuchezewa vts lakini pia nahisi ‘limiter’ ya spidi pia ilichezewa, si kwa mwendo ule baada ya kuvuka Rusumo border.

Chalinze hadi Moro basi lilitembea lakini ile kibongo bongo, minara ilikuwa inafanya kazi maana yule mhudumu muda wote alikuwa na simu sikioni na mkono mmoja ameweka juu ya dashboard, mara anapiga dashboard mara anainua kama vile anaita yani alikuwa anapata taarifa nje ya basi na yeye alifikisha ujumbe kwa dereva kwa kupiga dashboard, kuinua kiganja na kuita kwa kiganja.

Mwendo haukuwa hatarishi kiasi cha kuripoti kwa askari waliokuwa akiuliza sehemu za ukaguzi na dereva wala hakuwa mchafuzi wa overtake za ‘kubeti’ ila kwenye mwendokasi sehemu za hamsini hadi tulivyofika mbele kidogo ya Singida. Huko ilikuwa muda mwingi ni over 90kph.

Kabla ya kufika Morogoro, jirani yangu ambaye katika simulizi hii nitampa jina la Janeth, alikuwa ametulia, maana muda wote tangia Dar alikuwa kwenye simu akiongea mara akiandika jumbe za simu. Nikaanza kumsemesha sasa kwa Kiswahili ili kujuwa uwezo wake katika lugha hii adhimu, alikuwa anajibu kwa tabu sana ingawaje alifinyanga finyanga tukawa tunaelewana.

Kwa haraka haraka kutokana na maongezi ndani ya basi, nikajuwa mle ndani kuna Wabongo, Wanyarwanda, Warundi, Wakongo, wa Uganda na Wakenya. Pia kulikuwa kuna watu weupe wawili mmoja akiwa mwanamme, sijui ni Wazungu au Wamarekani lakini hawakuwa Waasia.

Janeth hakuwa mweupe wa rangi, bali maji ya kunde na aling’aa vyema kama ngozi yake ilivyokuwa ikionesha, alivaa ‘tracksuit’ na raba kama vile alikuwa ametoka kufanya mazoezi, nywele alisokota rasta bila kuunganisha nywele za bandia. Hakunizidi urefu, mana pale Chalinze tulipokuwa tunakunywa chai tuliteremka pamoja na kutembea pamoja kabla hatujaachana njia mimi nikielekea maliwatoni upande wa wanaume.

Kwakuwa mimi ni mpenda chai ya maziwa yenye kahawa, basi nilienda upade ule kwenye huduma hiyo na yeye Janeth wa sikumuona tena alipoelekea.

Kwenye jambo hili la kuwapa muda wa kutosha abiria wakati wa chakula, hawa jamaa nao walifaulu vizuri, maana mhudumu alipotangaza alisema tutatumia nusu saa kuchimba dawa pamoja na kupata chochote, tuzingatie namba ya basi maana yalikuwa mawili, baadaye sana ndio nikajuwa kuwa moja litaelekea Uganda na lile tulilopanda ndio litaelekea Kigali.

Kwakuwa siti yangu ilikuwa jirani na sikuwa nakaa dirishani, niliingia wa mwisho mwisho kwenye basi na kumkuta Janeth akiendelea kula nyama za kuchoma alizofungiwa kwenye bahasha fulani hivi ya khaki.

“Welcome nyama choma…” alinikaribisha huku akimaanisha nichukuwe msongo mmoja niendelee nao…

“Aaah, ahsante sana, unaitwa nani?” nilijibu huku moyoni nikikataa kuchukuwa nyama kwa ishara ya kuonesha nimetosheka (nimeshiba)

“Yaleyale ya kupewa chakula na usiyemjuwa wala kuona chakula kilipotoka mwisho wa siku unajikuta umeshaibiwa…” niliwaza.

Nikatoa ‘chewing gum’ za ‘mint’ na kuanza kutafuna ili kuweka kinywa changu katika hali ya kuanzisha maongezi ya kisafari safari.

“Karibu bublish…” nilinyoosha mkono na kumpatia kadhaa na akapokea kimya kimya na kuzihifadhi kwenye kimfuko kidogo kilichopo kwenye lile friji mbele ya siti zetu huku akiendelea kutafuna minofu ya mishikaki ya ng’ombe.

Safari ikaanza tena tukiitafuta mizani ya Mikese, mwendo mzuri, nane bila na uchafuzi wa speed kiasi maana dashboard nilikuwa naiona lakini ilikuwa haizidi 89kph. Pila nilikuwa na Garmin Drive 52 iliyoipata katika harakati za kutafuta ugali ambapo katika safari hii nilitarajia itanisaidia kule niendako ambako sikuwa na uhakika wa coverage ya internet.

Kelele za king’amuzi (vts) kilikuwa almost muda wote alipokuwa zaidi ya 85kph kinasikika kwa mbali sana, sijui waliweka kitu gani wale jamaa, maana kama sio mjuzi wala huwezi kuelewa ni kitu gani kinaendelea, dereva huyu Mtanzania alikuwa na nidhamu ya michoro ya makatazo ya kuovateki ila alikuwa ana ‘maintain maximum’ ya Latra muda mwingi, hii ilifanya tusiwe nje ya muda wa ratiba ya gari.

Janeth mkononi alikuwa amevaa kitu mama shanga hivi maarufu kama “culture” lakini ilikuwa na bendera ya Kenya.

“Wewe ni mkenya?” nilimuuliza huku nikiutolea macho mkono wake wa kushoto ambao ndio alikuwa amevaa hiyo shanga.

“No, Mnyrwanda” alijibu huku akitabasamu.

Nikachukuwa smartphone yangu, nikafungua playstore ili nidownload dictionary ya English – Kinyarwanda lakini haikunisaidia sana maana wakati huo bado haikuwa na maneno mengi.

“Do you speak English” nilimuuliza tena ili kama vipi tuhamier kwenye Kiingereza maana Kiswahili chake kilikuwa hakieleweki.

“Kidogo…” alijibu kisha akaendelea … “French and Kinyarwanda okay...”

Katika harakati za maisha sikubahatika kujifunza Kifaransa, bali niliyajuwa maneno machache sana maana rafiki yangu wa zamani sana, mototo wa Kihindi aitwaye Raani alinipatia kamusi ya Kifaransa kwa kiingereza lakini wala sikuwa na mzuka. Raani binti yule wa Kihindi urafiki wetu haukudumu kwa sababu ya Sue mototo wa Kispaniola ambaye naye pia wala hatukufika mbali, maana baada ya chuo tu miezi ishirini hivi baadaye mawasiliano yalikatika.

Alivyojibu kuwa kwenye Kifaransa na Kinyarwanda ndio yuko vizuri, basi sikuwa na chaguo lingine zaidi ya kuvumilia Kiswahili chake na kiingereza chake ingawaje kwenye kiingereza alikuwa yuko vizuri zaidi kuliko Kiswahili.

Hili ni jambo lingine la kushangaza, yani ukitoka Bongo kwenda Rwanda, hapo Rwanda wenyeji wanazungumza kilugha chao tu na Kifaransa, siyo wengi wazungumzao kiigereza. Ila ukivuka Rwanda kwenda Congo DR huko utakutana na Kiswahili cha aina yake, lakini angalau watu wanaelewana.

Kigali haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda, lakini huko Goma ndiyo ilikuwa ‘fisrt time’. Niliuchangamkia huo mchongo ingawaje Hamida alinikataza nisiende kwa kuhofia hatari iliyopo ya vita baina ya majeshi ya Serikali na watu wanaojiita waasi.

“The first time when I saw you, I knew for sure you are Mnyarwanda…” nilisema.

“Why?” aliniuliza.

Hapo ndipo nikafunguka kuhusu jinsi sisi Wabongo tunavyowaona Wanyarwada. Nilimwambia kuhusu maumbile yao ya urefu, sura nyembamba, urembo wa asili, nyama za kutosha sehemu ambazo huwafanya wanaume wageuke nyuma kuangalia ili kuburudisha macho, nikaeleza weee mwishoe naye akaniambia kuwa hiyo dhani si asilimia mia sahihi, siyo Wanyarwanda wote warembo kama nilivyowapamba…

Eeee ni kweli nilimpamba sana ‘mixer’ ukweli na chumvi ili kuwasifia kama ilivyo kawaida ya wanaume.

Kwakuwa Rwanda haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda, nilikuwa najuwa hawa warembo tunaowaona kwenye mitandao ni wachache tu, wanawake wa Kinyarwanda wapo kwa maumbile mbalimbali na sura tofauti wengi ni wa kawaida sana na tofauti kabisa na tunao waona hawa wa kwenye mitandao. Hata hivyo haiondoi ukweli kwamba wapo wanawake warembo wa sura na maumbile huko Rwanda. Tabia zao tu ndio zina ukakasi kiasi fulani juu ya kujiona wapo matawi ya juu sana, kuwa na ukatili uliojificha labda kutokana na historia yao nk.
“…Lakini sasa mbona umevaa bendera ya Kenya?” nilidadisi.

Hapa akafunguka kuwa yeye ni mfanyabiashara, ana duka la nguo za wanawake kwao Kigali na kabla hajajuwa machimbo ya Tanzania alikuwa akifungia mizigo yake Uganda na Kenya, na hiyo ‘bracelet’ aliyovaa aliipatia Kenya…

Mazungumzo ya kawaida yaliendelea kama ilivyo kawaida kwa abiria na abiria. Safari nayo ilisonga salama kabisa hadi tukafika Dodoma pale jirani na panapoitwa ‘four ways’, tukawa na ‘short break’ ya dakika kumi ya ajili ya kuchimba dawa kisha safari iliendelea hadi Singida baada ya mizani mbelembele kidogo gari ikaingia sehemu fulani kuna hoteli ambapo napo tulipata dakika ishirini za kuchimba dawa na kupata chochote kisha safari ikaendelea. Tulipokaribika Igunga giza fulani hivi lilianza kuingia, hadi tunapita mzunguko wa Nzega pale tayari dereva yuleyule tuliyetokanaye Dar akiwa anaendesha hadi muda huo aliwasha taa hafifu zilizowaka kwenye sakafu ya basi pembeni pembeni na kufanya mandhari kuwa nzuri sana ndani ya basi.

Awali nilidhani basi litanyoosha moja kwa moja hadi border ya Rusumo lakini kumbe hayapitilizi bali wanalala Kahama kisha asubuhi na mapema safari huendelea hadi boda.

“Have you made your reservation to pass your night at Kahama…” Janeth aliniuliza wakati gari ikiwa inakunja Tinde kuelekea Isaka.

Nilimjibu kuwa sijafanya chochote, si nitalala ndani ya basi!

“Please don’t sleep in the bus, you will get tired, and you won’t enjoy your looong journet from there to Kigali, its tiresome…” alisema Janeth na alikuwa anamaanisha. Nilijua hivyo siku ya pili baada ya kufika Rusumo.

“I don’t have enough cash with me…” nilitaka kujitetea akanikatisha…

“Don’t worry, I will pay for you and you will refund me when we reach border or Kigali…”

Sikumwambia kuwa mie pale mpita njia tu naelekea DRC. Nadhani alidhani namie ni mmoja wa wanaoelekea kwenye “sabasaba yao” (trade fair) maana tarehe hizo kulikuwa na maonesho ya kibiashara hapo Kigali iliyoanza kama siku mbili zilizopita na inayotarajiwa kuwepo kwa siku kadhaa zijazo.

“Why spend a lot of money! We can share the room…” nilichombeza huku nikiwa simaanishi.

“…Really!?” alihoji

“Why not!” nikajikuta tu neno limenitoka.

Mazungumzo yaliendelea na akaniambia yeye hufikia Gaprena Hotel. Nikatafuta review ya hotel hiyo harakaharaka kwenye simu nikaona ni zile wanazoita hotel kumbe ni lodge tu iliyochangamka. Anyway, ni Hotel. Sifa kuu aliniambia kuwa pako salama na ni karibu na stendi kuu pia gharama ni ndogo kulinganisha na hadhi ya hoteli yenyewe. Mimi wakati huo nimeshasoma review kadhaa na kupata picha halisi ya sehemu anayotarajia kufikia.

Tukaingia mizani Kahama na baada ya kutoka hapo mhudumu alitutangazia ratiba ya gari na kutupatia elimu maelekezo na tahadhari. Moja ya maelekezo aliyotoa ni kwamba basi halitoendelea na safri hadi kesho saa kumi na mbili asubuhi, hivyo anashauri abiria watafute lodge za kupumzika kwa watakaopenda kufanya hizo, na wale watakao amua kulala ndani ya basi wawe makini na mizigo yao ya ndani ya basi maana ulinzi wa mali iliyo ndani ya basi ni wa abiria husika.

“Muwe makini na mutu mugeni yanakuja ndani ya basi, hakuna abiria naingia usiku huu…” alimalizia yule mhudumu na Kiswahili chake kibovu.

Gari ikakunja kulia moja kwa moja hadi stendi kuu. Stendi ilikuwa imechangamka sana na ilikuwa ni majira ya saa tatu hivi usiku. Watu wengi, wauza vyakula mama lishe wengi huku wakikaribisha wateja, wapiga debe wa lodge pia wengi wakijitahidi kutafuta wateja, hakika Kahama palikuwa pamechangamka sana.

Wahudumu wa basi tulikuwa nao safarini wote waliondoka akaja wakala mkazi wa hapo ambaye alikuwa akisimamia ‘shoo’ bila shaka na walinzi wao pia walikuwepo ingawaje sikuwaona mara moja.

Abiria walikuwa wanajivuta sana kushuka mimi na Janeth tukiwemo. Nusu saa baadaye tuliamua kutembea kuelekea hoteli ambayo abiria mwenzangu alikuwa ameweka nafasi. Bajaj, tax na bodaboda zilikuwepo, lakini tuliamua kunyoosha miguu baada ya safari ndefu.

Tulivyofika pale mapokezi tulikaribishwa kwa bashasha lakini ‘walinikata maini’ nilipoulizia kama kuna chumba…

“Ishi, kwani hampo pamoja!...” aling’aka yule mhudumu

“Vyumba vyote vimejaa, basi ngoja nikupeleke hoteli ya jirani na hapa, pale unaweza kupata ila bei ipo juu kidogo…” aliongea yule mhudumu kwa lafudhi ya kisukuma.

Janeth akaingilia kati…

“Lets share as you said, no problem… are you going to swallow me!?”

