Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Nipo kwenye kozi inayoitwa The concept of plural marriage and fair treatment of co-wives na ninatakiwa kufanya presentation mbele ya panel wiki mbili zijazo. So maoni ya wadau hapa ni ya mhimu ili niweze kugraduate, naomba uache wenye michango waje kunisaidia.

Back to the topic, ndugu zanguni Qur'an ni kitabu kitakatifu pekee kinachoruhusu mwanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja yaani mwanaume anaweza akaoa mpaka wanawake wanne so long as anaweza kuwahandle.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanawake wa kiislamu wamekuwa hawataki kuwa mke wa pili, watatu ama hata wa nne. Pia hata yule mwanamke ambae tayari yupo kwenye ndoa akisikia kuwa mume wake ana plan ya kuoa mke wa pili nakuambia nyumbani hapatakalika.

Swali langu ni kwamba, je ina maana wanawake wa kiislamu wameamua kupingana na maandiko yanayoruhusu hicho kitu ama je siku hizi kitabu hicho siyo mwongozo tena?

Sababu 1.wanaume kushindwa kutimaza majukumu yao kama kuwalisha,kuwavisha na kuwapatia makazi ya kudumu 2.kukosekana kwa malengo ya ndoa km mapenzi,huruma n.k 3.kutofuata maelekezo ya ndoa kwa me/ke kama Qur'an na sun ah km wajibu Wa me/ke ktk ndoa.4.uelewa Mdogo kwa ME Wa namna ya ruhusa ya kuoa Mke zaidi ya 1,aya imesema oeni na Si chukueni,wanaume wengi huchukua badala ya kuoa!
 
Quran ifanyiwe mabadiliko.. Iundwe tume ya mabadiliko

mwenyekiti wa tume awe mwanamke

ahahahahahhahahaaaaah[/QUO## inawezekana tu wewe kufanyiwa mabadiliko hata ya jinsia yako but sio kitabu kile! Maana hakina shaka ndani yake heeheeeer!!!
 
Na ndio maana mwanamme anaweza kuzalisha hata akiwa na miaka 90 km ananguvu....
Huu ni ukweli usiopingika kuwa kuna wanaume ambao mwanamke mmoja hamtoshi...Kutokana na maumbile yao walioumbwa....

Na endapo akiwa na mwanamke mmoja huyo mwanamke hatomuweza...Huko naniiii kutachubuka kwa shughuli...Wanawake ni wakukinai mapenzi...Ila mwanaume hakinai...

we thread yangu uliielewa sana....nataka niongeze wawili kwa mpigo..."Raha ya ndoa wake wengi" Lol
 
Msiangalie suala la kuoa mke zaidi ya mmoja kwa upande wa dini Tu yA kiislam Bali kiasili wanawake wanaweza kuolewa hata ishirini na mwanaume mmoja hata kwa Mila za kiafriKa haya mambo hufanyika babu yangu alikuwa na wanawake tisa Na kila mmoja alimpa heshima mwenzie ingawa wivu haukosekani lakini babu aliniambia lazima kauli ya mwanaume iheshimiwe kwahiyo lazima kuwa strong Kama mzee wa boma.wasichana WA siku hizi hawataki kusikia hiyo habari.
 
Hhhaaaaaa hua halichomi kabisaaaa!

kuna siku tunatoka zetu shule tupo kama watu watano wakapita wahindi wakataka kama kutubagua wakaanza matusi yao ya kingereza na wenzangu wakawajibu kwa kingereza nilichosema mimi aibu waliona wao nikawapa lile kubwa kwa kiswahili noma kweli ndipo nikagundua ya kiswahili noma
 
Naongea mim kama mim

Ukiolewa n mume ambae n.musilamu na akataka kuongeza mke wa pili bas shart la kwanza akupe taarifa. Na pia ikunbukwe kuoa mke zaidi ya mmoja sio watu wamejiweke bali ni sheria zipo na pia mke wa pili unaoa ikiwa yafuatayo yapo ndani yako
Una uwezo wa kuwalisha wote
Una uwezo wa kuwapa kile wanachostahili na kuwatoshelezea kimahitaji ya kimwili na mengineyo
Na kama huku utaacha elfu tano bas kwa mke mkubwa uache hiyo elfu tano sio huku elfo moja kule msimbazi.
Na kuoa mke wa pili yataka mshauriane ww na mkeo. Sasa mke akikataa mume hilo sio jukumu lako tena bali kalibeba mkeo. Na akikataa akupe sababu hasa za msingi.


Mim binafsi mume anipe mahitaji yangu stahiki anitimizie nitakacho akitaka kuoa mke wa pili akimudu kutugharamia ruksa.

