Nilitegemea Jeshi la Polisi lingejikita kwenye bodaboda kuliko ving'ora kwani bodaboda ni wavunjifu wa makusudi wa sheria za usalama barabarani

Mzee wa Twitter

JF-Expert Member
Nov 5, 2023
1,272
2,031
Nimeshangazwa na mkuu wa usalama barabarani akitangaza vita dhidi ya walioweka vimulimuli honi na mataa yenye mwanga mkali.

Binafsi madhara ya vimulimuli honi na mataa yenye mwanga mkali siyaoni kama ni makubwa bali ni madogo sana tofauti na madhara yafanywayo na bodaboda.

Bodaboda wamekuwa kero kubwa kwa maisha ya binadamu kwani bodaboda wamekuwa wanashiriki au kutumika kwenye matukio mengi ya uhalifu ukiwepo wizi, mauaji na kadhalika.

Bodaboda wamekuwa chanzo kikubwa cha ajali nyingi za barabarani na kupelekea vifo na ulemavu wa kudumu.

Bodaboda wamekuwa watu wa kujichukilia sheria mikononi na kuharibu mali za watu kwa mfano hivi majuzi tumeshuhudia wakilichoma moto bus bila kujali chanzo cha ajali ni bodaboda mwenzao au bus.

Katika kikao cha bunge lililopita naibu spika ambaye ni mbunge wa ilala mh.Zungu aliwalaani sana bodaboda na kuwaita bodaboda ni kero kubwa sana"

Pia mh lema aliwahi kusema kazi ya bodaboda ni kazi la laana waliomwelewa kama sisi tunaungana nae kwani matukio ya bodaboda yanatisha sana. Hebu amua tembea pale muhimbili kitengo cha moi kaangalia wagonjwa wa ajali za bodaboda unaweza kuapa kuwa hutapanda tena bodaboda.

Niliombe jeshi la polisi kitengo cha usalama barabara wajikite kipambana na hawa bodaboda wamekuwa vinara wa makosa ya usalama barabarani bodaboda wamekuwa wanapita licha ya taa za kuongoza kuwazuia.

Shame Jeshi la Polisi bodaboda hawawezi kuwa juu ya sheria za nchi.
 
Kah we jamaa
Kuna siku nilitaka kuweka bandiko la kuishauri mamlaka kuajiri vijana watakaokua wanakaa kŵenye makutano ya barabara na fimbo jukumu Lao likiwa ni kuwachapa boda boda maana wamezidi.
😃😃😃
 
Yani BODABODA Daaa!!!

Mtu unakutana nae Leo Mstaarabu kabisa ila Kesho akiwa Bodaboda tu anakua CHIZI sijui hii kazi ina Mdudu gani???
 
Bodaboda imestiri nchi yetu dhidi ya janga la ukosefu wa ajira. Hawa watu ni wengi na ndio kundi la watu wenye nguvu katika jamii (vijana)

Ninao graduates wengi ninaowafahamu nowadays ni bodaboda kutoka kwenye kila fani unayoijua wewe kutoka vyuo tofauti tofauti

Ninachokiona kilichopungua hapo ni swala la kurasimisha hii sekta mfano wawekewe utaratibu maalumu na security kwenye vyombo vyao, bima, na masharti maalumu ya kuwa dereva boda boda haya ni machache kwa kuyaandika

Nchi hii huwa hatuangalii sekta zinazoajiri watu wengi na kuzipa utaratibu maalumu kwanza itakuwa hata chanzo cha mapato cha serikali
 
Mwanga mkali wanasababisha sana ajali usiku hao watu na pia unakuta mtu kaweka mwanga mkali kwenye kagari kama kadogo kibiriti akiwa Road apunguzi mwanga sehemu yeyote..
 
Boda wanahitaji sheria kali mno tatizo ni wanasiasa na uchaguzi
 
Kuna wakati nawaza Bodaboda anavunja sheria na polisi kasimama mbele yake hakuna Hatua anachukiwa inawezekana BIDABODA nyingi ni Miradi ya hao hao POLISI na Wanasiasa na Watumishi wa umma
 
Back
Top Bottom