Yani hapa angalau kwenye uandishi inabidi nikinyooshe kidogo hivi vilugha vya watu maana jinsi alivyokuwa akiongea Janeth unaweza ukawa unacheka tu kila mara.

“Well, its okay, lets share the room and I promise will not swallow you…” tukawa tunacheka huku tukielekea chumba husika maana mwenzangu pale inaonekana ni mwenyeji.

======

INAENDELEA…

Utatu1.jpg
Utatu3.jpg
Utatu2.jpg
 
INAENDELEA…

“Well, its okay, lets share the room and I promise will not swallow you…” tukawa tunacheka huku tukielekea chumba husika maana mwenzangu pale inaonekana ni mwenyeji.

2. Sehemu ya pili – KISOMO CHA WATU WAZIMA

Tahadhari zote nilikuwa nazo, za kiusalama wangu na mali zangu pamoja na kifaragha maana matukio ya kusikitisha hutokeaga kama hivi. Hoteli ilikuwa ni ghorofa, sisi tulipata’ first floor’ na chumba kilikuwa kikubwa kiasi cha kusema kwa hela ile ni halali tu.

Nilikagua kila chumba kama kuna kamera-fiche, nikaona pako salama, nikawa nimekaa kwenye kochi na mwenyeji wangu wakati huo alikuwa kwenye kitanda. Mara simu ya mezani pale chumbani ikaita, Janeth akaipokea , kumbe aliweka oda tayari ya chakula kwa ajili ya watu wawili. Mlango ukabishwa na akaingia mhudumu kuleta chips kuku mbili na kuondoka.

“Tule kwanza kisha ndio tuangalie utaratibu wa kulala…” nilipendekeza na ikapita bila kupingwa.

Nilipendekeza pia tuanze sahani moja kwanza wote kwa pamoja na kama hatujashiba basi tuhamie sahani nyingine. Hii ilikuwa mbinu ya kujihami na madhara ya kwenye vyakula, kama yapo basi yatupate sote na wakati wa kula nilihakikisha nasoma lugha ya uso wake ili kujiridhisha.

Maskini binti wa watu wala hakuwa na makuu bali ni ukarimu tu wa kawaida na kama alikuwa na agenda ya siri basi sikuiona haraka ukiachilia mbali na suala la kushiriki tendo la ndoa.

Mfukoni kweli sikuwa na hela za kutosha kwa mambo ya ziada, zaidi ya yale niliyo jipangia hadi kufika Congo, hivyo sikuwa na mzuka maana boom la kustaafu lilikuwa bado kutoka na tayari nilishasota mtaani miezi kadhaa hivyo vihela vyangu vilikuwa vya kuunga unga. Nikatuma ‘txt msg’ kwa Jason Jr ili aniazime dola mia tano atume kwenye account yangu ya benki just incase. Kabla sijalala muamala ulisoma kwenye akaunti yangu.

Janeth alikuwa huru tu, akaingia bafuni na kibegi kidogo na alipotoka alikuja amevaa kaptura na juu alikuwa amevaa fulana nyepesi (haikuwa night dress hizi tunazozijua)

“I am in my period so don’t try anything nasty…!” aliniambia huku akiingia kwenye blanket tayari kuutafuta usingizi.

Moyoni nikajisemea afadhali maana umenirahisishia mambo mengi ambayo tayari nilikuwa nawaza kichwani. Sikuwa na soksi wa vipimo vya kupimia tanesco kama ipo. Nikaingia bafuni na kuanza kuoga, wala sikutumia muda mrefu nikatoka kuja kuungana na Janeth ndani ya blanket na kuanza kuzungumza mengi katika kutaka kufahamiana zaidi.

Saa sita kasoro hivi usiku, Janeth alipitiwa na usingizi akiwa bado amelalia mgongo, nilijuwa baada ya kumuuliza swali fulani ili niendeleze stori niliyokuwa namsimulia lakini hakujibu, kugeuka ndio nikaona amelala hana habari. Nikamfunika blanket vizuri nami nikavuta upande wangu nikawa kama nimelala lakini nipo hadhiri masikio waruuu!

Saa tisa na nusu hivi usiku aliamka kwenda maliwatoni , nilikuwa macho bado maana sikutaka usingizi unipitie hata chembe ingawaje nilifunga macho.

Huwa nina kawaida ya kuamka asubuhi saa kumi na robo kwa ajili ya maandalizi ya siku pamoja na ibada za asubuhi lakini siku hiyo sikusikia alarm hadi saa kumi na moja haja ndogo iliponibana nikaamka na kuangaliaa saa! Nilishangaa sana. Janeth bado alikuwa amelala. Nikaenda maliwatoni na kujimwagia maji safi ya moto tayari kwa maandalizi ya kuendelea na safari. Nilivyotoka bafuni nilimkuta Janeth naye ameamka amekaa kitandani.

“Goodmonring Jane! Leo nimechelewa kuamka na wala sikusikia alarm ya simu…” Nilimsalimia na akajibu…

“Goodmornind Dad, pole kwa uchovu…”

Nje pilika za bodaboda zilikuwa zinazidi kuongezeka, bajaji na magari madogo maana tulikuwa kando kando tu ya barabara ielekeayo stendi.

“Kumekucha, kajiandae tusije tukachelewa…” nilimwambia.

“Bado kuondoka, saa kumi na mbili ndio basi litaondoka, muda bado hata hivyo ngoja nijiandae haraka haraka…” alisema.

Kama nilivyoeleza awali kuwa katika kuandika najaribu kunyoosha maneno yake angalau wewe unayesoma uelewe, lakini ilikuwa ni lugha gongana kwenda mbele ingawaje tulielewana kwa kuchanganya lugha zote mbili Kiswahili na Kiingereza.

Awali nilimuona Janeth kama ni aina ya wale wanawake wafanya biashara ambao wapo tayari ku ‘risk’ chochote ili mradi aingize hela hivyo nami nika ‘adopt’ uelewa ule ndio maana nikaomba nitumiwe hela ambayo hata haikuwa kwenye bajeti ya safari yangu. Uchumi wangu ulikuwa ni wa kawaida tu wa kujikimu ndio maana fursa hii ya kufanya kazi siku 90 DRC niliichangamkia.

“Uko mubaba muzuri, hujanisumbua…” alisema Janeth wakati akimalizia kujipamba.

“My period ended the day before yesterday but I’m not that clean for the game ndio maana nilikuambia nipo kwenye siku zangu…” Aliendelea kujisemesha.

“it’s okay Janeth, mimi wala sikuwa na mpango wowote na nilidhani ningelala kwenye basi, ahsante kwa ushauri wa kupumzika lodge…” nami nilijiongelesha.

Tulitoka pale huku akikataa mimi kuchangia gharama za lodge na chakula, lakini nikawahi kulipia bodaboda mbili ambazo zilitufikisha stendi saa kumi na mbili kasoro dakika kumi.
===

Kifungua kinywa tulipata Ushirombo ambapo pia walitumia nafasi hiyo kujaza mafuta kwenye basi, baada ya hapo moja kwa moja hadi Nyakanazi tulipoacha lami na kuanza njia ya vumbi na mashimo kuelekea Rusumo. Ni kilomita chache tu lakini tulitumia muda mwingi sana kufika border ya Rwanda na Tanzania.

Baada ya kukamilisha taratibu za border na kuvuka, nikaenda kwenye ‘restaurant’ upande wa Rwanda sasa ili nipate chakula, wakati huo Janeth yeye na wafanyabiashara wengine walikuwa wakikaguliwa mizigo yao hapo border ya ajili ya mambo ya ushuru nk. Alinirusuhu nikale maana huenda yeye angechukuwa muda mrefu kukamilisha zoezi. Ni kwamba hapo mpakani kwenye basi hushuka abiria wote na mizigo yote hushushwa ya kwenye buti na ndani ya basi na kila mmoja kupitia ukaguzi kulingana na mzigo wake kisha kwenda uhamiaji kama taratibu za kuvuka boda zilivyo.

“Nipatie mashilingi hayo nikupe faranga, ‘rate’ nzuri kabisa nakupatia…” alisikia ‘husler’ mmoja hapo nje ya restaurant.

Nilibadili dola mia kwake na nikamwomba anipatie kijana anayesajili line ya mtandao wa MTN ili nipate simcard ya Rwanda.

Zoezi la kuvuka hadi basi kuwa tayari kuondoka lilichukuwa zaidi ya saa tatu na kufanya tuwe nyuma ya ratiba ya kawaida ya basi. Abiria wengi walikuwa na mizigo ambayo ilikuwa na utata katika kuvusha lakini hatimaye wote tulifanikiwa kuvuka.

Baada ya kuvuka, dereva tuliyetoka naye Dar alipumzika kwenye siti namba moja na yule dereva wa pili, Mnyarwanda alichukuwa nafasi.

Sasa sijui kwa kuwa tulikuwa nyuma ya ratiba ama ndio uendeshaji wake, ee bwana ee, mwendo ulikuwa si wa kitoto, kuna wakati kwenye gps yangu speed ilisoma hadi 160kph ikabidi niinuke niangalie dashboard ya basi. Njia ilikuwa ya lami lakini nyembamba halafu basi lilikuwa linatembea upande wa kulia, kila mara nikajikuta nabana breki mimi ilhali siye ninaye endesha maana si kwa kuhisi hatari zile! Tena mpambe nilimsikia akisema amsha amsha!

Kabla ya kufika Rusumo, njiani kuna baadhi ya abiria washuka, mmoja tulimwacha pale kizuiani maana watu wa uhamiaji walimtuhumu ame ‘overstay’, wengine walishukia Lusahunga, Benaco na Mizani. Hivyo basi ilipata nafasi kiasi cha kupakia abiria wengine pale boda baada ya kuvuka. Mmoja wa hao abiria nadhani alikuwa wakala wapo ndiye alikuwa akihamasisha sana kuwa gari imechelewa.

Nilikuwa nadhani Rwanda mabasi hayakimbii kama nilivyosikia awali lakini ilikuwa kinyume chake hadi tuliposogea mbele mbele sana na giza likaanza kuingia ndip mwendo ukawa wa kawaida. Ni wastani wa kilomita 160 hivi kutoka Rusumo border hadi Kigali, lakini huwezi kuamini, tulifika saa tatu hivi usiku iwakuwa wakati tunakaribia mjini Kigali tukakuta foleni ndefu sana iliyotulazimu kutembea ‘jino moja moja’.

Safari ilichosa sana kipande cha Nyakanazi hadi Rusumo, tulitembea taratibu mno kwakuwa njia ilikuwa na mashimo na rasta baadhi ya sehemu, haikuwa njia rafiki kwa kweli licha ya umuhimu wake njia kuu hiyo. Nadhani sikuhizi pako vizuri, sijapita tena kwa barabara.

Janeth alinipa ofa ya kwenda kufikia kwao, ingawaje niliikataa na kumweleza kuwa mimi ni mpita njia tu naelekea Rubavu (nilimdanganya). Rubavu ni moja ya majimbo ya Rwanda jirani na Congo huko. Akaniambia basi kesho yake nisiondoke ili anitembeze Kigali kwenye ‘sabasaba’ yao. Focus yangu haikuwa kwenye kutalii bali kibarua kinachonisubiri huko Goma. Lakini nikaangalia kalenda nikaona bado nipo mbele ya muda na nina siku 4 mbele kabla ya kuripoti nikamkubalia ombi la kunitembeza Kigali.

Haikuwa mara yangu ya kwanza kuwepo Kigali lakini nilitaka nipate ‘experience’ nyingine kupitia huyu Janeth ambaye naona kama anataka kunizibia kufurahi na watoto wengine wa Kinyarwanda. Alikuwa anakaba sana kana kwamba tumekubaliana chochote.

Wajihi wangu ni bonge la mtu, mrefu futi sita hivi, maji ya kunde, heavy weight 105Kgs, ndevu zote mvi kichwani nimenyoa unga kuficha wingi wa mvi, nilivalia kawaida tu suruali ‘cadet’ na shati ‘cadet’ la mikono mirefu nililovaa Kahama maana kutoka Dar nilivaa ‘tshirt simple’. Sura yangu haijazeeka ingawaje ukiniangalia kwa makini ndio utaona kilomita zimeenda, hivyo nadhani nilikuwa naonekana bonge la Bwana. Yeye Janeth alibadili nguo zote pale Kahama, mimi suruali sikubadilisha. Alivaa gauni refu na mapambio yake.

Tulibadilishana namba za whatsapp na nikampa namba yangu ya MTN. wote tulishuka Nyabugogo bus terminal. Yeye Janeth alichukuliwa na pickup townhiace ambayo pia ilipakia na mizigo yake, mimi nikachukuwa TOYO (bodaboda) na kunipeleaka Kaizen Hotel ambayo haikuwa mbali na stendi.

Pamoja na mambo mengine, chumbani nilipokelewa na kitanda chenye godoro lenye ‘finishing’ ya material yasiyopitisha maji. Mawazo yakarudi kwa Janeth.

“Hawa si ndio mabingwa wa kurusha maji katika harakati za kilimo ya umwagiliaji!, kwanini nisitumie fursa hii kupata elimu ya watu wazima…” niliwaza. Nikaanza kuona saa haziendi. Kabla ya saa tano usiku kwa saa za Bongo nilikuwa nimeshaegesha, na usingizi haukuchukua muda kunipata kwa kuwa nilikuwa na uchovu uliotokana na usingizi wa mang’amng’am wa Kahama na uchovu wa safari. Nikakumbuka maneno ya Janeth kuwa nisilale kwenye basi nitachoka sana, nikaona kumbe alinishauri vyema ingawaje uchovu mwingi ulitokana na mimi kutolala vema kule Kahama.

Saa kumi na robo simu iliniamsha, nikachungulia nje bado giza sana, ikabidi nirekebishe saa yangu iendane na majira ya kule, hivyo nikarudisha dakika sitini nyuma. Nikaendelea kuegesha huku nikitafakari baadhi ya mambo. Usingizi ukanichukuwa tena hadi nilipostuka saa moja asubuhi kwa saa za Rwanda. Nikaamka na kujiandaa kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.