Sijui ni ku PM maana ful kunihamsisha
 
Wakati wa uumbaji Mungu hakuwahi kutamka kuwa mtu aoe mke mmoja tu. Kama alitamka weka hapa huo mstari. Pia uumbaji ulikuwa ni mwanzo na aliwaachia hao aliowaumba kazi ya kuendeleza uumbaji huo. Ndipo baada ya kuwaumba aliwaagiza wakaongezeke kwa kuendelea kuzaana wala hakuna sheria yoyote aliyoweka kuhusu idadi ya wake. Hata katika amri kumi za Mungu wala torati yote hakuna amri inayosema mtu aoe wake wangapi. Tena katika torati inaagiza kama mtu ndugu yake akifa hali akiwa hajazaa na mke wake, ndugu aliyebaki hata kama ana mke wake amchukue yule mke (mjane) na kumzalia ndugu yake aliyekufa wana. Kwa hiyo maneno ya idadi ya wake ni yako wewe unataka kumwekea Mungu mdomoni hali hajawahi kuyatamka. Na pia narudia tena, hivi kama kuoa wake wengi ni dhambi ilikuwaje Mungu amwache mfalme Daudi aifanye hiyo dhambi au ni wapi alipotubu kwa Mungu kwamba hiyo ilikuwa ni dhambi? Kumbuka mfalme Daudi alitubu dhambi nyingi hata kwenye zaburi unaweza kusoma toba zake nyingi lakini hakuna hata sehemu moja kwenye Biblia ambapo ametubu dhambi ya kuoa wake wengi na Mungu hajawahi kumwacha mtumishi wake Daudi kwa sababu eti ameoa wake wengi wala hajawahi kumwonya wala kumkemea kuhusu suala hilo. Ina maana Mungu hakuona msururu huo wa wake? Sana sana Mungu mwenyewe amemsifu kuwa Daudi ni mtumishi mwema na mwenye moyo wa kumpenda Mungu na Mungu alifanya mambo mengi makubwa kwa ajili ya mtumishi huyo Daudi. Kwa hiyo ndugu MO11 pamoja na wengine wenye kupenda kupotosha biblia acheni huo upotoshaji.

soma kwa makini sio kwa sababu tunapishana ndio maana hujifunzi unapinga
mathayo 19
4 Yesu akawajibu, "Je,
hamkusoma katika Maandiko
Matakatifu kwamba Mungu
aliyemuumba mtu tangu mwanzo
alimfanya mwanamume na
mwanamke,

huu umeelewa nini ??

kwa nini waliumbwa Adam na Eva ??
kwa nini hawakuumbwa Adam na wanawake wengine wanne ??
 
Hapa umechapia. Soma jibu nililomjibu MO11. Siyo kweli Daudi aliishi zama za giza. Musa na Daudi walikuwa wakiongozwa na kuongea na Mungu kwa karibu zaidi kuliko ilivyo kwa watu wa siku hizi. Pia Daudi alitumiwa nabii kila mara alipofanya dhambi ili kuonywa lakini hakuna hata siku moja alipotumiwa nabii kuonywa kwa sababu ya kuoa wake wengi. Pia watumishi hao walikuwa wakiongozwa na dhamiri safi ambayo Mungu aliwawekea na ndiyo maana kila akikosea alitubu. Lakini ni wapi alipotubu kuhusu kuoa wake wengi? weka hapa mistari ya biblia tuisome. La sivyo acha upotoshaji kwa kuweka mawazo yako na mtazamo wako badala ya kuonyesha biblia inasema nini kwenye suala hilo.



kuna matendo yalifanywa na watumishi zama za giza lakini haimaanishi ni halali, ni pamoja na hizo ndoa za kina daud na suleiman. musa pia aliwahi kuua mtu je ni halali kuua sababu nabii aliua? kifupi ni kuwa kuna makosa watumishi wa Mungu waliyafanya na biblia inasema mke na mme sio mme na wake
 
Utafiti upo wazi kabisa.

Kwa nini mke anakataa uke wenza?
Jibu walio wengi huoa mke wa pili bila kuzingatia sheria zinavyojieleza kuhusu kuoa mke wa pili ndio maana mke wa mwanzo hulipinga kwa nguvu zote.
Jifunze kujifunza panapohitajika kujifunza sio kuleta hadithi zisizokuwa na ushahidi ili uonekane na wewe umechangia.
Hivi unajua maana ya neno UTAFITI wewe?
 
Ungezama zaidi kwenye mada badala ya kuzungumzia Biblia.

Mifano uliyoitoa haimaanishi ndoa za mitala ni ruksa.

