Ilikuwa siku ya jumatano usiku , mishale ya saa 6 hivi usiku , niko zangu sehemu na rafiki zangu kadhaa , ghafla nikapata simu natakiwa niangalie email zangu kuna ujumbe wa kujibu hapo hapo , nikaamua kutafuta internet café ya jirani na hapo .
Nikapata café moja , kwa taarifa yako kuna café mbazo zinafungwa milango lakini taa zinawaka ndani hapa kinondoni na baadhi ya maeneo ya ilala , kariakoo na mwananyamala , ukienda katika hizo café usiku huo utakutana na watu wa ajabu ajabu lakini wengi ni vijana wanafanya kazi zao
Nikapata sehemu ya kukaa , ilipofunguka hiyo computer nikakuta mtu aliyekaa kabla yangu ni mwanamke na alikuwa anachat katika chatmoja inaitwa darhotwire , jambo na darchat kwa mpigo , kufungua hizo chat nikakuta kumbe aliongea na kijana mwingine ambaye naye alikuwa yuko nyumbani kwao wakapeana namba yule kijana akamwambia atamfuata kinondoni .
Na hii ndio aina mpya ya maisha kwa baadhi ya watu haswa wale wanaouza miili yao anangoja muda wa usiku hata mchana anaenda internet café anajipachika jina nzuri anasema yuko nyumbani au anajiita mwanafunzi ametoroka shule wanaume wanajichanganya wanamtaka anawakubali wanamalizana juu kwa juu
Internet café hizi ziko nyingi kama nilivyosema , na hawa wasichana hawalipi karo ya kutumia internet wakati huo wanalipa kesho yake akishapewa posho na mtu ambaye amekubaliana nao wakati huo , ndio maana ukikutana na mwanadada katika mtandao akasema anajiuza uwe makini sana
Kuna wengine ni ukweli kabisa wanajiuza hiyo sio siri , na wengi wanajigeuza kujifanya yeye mwanafunzi wa chuo Fulani au sekondari Fulani ili kuwavuta watu zaidi na ili hata wewe ambaye unamchukuwa uwe a wasi wasi lakini usiweze kumiliki ufikiri ni mwanafunzi si unajua wanafunzi wako chini ya wazazi au walezi wao ?
Kwahiyo hata siku ukimkuta na mwanaume mwingine anaweza kusema kaka yake au mwanafunzi mwenzake wewe utafanya nini ? na ninajua vijana wengi siku hizi wako bize hawana muda wa kumfuatilia na kumjua mwanamke au mwanaume anayemtaka yeye anaingia tu kichwa kichwa mpaka mwishoni anakuja kushituka ameshaliwa .
Na vijana wengi wanaathirika sana na magonjwa haswa ukimwi kwa njia hii kwa sababu ya kukutana na watu waongo wanaotumia mitandao kujifucha ukweli wao , wazazi angalieni sana watoto wetu wanavyochat na kukutana na watu kadha wa kadha adhari zake na mambo mengine yanayotokea katika hii dunia ya sasa
Kuna umuhimu wa hizi internet café kupitiwa upya kuangaliwa mambo wanayoyafanya haswa nyakati za usiku , kama sio kufanya biashara hizi za kuuza wasichana wengine wanashikiri katika kudurufu miziki haswa ya nyumbani , nilishangaa siku moja nimeingia
www.aresgalaxy.org na kukuta kuna top10 bongo flava za kitanzania mtu anazo katika computer yake hapo kinondoni na hana wasi wasi .
Wengine wanatumia mida hiyo kufanya mipango yao mengine ya kihalifu kama unavyojua , usiku huku miji mingi haswa marekani ni asubuhi au mchana kule wanaamka na wanafanya kazi ni rahisi zaidi kwa vijana kuingia net huku wakaanza kudanganyana na watu wa ulaya kupata ulaji na fadhila zingine .
La mwisho zaidi tembelea
www.youtube.com tafuta mfano bongoflava utakuta miziki kibao ya vijana wetu mengine imewekewa hati miliki na kampuni ambazo mimi zijawahi kuzisikia hapo bongo kwa shuguli za utengenezaji wa video hata muziki lakini katika mtandao unazikuta
Ndio maendeleo hayo au sio ?