Restaurant wageni wenzangu walikuwepo wengi wakijihudumia kupata breakfast, nami nikaungana nao, wengi wao walikuwa wakiongea kinfaransa na baadhi Kinyarwanda. Wahudumu wa kike wa hoteli walikuwa kama wale tunaowaona kwenye mitandao lakini huko mitaani wanawake wengi sana ni wa kawaida tu tena wengine wala si warefu ama warembo kivile ama wenye maumbile hamasishi. Nikakumbuka ule usemi, ukitaka kuifaidi Kigali, fikia hotel zenye hadhi ya juu ama tembelea kwenye ma-‘shopping mall’ na sehemu kama hizo huko ndiko kuna vile vitu wabongo wengi tunababaikaGa navyo.

Wakati nikiendelea kupata staftahi nilipokea simu ya kwanza kwenye line ya MTN kutoka kwa Janeth, nilijuwa tu ni yeye maana namba bado sikuwa nimeigawa kwa watu wengine.

“…I will be at Nyabugogo terminal at ten thirty, lets meet at Trinity Bus office…” aliniambia.

Ilipofika saa nne kasoro kidogo nami nikakabidhi mzigo wangu mapokezi na kushuka chini kuchukuwa toyo ili inifikishe jirani hapo stendi. Saa nne na dakika chache nikaona nafwatwa kwa ishara ya kukumbatiwa, alikuwa na tabasamu na mwenye uso uliokunjuka.

Baada ya kumbatio motomoto pale na kupeana pole za uchovu akaniambia kuwa yeye hakai mbali sana na hapo, anaishi maeneo ya Kacyiru. Akaniahidi kunipelea kwao. Nikakubali. Lakini akaniambia tuelekee kwenye maonesho kwanza ili tuzunguke humo wee kisha ndio tuende kwao kisha kuzurura jijini Kigali.

Akaniambia tuchukuwe taxi.

“Nyamuneka utujyane i Magerwa…” alisema Janeth akimwambia yule dereva wa teksi atupeleke sehemu iitwayo Magerwa.

Dakika chache tu baadaye tukafika hapo Magerwa, ni kama vile bandari kavu fulani hivi, hatukuingia ndani badala yake akaniambia tutembee kuelekea upande uliouoneshea kidole.

“We are heading to Gikondo area, sio mbali ni paleeee…” alisema.

Kumbe hapo Gikondo ndio kuna sabasaba yao, tukalipa kiingilio na kuingia ndani. Pamoja na mambo mengine ya ki-‘trade fair’, nilikutana na visu hasa, yani Jane wangu nilimuona wa kawaida sana, ingawaje yupo vizuri kisu haswa lakini asikwambie mtu, macho ya wanaume hayachoki kuona vitu vizuri. Tulijifunza mengi humo na baada ya kuchoka tuka kaa sehemu kama mghahawa hivi mumohumo kwenye maonesho na kuanza kuongea mawili matatu huku tukipata viazi mbatata, maharage na samaki kama sato.

Baada ya hapo tulifanya mzungukowa pili ambao sasa huu ulilenga sehemu maalumu tulizoziona kwa ajili ya kununua baadhi ya bidhaa alizotaka nami nikaambulia kununuliwa mkanda wa ngozi pamoja na wallet kutoka kwa wafanyabiashara waliotoka Misri.

“Zawadi yako uwe unanikumbuka…” alisema Janeth.

Baada ya muda kidogo tulitoka tukiwa na mizigo yetu na kuchukuwa Taxi.

“…Kacyiru…” Janeth alimuambia yule dereva na tukaanza kuondoka.

Nilifurahia nidhamu ya barabarani ya madereva wa kule, yani madereva wote wa vyombo vya moto. Sheria za usalama barabarani zilikuwa zinafuatwa vyema.

Baada ya kona mbili tatu nikaona dereva akiuliza maelekezo ya ziada, alipopatiwa nikaona amekuja tena kona kadhaa kisha tukafika eneo tulivu lenye nyumba nzuri yenye ‘umatemate’ fulani hivi.

Nilikaribishwa vizuri na tulikuja kupokelewa na watu wengine mle ndani. Baada ya utambulisho mle ndani mwao kwa waliokuwepo tukaletewa chakula. Kulikuwa na ndizi nyama na vikorobwezo vingine, tukala huku tukiendelea na mazungumzo ya kawaidia.

Baada ya kama saa moja hivi akaniambia twende sasa nikutembeze Kigali. Tukatoka mle ndani, akawasha gari yake vw golf (baby walker) na tukaelekea katikati ya jiji moja kwa moja kwanza kwenye duka lake. Awali nilidhani ni duka dogo tu la wajasiri-amali, lakini kumbe dooo! Ni bonge la duka lililosheheni nguo za wanawake tu.

Alinitembeza kwa gari pale mjini, kisha kwa miguu hadi ilipofika saa moja jioni kwa saa za Rwanda tukarudi dukani kwake ili achukue gari turudi nyumbani kwao. Kwa kweli nilifurahia kubaki Kigali siku hiyo. Tulifika kwao saa mbili kasoro hivi kwa saa za kule na kukaribishwa. Safari hii nilikuta familia imeongezeka, yaani baba yake alikuwepo, mama yake, dada zake na kaka zake. Ilikuwa ni familia yenye furaha. Ilikuwa ni familia ya aina yake ambayo baba ni Mhutu na mama ni Mtutsi, ni familia ambayo imejaribu kuvuja jambo la ukabila katika nchi hiyo na Baba ni afisa wa Polisi katika Serikali ya Rwanda.

Niliwaza hapa nikijichanganya tu napata ndoa ya uzeeni, maana si kwa ukarimu ule sijui hata Janeth aliwaambia nini. Janeth alikuwa mtoto wa tatu kuzaliwa akitanguliwa na dada zake wawili kisha kufuatiwa na kaka zake wawili. Dada zake wote walikuwa wameshaolewa, lakini yeye na kaka zake walikuwa bado hawajapata ndoa. Baada ya chakula cha jioni, niliaga ili niwahi kupumzika maana asubuhi nilitaka nianze safari kwenda Gisenyi -Rubavu Province kama nilivyomuambia Janeth. Sikutaka ajuwe kama nitavuka mpaka na kuingia Congo kwa wakati huo.

Tulitumia gari ya Janeth hadi aliponifikisha Hotelini kwangu na nikamkaribisha hadi chumbani.

Dhambi iliyofuata nilishaitubu na ugomvi wake na Hamida ulishaisha maana hata yeye alifurahia elimu ya watu wazima niliyoipata huko Kigali niliporudi. Nilikuwa najuwa ‘katerero’ lakini hapa nilipata elimu ya ‘kuyanza’, sijui hata kama nimepatia inavyoandikwa. Ni hatari sana.

Katika kuitumia elimu hii ni muhimu wote muwe na afya njema vinginevyo mtaambukizana maradhi yatokanayo na kujamiiana (ngono). Ni kama vile katerero lakini hii tuseme ni katerero promax. Mtanisamehe, siwezi kuielezea hii hapa kwa sababu ya kuepuka matumizi mabaya ya hii kitu kwa wasiokuwa na ndoa.

“Usiondoke na basi za asubuhi, ondoka saa nne ili upate kupumzika vizuri…” yalikuwa maneno ya Janeth baada ya kumuomba anifundishe kilimo cha umwagiliaji kama kifanywavyo na wanyarwanda.

Nilipata elimu murua, na hakika wana haki ya kuweka sheria ya kila nyumba ya kulala wageni kuwekwe zile foronya zisizopitisha maji. Ewe kijana unayefikiria kuoa Mhaya ama Mnyarwanda, hakikisha unajifunza kilimo cha umwagiliaji maana kwao ni muhimu na haki ya msingi vinginevyo tarajia kutembelewa na kutambulishwa ndugu zake wa kiume usiowajuwa ama kuombwa safari ya kurudi kusalimia mara kwa mara alipotoka ili mradi tu kilimo cha umwagiliaji kifanyike.

Nilikubaliana na wazo lake la mimi kuondoka saa nne asubuhi, hivyo sehemu kubwa ya usiku nilikuwa darasani hadi maji yalipoamua kukatika kabisa, tukalala.

Saa nne na nusu tayari nilikuwa stendi kuu, pale kulikuwa na basi ziendazo Gisenyi, kila baada ya dakika kadhaa basi moja hutoka. Nilipanda RITCO, kampuni yenye huduma bora kabisa Rwanda ambayo baadaye nikaja kujuwa ni mpango mzuri wa viongozi wa Jeshi lao kubuni mradi huo. Safari ilikuwa nzuri na mwendo mzuri kwa sheria za kwao lakini nilikerwa na waendesha baiskeli ambao hushikilia malori kwa nyuma na kupata lifti hatarishi isiyo rasmi.

Kuna sehemu nimeshapasahu, tulipumzika kupata chakula kisha tukaendelea na safari. Yes panaitwa Nyirangarama, nimeona kwenye picha niliyopiga. Njia ni ya milima na mabonde, dereva huko inabidi awe timamu kuweza kuendesha bila kusababisha ajali. Takribani kilomita 150 kutoka Kigali nikaanza kuona ziwa upande wa kushoto, nilipouliza nikaambiwa ni ziwa Kivu, basi lilikuwa linashuka mlima taratibu maana kona ni kali mlima una mwinamo mkali lakini hatimaye tukafika Stendi kuu ya Gisenyi mpakani kabisa na mji wa Goma – Congo, Kivu Kaskazini.

Kwakuwa ilikuwa jioni, sikupenda kuvuka mpaka siku hiyo, bado nilikuwa nina siku mbili za ziada kabla muda wa kuripoti kibaruani. Hivyo niliamua kutafuta sehemu nzuri ya kupumzika. Baada ya kuuliza wenyeji sehemu ya bei nafuu lakini patulivu na usalama mkubwa ndio nikaaelekezwa sehemu Fulani wanapaitwa kwa Mapadri. Nikachukuwa bodaboda hadi huko. Ile sehemu ni kama Msimbazi centre ya Dar es Salaam. Wana rest house nzuri na tulivu sana. Hapo ndipo akili ya kazi ikaanza kurudi upya maana nilitulia na kuanza kutafakari kibarua ninachokiendea.

Ilikuwa siku ya Ijumaa jioni nikiwa hapo kwa Mapadri, nikapata wasaa wa kutembea kwa miguu hadi ufukweni mwa ziwa Kivu sehemu ambapo watu hupenda kutembelea jioni kama vile Coco beach ya Dar. Hapo uzalendo ukanishinda ikabidi niingie kuogelea na kuchanganyika na wenyeji lakini sehemu ya upande wa watu wazima maana kama vile watu walijigawa, hapo nikakutana na visu vingine hatari. Pia kulikuwa na boti kadhaa za wajasiri-amali ambao walikuwa wanapiga debe ili wapate wateja wa kuwatembeza ziwani kwa ujira wa fulani (dola 10).

Siku yangu iliisha vizuri na giza lilipoingia nilitembea kurudi kiotani kwangu hapo kwa Mapadri. Baada ya chakula cha jioni ambacho nilikipata jirani na hapo kwa Mampadri nilirudi chumbani na kuendelea kuandika simulizi ya Hamida nikisogeza ‘episode’ kuwapunguzia arosto wafuatiliaji wa kila siku mwaka huo. Baadaye nikaanza kupitia yanayohusu kinachonipeleka Goma kwa kuhakikisha nimehabarika ipasavyo kufikia tarehe ya siku hiyo.

INAENDELEA…
 
Attachments

  • Rwa1.jpg
    Rwa1.jpg
    70.4 KB · Views: 68
  • Rwa3.jpg
    Rwa3.jpg
    38.3 KB · Views: 68
  • Rwa2.jpg
    Rwa2.jpg
    22.4 KB · Views: 67
  • image_2023-03-07_121759886.png
    image_2023-03-07_121759886.png
    150.8 KB · Views: 79
  • Sehemu ya tatu – MAKUTA (Rushwa), MADINI MENGI NA VITA ISIYOISHA
Kesho yake asubuhi kulikuwa na pilikapilika za usafi wa mji. Ni kwamba kila ikifika Jumamosi ya mwisho wa mwezi wananchi wa Rwanda husafisha maeneo yanayo wazunguka na kufanya miji yao kuwa misafi muda wote. Hii siku wao huiita ni umuganda. Ingawaje hata Goma pia nilikuta utaratibu huu lakini kwa jina tofauti. Sisi Watanzania tuliiga lakini sidhani hadi leo kuna huu utaratibu, watu waishio mijini wataleta mrejesho.

Msururu ulikuwa mrefu sana pale mpakani, saa tano na nusu nikawa miongoni mwa watu waliopanga foleni ili kuvuka mpaka kwa utaratibu. Upande wa idara ya uhamiaji Rwanda hakukuwa na shida ila sasa nilipofika upande wa uhamiaji DRC shughuli zilianza.

“Paspo ?!” alisikika yule afisa uhamiaji huku akiniangalia usoni.

Nikampatia nikamweleza kwamba nitakaa kwa miezi mitatu, akaniambia inabdi kulipia visa ya muda huo ambapo nililipa dola kadhaa, hapo ikawa imeisha lakini nikaelekezwa niende sehemu ya idara ya afya ili wakague kadi ya njano (yellow card). Kwa ambao hawajasafiri nje ya nchi ni kwamba kila mtu anatakiwa kuchanjwa kama kinga kwa baadhi ya magonjwa ikiwemo homa ya manjano nk, uthibitisho wa chanjo hizo ndio mtu hupewa kadi fulani hivi ambazo ndio huitwa yellow card.

“…hujachanja cholera …” alisikika yule afisa wa afya na kuzuia passport yangu na kadi yangu.

Mara akaja afisa mwingine na kuniambia nimfuate, nilipoingia ofisini kwake akaniambia..

“…lete makuta, nitatosha passpo na kadi yako…” akimaanisha nimpatie hongo ili alipatie passport pamoja na kadi ya njano.

Nikatoa dola kumi nikaweka mezani, lakini akacheka sana…

“…hayo sio makuta… ongeza makuta…”

Yani hii haikuwa kwangu tu, ilikuwa kwa wageni wote waliokuwa wanaingia Goma kwa mara ya kwanza, lazima wachomolewe hela, na ilikuwa inafanyika waziwazi hawaogopi chochote kama ni halali vile. Kisheria sikupaswa kulipa chochote pale na kile ambacho wao hupata kwa njia hiyo hakiingizwi kwenye mfuko wa serikali yao bali wanagawana wao.

Nikazama mfukoni nikatoa dola 20 nikaweka mezani.

“…ongeza ingine kama hii natosha paspo yako sasa hivi…” akasema.

