Tanzania limejitokeza tabaka la "wenye nchi" ambao wanaona hawastahili kuendesha gari kwenye foleni na wana haki ya kutofuata sheria za barabarani

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Tumefikia sasa kwamba hapa nchini tuna watumiaji wa barabara wa aina mbili - Watanzania wa kawaida, na Watanzania "wenye nchi" ambao sheria za barabarani haziwahusu.

Hili kundi la "wenye nchi" ni wale ambao hawataki kabisa wabugudhiwe katika kuendesha juu ya spidi inayoruhusiwa, au wakae kwenye foleni wakiwa kwenye magari yao. Kikundi hiki kinatia ndani waendeshaji wa gari za ST, polisi na Usalama wa Taifa. Baadhi yao wamekuwa wakitumia zile namba nyeusi kama sababu ya wao kutaka kutumia barabara kwa namna tofauti na wengine. Na pia utaona wamejipa hizi taa za blue na nyekundu ambazo wanazitumia kujihalalishia ukiukwaji wa sheria barabarani.

Kwa mfano najiuliza, hata kama wewe ni waziri, au kigogo wa serikali, au Usalama wa Taifa, na unaendesha gari kwenda nyumbani, kitu gani kinakufanya wewe uwe na umuhimu zaidi wa kwenda haraka kwa mkeo na watoto wako kuliko Watanzania wengine? Kwani mkeo au watoto wako wana tofauti gani na mke au watoto wangu? Asietaka kufika nyumbani mapema baada ya kazi ni nani?

Nimeona matukio mengi sana ya uendesheshaji wa hatari sana barabarani ambao unafanywa na watu hawa. Kuna wakati nimehusika katika ajali kwa sababu Landcruiser ya STL ilikuwa inaendeshwa kwa kasi usiku upande usio wake, na niliposhika breki baada ya kuiona, gari iliyokuwa nyuma yangu ilinigonga. Hiyo STL iliondoka bila hata kusimama.

Juzi usiku nikitoka kazini niliona watu wa Usalama wa Taifa wakiendesha gari kwa fujo na kuhatarisha watumiaje wengine wa barabara, na waliposimamishwa na trafiki wakaonyesha utambulisho wa kuwa wafanyakazi wa Usalama wa Taifa na kuaruhusiwa waendelee. Dereva aliyekuwa nyuma yao akichukulia advantage iliambiwa aweke gari pembeni. Nina amini kwamba hawa watu walikuwa wakirudi nyumbani na waliendesha kwa fujo hizi kwa sababu hawakuvumilia kuwa kwenye foleni.

Hasa hapa Dar es Salaam, hiki kikundi kinachojiona wao ni wa pekee katika utumiaji wa barabara na wana haki zaidi ya watumiaji wengine, kinazidi kukua kila siku. Kuna siku madhara makubwa yatatokea, na najua yameshatokea, kutokana na hasira za watumiaji wengine barabarani. Kuna siku tutasikia watu wamekufa kwa sababu ya ujinga huu ambao nchi hii inauendekeza. Tunaimba hakuna aliye juu ya sheria lakini ni wazi wale wanaoongoza kutuimbisha wimbo huu wao hili haliwahusu, wanajiona wako juu ya sheria. Tunakoelekea si kuzuri.
 
Haiwezekani kabisa mkuu vieite ni ngoma ingine hata ikiwa nyuma ya usafiri wako unajiskia umpishe tu aende..... Siku moja nilikua road kwenye mataa nimepenya na ka pikipiki kangu nikakaa mbele wakiruhusu nichomoke wakwanza basi nyuma yangu kulikua na LC 100 ila imepimpiwa mbaya nyeusi Full tinted na namba hazieleweki basi nasimama tu naskia mlio wa honi zao zile kapiga mara mbili tu tooooo tooooo akawasha taa zile blue na red anasokota mzigo akasepa pale pale na pembeni trafiki wapo nikabaki najisemea wenye nchi yao haooooo😂😂
Mkuu japo sijasoma ulichoandika lakini hata kama ni ww unataka Vieite ikae nyuma ya IST kwenye foleni pale Nelson Mandela road?
 
