Kweli hakuna mwanaume bahili akipenda kweli

Kweli hakuna mwanaume bahili akipenda kweli

Ya fundi tiles yatakukuta tu. Naye alisimulia kama wewe akaishia kutaka kuruka juu ya ghorofa ajiue. Upe moyo wako subira na uvumilivu yatakayojiri. Kiumbe mwanamke ni hatari tena futa hiyo mihamala itakuletea machungu

Hibernating.........
 
Sio kwa bongo, hio ina apply msemo ulipotokea tu! Wengine wanadai keki za besdei kama pumzi hapa hapa jukwaani [emoji23][emoji23][emoji23]!!! Bongo mapenzi ni hela yako tu...vinginevyo utaishia kutubu tu!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kutubu tena lol
 
Nikidhani umeandika 32, kumbe 22. Hongera ilà kwa umri huo tunasubiri mrejesho tu.
 
Umesema ukweli umri wa kuolewa ni miaka hiyo.
At least msichana anakuwa ameshajua maisha ya kitaa.
Anajua nyama robo ikiongezewa na mchicha fungu moja inatosha kula familia nzima.

[emoji23][emoji23][emoji23] nyama robo na mchicha fungu moja inatosha kula familia nzima...[emoji23][emoji23]
 
Miaka 22???[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nasema utaliaaa tuuu hakunaa namnaa...afu ulivyofalaa unafutaa namba za mademu wengine as if huyo ni mkeoo... Utapigwaa uchakaee
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Kwani kaka hujawahi kuona hiyo? Nyama kuongezewa kabichi ili iwe nyingi.
Umewasema wake zetu mdogo wangu, kweli ukubwa dawa[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata nature na sinta walianza hivihivi kabka sitaki demu
Bow bow na ciara na hivi hivi kabla ya like a man
Nakuombea kila la kheri mkuu, ila najua akili bado umebaki nazo
Ukipata muda msikilize deceased roho 7, Waite polisi
Ila maisha ndo hayahaya enjoy the happiness
 
Habari zenu wakuu,

Zamani nilikuwa nashangaa sana kuona mwanaume mwenzangu anahonga gari, nyumba, ticket ya flight kumpeleka mwanamke vacation kwenye nchi ya chaguo lake, ila now I know the motive behind. TRUE LOVE.

Iko hivi, ukipenda hakuna kitu mpenzi wako atakwambia usimtendee. Baada ya kuishi miaka takribani 15 ya uzinzi 'mtambuka', nimejikuta nimenasa kwa kabinti kadogo sana ka miaka 22!! Nimekutana nako recently, baada ya kukafanyia thorough assessment nikagundua kana sifa zote za mke

Nimejikuta nakafanyia mambo ambayo sikuwaza nitakuja kumfanyia mwanamke! Love is a beautiful thing. Nafanya hadi vitu ambavyo baada ya kuvifanya najishangaa mwenyewe! Hela natoa bila kuombwa. Juzi nikajikuta naitembelea 'phonebook' yangu na kuanza kufuta namba za wapenzi wangu wa zamani! Msukumo wa ndani ndiyo unanishawishi kuyafanya haya.

Ukiona unatumia nguvu ya ziada kuomba au kufanyiwa kitu na mwanaume wako ujue hapo sio mahali pako, kuna tatizo mahali. Kimbia. Mwanaume anayekupenda ataifanya furaha yako iwe kipaumbele chake.

Guys, I am in love. Simu napiga hadi najishangaa. Text ndiyo usiseme. Nazidi kumuomba Mungu huyu binti asibadilike ili aje kuwa mama wanangu panapo majaliwa. Mniombee pia wakuu (ingawa hatufahamiani).

Msamiati 'uzinzi mtambuka' ni umalaya usio na staha wala mipaka (kwa tafsiri isiyo rasmi sana).

Nawatakia jioni njema. Mapovu ruksa.
Hakika tumenaswa jamaa angu...nlikua km wewe ama zaidi...nimepata kabinti. .nafunguka isivyo kawaida...kila mtu ana mjanja wake.
 
Back
Top Bottom