Nikampa tena dola 20 na tukasimama akaniambia nimfuate.

“…Tosha hiyo passpo ya mtz amenipa makuta..” alimwambia yule afisa aliyezuia passport yangu pamoja na kadi.

Nikakabidhiwa na kukaribishwa Goma.

Baada ya kuvuka mpaka, mimi pamoja na watu wengi sana kama vile uonavyo watu wanapotoka kushuka kwenye kivuko pale kigamboni, nilitembea kilomita kama moja hivi kisha nikachukuwa motoo (bodaboda) ili inipeleke hoteli ambayo nilipanga kufikia kwa kupumzika kabla Jumatatu sijawatafuta wenyeji wangu. Nilifikia Hotel Cap Kivu ambapo niliona karibu na ofisi ya wenyeji wangu.

Goma kwa wakati huo kulikuwa na ugonjwa wa ebola na tishio la uviko19. Walikuwa wamejipanga vizuri tangia mpaka wa Rusumo, walikuwa wanapima joto la wavukaji na kunawa mikono ilikuwa ni lazima, vivyo hivyo Kigali huingii dukani ama ofisi yoyote hadi upimwe joto na unawe mikono kwa sabuni ama kitakasa mikono na Goma ulikuwa mtindo ni huohuo.

Kunawa mikono ni utaratibu mzuri maana hutuweka kuwa na mikono misafi muda wote. Hebu siku ukipata nafasi kaa/simama pembe fulani hivi angalia watu wanavyojishika sehemu zao, tumia nusu saa tu kufanya uchunguzi huo. Utaona watu wanajishika sehemu zao za siri kwa kujikuna ama kuweka sawa, wanashika sehemu zingine chafu chafu ama zenye kuhisiwa na bakteria wengi, kuchokonoa pua na kadhalika halafu unakutana naye mnapeana mikono…Uviko19 angalau ilitulazimisha kunawa mikono.

Jioni wakati wa kumwagilia moyo kwa burudani ya macho masikio na vinywaji baridi nikakutana na mwanamke mwingine aitwaye Bosio. Nilikuwa nimekaa pembeni nikibarizi upepo mwanana kutoka ziwa Kivu maana ilikuwa ni kandokando ya ziwa, kwa mbali nilimuona bibie Bosio akimwagilia moyo kwa pombe. Nikamsogelea ili kupata mtu wa kuongea naye kupitisha muda uende.

“Hi, can we share the table?” nilimsalimia na kuvuta kiti na kukaa mkabala naye.

“Ok” alijibu kwa kifupi.

“Do you speak English?” nilimpachika swali lingine

“Are you from Nigeria?! Aling’aka

“Here we do speak English, Frech, Lingala, Swahili altogether in conversation…” aliendelea

Nilivyosikia Kiswahili si nikasema mambo si haya!

“Kumbe unazungumza Kiswahili..” nilirudi kwenye lugha adhimu.

“Eee Kiswahili yako ya nguvu sana iko byee (bien)..” alijibu huku akikaa vizuri kama anataka kujuwa kitu fulani hivi…

“Unaikala fasi ya Kenya…” aliuliza.

“Hapana mimi ni Mtanzania…” nilijibu kwa kifupi ili nimsikilize

“Unaspikee Kiswahili ya nguvu papaa, umekuya kufanya nini Goma, huogopi masasi wana tu danjere sana na masasi yao…” alisema akimaanisha wanatishiwa sana usalama wao kwa risasi zinazoridima mji huo.

Hadi wakati huo mimi nilikuwa sijasikia milio ya risasi wala nini labda kwa kuwa ni muda mfupi tu ndio niliingia mjini Goma.

Bosio alikuwa ni mwanamke wa kiafrika haswa, ni mfanya biashara kati ya Bukavu na Goma kupitia ziwa Kivu. Huwa analeta vitenge vingi kutoka Kinshasa na kusambaza Bukavu na Goma.

“Nimekuja kutembea tu Goma na kuangalia fursa za biashara, je nini naweza kuleta huku kutoka Tanzania?” nilimjibu na kumuuliza.

“Eee sikia papaa, Goma iko biashara, Bukavu pia iko biashara, lete mchele papaa au maharage, chakula ndio iko shida pande ya huku…” alijibu kwa kirefu pale akizungumzia biashara ya nafaka.

Bosio japo ilikuwa jioni giza linataka kuingia, lakini uzuri wa macho yake hayakujificha, alikuwa na macho mazuri hatari, kama vile yanasema “kama unanitaka basi nitongoze..” ngozi yake nyeupe iliyopatikana kutokana na dawa za kubadilisha ngozi, mwili mnene kiasi na yaliyomo yamo ugonjwa wa wanaume wengi. Kichwani alikuwa amejifunga kilemba cha kitenge ambacho rangi hiyohiyo ndicho alichovaa, ilikuwa ni gauni refu la kitenge lililodariziwa vyema na fundi wake.

“Uko na macho mazuri sana…” nilimsifia maana nilikuwa nayaangalia hadi anaona aibu.

“Ndio jina yangu, Bosio, mama alinipatia jina hiyo nadhani baada ya kuona nina macho mazuri, Bosio ni Kifaransa ndio kusema macho mazuri kwa Kiswahili. (Bosio = beaux yeux)

“Na wewe unaitwa nani?” aliniuliza.

“Jamaal, ninaitwa Jamaal Jason” nilimjibu.

“Nimefurahi kukufaham Jamaal…” alisema

“Ni furaha yangu pia bibie Macho mazuri…” nilimjibu na tukacheka pale na kugonganisha glasi kwa kufurahi kufahamiana, cheers!

Niliendelea kunywa Bavaria zero yangu taratiibu huku yeye akijimimia mvinyo niliomkuta nayo.

Jioni hiyo maeneo hayo hapakuwa na watu wengi bali kulikuwa na wazungu wachache na waafrika kadhaa wote wakibarizi upepo mwanana kutoka ziwa kivu huku wakimwagilia moyo na mziki mororo uliendelea kuburudisha.

Nilimjulisha mwenyeji wangu namba moja kuhusu uwepo wangu mjini Goma na nikamweleza nilipofikia, akanijulisha kuwa kesho atakuja hotelini kwa ajili ya kunikaribisha. Usiku ule ulienda vizuri na tulibadilishana namba za mawasiliano ya Bosio kila mmoja akashika hamsini zake.

Wakati nipo chumbani nimepumzika nikapokea simu kutoka kwa Janeth. Kama kawaida aliyojiwekea, kila siku jioni ama usiku tangia tulivyoagana siku ile pale Nyabugogo stendi atakuwa akinijulia hali kwa jumbe fupi za maandishi kwenye simu au alipiga kabisa. Tuliongea tukafurahi na akanikumbusha kuwa Goma kuna SIDA kwa wingi hivyo nijilinde na pia kuchukuwa tahadhari ya ebola na magonjwa mengine yaambukizayo.

Janeth sijui aliona nini kwangu maana nilikuwa kawaida sana kama ambavyo huwa siku zote ninapokuwa katika mazingira ya kawaida, sikuwa na hela na wala sikuwa mtu wa kujikweza. Labda alikuwa na kiu sana ya mume hivyo alitaka apate ‘Sugar Dady’, ama ilitokea tu ‘damu’ kuendana, ama ni namna ya kutengeneza ‘connection’ na Tanzania ili kurahisisha biashara zake, yani sikupata majawabu sahihi kwa wakati huo. Usingizi ulinichukuwa hadi siku ya pili ambapo wao wanaita siku ya Mungu (Jumapili)
===

Saa nne asubuhi nilipokea mgeni ambaye baadaye nilijuwa kuwa ndiye mwenyeji wangu namba mbili. Baada ya mazungumzo machache ya kujitambulisha, akaniambia atanisubiri chini kwenye gari fulani (aliitaja). Baada ya kujiandaa na kuaga pale hotelini (check out), nilishuka hadi kwenye gari nililoelekezwa. Niliagwa kwa heshima za kijeshi (salute) mbaya kutoka kwa walinzi wa hoteli ambapo mmoja alikuwa na silaha kubwa inayoonekana.

Nje kwenye gari niliyo elekezwa nilikuta Toyota landcruiser pickup ambayo nyuma kulikuwa na askari wawili wa jeshi la RDC na dereva alikuwa huyo mwenyeji wangu namba mbili. Nikafunguliwa mlango na kuingia upande wa kulia mwa gari (gari lilikuwa left hand drive – LHD) na kupokea salute kwa mara nyingine angalau hizi zilikuwa na kamuelekeo fulani hivi hahahah nikakaa vizuri na kufunga mkanda na gari ikaanza safari.

Mwenyeji wangu namba mbili alikuwa ni mkongoman, alikuwa anazungumza Kiswahili kile cha Kikongo hivyo haikuwa tabu kuelewana.

“… Goma sasa usalama uko mdogo, ndo vile tunatembea na askari kwa tahadhari…” alisema huku akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida.

Baada ya kona mbili tatu tukashika barabara kuu tukawa tunaelekea kama kurudi mpakani, na baada ya kupita ‘round about’ kubwa ya tatu tukakunja kulia na kuelekea njia ya kuikabili ziwa kivu na hatimaye tukafika kwenye geti la Goma Serena Hotel na kupokelewa kwa salute mbaya mbaya vilevile kisha tukaegesha sehemu ya maegesho ya wageni na nikakaribishwa kumfuata mwenyeji wangu namba mbili.

Katika kile chumba cha mkutano (haukuwa ukumbi bali chumba cha mwenyeji wangu namba moja) tulikuwepo watu wane, yaani mimi, mwenyeji wangu namba mbili, mzungu mmoja na mwafrika mmoja.

“Welcome to Goma Mr. Jamaal…” alinikaribisha yule mwenyeji mwafrica ambaye hakuwa mkongoman bali alikuwa mtu kutoka Afrika ya kusini na yule mzungu nilijuwa baadaye kuwa ni alitoka Nepal, hivyo alikuwa ni mu Asia fulani hivi kama mzungu.

Baada ya maongezi merefu ya awali, nikaambiwa kuwa kuanzia usiku huo wa Jumapili kuwa nitalala hoteli hiyo ambako wao walisema ni salama zaidi kuliko kwingine. Mpaka wakati huo sikuona hatari yoyote iliyokuwepo Goma.

Nikasindikizwa chumbani kwangu ghorofa hiyo hiyo bawa lingine. Nikaambiwa nipumzike kwa kuwa kesho nitakuwa na kazi ngumu ya kuchosha. Niliambiwa kuwa nitapitiwa kuelekea huko kibaruani.

Asubuhi mapema lilikuja gari fulani hivi jeupe kama la deraya na sisi watu watatu (mwenyeji namba moja, mwenyeji namba mbili. Mzungu muasia ambaye sasa tumuite mwenyejinamba tatu) tukaingia na kuondoka kulekea ofsi fulani si mbali sana, hapo wakaongezeka watu wawili na kuanza safari…

Tulikamata barabara ya kueleka airpot ya Goma na hatimaye tukaingia ndani, baada ya itifaki za hapa na pale tukaingia kwenye helicopter na kuruka kuelekea kisiwani, hapakuwa mbali na mjini goma. Ni kwamba kulikuwa na mtambo fulani wa kisasa ambao ulihitaji kutumika lakini wataalamu wenye fani hiyo hapo hawakuweza kuufanya utumike licha ya kufuata taratibu zote muhimu. Mitambo hiyo ilikuwepo kadhaa nchini DRC.

Kijasho kilikuwa kinanitoka licha hali ya hewa nzuri kama ya Arusha nyakati za baridi iliyokuwepo Goma.

“…Huku hakuna fukuto kama la Bongo…” alisikika jamaa mmoja kati ya wale wawili walioongezeka. Yani alikuwa ananishangaa jinsi ninavyotokwa na kijasho chembamba wakati nikioneshwa mitambo hiyo.

Sisi watu watano hapo wote tulikuwa ni wataalam kuhusiana na mitambo hiyo lakini kwa bahati mbaya wote iliwashinda kuifanya ifanye kazi na kuomba msaada nchi ilipotoka. Walijibiwa kuwa Tanzania kuna watu watatu wanaweza kuishughulikia mitambo hiyo, bahati mbaya mmoja alifariki miezi kadhaa iliyopita na mmoja ndiye huyo aliyenipa dili mimi, yeye alikuwa na udhuru wa jambo lingine.

Basi, nikuangalia ule mtambo na kufuata hatua moja baada ya nyingine na hatimaye nikaona matatizo yalipo.

“…Nilikuwa nafikiri sana hadi kichwa kikapata moto ndio maana nilikuwa natokwa na jasho…” nilimjibu baada ya kuona matatizo na mmoja wa wale jamaa akawa anawa tafsiria kiingerza ili tuwe wote ukurasa mmoja.

Niliwaonesha sehemu mbili kubwa zenye kasoro. ‘Actually’ hazikuwa kasoro bali ni njia za usalama ili mtambo usiwashwe ama kuwaka bila kukusudiwa. Kulikuwa na main fuse kubwa ilikuwa haijaungwa sehemu husika ingawaje ilikuwepo imebanwa na ‘tape’ hapo inapotakiwa iwekwe, pili kulikuwa na sehemu ya kuvuta ili nailoni nyembamba inayotenganisha umeme mdogo kupenya iondoke haikuwa imetolewa.

Baada ya mazoezi hayo mtambo ulianza hatua za kuwaka na wote tukawa tumefurahi. Tuliondoka na mtambo huo eneo hilo hadi site husika na kuuwasha na kufanya kazi yake. Ilikuwa ni mwendo wa nusu saa angani kwa helicopter hadi tuliposhuka eneo la kwanza.

Baada ya kufanya kazi hapo siku nzima bila kuwa na kiashiria cha kuleta shida yoyote ndipo tukarudi Goma airport na kupokelewa na gari jingine lakini safari hii tukiwa pungufu maana mtu mmoja alibakishwa kule ‘site’ kwenye mtambo. Sisi watatu tulirudishwa hotelini kwetu na yule mwingine alirudishwa sijui hata wapi. Ahadi ikawa ni kesho tena tuelekee site nyingine.

Lile zoezi tulilifanya kwenye ‘site’ nne nzingine kila siku ‘site’ moja na hatimaye mitambo yote ya aina hiyo ikwa ipo kazini.