Haiwezekani kabisa mkuu vieite ni ngoma ingine hata ikiwa nyuma ya usafiri wako unajiskia umpishe tu aende..... Siku moja nilikua road kwenye mataa nimepenya na ka pikipiki kangu nikakaa mbele wakiruhusu nichomoke wakwanza basi nyuma yangu kulikua na LC 100 ila imepimpiwa mbaya nyeusi Full tinted na namba hazieleweki basi nasimama tu naskia mlio wa honi zao zile kapiga mara mbili tu tooooo tooooo akawasha taa zile blue na red anasokota mzigo akasepa pale pale na pembeni trafiki wapo nikabaki najisemea wenye nchi yao haooooo😂😂
V8 kitu kingine! mi nkionaga mtu anaendesha namheshimu sana
 
Tumefikia sasa kwamba hapa nchini tuna watumiaji wa barabara wa aina mbili - Watanzania wa kawaida, na Watanzania "wenye nchi" ambao sheria za barabarani haziwahusu.

Hili kundi la "wenye nchi" ni wale ambao hawataki kabisa wabugudhiwe katika kuendesha juu ya spidi inayoruhusiwa, au wakae kwenye foleni wakiwa kwenye magari yao. Kikundi hiki kinatia ndani waendeshaji wa gari za ST, polisi na Usalama wa Taifa. Baadhi yao wamekuwa wakitumia zile namba nyeusi kama sababu ya wao kutaka kutumia barabara kwa namna tofauti na wengine. Na pia utaona wamejipa hizi taa za blue na nyekundu ambazo wanazitumia kujihalalishia ukiukwaji wa sheria barabarani.

Kwa mfano najiuliza, hata kama wewe ni waziri, au kigogo wa serikali, au Usalama wa Taifa, na unaendesha gari kwenda nyumbani, kitu gani kinakufanya wewe uwe na umuhimu zaidi wa kwenda haraka kwa mkeo na watoto wako kuliko atanzania wengine? Kwani mkeo au watoto wako wana tofauti gani na mke au watoto wangu? Asietaka kufika nyumbani mapema baada ya kazi ni nani?

Nimeona matukio mengi sana ya uendesheshaji wa hatari sana barabarani ambao unafanywa na watu hawa. Kuna wakati nimehusika katika ajali kwa sababu Landcruiser ya STL ilikuwa inaendeshwa kwa kasi usiku upande usio wake, na niliposhika breki baada ya kuiona, gari iliyokuwa nyuma yangu ilinigonga. Hiyo STL iliondoka bila hata kusimama.

Juzi usiku nikitoka kazini niliona watu wa Usalama wa Taifa wakiendesha gari kwa fujo na kuhatarisha watumiaje wengine wa barabara, na waliposimamishwa na trafiki wakaonyesha utambulisho wa wa kuwa wafanyakazi wa Usalama wa Taifa na kuaruhusiwa waendelee. Dereva aliyekuwa nyuma yao akichukulia advantage iliambiwa aweke gari pembeni. Nina amini kwamba hawa watu walikuwa wakirudi nyumbani na waliendesha kwa fujo hizi kwa sababu hawakuvumilia kuwa kwenye foleni.

Hasa hapa Dar es Salaam, hiki kikundi kinachojiona wao ni wa pekee katika utumiaji wa barabara na wana haki zaidi ya watumiaji wengine, kinazidi kukua kila siku. Kuna siku madhara makubwa yatatokea, na najua yameshatokea, kutokana na hasira za watumiaji wengine barabarani. Kuna siku tutasikia watu wamekufa kwa sababu ya ujinga huu ambao nchi hii inauendekeza. Tunaimba hakuna aliye juu ya sheria lakini ni wazi wale wanaoongoza kutuimbisha wimbo huu wao hili haliwahusu, wanajiona wako juu ya sheria. Tunakoelekea si kuzuri.
Mwarobaini ulikuwa Magu, mkauponda acha watumie barabara nawe ikikuuma tumia hivohivo
 
Leo pale Mbezi Temboni sijui ndiyo wanamuita CDF au mkuu wa majeshi alikuwa anapita asubuhi tukiwa tunasubiri taa ziruhusu aisee wale MPs ni totally crazy,jamaa wanagonga gonga body hovyo gari inayoongoza msafara iko mbio aliyopanda huyo jamaa iko mbio

Halafu ni kwenye mataa,vitu vya ajabu kabisa.
 
Back
Top Bottom