azithromycim
JF-Expert Member
- Apr 18, 2019
- 577
- 1,287
Ukimwi bado ni janga la afya ya jamii linalosumbua dunia, hasa katika nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania.
Kulingana na Utafiti wa Hali ya Ukimwi Tanzania (Tanzania HIV Impact Survey - THIS 2022-2023), kiwango cha maambukizi (prevalence) cha Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa Tanzania Bara ni 4.5%.
Hii inaashiria kuwa maambukizi mapya bado yapo na jitihada za ziada zinahitajika mafano huduma za dawa kinga (prophylaxis) zimeanzishwa na kusambazwa katika vituo mbalimbali vya huduma za afya nchini ili kusaidi kufikia lengo la Tanzania bila ukimwi
Dawa kinga (Prophylaxis) ni matibabu ya kidawa anayopewa mtu kabla au mara baada ya kukutana na hatari ya kupata maambukizi ili kuzuia virusi visiingie au kushambulia mwili
Nchini Tanzania, kuna aina mbili kuu za dawa kinga zinazotumika.
1. PrEP (Pre-Exposure Prophylaxis)
Tafsiri: Dawa kinga kabla ya kukutana na hatari ya maambukizi ya VVU.
Dawa hizi zimeletwa kwa ajili ya kuwasaidia makundi yaliyo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi makundi hayo yanajulikana kama key vulnerable population.
Ambayo ni
1. Wafanyabiashara ya Ngono (Commercial Sex Workers - CSW), wakiwemo wanawake (Female Sex Workers - FSW) na wanaume waliojiingiza kwenye biashara hiyo
2. Wanaume Wanaofanya Ngono na Wanaume Wenzao (Men who have Sex with Men - MSM).
3. Watu Wanaojidunga Dawa za Kulevya (People Who Inject Drugs - PWID).
4. Wasichana na Wanaume Rika Barehe (Adolescents and Young People).
5. Makundi ya Watu Wanaohamahama (Migrant populations), mfano madereva wa magari ya masafa marefu.
6. Wachumba/Wenza Tofauti Kiasili (Serodiscordant Couples), ambapo mwenza mmoja ana VVU na mwingine hana, na hakuna ushahidi wa kutosha kuwa yule mwenye VVU amefubaza virusi vyake.
7. Wafanyakazi wa Maeneo ya Burudani (mfano wahudumu wa baa) na watu wenye tabia za unywaji pombe kupindukia au wenye wenza zaidi ya mmoja au wanofanyakazi katika mashamba makubwa
Watu katika makundi hayo wanapaswa kucheki afya zao na wakiwa na majibu hasi yaani hawana maambukizi ya virusi vya ukimwi wanastahilikuanza kutumia PrEP.
Kunywa kidonge kimoja kila siku katika muda huohuo bila kuacha mpaka pale atakapojihakikishia kuwa kwasasa hayupo katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi
2. PEP (Post-Exposure Prophylaxis)
Tafsiri: Dawa kinga baada ya kukutana na hatari ya maambukizi ya VVU.
Hutumika kama tiba ya dharura kwa mtu aliyekumbana na hatari ya maambukizi hivi karibuni.
Mfano wa mazingira haya ni:
1. Mtu aliyebakwa au kufanyiwa shambulio la kingono.
2. Mfanyakazi wa afya au raia aliyechomwa na sindano/kitu chenye ncha kali kilichokuwa na damu yenye VVU
3. Mtu aliyefanya ngono zembe au pale ambapo kondomu imepasuka/kutumika vibaya.
Muda wa Matumizi: Lazima ianzishwe mapema iwezekanavyo, ndani ya saa 72 (siku 3) tangu tukio la hatari litokee Baada ya kupima na kukutwa huna VVU, utatumia dawa hizi kwa siku 28 mfululizo.
Tanzania bila Ukimwi inawezekana kabisa. Iwapo unajiona upo kwenye kundi hatarishi au umekumbana na dharura ya kuambukizwa, chukua hatua sasa. Pima afya yako, na ikipatikana huna maambukizi, tumia fursa ya huduma za PrEP au PEP zilizopo katika vituo vya huduma za afya nchini kote bila gharama