“…So you have to stay here for more three weeks to make sure everything is running propery” alisema yule mwenyeji wangu namba moja wakati nikimuacha kwenye site ya mwisho.
===

Nilikaa siku tatu zaidi Goma kabla sijaomba kwao ili nikae wiki mbili na kama hakuna tatizo basi nivuke mpaka kurudi Tanzania kuendelea na shughuli za kawaida.

Katika zile wiki tatu nilizokaa Goma ndipo nilipojuwa kwa nini walikuwa wanasisitizia usalama, maana kila siku nilikuwa nasikia milio ya risasi na silaha nyingine, nikulizwa naambiwa na waasi hao wanafanya fujo sehemu.

Kwamba kuna waasi fulani wa jeshi wapo msituni, kila wakiishiwa vyakula basi huingia mtaani ama kijiji fulani na kuvamia na kushurtisha watu wawape vyakula na mahitaji mengine, na mbaya zaidi walikuwa wanaua, inasikitisha sana.

Pale Goma Serena palikuwa pametulia sana, hivyo nilikuwa natoka kwenda mjini kwa ajili ya kumwagilia moyo kwa burudani mbalimbali ikiwemo macho kuona, sasa uko ndipo nilipokuwa naona ile hali ya hatari niliyokuwa naambiwa. Mfano kuna siku nilikuwa sehemu fulani hivi kulikuwa na mziki wa bendi live, ghafla tukasikia sauti za risasi kadhaa… kisha pakawa kimya, wale wenye mziki waliendelea na mziki wao wala hawakuwa na wasiwasi, ila mwanamziki mmoja aliyekuwa anabonga (rap) alisikika akisema “…wameanza na masasi yaoo, wameanza na masasi yaoooo…” yani ilionekana kama ni kitu cha kawaida kwao. Nilipo muuliza jirani yangu ndio akaniambia kuna jamaa (askari jeshi) yupo hapo baa ya pili amelewa na alikuwa anarusha risasi hewani bila kumdhuru yoyote moja kwa moja. Hebu fikiria (imagine).

Njia ya kwenda Uganda kutokea Goma haikuwa salama hata kidogo kwani ilisemekana kuna makambi ya waasi sehemu kadhaa huko maana matukio ya vijiji kuvamiwa yalikuwa yakiripotiwa mara kwa mara. Pia njia ya kwenda kaskazini mashariki huko kuna msitu mnene ambako napo hapakuwa salama na matukio kadhaa yalikuwepo. Kimsingi sehemu zote ambazo kuna uchimbaji wa madini unaoendelea kumekuwa na hali ya sintofahamu ya usalama mara kwa mara. DRC ni nchi iliyobarikiwa kwa madini mengi na ya aina nyingi yakiwemo madini muhimu ya cobolt ambayo yanatumika hata kwenye kifaa hicho unachosomea simulizi hii pamoja na magari ya kisasa, ndege (aeroplane) na vifaa vingine vingi vya kieltroniki.

Wiki ya tatu kabla sijavuka mpaka kuingia Gisenyi, ziliingia hela za malipo yangu kupitia akaunti ya KBC niliyofungua Goma ili kurahisisha utumaji na upokeaji fedha kwenda Tanzania. Pale pale nilihamisha kiasi cha dola mia tano kumrudishia Jason Jr. hela alizonikopesha na kubakiwa na hela za kutosha kiasi cha kuona hata sikustahili kulipwa kiasi kile baada ya kazi ya siku 5. Nikawasiliana na jamaa aliyenipa mchongo, Dar es Salaam naye nikamtumia asilimia zake na wote tukawa tumefurahi. Ni hekaheka za uzeeni tulijisemea.

Bahati nyingine mbaya ni kwamba Afrika mashariki yote ikawa imevamiwa na uviko19. Goma ikawa na ziada ya ebola na nikaona ni muda muafaka sasa wa kuvuka mpka niwe upande wa Rwanda ili hali ikizidi kuwa mbaya basi niwe na njia nyingi za kutokea kuliko nikiwa mjini Goma. Hivyo wiki ya sita nilikaa Gisenyi na wiki kadhaa zingine nikakwama Kigali, kama tutakavyoona mbele.

Jiografia ya Goma na Gisenyi jinsi ilivyo ni kwamba, Gisenyi ni kama hakuna biashara hivi ila watu wengi hupenda kukaa mji huo na Goma kuna biashara nyingi sana na mzunguko mkubwa wa hela lakini wafanya biashara wengi ni wale wanaokuja kutoka Gisenyi na kurudi. Hivyo mpaka wa Goma na Gisenyi upo bize sana licha ya kuwa na mipaka miwili ya kuvukia, (two borders) kuna wanayoita boda ndogo nah ii boda kubwa, zote zinatumika na zote muda wote zipo ‘bize’.

Niliona ombwe la biashara ya mchele na maharage kama ambavyo bibie Bosio alivyoniambia, lakini changamoto katika utafiti nilioufanya ilikuwa na namna ya kufikisha nafaka hizo mjini Goma, soko ni kubwa sana hata la unga wa ugali. Nilitumia siku sita kuingia na kutoka Goma kwa ajili ya matembezi maana pamoja na matishio ya usalama lakini shughuli zao zilikuwa zinaendelea kama kawaida. Nilitembelea baadhi ya maofisi ya serikali ya DRC, baadhi ya maofisi ya wananchi tu wa kawaida, mtaani, mahotelini n ahata bandarini kwao ambapo niliona kitu fulani kinafurahisha sana.

Katika maofisi ya serikali niliona vile wat wanavyojisikia kwenye nafasi zao, muda mwingi wanapiga soga tu na kujadili mambo ya siasa, kupenda kuvaa vizuri na kuwa na vifaa vya gharama kubwa mfano simu na hata mtu mmoja kumiliki simu zaidi ya tatu kwao ni kawaida.

Bandarini pale sehemu ya kupakia abiria ni kama stendi ya mabasi tu, yaani watu wengi, pilika nyingi lakini pia kuna wapiga debe na mawakala wa kukatisha tiketi za meli. Sasa jambo lililonifufahisha ni wapiga debe wa pale bandarini! Yani unakuta meli kadhaa zinasubiri kupakia abiria ambapo usiku huondoka kuelekea Bukavu na maeneo mengine huko hufika asubuhi. Sasa hawa wapiga debe wa meli tofauti tofauti huvutia wateja wao kwa kufanya ‘show’ ya kucheza mziki wao wa Kikongo. ‘very interesting’ ukiwaona, wamejipanga vizuri na kuweka sauti ya mziki huo wauchezao kwa stepu matata sana. Sasa kila meli zilikuwa na ‘stage show’ wao na ni meli zaidi ya sita zilikuwa zinapakia kwa wakati mmoja. Ilikuwa ni burudani maridadi kabisa.

Katika hekaheka za kutembea mjini Goma nilikutana na wadada wanao uza bidhaa za asili, Dar es Salaam maarfuru kama vifurushi, yaani wale wadada wauzao mihogo mibichi, karanga, nazi nk. Sasa Goma walikuwa wanauza mizizi fulani hivi na mbezu fulani hivi na kupata hali ya udadisi ili kujifunza.

“.. Hii ndo yenyewe, inatoka Lubumbashii…” alisema yule dada muuzaji huku mwenzake akiwa ananiangalia usoni.

“... Matumizi yake?! “ niliuliza

“.. hii changa na karaga tafuna na hii ponda ponda wala saga na mashine halafu changa na uji unakunywa…” alielezea

“…Sasa nitajuwaje kama inafanya kazi, mimi nimekuja tu narudi kwetu…” nilimuuliza

Waliangaliana kisha wakacheka sana wote pale na yule muuzaji akasema…

“ Hi indo yenyewe kabisa, uliza madereva wenzako wote bananijuwa mimi ndo nawaleteaga kutoka Lubumbashii…”

Kwa mwonekano wangu hakika nilifanana na maderva wa malori maana huwa sipendi kuwa tofauti na mazingira ya walio wengi maeneo husika.

“…wala nikupatie depusierele Lubumbashii…” alisema huku akifungua kitu kutoka kwenye mkoba wake mwingine kama vile wafanyavyo wauzao madawa baridi (DLDM) pindi ukitaka kununua dawa sizoruhusiwa kuuza dukani kwake…

Alitoa unga fulani kama mizizi iliyosagwa na kuwa unga ambao ulifungwa vizuri kwenye nailoni kama vile ugolo.

“Hahahahaha hii ndio vumbi la Congo!??” nilicheka na kufurahi kuliona vumbi la Kongo kwa mara ya kwanza

“Ndo yenyewe hii depusiere le Lubumbashii…” alijibu akimaanisha kuwa hiyo ndio yenyewe vumbi la Lubumbashi.

Yani mimi nasema vumbi la Congo, yeye anasema vumbi la Lubumbashi. Ni kama vile ukiwa nje ya Tanzania, Bongo ni Tanzania, na ukifika Tanzania kwenyewe, Bongo ni Dar es Salaam. Au kama vile ukiwa Dar es Salaam na mikoa mingine nje ya Rukwa, ukifika Sumbawanga utaambiwa kuna Rukwa yenyewe sasa huko Bondeni.

Hivyo haikunichukuwa muda kujuwa kuwa lile ndilo vumbi la Congo.

“Faranga ngapi unauza?!” nilimuuliza

“Demilfra!” alijibu haraka haraka akimaanisha kama elfu mbili na kidogo ya Tz

“Okay, sasa nipajuwaje kama dawa zako zinafanya kazi?!” nilirudia swali langu la awali.

“Papaa, hii iko bye! (bien), wala naweza kupa utumikishe halafu uniite kwa lojzhee umefikia tuje tufanye…” alijibu huku akijiamini

Nikasema moyoni “ yaleyale ya kufanya unauza karanga mbichi kumbe wana ya ziada wanayouza…”

Nilimuangalia yule binti, alikuwa mfupi, amekomaa kienyeji halafu umri kama thelathini au zaidi kidogo hivi. Nikaoana huyu ngoja niachane naye niendelee kujifunza mengine.

Nikawa naondoka eneo hilo, akaniita, “Papaa nipatie sanchi dolaa nikupatie hii yote…”

Alikuwa anatia huruma, sinia lake lilikuwa lina mzigo mkubwa bado kama vile ndio amefika kutoka alipofuata mzigo wake, nikamuonea huruma na kumpatia dola tano hivi…

“Kamata hii dimilefra…” nilimwambia chukua hii faranga elfu kumi (kama dola tano hivi) na kupokea ule mzigo ambao sasa nikauangalia nikaona ameweka zile ugolo pakti tatu, kokwa fulani mbili ni mizizi fulani kadhaa.

“Mercii Papaa..” alishukuru kwa unyenyekevu na kurudi kwa mwanzake.

Mitaa ile ilikuwa ni pale ambapo madereva wengi wa Tanzania hupenda kujivinjari, lakini muda huo palikuwa bado hapaja changanya lakini nilimuona mmasai mmoja nikamuita “rafiki!…” akageuka na kuja upande wangu huku akitabasamu.

“Jambo rafiki..” alisema yule mmasai na kuendelea kutangaza biashara yake kama kawaida yao…

“Ninayo hiyo ya ngirimo mara! Nikupatie?” usoni kwangu upande fulani kuna vinyama fulani vidogo vidogo ambavypo wengine wanaviita visunzua, lakini siyo sunzua maana zunzua nazifahamu, wamasai ndio huita ngirimomara.

“Hapana rafiki, nilikuita kukusalimia tu” nilimjibu

“Unatokea pande ipi Kenya!” aliniuliza

Inaonekana, wafanya biashara wengi na kutokea Kenya pale goma na Uganda maana wengi hudhani ama mimi ni Mkenya au Mganda.

“Hapana rafiki mimi natokea Tanzania…” nilimjibu

Tulibadilishana maneno kadhaa pale katika kufahamiana tu ile ki barabarani na nikajuwa yeye pia ni Masai wa kenya.

Nilitumia muda wangu mwingi kufanya manunuzi ya vitenge maridadi kwakuwa hapo ni bei nafuu kuliko Kigoma ama Dar es Salaam.

“Vikwembe viko byee, hapana imitee hivi..” Mama moja alisikika akisema kwa kunivutia kwamba vitenge vyake ni vizuri na wala siyo nakala/kopi (copy) ya orijino fulani.

Nilichaguwa nilivyovipenda kadhaa kisha nikamshirikisha Hamida wangu kwa whatsapp ili kati ya hivyo achaguwe anataka vipi…

“…lete vyote tu mbona vizuri sana…” ndilio lilikuwa jibu la Hamida

Hakika vile vitenge vilikuwa vizuri sana, kuna vilivyouzwa pande tatu kwa dola 50, dola 80 na dola 100. Vitenge vya dola 20 kushuka chini ndio vingi vimejaa kule Kitumbini Dar. Pia nikaelekezwa namna ya kujuwa kitenge imitee na halisi. Nikajifunza kumbe wao wenyewe Congo hawazailshi vitenge bali huletwa kutoka nchi mbalimbali kama vile Ghana, Nigeria nk. Nikajuwa kuwa pia kuna vitenge vya zaidi ya laki 4 na kuendelea kwa pande tatu na kwa ‘texture’ na ‘material’ mbalimbali.

Nikamchulia Hamida vile vitenge vyote nilivyochaguwa, na nikaongeza kadhaa vya dola hamsini 50 kwa ajili ya zawadi kwa baadhi ya ndugu.

Shughuli ilikuwa kuviingiza Rwanda, yaani kuvuka navyo pale boda maana Upande wa Rwanda wanakaba ushuru wa maana, lakini nilifankiwa kuvivusha vyote kwa nyakati tofauti nikiwa navuka na kitenge kimoja na jamaa wengine wakinivushia kitenge kimoja kimoja na kuwapatia hela kidogo tunapofika Gisenyi changanyikeni, hakika mwananchi ukimkandamiza kwenyekodi lazima atatafuta unafuu kwa njia zisizo rasmi.

