Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 234
Siku moja nilikuwa katika ofisi fulani nataka kufanya kazi, kabla sijaanza ile kazi, dada moja wa office ile akaniambia kwamba anayetumia office hiyo ni muadhirika wa UKIMWI, angalia vizuri sana hapo mezani unavyofanya kazi na kushugulika, ni kweli nilishangaa yule jamaa ni kigogo lakini ana viwembe mezani kwake, kuna pini ameziweka tu bila mpango na mambo mengine ambayo ukigusa unaweza kuchomwa na kuweza kuambikizwa labda
Kuona vile sikuendelea kufanya ile shuguli, nilimwomba huyu mama abebe mzigo wake aulete kazini kwangu kwa pale ni ngumu kuendelea nayo kwa sababu ni mtu ambaye ninatembea na kuzunguka naweza kujisahau na kushika vitu vyake alinikubalia
Kwa hiyo hii ndio jamii ya watu tuliokuwa nao katika jamii yetu wameadhirika na ugonjwa Fulani lakini, anaweka mitego au chambo kwa wenzake waingie katika mambo yake ambayo kwa kweli hayavutii mbele ya jamii iliyostarabika hata kidogo hata kama anacheo gani
Huo ni ukumbusho tu -- KUMBUKA KWAMBA
Tarehe 1 Desemba kila mwaka ni siku ya UKIMWI duniani, siku hiyo watu mbalimbali hukumbushana na kuelimishana kuhusu Ugonjwa wa UKIMWI na kushirikiana katika mambo mengi ambayo nia yake au malengo yake ni kupunguza maambukizo ya UKIMWI sio kuzuia, kuzuia ni ngumu kwa sababu watu wengi wameshaadhirika na wengi wao wamejificha majumbani, maofisini, mashuleni, vyuoni na sehemu zingine nyingi sana ndio maana tunaongelea kupunguza na sio kuzuia.
Kuzuia maambukizi ya UKIMWI au ugonjwa wowote wa zinaa ugumu wake unakuja kuwa ngumu kwa sababu ni jukumu la mtu binafsi ( personal ) yeye mwenyewe ajizuie sio wewe umwambie aache , na mbaya zaidi watu wengi wanaoambukiza au kuambukizwa ukimwi ni watu wenye akili timamu na wengi wao wanajijua wameadhirika na kuendelea kuambukiza wengine na wengine kadri ya siku zinavyozidi kwenda
Kwa upande wa wale watu wenye kipato kidogo wao hawana wasiwasi , si ARV ziko ? kwahiyo atafanya anachojua yeye akiadhirika anapesa kidogo, za kuweza kuzitumia anunue hizo dawa za kuongeza nguvu na mambo kama hayo pamoja na madawa mengine mengi ambayo masikini wa kawaida sio rahisi apata, I wish kungekuwa hakuna ARV watu wengi wangeona hali halisi ya mtu anayeadhirika yukoje inakuwaje .
Wengi wameadhirika tunatembea nao njiani , wamependeza , wanavutia , wana furaha na mambo mengine mazuri lakini siri wanazijua wao wenyewe kwa hapa Tanzania hakuna mtandao maalumu wa kuwaweka wazi watu wanaosumbuliwa au walioadhirika na ukimwi , mfano USA kuna website maalumu yenye majina ya wagonjwa wote wa ukimwi kwahiyo unaweza katika tovuti ya serikali na kuangalia majina halisi na mahala wanapoishi waadhirika.
Hali hiyo na ujuzi huo umesaidia kupunguza maambukizi na kuzuia kabisa maambikizi kwa baadhi ya watu na jamii zingine , kila mtu sasa najua nani ameadhirika na anakuwa makini katika mahusiano yake na maisha yake ya kawaida bila hofu bila hiyana yoyote .
Wakati hapa naendelea kuandika , kuna mambo nafikiria kuhusu aina za jamii ambazo ziko hapa duniani kuhusu huu ugonjwa wa ukimwi , MWINGINE ATASEMA AHH NAJUA KUNA UKIMWI KWAHIYO ?? , HUYU NAE ATAKUJA NA LAKE , NAJUA UPO NA NINATUMIA KONDOM , MPENZI WAKE NAYE ANASEMA AHH BWANA MIMI NAMWAMINI MPENZI WANGU , MZAZI WAKE ANASEMA MIMI NIMEKUWA NA MKE WANGU KWA MUDA MREFU KWAHIYO SIWEZI KUADHIRIKA , NA MTOTO WAKE NAYE ATASEMA SIKU HIZI KUNA ARV NIKIPATA UKIMWI NTATUMIA ARV NIISHI MUDA MREFU .
Vituko kibao na majigambo kibao ambayo hayana msingi wala maana ukifikiria kwa umakini zaidi , lakini yote tisa , la kumi na mwisho ni mtu kujua kwamba ukimwi upo , utaendelea kuwepo na kusambaa zaidi kama hujaadhirika basi rafiki yako ameadhirika , ndugu yako , mpenzi wangu au jirani yako , mfanyakazi mwenzako na watu wengine ambao huwa unakutana nao mitaani au sehemu za mihangaiko yako .
Inahitajika jitihada za dhati na za uhakika kuweza kupunguza na kufanya ugonjwa wa ukimwi historia na usiendelee kuuwa na kuambukiza ndugu zetu na jamaa zetu wengine wa karibu , hawa tunawapenda , wengine ndio wametusomesha mpaka kufikia hapa tulipo , wengine wanatufundisha mashuleni , wengine tunashirikiana nao katika mambo kadhaa , tunaenda kuendelea kushirikiana nao kwa vitu vingi zaidi ili kujenga jamii na taifa lililo kuu na lisilo na wagonjwa wa UKIMWI .
UKIMWI UPO , UTAENDELEA KUWEPO , KUANGAMIZA WATU NA KULETA MADHARA KATIKA JAMII NYINGI , DUNIANI , NA WEWE NI TARGET YA UKIMWI , LAKINI UNAWEZA KUUKWEPA USILENGWE NJIA ZINAJULIKANA NA ZIKO WAZI KABISA .