Mzee wa Twitter
JF-Expert Member
- Nov 5, 2023
- 1,282
- 2,041
Wadau nawasabahi.
Nichukue fursa hii kuchangia kidogo juu ya hili zoezi linaloendelea la jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani la kuyakamata magari yote yenye namba za 3D.
Najaribu kujiuliza kama kutumia namba za 3d ni kosa je aliyezitengeneza na kuziuza mbona hatusikii hatua alizochukuliwa?
Nije kwenye hoja yangu ya msingi, madhara yatokanayo na hizi namba za 3D binafsi nayaona ni madogo sana ukilinganisha na ajali zinazosababishwa na hawa bodaboda.
Hivyo nilitarajia jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wangejikita kupambana na hawa bodaboda ambao wamekuwa ni wavunjifu wa makusudi wa sheria za usalama barabarani na kusababisha vifo na ulemavu wa kudumu kwa wananchi kuliko hili la kukamata na kubandua namba za 3D.
Tunaliomba jeshi la polisi lijikite zaidi kwenye hawa bodaboda kwani wamekuwa kero nchi nzima