Sikuwa natumia usafiri wowote zaidi ya kuvuka kwa kutembea kwa miguu. Mji wa Goma na Mji wa Gisenyi ni kama vile kutoka Magomeni Dar es Salaam hadi kufika mataa ya ‘Fire’. Na katikati hapo siyo jangwa wala pori, bali ni makazi ya watu tu na ofisi kadhaa, hivyo nilikuwa nafurahia ule uzoefu wa kuvuka pale mpakani kwa foleni ndefu, na kutembea nikichanganyika na wenyeji pamoja na wageni. Kwa kuchanganyika huko na watu hatimaye nikapata fununu kuwa mpaka wa Goma na Gisenyi utafungwa kwa sababu ya uviko19. Hivyo nilivyofanikisha kuvusha mzigo wangu wote siku hiyo ya Ijumaa, sikurudi tena Goma na kwa kuogopa mabasi pia kutosafiri nilikimbilia Kigali ili nisikilizie kama kuna lolote katika ile mitambo kwa wiki mbili zingine. Posho za kujikimu ziliendelea kutiririka na kunifanya niwe na hekaheka nyingine jijini Kigali.
====

INAENDELEA…
 
Attachments

  • rwa0.jpg
    rwa0.jpg
    32.7 KB · Views: 75
  • Rwa4.jpg
    Rwa4.jpg
    32.6 KB · Views: 77
  • rwa6.jpg
    rwa6.jpg
    100.6 KB · Views: 62
  • rwa7.jpg
    rwa7.jpg
    102.6 KB · Views: 65
  • rwa8.jpg
    rwa8.jpg
    59 KB · Views: 72
Sehemu ya nne – USILOLIJUWA NI KAMA USIKU WA GIZA

Hapakuwa na shida nyingine yoyote katika ile mitambo kwa wiki tatu za matazamio, lakini kukawa na shida kubwa ya uviko19 na hali ya kujilinda kwa kujifungia ikaanza nikiwa nipo Hotelini Kigali. Ni Janeth aliyekuja kunipokea pale Nyabugogo bus termina na kunipeleka hotel iliyo jirani na kwao Legend Hotel.

Hapo nilipata wasaa mzuri wa kumalizia kuandika simulizi ya Hamida na muendelezo uliotokana na simulizi hiyo, wiki ya kwanza ilikuwa na kawaida tu sikuona tabu yoyote maana karibu kila siku nilikuwa nakutana na Janeth na kupata chakula cha jioni nyumbani kwao maana palikuwa ni mwendo wa kutembea tu. Familia ilinizoea na nikawa kama sehemu ya familia.

Nilikuwa nachukuwa tahadhari zote kuhusu Janeth, maana inasemekana wanawake wa Kinyarwanda hupenda kujishikiza kwa watu wa nje ya nchi yao kwa ajili ya manufaa ya nchi yao, hivyo nilikuwa makini sana na nilidhamiria kutaka kujuwa haswa nini kilimvutia Janeth kwangu kiasi cha kunikaribisha kwao namna ile.

“Nipo single, sijawahi kuolewa, wewe ni sawa tu na baba yangu kiumri lakini najaribu kupunguza upweke…” alianza kufunguka.

“Wanaume wa Kinyarwanda wapo lakini wengi wao sio romantic, ni kweli watakunyaza utafurahia lakini hawako kama watanzania….” Alisema

“Watanzania wana upendo na ukarimu, hawachukii wageni, siyo kama kule Kenya, Tanzania hata lugha yao katika biashara ni nzuri hadi nilijilaumu kwanini sikuwa nakuja pande ya kwenu kununua bidhaa…”

“Kwakuwa ile ilikuwa mara yangu ya tatu kwenda TZ niliazimia siku nikimpata mtu mwenye kujiheshimu basi nitajenga urafiki naye ili aje anisaidie katika mambo yangu ya biashara na kunipunguzia upweke…”

“Ukaribu na nidhamu uliyo nionesha kule Kahama, nikaona wewe ni mtu sahihi kwangu japo umenizidi umri sana lakini umetulia na naamini utanisaidia sana katika mipango yangu ya baadaye…”

“That day I was not bleeding, nilikuwa nimemaliza juzi yake tu lakini like sikutaka ku meet na wewe ati nikiwa niko na smell za mabaki ya period, so nikaamua niseme niko period ili kwanza nione kama utanisumbua, pili nipitishe siku ili huko mahali pazidi kuwa safi…”

Alifunguka mengi sana Janeth na mie nilikuwa msikilizaji na kusoma lugha ya mwili maana lugha ya mwili huwa haiongopi isipokuwa kwa watu wachache sana wanaoweza kudanganya kwa lugha ya mwili.

Baada ya wiki moja, mkazo wa ‘curfew’ ukazidi, ikawa hakuna tena kutembea mitaani, baina ya jua likizama na kabla jua halijachomoza. Watu kadhaa waliuwawa na askari wa Rwanda kwa kukaidi amri hiyo kitu kilichowafanya Wananchi wote kufuata maelekezo ya Serikali.

Nilishauriana na Janeth naye akashauriana na familia yao hatimaye ikakubalika mimi kutoka kule hotelini na kufikia nyumbani kwa akina Janeth. Hapo niliepusha gharama fulani pia kuongeza muda wa kuonana na Janeth kuwa kila siku tulikuwa tunaonana. Nilipewa chumba cha peke yangu ambacho alikuwa analala Janeth naye alikuwa analala chumba kingine. Wale dada zake walio olewa walikuwa wapo lockdown majumbani mwao pia, pale walikuwepo wale kaka zake wawili, Janeth mwenyewe na wazazi wao.

Mitandao ya kijamii ikiwemo JF ilinifanya niwepo nyumbani TZ kwa namna ya kipekee. Wadau walikuwa wameifurahia simulizi ya Hamida na kutaka niende mbali zaidi katika kutoa elimu simulizi. Baadhi ya members tulikuwa tunawasiliana PM na kuwaahidi nikirudi Tanzania nitafanya juhudi za kuonana nao ili tumwagilie mioyo.

Wiki iliyofuata amri ya kutotoka kabisa majumbani ikatoka. Watu walikuwa wakifa kwa kwa mia hospitalini na majumbani katika nchi zote za Afrika mashariki. Nchi za Asia, Ulaya na Marekani hali ilikuwa mbaya zaidi. Watu wakaanza kuhimizana kutumia njia za asili za kiafrika katika kujikinga na kujitibu ili kupunguza changamoto za upumuaji maana hali kila siku ilizidi kuwa afadhali ya jana.

Kila siku nilikuwa nawasiliana na Tanzania (Hamida) kujuliana hali, na miamala ya fedha kwa njia ya mpesa ilisaidia kumfikia kwa wakati. Aliniambia Tanzania hakuna lockdown ila wanavaa barakoa na kutembea na vitakasa mikono na kuchukuwa tahadhari ya kukaa mbali na makundi ya watu lakini biashara zilikuwa zinaendelea kama kawaida.

Kwa wiki kumi zingine nilikuwa nimekwama Kigali nisijue jinsi ya kuingia Tanzania maana hata usafiri ulikuwa ni wa shida hususani mabasi yote yalisitisha safari, nadhani na hili janga la uviko19 ndilo liliouwa kampuni ya mabasi ya utatu kama nililopanda kuingia nalo Kigali kutokea Tanzania, nasikia yaliuzwa kwa Kampuni moja ya baba wa Isaac na Rebeca kutoka kwenye biblia iliyoanzisha safari kwenda Makete kutokea Dar lakini ruti hiyo haikudumu na sasa nasikia kuna basi lingine limechukuwa faida ya uanzishwaji wa ruti hiyo kufanya biashara.

===

Familia ya Janeth ilikuwa karimu sana, nikaanza kuzoea kula vyakula vya Kinyarwanda na kupata muda mwingi wa kuongea na kaka zake Janeth ambao muda mwingi walikuwa nyumbani isipokuwa siku za mwisho wa juma ndio hutoka out na kurudi jumapili.

Nilikuwa nawaeleza kuhusu fursa zilizopo Tanzania na ombwe la chakula lililopo Goma, hivyo kama watakuwa tayari wafanye baishara hiyo maana inalipa sana. Walinijibu kuwa baada ya wimbi la uviko19 kupita wataomba mtaji kutoka kwa baba yao ili wajaribu kwa uchache kwanza huku wakijifunza.

Janeth naye nilimshibisha kwa maelezo ya kwamba nimeshafanya utafiti huko Goma juu ya biashara ya nafaka na kuona kuna fursa hiyo…

“…Hali ya usalama na uviko19 ikiwa shwari, nimejiridhisha kuwa biashara ya nafaka Goma inalipa sana.” Nilimwambia Janeth katika moja ya mazungumzo yetu.

Katika familia ile, Janeth pekee ndiye mjanja wa biashara, kaka zake wavivu wavivu kupenda starehe za mjini na dada zake walikuwa wameolewa hivyo walikuwa wana familia zao na maisha yao huko walipo. Dukani kwa Janeth ameajiri vijana watano, wakiume watatu na wakike wawili, mmoja kati ya hao wanaume yeye kazi yake ni kulinda duka wakati wa mchana kwa nje kama vile mtu wa mapokezi ya nje, na hao wengine wane walikuwa wauzaji, mmoja akiwa mpokea fedha “cashier” na wawili wakiuza ndani na huyo mmoja wa kiume akiwa kama mlinzi wa ndani kuangalia angalia huku naye akiuza lakini. Mama yake Janeth alinishukuru kwa kuwatia moyo vijana wake ili wajitafutie riziki maana wapo legelege (kwa mujibu wa mama). Baba yake Janeth alifurahi kunifahamu na kusema Tanzania tuna bahati tulipata kiongozi (Mwl. Nyerere) aliyetuweka pamoja tofauti na nchi zingine za maziwa makuu ikiwemo Rwanda ambapo alikiri kuwa jitihada kubwa bado inahitajika ili kabila hizo mbili ziwe pamoja na yeye amekuwa mfano kwa kuoa kabila lingene lisilo lake ili kujaribu kuvuja uhasama usiokuwa na maana.

Mwezi wa tatu ukawa unaisha nikiwa nipo nje ya nyumbani Tanzania, hamu ya kutaka kuchoropoka Kigali kurudi Tz ikazidi kuwa kubwa lakini changamoto ikawa ni usafir na njia ya kupita. Rwanda na Uganda na Kenya waliruhusu malori ya vyakula na bidhaa muhimu tu kuingia nchini mwao hivyo nami nikaona nitafute upenyo ya kupitia malori ili nirudi Tanzania.

Kwa kushirikiana na wale kaka zake Janeth, niliweza kupata usafirila lori liendalo Kampla -Uganda kutokea Kigali. Niliambiwa nijiandae ili siku ya jumatatu ijayo ndio wataondoka bohari (godown) asubuhi.

Siku hiyo Janeth akiwa na kaka zake wale wawili alinipeleka hadi eneo ambalo yule dereva wa lori alisema ndio atashushia mzigo wa mwisho hapo, ilikuwa ni eneo la uwekezaji kaskazini KPEZ maeneo ya bohari, ghafla nikapokea simu kutoka kwa Bosio. Akiniambia kuwa kuna mzigo wake (kontena) limefika Bandari ya Dar es Salaam hivyo anapigana aweze kwenda Tanzania. Nikamuuliza yupo wapi muda huo akaniambia yupo Gatuna anapambana. Wala hata sikuelewa Gatuna ni wapi na kwa vile nilikuwa na wenyeji wangu wala sikutaka kuwapa ‘faida’ ya simu ile badala yake nikaendelea na maongezi mengine.

Ilipofika saa tano hivi za Kigali tukawa tupo tayari eneo ambalo dereva wa lori alitaka tumsubiri. Hatimaye nifanikiwa kuingia kwenye lori hilo na kwa heshima ya utu uzima nikaambiwa nikae siti ya msaidizi wa dereva ambapo yeye msaidizi akarudi kukaa kwenye kitanda cha lori. Niliagana vizuri na Janeth na wadogo zake kwa ahadi ya kuendelea kuwasiliana mara kwa mara.

Ilituchukuwa saa mbili na nusu hivi hadi kufika border ya Rwanda na Uganda na ndipo nikajuwa kumbe ndio Gatuna. Ilibidi mimi niwe mmoja wa wafanyakazi wa lori lile kama dereva mwenza. Askari waliniambia niweke vizuri lori ili likaguliwe na pia wathibitishe kama mimi ni dereva pia. Lilikuwa ni Scania R420 Semi trailer, haukinipa shida kulipaki vizuri maana mimi pia ni dereva mahiri hivyo hawakutulia shaka maneno ya kwamba mimi ni dereva mwenza ingawaje walihoji kwa nini nina passport ya Tanzania na leseni ya Tanzania. Ndipo nilipomweleza kuwa nilikuwa ni msimamizi mpya wa kampuni hivyo nilikuwa nakagua njia… yule dereva halisi wa gari akaweka dola 20 kwenye passport yangu na mambo hayakuwa mengi tena.

Wakati tunahangaika na afisa uhamiaji upande wa Uganda nikaona naguswa bega, kugeuka Boiso huyu hapa!

Tulikumbatiana eti kwa furaha kana kwamba tulikuwa wapenzi au ndugu au tuliofahamiuana kwa muda mrefu. Baada ya salamu ndipo akashangaa imekuwaje mimi niko pale na nisimjulishe.

Hekaheska za uzeeni hizi sijui hata nilianzaje kumueleza, lakini hatimaye alielewa hali niliyopitia na kuamua maamuzi ambayo na yeye ndiyo hayo hayo aliyafanya ya kupitia mpaka wa Gatuna ili aje atokezee Tanzania.

Nikamshawishi yule dereva kuwa huyo binti ni rafiki yangu, tumetokea wote Goma na tunaelekea Tanzania hivyo amchukue hadi atakapoona inafaa sisi kuunganisha gari nyingine kwenda Tanzania. Baada ya ushawishi wa pesa kazi ikawa rahisi, akakubaliwa, hivyo kwenye gari sasa tukawa watu wane. Stori zikawa nyingi sana lakini safari haikuwa fupi wala rahisi. Safari haikuwa nyepesi hata kidogo ingawaje gari lilikuwa likirudi tupu. Tulivyotoka mpakani tulienda hadi Kabale, kutoka Kabale hadi Ntungamo, kutoka Ntungamo hadi Mbarara na kutoka Mbarara hadi Masaka ambako sasa dereva alisema hapa ni rahisi kupata malori yatokayo Kampala yanayoenda Tanzania, ingawaje kulikuwa na njia huko nyuma lakini alisema si nzuri kwa nyakati hizi za lockdown maana usafiri haukuwa wa uhakika.

Tulifika saa tatu asubuhi siku inayofuata pale Mbarara kwa kuwa eneo la Ntungamo dereva aliamua tupumzike apunguze uchovu. Tulibaki pale Mbalala kwa saa kadhaa kabla ya kupata gari dogo liliokuwa likielekea Mtukula. Kwa saa mbili na kidogo tu tayari tukawa tumefika Mtukula upande wa Uganda. Na baada ya kusoma mazingira na kutembeza dola hatimaye tukavuka kuingia upande wa Tz, vitenge vyangu walikaba koo lakini nililipa kiasi na vingine nililipa mifukoni wa maafisa forodha nikapita.

