BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,377
- 8,121
Pia, Trafiki husimamisha Magari ya Watu binafsi, Malori na Mabasi ya Abiria ili tu Viongozi wanaotoka nyumbani kwao au mafisini wapite bila kujali baadhi ya Magari Binafasi yanaweza kuwa na Wagonjwa au watu wenye haraka pia. Jambo ambalo sio sawa. Misafara mingine huwa haina ulazima wa kusimamisha Magari.
Lakini pia kuna suala la Trafiki kufanya kazi kwa maelekezo ya "Wakubwa" unakuta Kiongozi anatoka Posta Mpya, anasimamisha Magari kutoka Morocco hadi Mwenge ili apite, kusema ukweli sio sawa kabisa. Ifike wakati baadhi ya Viongozi wakuu kama Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Wakuu wa Majeshi au Spika wawe wanatumia Helicopter wakiwa Dar ili kupunguza hiyo misongamano.
Viongozi watambule watu waliowachagua nao wana uhitaji wa muda na uharaka wa mambo yao sio wao tu ndio wenye haki hiyo.