Kwenye kupambana na foleni, je sheria hii ni kandamizi au sio kandamizi?

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,074
Foleni ni tatizo linalosumbua wananchi wote tu.

Magari ni mengi.

Wenye uwezo wananunua magari yao.

Magari mengine madogo, mengine makubwa ya familia.

Magari ya usafiri wa umma yanabeba watu 45, 72, mia etc.... wakati huo ya binafsi yanaanzia mmoja hadi kadhaa tu. Lakini yote yanachukua karibu nafasi sawa barabarani na folenini (folenini🤯, kwenye foleni bhanaa)

Sasaaa 🤔 tujitungie muswada wa sheria na sheria ya kwamba: Chombo chochote cha usafiri hakiruhusiwi kupita baadhi ya barabara bila ya kuwa na angalau nusu (au zaidi ya nusu ikipendeza) ya uwezo wake wa kubeba watu (seating capacity) ili kupunguza msongamano.

Ufafanuzi;
1. Mtembea kwa miguu ni level seat - anaruhusiwa popote.
2. Mwenye pikipiki ni aidha yupo peke ake siti 1/2 so anaruhusiwa au amebeba mtu 2/2 level seat naye anaenda popote.
3. Magari ya abiria haya automatically yanajitahidi kujaza hadi watu wanasimama - so yanaruhusiwa
4. Waendesha baiskeli - level seat wanaruhusiwa.
5. Bajaj na bodaboda wenye abiria wanaruhusiwa.
6. Gari binafsi la mzigo, zinaruhusiwa maana zenyewe ni kuhusu bidhaa zaidi kuliko watu.
7. Gari binafsi za kutembelea, ndio hizo zinaruhusiwa kuwa na angalau nusu ya siti zina watu ndio itembee.🤩

Sheria hii itakuwa na faida zifuatazo;
1. Msongamano utapungua
2. Watu watapata lifti kwa urahisi zaidi maana mtu lazima awe na watu kadhaa. So lifti inakuwa ni kusaidiana na utu kwa pande zote mbili✌.
3. Familia zitajipanga vizuri zaidi mitoko yao, itaongeza hata ukaribu na mawasiliano baina yao (harmonization for the journey na mizunguko). Itapunguza hata kiasi matendo ya mafichoni na gizani.
4. Watu wote bila ubinafsi watashiriki kupunguza msongamano, sheria yetu itatuunganisha.
5. Sheria itawabembeleza watu kununua zaidi magari madogo madogo na baiskeli au mapikipiki yale makubwaa ili wavimbe bila bugudha, lakini automatically wanapunguza foleni.
6. Usafiri mwingi ukiwa publicisized kiaina mwisho wa siku utapunguza uchafuzi wa mazingira.
7. Muda ni mali, tutaokoa sana muda.

Sheria ya namna hii itasaidia kuchekewesha uhitaji wa sheria nyingine kali zaidi kama KUPIGA MARUFUKU KABISA USAFIRI BINAFSI kama ilivyo kwa baadhi ya barabara na maeneo ya miji ya mambele huko.

Msiogope sheria sio kandamizi.....

Haitakuwa lazima na wala hatulazimishani kidikteta 100%. Maana pia ma don wapo na watataka kuenjoi magari yao bila bugudha yoyote popote. Basi tunafanya kama tulivyofanya kwenye plate numbers. Anayetaka, analipia kodi kubwa tu (hata 5M hivi) plate number yake inakuwa ya kipekee hata ya bluu anapita popote muda wote hata akiwemo peke yake.

Pia sheria inaweza kuwekewa muda maalumu. Labda saa moja asubuhi hadi saa tano af free 6,7,8 halafu saa kumi hadi saa mbili usiku.... halafu free. Na weekend labda free. Tunaangalia tu zile rush hour au inakuwa mda wote ikipendeza. Jopo litaamua

Maana hivi ndugu wananchi tutaongeza kupanua hizo barabara hadi lini? Mwisho mji wote uwe ni libarabara tu aaargh!

Nawasilisha kwenu wanasheria, je sheria hii inaweza kupita? Imevunja katiba? Sidhani na katiba yenyewe ya kijamaa jamaa hii
 
Hakuna haja ya uanzisha sheria ambayo ufuatliaji katika kuitekeleza itakuwa ni changamoto nyingine. Sijaangazia namna inavyokiuka uhuru na usiri wa wenye vyombo binafsi.

Tuangalie tu namna ya kuboresha miundombinu ya barabara na kuzingatia sheria za matumizi ya barabara na za usalama barabarani.

Mbona wenzetu wameweza. Inawezekana
 
Tuangalie tu namna ya kuboresha miundombinu ya barabara na kuzingatia sheria za matumizi ya barabara na za usalama barabarani
Tukiweka mdahalo na wenye magari, je wao wenyewe kwa umoja hawawezi kuridhia kwa uhuru?

Miundombinu ya barabara mfano upanuzi ina mwisho wake.

Anyway labda niseme kwamba, kama kuna nchi private cars haziruhusiwi kabisa miji fulani..... je? Hii sheria ya kujaza huoni kama ni laini zaidi ukilinganisha na sheria kali ya marufuku ya magari binafsi?
 
Back
Top Bottom