“Jamaal hajui kupiganisha border, uko unatumia faranga nyingi kupita..” aliniambia Bosio maana aliona kila kitu.

Nikamjibu kwa mazingira niliyokuwa nayo sikuwa na uchaguzi wala muda wa kuongea sana maana nimechoka nahitaji kufika kwetu.

Ilibidi tutafute sehemu ya kupata chakula na kujimwagia maji, maamuzi yakawa kwenda ku ‘check in’ Mamaland Lodge. Kwa zamu tulijimwagia maji na kubadili nguo na tukawa wasafi. Nilimwacha Bosio akipumzika hapo na nilirudi centre kuangalia usafiri. Kutoka Mtulula kwenda Bukuba usafiri ulikuwepo wa kutosha hivyo tuli check out na kuelekea Bukoba ambapo tulifika mida ya alasiri. Jumatano tukapanda bus Frester na kufika Dar siku ya pili yake.

===MWISHO===

NB

Hekaheka ziliendelea…

Season II ipo post #90.
 
Attachments

  • rdc0.jpg
    rdc0.jpg
    64.3 KB · Views: 74
  • rdc1.jpg
    rdc1.jpg
    46.9 KB · Views: 78
  • rwa10.jpg
    rwa10.jpg
    47.1 KB · Views: 66
  • rdck.jpg
    rdck.jpg
    20.4 KB · Views: 77
  • retired0.mp4
    9 MB
UTANGULIZI

Maisha baada ya kustaafu huwa yana ‘stress’ nyingi. Kujaribu kupunguza stress hizo nilifungua ‘account’ hii JF ili kujiburudisha na kuburudishwa. Account zangu nyingine JF zina ‘personality’ tofauti kabisa.

Michengesho (decoys) zipo kama kawaida ili kulinda nukta kuunganishwa.

HEKAHEKA UZEENI

Sehemu ya kwanza – KUSTAAFU UTUMISHI WA UMMA SI JAMBO LA GHAFLA.

Katika kazi za utumishi wa umma, wapo wanao staafu wakiwa na miaka arobaini na mitano na kuendelea, mimi nilibahatika kufanya kazi hadi miaka sitini na kustaafu kwa mujibu wa sheria. Kujifunza ‘hakwishi’, kuna karaha zake baada ya kustaafu hususani wakati wa kufuatilia stahiki zako. Angalau siku hizi utaratibu ni mzuri sana usumbufu umepunguwa kwa kiasi kikubwa.

Kwakuwa kustaafu ‘hakukuji’ ghafla, yampasa mtumishi yeyote aliyeajiriwa kuajiandaa na maisha baada ya kustaafu. Tumeshuhudia wengi baada ya kustaafu kuendelea Kwenda eneo la kazi na kukaa kupiga soga nk, hii hutokana na ama kufuatilia mambo yake ama kukosa sehemu muafaka ya Kwenda kwakuwa labda hakujiandaa na mahali ya Kwenda baada ya kustaafu.

Miaka 45 ni mtu mwenye nguvu bado, hivyo anaweza kufanya Maisha yaendelee kwa mtindo mwingine bila kuathirika na kazi alizozioea kazini, vivyo hivyo kwa miaka 50 ama 55 ama 60 na hata 65 bado mtu anaweza kujishughulisha na mambo ambayo yatamfanya asiwe ‘bored’

Mara nyingi kwa watumishi wengi maisha yao baada ya kustaafu huwa ni ya upweke, ‘kupigwa mizinga’ kutoka kwa ndugu na jamaa na usipokuwa makini utajikuta unapata magonjwa ya kisukari na moyo pasipo kutarajia kutokana na mtindo wa maisha utakao kuwa nao.

“…hela ya mafao ya kustaau siyo ya kujengea kaka…!” aliwahi kuniambia mzee mwenzangu mmoja aliyetangulia kustaafu.

“…hiyo hela ni ya kukutunza wewe, ni ya kufurahia maisha yako ya uzeeni hadi siku Mwenyezi Mungu atakapo kuchukuwa…”

“…ndugu na jamaa wengi watakuletea shida zao, sisemi usiwasaidie, lakini saidia kwa kiasi tu ili usiharibu fungu lako wala uhusiano wako na ndugu na jamaa, ikiwezekana tangaza hali mbaya ya uchumi kabisa ili wasiweke dhana kwamba una hela, singizia chochote kuepusha usumbufu, mwenzako yamenikuta sana…” Ni maneno yamzee mwenzangu mwingine ambaye yeye alitangulia kustaafu pia.

Sentesi ya ‘hela ya kustaafu ni ya kufurahia maisha..’ ndiyo iliyonifanya nianze kuandika simulizi hii.

Kama nilivyoserma awali, kwakuwa kustaafu ‘hakukuji’ ghafla yapaswa kujiandaa kwa kuwa na miradi midogo midogo wakati ukiwa bado katika utumishi. Hii ni kwa wote, watumishi wa umma na wa sekta binafsi. Anzisha mradi wowote wenye kukuingizia kipato hata kama ni kidogo ili mradi kiweze kukidhi mshahara wa anayesimamia, kutunza mtaji, kukuza mtaji na kujipatia faida kidogo. Hapa nazungumzia wale ambao kima chao cha mshahara ni cha chini. Kwa wale wenye vima vya juu nawashauri wafikirie kufanya miradi mikubwa yenye kuleta ajira kwa vijana na kutopeleka hela nje ya nchi, wekezeni humu humu nchini hiyo miradi yenu mikubwa kwa maana mzunguko wa fedha hizo zitabaki ndani. Sisemi msiwekeze nje ya nchi lakini nasema msisahau kuwekeza ndani kuwasaidia hawa vijana wetu wanaomaliza masomo yao kila mwaka.

Hebu niache haya mambo ya ushauri-nasihi usio rasmi maana kila mtu anajipangia mambo yake mwenyewe, lakini usisahau pia kuishi na mkeo / mmeo vizuri maana ukitangulia kustaafu kabla ya mwenza wako na haukuwa unaishi naye katika mahaba tarajia ‘stress’ za vijimambo vidogovidogo tu ambapo sasa vitakusanyika na kuwa kero.

nijikite sasa kwenye hii sentesi …”..hela baada ya kustaafu ni za kufurahia Maisha…”

Wakati na mbwela-mbwela kusubiria ‘fuba’ la mkupuo si nikapata mkataba fulani hivi kusaidia mambo fulani nchini DRC!. Ulikuwa ni mchongo wa miezi mitatu. Namshukuru sana yule jamaa aliyeniunganisha maana alikuwa anajuwa uwezo wangu katika fani ile kuhusiana na mchongo huo.

‘Paapu’, nikaambiwa niripoti Goma – Kivu ya kaskazini DRC tarehe fulani. Nikajiangalia mfukoni nikaona kuchukuwa flight hakunifai.

“…bora nipande basi kwa kuwahi wiki moja kabla ya tarehe husika…” nilijisemea moyoni.

Wakati huo Stendi ya Mbezi, “Magufuli Bus Terminal” ilikuwa bado haijaanza kutumika, hivyo nikatinga Ubungo bus terminal kuangalia usafiri maridhawa. Nilikuta kuna basi mbili za kampuni moja ambayo niliambiwa ni wazuri kwenye huduma ambazo zote zilikuwa zinaenda Kigali. Nikakata tiketi ya basi kubwa kama walivyokuwa wakiita wenyewe.

Kwakuwa huwa napenda kuona mbele ya basi kwenye lami, nilichaguwa siti ya nyuma ya dereva siyo upande wa dirishani lakini ingawaje palikuwa bado hapajachukuliwa. Sababu nyingine iliyonifanya kuchukuwa nafasi hiyo nili ile nafasi kati ya dereva na siti nyuma yake ni kubwa pa kuweza kunyoosha miguu na pia kuna kama meza fulani hivi mbele (fridge) hivyo kufanya paonekane ni sehemu muafaka kwangu kwa safari ndefu kama ile.

Siku ya safari nikafika mapema sana Ubungo bus terminal, moja kwa moja kwenye eneo ambalo basi husika lilikuwa linapakilia abiria, nilikuta baadhi ya abiria wakiwa tayari ndani ya basi ingawaje nilifika takribani nusu saa hivi kabla ya safari. Sikuwa na mizigo bali backpack Fulani hivi kubwa kiasi ambayo iliweza kubeba laptop yangu pamoja na nguo zangu chache ambazo nilidhani kwa kazi ya siku 90 ningeweza ‘kupiganisha’ bila kuhisi sina nguo za kubadilisha.

Kampuni ya basi ilikuwa inaitwa ‘utatu mtakatifu’, kwa kweli basi nililopanda walijitahidi sana kufanya liwe na hadhi yake mle ndani, viti vyenye vitambaa vya ngozi (synthentic leather), nafasi kubwa kati ya siti na siti, ila kwenye lugha za kuhudumia wateja walikuwa wanafeli sana, sijui ni kwa sababu ya kutojuwa Kiswahili vizuri ama nini. Hakika kwenye hili walikuwa wanafeli, siku hiyo kulikuwa na madereva wawili, mmoja Mtanzania na wa pili ni Mnyarwanda, na mhudumu tuliye safiri naye mmoja mwanume na mwingine ambaye alishukia njiani alikuwa ni wakala wao, akisindikiza gari.

Nilitulia kwenye kiti vizuri huku basi likiwa limekaribia kujaa kabisa abiria lakini kwenye kiti changu bado hapakuwa na abiria aliyekuja. Shingo nikiwa nimeinua juu kidogo kuangalia kwaya walizoweka kwenye runinga ya basi pale mbele mara nikasikia sauti ikiniambia…

“Excuse me, let me pass that is my seat..” alikuwa ni binti mrembo na kwa sura ile moja kwa moja nikajuwa huyu ni Mnyarwanda.

Nikampisha bila kusema neno, na alipokuwa ameketi sasa ikanibidi siti nibonyeze sehemu ili kuongeza nafasi ili tuenee vizuri maana si kwa ma ‘hips’ yale.

“Hujambo?” nilimsalimia na akaitikia kwa kichwa huku akiendelea na mambo yake mara kashika hiki mara kashika kile ili mradi alikuwa hatulii kama ana wasiwasi fulani hivi kama vile kuna jambo halijakamilika.

Macho nikarudisha kwenye runinga kuendelea kuburudika na kwaya za kisabato, ‘what a beautiful melody!’

Punde si punde mlango wa basi ukafungwa na tukawa kwenye foleni ya kutoka nje ya bus terminal. Ajabu ni kwamba vurugu za mabasi kugombania kutoka nje ya geti zilikuwepo licha ya utaratibu mzuri ambao uliwekwa na uongozi wa kituo na kusimamiwa na askari.

Baada ya chekecha chekecha ya hapa na pale hatimaye tukawa kwenye mstari ulionyooka sasa wa kutoka nje. Nikageuza shingo kuangalia nyuma, hakika basi lilikuwa limejaa na hakukuwa na mtu aliyesimama zaidi ya mhudumu mmoja na Yule msindikizaji ambao wote walisimama pale mlangoni, wakati huo tayari yule wakala msindikizaji alikuwa amesha maliza mambo ya ushuru wa getini nk.

===

Safari iliendelea hadi maeneo ya Mbezi Luis ambapo yule msindikizaji alikuwa ameshakamiliza zoezi lake la kukabidhi kila abiria tiketi ya mashine ingawaje tulikuwa na zile tiketi za karatasi. Tiketi hizi za mashine (POS) hazikuwa hizi zilizounganishwa na mifumo ya LATRA na TRA bali zilikuwa kwa ajili ya udhibiti wa kiofisi yao tu.

Niliangalia begi langu kwa mara nyingine, nikajiridhisha lipo salama haliwezi kumuangukia abiria wa jirani maana nililiweka kwenye kibebeo (carrier) cha upande wa kushoto wakati mimi nipo siti za upande wa kulia ili niweze kuliona muda wowote ninapotaka ingawaje watu wengine hupenda kuweka upande huo huo alipo kaa yeye tena juu sehemu aliyokaa.

Safari iliendelea, wakati huo video ilikuwa imezimwa na kufunguliwa radio (RFA) tukiendelea kupata habari. Kwenye hili la kelele za miziki, video za ndani ya basi walikuwa wamefanikiwa, maana hawakuwa wakifungulia kwa sauti za juu, ilikuwa sauti ya kadri tu ambapo hata ukiongea na simu kwa sauti ya chini bado mtasikilizana.

Basi lilitembea mwendo wa Serikali, ‘tatu bila, tano bila nane bila’ hadi tulivyofika Chalinze na misafara ya mabasi kuongozana na kukimbizana ikapungua na mabasi kuanza kumwaga moto. Kutoka Mbezi hadi Chalinze nadhani siku hiyo kulikuwa na fatiki kabambe ya ‘traffic police’ kwa maagizo ya kamanda wa wakati huo, maana kabla ya safari kulisikika tangazo pale Ubungo bus terminal kuwa madereva wote wakusanyike sehemu husika kwa ajili ya kuongea na Kamanda (alitajwa). Nadhani semina fupi ile iliwaingia hadi Chalinze tu, sijui madereva wa mabasi wana matatizo gani, kha!

Basi lilikuwa ni YUTONG, sijui namba ngapi ngapi lakini wenyewe wanasema ndio kubwa katika mfululizo wa wakati huo. Huko mbele ya safari ndio nikajuwa maana niliona ilivyokuwa inafunguka. Licha ya kuchezewa vts lakini pia nahisi ‘limiter’ ya spidi pia ilichezewa, si kwa mwendo ule baada ya kuvuka Rusumo border.

Chalinze hadi Moro basi lilitembea lakini ile kibongo bongo, minara ilikuwa inafanya kazi maana yule mhudumu muda wote alikuwa na simu sikioni na mkono mmoja ameweka juu ya dashboard, mara anapiga dashboard mara anainua kama vile anaita yani alikuwa anapata taarifa nje ya basi na yeye alifikisha ujumbe kwa dereva kwa kupiga dashboard, kuinua kiganja na kuita kwa kiganja.