Hayo yote ni ubatili. Hakuna dini ya kikristo inayoruhusu ndoa hizo
Umesema kweli mkuu,ktk agano jipya Yesu alisema tangu mwanzo Mungu aliumba mme mmoja na mke mmoja baba yenu Ibrahimu aliwaruhusu kwa sababu ya tamaa zenu.Kuna aliyemtaja Yakobo,ukisoma kitabu cha mwanzo unaona Yakobo wake zake walimshinda ikabidi kijana wake mkubwa alale na mmojawapo nadhani alitaka amsaidie mzee,mzee alipojua akamnyima urithi wa kwanza
nadhani hii ni mojawapo ya mapungufu ya kushare mapenzi,mmoja anaona kama anapunjwa na hivyo kutafuta mbadala.
Ila hoja ni wanawake wanajisikiaje,kushare mapenzi na wenzao kwa kisingizio cha maandiko,awe mkristo au muislam
suala ni unajisikiaje? nadhani tujikite hapo na siyo malumbano ya kidini.Mama facebook yeye kashajibu anajisikia poa
wengine mnasemaje ili jamaa amalizie project yake.
 
kumhandle mmoja tu shughuli nzito halafu leo uniongezee mke mwenza! ntakupasua na chungu.
Umeona eeeh,kuna ndugu yangu wa ukoo,kaongeza mke wa pili.mara ananipigia simu ananiomba nimpige tafu aezeke nyumba ya mke wake,mimi nadhani mafundisho yanahitajika kusisitiza siyo kuwatosheleza kitandani tu na mahitaji yao pia.Siyo mtu unapinga ndinga, asubuhi unaamka hoi nguvu ya kwenda kazini hamna matokeo yake wakezo wanajiangaikia ka kuku wa kienyeji.
 
Kuoa hawaoi, ila kuzini na michepuko wanazini teh
Hivi yule profesa aliyetuhumiwa kumpa ukimwi mwanafunzi ni dini gani vile?
Mi naona uzinzi ni ugonjwa hata uwe na wake rundo lazima utachepuka,tunaishi nao mitaani tunawaona.
 
Kwanza kabisa unapoinukuu Qur'an inabidi uiweke na hiyo aya, labda umeinukuu vibaya.

Kwa kukujuza tu, hakuna kitabu chochote cha dini nyingine yeyote kilichosema "marry only one" isipokuwa qur'an pekee.

Pata darsa:

Qur'an 4:3

4_3.png
​
Sahih International
And if you fear that you will not deal justly with the orphan girls, then marry those that please you of [other] women, two or three or four. But if you fear that you will not be just, then [marry only] one or those your right hand possesses. That is more suitable that you may not incline [to injustice].

Sasa wewe tuoneshe kitabu kingine chochote ukijuwacho chenye nukuu ya "marry only one".

Isitoshe, mwanamke wa Kiislam halazimishwi kukaa kwenye ndoa yoyote ile ambayo haridhiki nayo, si kama ukristo ambao ni marufuku ku achana.
Jibu swali unataka mke mwenza hutaki? ili mwenzetu afanye project apate digrii yake hayo ya haya leta baadaye.
 
Nguvu za kiume kupungua kwa kasi pili buddget ni finyu sana hajitoshelezi heri hawe hawara amwibie mtu kuliko uke wenza ni shida
 
Jibu swali unataka mke mwenza hutaki? ili mwenzetu afanye project apate digrii yake hayo ya haya leta baadaye.

Ungana na mleta mada kuweka nukuu kwanza za mliyoyaandika kuhusu Qur'an ha pia mtuoneshe hivyo vitabu vingine vinapokataza kuoa zaidi ya mke mmoja.

Halafu pata darsa: [video=youtube_share;IbdaaDMje_8]http://youtu.be/IbdaaDMje_8[/video]
 
mathayo 19:

7 Lakini wao wakamwuliza, "Kwa
nini basi, Musa alituagiza
mwanamke apewe hati ya talaka
na kuachwa?"
8 Yesu akawajibu, "Musa
aliwaruhusu kuwaacha wake zenu
kwa sababu ya ugumu wa mioyo
yenu.
9 Lakini haikuwa hivyo tangu
mwanzo. Basi nawaambieni,
yeyote atakayemwacha mke wake
isipokuwa kwa sababu ya uzinzi,
akaoa mke mwingine, anazini."

Hahahaa
Sijui kama watakuelewa hapa mkuu.....watakwambia agano jipya wakat wenyewe wana deal na agano la kale tu
 
Hapa biblia inazungumzia kuhusu talaka na haijasema mtu asioe wake wengi. La sivyo itakuwa inajipinga yenyewe kama sehemu moja iruhusu wake wengi halafu ije tena ikataze, ina maana Mungu atakuwa kigeugeu? Pia mfalme Daudi hakuoa na kuacha bali alioa na kuishi nao wote. Mfalme Solomon na Baba Yakobo vivyo hivyo.

Mkuu
Biblia hairuhusu!
Hayo yalifanyika ndio lkn haina maana kuwa yalikuwa sahihi!
Na ndo maana sisi tuna agano jipya ambalo lilikuja kutimiliza hayo mapungufu!
 
Back
Top Bottom