Mwendo haukuwa hatarishi kiasi cha kuripoti kwa askari waliokuwa akiuliza sehemu za ukaguzi na dereva wala hakuwa mchafuzi wa overtake za ‘kubeti’ ila kwenye mwendokasi sehemu za hamsini hadi tulivyofika mbele kidogo ya Singida. Huko ilikuwa muda mwingi ni over 90kph.

Kabla ya kufika Morogoro, jirani yangu ambaye katika simulizi hii nitampa jina la Janeth, alikuwa ametulia, maana muda wote tangia Dar alikuwa kwenye simu akiongea mara akiandika jumbe za simu. Nikaanza kumsemesha sasa kwa Kiswahili ili kujuwa uwezo wake katika lugha hii adhimu, alikuwa anajibu kwa tabu sana ingawaje alifinyanga finyanga tukawa tunaelewana.

Kwa haraka haraka kutokana na maongezi ndani ya basi, nikajuwa mle ndani kuna Wabongo, Wanyarwanda, Warundi, Wakongo, wa Uganda na Wakenya. Pia kulikuwa kuna watu weupe wawili mmoja akiwa mwanamme, sijui ni Wazungu au Wamarekani lakini hawakuwa Waasia.

Janeth hakuwa mweupe wa rangi, bali maji ya kunde na aling’aa vyema kama ngozi yake ilivyokuwa ikionesha, alivaa ‘tracksuit’ na raba kama vile alikuwa ametoka kufanya mazoezi, nywele alisokota rasta bila kuunganisha nywele za bandia. Hakunizidi urefu, mana pale Chalinze tulipokuwa tunakunywa chai tuliteremka pamoja na kutembea pamoja kabla hatujaachana njia mimi nikielekea maliwatoni upande wa wanaume.

Kwakuwa mimi ni mpenda chai ya maziwa yenye kahawa, basi nilienda upade ule kwenye huduma hiyo na yeye Janeth wa sikumuona tena alipoelekea.

Kwenye jambo hili la kuwapa muda wa kutosha abiria wakati wa chakula, hawa jamaa nao walifaulu vizuri, maana mhudumu alipotangaza alisema tutatumia nusu saa kuchimba dawa pamoja na kupata chochote, tuzingatie namba ya basi maana yalikuwa mawili, baadaye sana ndio nikajuwa kuwa moja litaelekea Uganda na lile tulilopanda ndio litaelekea Kigali.

Kwakuwa siti yangu ilikuwa jirani na sikuwa nakaa dirishani, niliingia wa mwisho mwisho kwenye basi na kumkuta Janeth akiendelea kula nyama za kuchoma alizofungiwa kwenye bahasha fulani hivi ya khaki.

“Welcome nyama choma…” alinikaribisha huku akimaanisha nichukuwe msongo mmoja niendelee nao…

“Aaah, ahsante sana, unaitwa nani?” nilijibu huku moyoni nikikataa kuchukuwa nyama kwa ishara ya kuonesha nimetosheka (nimeshiba)

“Yaleyale ya kupewa chakula na usiyemjuwa wala kuona chakula kilipotoka mwisho wa siku unajikuta umeshaibiwa…” niliwaza.

Nikatoa ‘chewing gum’ za ‘mint’ na kuanza kutafuna ili kuweka kinywa changu katika hali ya kuanzisha maongezi ya kisafari safari.

“Karibu bublish…” nilinyoosha mkono na kumpatia kadhaa na akapokea kimya kimya na kuzihifadhi kwenye kimfuko kidogo kilichopo kwenye lile friji mbele ya siti zetu huku akiendelea kutafuna minofu ya mishikaki ya ng’ombe.

Safari ikaanza tena tukiitafuta mizani ya Mikese, mwendo mzuri, nane bila na uchafuzi wa speed kiasi maana dashboard nilikuwa naiona lakini ilikuwa haizidi 89kph. Pila nilikuwa na Garmin Drive 52 iliyoipata katika harakati za kutafuta ugali ambapo katika safari hii nilitarajia itanisaidia kule niendako ambako sikuwa na uhakika wa coverage ya internet.

Kelele za king’amuzi (vts) kilikuwa almost muda wote alipokuwa zaidi ya 85kph kinasikika kwa mbali sana, sijui waliweka kitu gani wale jamaa, maana kama sio mjuzi wala huwezi kuelewa ni kitu gani kinaendelea, dereva huyu Mtanzania alikuwa na nidhamu ya michoro ya makatazo ya kuovateki ila alikuwa ana ‘maintain maximum’ ya Latra muda mwingi, hii ilifanya tusiwe nje ya muda wa ratiba ya gari.

Janeth mkononi alikuwa amevaa kitu mama shanga hivi maarufu kama “culture” lakini ilikuwa na bendera ya Kenya.

“Wewe ni mkenya?” nilimuuliza huku nikiutolea macho mkono wake wa kushoto ambao ndio alikuwa amevaa hiyo shanga.

“No, Mnyrwanda” alijibu huku akitabasamu.

Nikachukuwa smartphone yangu, nikafungua playstore ili nidownload dictionary ya English – Kinyarwanda lakini haikunisaidia sana maana wakati huo bado haikuwa na maneno mengi.

“Do you speak English” nilimuuliza tena ili kama vipi tuhamier kwenye Kiingereza maana Kiswahili chake kilikuwa hakieleweki.

“Kidogo…” alijibu kisha akaendelea … “French and Kinyarwanda okay...”

Katika harakati za maisha sikubahatika kujifunza Kifaransa, bali niliyajuwa maneno machache sana maana rafiki yangu wa zamani sana, mototo wa Kihindi aitwaye Raani alinipatia kamusi ya Kifaransa kwa kiingereza lakini wala sikuwa na mzuka. Raani binti yule wa Kihindi urafiki wetu haukudumu kwa sababu ya Sue mototo wa Kispaniola ambaye naye pia wala hatukufika mbali, maana baada ya chuo tu miezi ishirini hivi baadaye mawasiliano yalikatika.

Alivyojibu kuwa kwenye Kifaransa na Kinyarwanda ndio yuko vizuri, basi sikuwa na chaguo lingine zaidi ya kuvumilia Kiswahili chake na kiingereza chake ingawaje kwenye kiingereza alikuwa yuko vizuri zaidi kuliko Kiswahili.

Hili ni jambo lingine la kushangaza, yani ukitoka Bongo kwenda Rwanda, hapo Rwanda wenyeji wanazungumza kilugha chao tu na Kifaransa, siyo wengi wazungumzao kiigereza. Ila ukivuka Rwanda kwenda Congo DR huko utakutana na Kiswahili cha aina yake, lakini angalau watu wanaelewana.

Kigali haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda, lakini huko Goma ndiyo ilikuwa ‘fisrt time’. Niliuchangamkia huo mchongo ingawaje Hamida alinikataza nisiende kwa kuhofia hatari iliyopo ya vita baina ya majeshi ya Serikali na watu wanaojiita waasi.

“The first time when I saw you, I knew for sure you are Mnyarwanda…” nilisema.

“Why?” aliniuliza.

Hapo ndipo nikafunguka kuhusu jinsi sisi Wabongo tunavyowaona Wanyarwada. Nilimwambia kuhusu maumbile yao ya urefu, sura nyembamba, urembo wa asili, nyama za kutosha sehemu ambazo huwafanya wanaume wageuke nyuma kuangalia ili kuburudisha macho, nikaeleza weee mwishoe naye akaniambia kuwa hiyo dhani si asilimia mia sahihi, siyo Wanyarwanda wote warembo kama nilivyowapamba…

Eeee ni kweli nilimpamba sana ‘mixer’ ukweli na chumvi ili kuwasifia kama ilivyo kawaida ya wanaume.

Kwakuwa Rwanda haikuwa mara yangu ya kwanza kwenda, nilikuwa najuwa hawa warembo tunaowaona kwenye mitandao ni wachache tu, wanawake wa Kinyarwanda wapo kwa maumbile mbalimbali na sura tofauti wengi ni wa kawaida sana na tofauti kabisa na tunao waona hawa wa kwenye mitandao. Hata hivyo haiondoi ukweli kwamba wapo wanawake warembo wa sura na maumbile huko Rwanda. Tabia zao tu ndio zina ukakasi kiasi fulani juu ya kujiona wapo matawi ya juu sana, kuwa na ukatili uliojificha labda kutokana na historia yao nk.

“…Lakini sasa mbona umevaa bendera ya Kenya?” nilidadisi.

Hapa akafunguka kuwa yeye ni mfanyabiashara, ana duka la nguo za wanawake kwao Kigali na kabla hajajuwa machimbo ya Tanzania alikuwa akifungia mizigo yake Uganda na Kenya, na hiyo ‘bracelet’ aliyovaa aliipatia Kenya…

Mazungumzo ya kawaida yaliendelea kama ilivyo kawaida kwa abiria na abiria. Safari nayo ilisonga salama kabisa hadi tukafika Dodoma pale jirani na panapoitwa ‘four ways’, tukawa na ‘short break’ ya dakika kumi ya ajili ya kuchimba dawa kisha safari iliendelea hadi Singida baada ya mizani mbelembele kidogo gari ikaingia sehemu fulani kuna hoteli ambapo napo tulipata dakika ishirini za kuchimba dawa na kupata chochote kisha safari ikaendelea. Tulipokaribika Igunga giza fulani hivi lilianza kuingia, hadi tunapita mzunguko wa Nzega pale tayari dereva yuleyule tuliyetokanaye Dar akiwa anaendesha hadi muda huo aliwasha taa hafifu zilizowaka kwenye sakafu ya basi pembeni pembeni na kufanya mandhari kuwa nzuri sana ndani ya basi.

Awali nilidhani basi litanyoosha moja kwa moja hadi border ya Rusumo lakini kumbe hayapitilizi bali wanalala Kahama kisha asubuhi na mapema safari huendelea hadi boda.

“Have you made your reservation to pass your night at Kahama…” Janeth aliniuliza wakati gari ikiwa inakunja Tinde kuelekea Isaka.

Nilimjibu kuwa sijafanya chochote, si nitalala ndani ya basi!

“Please don’t sleep in the bus, you will get tired, and you won’t enjoy your looong journet from there to Kigali, its tiresome…” alisema Janeth na alikuwa anamaanisha. Nilijua hivyo siku ya pili baada ya kufika Rusumo.

“I don’t have enough cash with me…” nilitaka kujitetea akanikatisha…

“Don’t worry, I will pay for you and you will refund me when we reach border or Kigali…”

Sikumwambia kuwa mie pale mpita njia tu naelekea DRC. Nadhani alidhani namie ni mmoja wa wanaoelekea kwenye “sabasaba yao” (trade fair) maana tarehe hizo kulikuwa na maonesho ya kibiashara hapo Kigali iliyoanza kama siku mbili zilizopita na inayotarajiwa kuwepo kwa siku kadhaa zijazo.

“Why spend a lot of money! We can share the room…” nilichombeza huku nikiwa simaanishi.

“…Really!?” alihoji

“Why not!” nikajikuta tu neno limenitoka.

Mazungumzo yaliendelea na akaniambia yeye hufikia Gaprena Hotel. Nikatafuta review ya hotel hiyo harakaharaka kwenye simu nikaona ni zile wanazoita hotel kumbe ni lodge tu iliyochangamka. Anyway, ni Hotel. Sifa kuu aliniambia kuwa pako salama na ni karibu na stendi kuu pia gharama ni ndogo kulinganisha na hadhi ya hoteli yenyewe. Mimi wakati huo nimeshasoma review kadhaa na kupata picha halisi ya sehemu anayotarajia kufikia.

Tukaingia mizani Kahama na baada ya kutoka hapo mhudumu alitutangazia ratiba ya gari na kutupatia elimu maelekezo na tahadhari. Moja ya maelekezo aliyotoa ni kwamba basi halitoendelea na safri hadi kesho saa kumi na mbili asubuhi, hivyo anashauri abiria watafute lodge za kupumzika kwa watakaopenda kufanya hizo, na wale watakao amua kulala ndani ya basi wawe makini na mizigo yao ya ndani ya basi maana ulinzi wa mali iliyo ndani ya basi ni wa abiria husika.

“Muwe makini na mutu mugeni yanakuja ndani ya basi, hakuna abiria naingia usiku huu…” alimalizia yule mhudumu na Kiswahili chake kibovu.

Gari ikakunja kulia moja kwa moja hadi stendi kuu. Stendi ilikuwa imechangamka sana na ilikuwa ni majira ya saa tatu hivi usiku. Watu wengi, wauza vyakula mama lishe wengi huku wakikaribisha wateja, wapiga debe wa lodge pia wengi wakijitahidi kutafuta wateja, hakika Kahama palikuwa pamechangamka sana.

Wahudumu wa basi tulikuwa nao safarini wote waliondoka akaja wakala mkazi wa hapo ambaye alikuwa akisimamia ‘shoo’ bila shaka na walinzi wao pia walikuwepo ingawaje sikuwaona mara moja.

Abiria walikuwa wanajivuta sana kushuka mimi na Janeth tukiwemo. Nusu saa baadaye tuliamua kutembea kuelekea hoteli ambayo abiria mwenzangu alikuwa ameweka nafasi. Bajaj, tax na bodaboda zilikuwepo, lakini tuliamua kunyoosha miguu baada ya safari ndefu.

Tulivyofika pale mapokezi tulikaribishwa kwa bashasha lakini ‘walinikata maini’ nilipoulizia kama kuna chumba…

“Ishi, kwani hampo pamoja!...” aling’aka yule mhudumu

“Vyumba vyote vimejaa, basi ngoja nikupeleke hoteli ya jirani na hapa, pale unaweza kupata ila bei ipo juu kidogo…” aliongea yule mhudumu kwa lafudhi ya kisukuma.

Janeth akaingilia kati…

“Lets share as you said, no problem… are you going to swallow me!?”

Yani hapa angalau kwenye uandishi inabidi nikinyooshe kidogo hivi vilugha vya watu maana jinsi alivyokuwa akiongea Janeth unaweza ukawa unacheka tu kila mara.

“Well, its okay, lets share the room and I promise will not swallow you…” tukawa tunacheka huku tukielekea chumba husika maana mwenzangu pale inaonekana ni mwenyeji.

======

INAENDELEA…

View attachment 2540333View attachment 2540338View attachment 2540341
Uzi mzuri sana ila mzee mwenzangu una heka heka sana wewe .

Haya wacha niendelee kujiandaa maana ni miezi minne tu nitaachia ofisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom