G
guest-1790917349
Guest
Kuoa hawaoi, ila kuzini na michepuko wanazini teh
Hapo tayari wanakuwa wametenda dhambi kama ambavyo dhambi nyingine zinatendwa.....lkn hairuhusiwi kuwa na.mke zaidi ya 1
Kuoa hawaoi, ila kuzini na michepuko wanazini teh
Nina Dada yangu Mumewe kaongeza mke wamekuwa 2 , basi toka Mwenzake aolewe yeye kutwa anauguza fangasi za ukeni ! akimshauri mumewe avae mpira Ugomvi , keshapima VVU yupo sawa ina fangasi haziishi !
Mkuu
Biblia hairuhusu!
Hayo yalifanyika ndio lkn haina maana kuwa yalikuwa sahihi!
Na ndo maana sisi tuna agano jipya ambalo lilikuja kutimiliza hayo mapungufu!
Kama yeye alivyomdhalilisha wa kwangu? Kwamba nimezaliwa kilabuni?
Acha unafiki wewe! Au ndio chama kimoja!
What is so funny to laugh about?? Qur'an is sio kama bible kua kuna agano jipya na zamani hakuna qur'an ya kiswahili wala ya kujerumani maandish ni ya kiarabu isipokua tafsir hua ya lugha yako ili uelewe kile kilichoandikwa ndani ya qur'ani unataka ifanyiwe mabadiliko yapi????
Kama hairuhusiwi kwa nini imeandikwa kwenye Biblia? Na wapi kwenye Biblia mfalme Daudi au Solomon au Yakobo (Baba wa kabila 12 za Israel) aliwahi kukatazwa au hata kukemewa kwa kuoa wake wengi? Kama hawa watumishi wakubwa wa Mungu kutokana na Biblia hawakukatazwa ina maana inaruhusiwa. Kwa hiyo wewe usilete mambo yako yasiyo ya kibiblia. Au wewe ni mkristo ambaye husomi na kuamini Biblia? Pia mtoa mada amezungumzia vitabu vitakatifu vinavyoruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja na Biblia kama nilivyosema inaruhusu, labda kama hukuisoma mada vizuri na labda kama wewe una Biblia yako ambayo haina mfalme Daudi (Mtumishi wa Mungu) wala mfalme Solomon. Ilete hapa tuione.
mmmmhhhh tuko tofauti jaman huu huu upenzi ukigundua uko na mwenzio ni timbwili asa najaribu kuangalia iwe mke kabisa looo ni shida..
Kwa hiyo agano la kale siyo biblia? Kwa nini vitabu vya agano la kale viko kwenye biblia? Kwa hiyo Mungu wa agano la kale ni tofauti na Mungu wa agano jipya? Katika agano hilo jipya ni wapi ambapo Yesu alisema mtu asioe wake wengi? Usiweke mtazamo wako na mawazo yako hapa weka neno lililotamkwa na Mungu kuhusu jambo hilo.
na ni wapi inapoonesha kuwa hao akina daudi na solomon walifunga ndoa????
Katafsiri kiarabu kwenye quran huko.. Biblia haisemi hivyo.. Kuwepo kwa stori ya kuwa daudi alikuwa na wanawake wengi haimaanishi kuwa ni halali
wapo wanaozini lakini wakijua fika kuwa uzinzi ni dhambi
hivyo ht daudi au solomon kama alikuwa na wanawake wengi haileti tafsiri kuwa ni halali. HAIRUHUSIWI.... Una uume mmoja wake wengi wa nini
Hata biblia yenyewe huijui. Mbona huweki mistari inayothibitisha hayo unayosema. Unang'ang'ania tu hairuhusiwi hairuhusiwi bila kuweka ushahidi? Katika biblia kila walipooa kulikuwa na sherehe ya harusi wewe unasoma biblia gani ambayo haionyeshi harusi zilizofanyika? Tatizo unalazimisha mawazo yako uliyokaririshwa bila wewe mwenyewe kujisomea biblia na kuitafakari. Hivyo unamsingizia Mungu kitu ambacho hajawahi kutamka na hakiko kwenye biblia.
Kwanza kabisa jua siwezi kuweka mawazo yangu kwenye neno la Mungu. ..
Pili biblia haiongelei wake inaongelea mume na mke 1 kuwa mwili 1....
Agano la kale na agano jipya yote ni biblia!
Na Mungu ni yule yule 1....
Yesu alisema kwenye agano jipya kuwa 'sikuja kuitangua torati bali kuitimiliza'.....
.....kwenye agano la kale walienenda kisheria tu...(wakristo hapa ss baada ya agano jipya hatupo uko ss tunaenenda kiroho)na ndo tofaut yenu na sisi coz nyie bado mnaenenda kwa sharia....
Sasa basi kwenye agano la kale kuna mambo ambayo yalifanyika,mfano na hao kina suleiman na wengineo kuoa wake wengi ambalo halikuwa agizo la Mungu tangu mwanzo na hivyo lilikuwa chukizo (wapi imeandikwa kuwa hili la kuoa wake wengi lilikuwa chukizo? - acha uongo au weka uthibitisho)(biblia inasema zama za giza)....na ndio maana baada ya agano jipya ss mambo mengi yaliwekwa sawa na Mungu mwenyewe (Kwa hiyo agano la kale lilikuwa siyo la Mungu mwenyewe? Mbona unadanganya? Torati yote iliandikwa na Musa kwa kupewa maneno na Mungu mwenyewe. Kila mara Musa alienda mlimani kuongea na Mungu moja kwa moja na kuandika maagizo yote, sijui wewe unasoma biblia gani?) ndo maana akasema 'sikuja kuitangua torati bali kuitimiliza ' ...
Kuhusu kuweka neno hapa ushawekewa na Mo11 ameku- quote post za awali.....
Hakuna biblia inayozingumzia uhalali wa wake wengi.. Mke ni mmoja tu.... Na ndyo maana Mungu aliumba Adam na Eva... Hakuumba akina eva wengi.....
Amini tunawaambia ipo siku mtakuja kuamini
sheria za kiislam zina mapungufu yaliyopitiliza yaliyolenga kumfanya mwanamke awe mpweke kwa tamaa za kimwili za wanaume
Kwa hiyo Daudi na Solomon hawakuwa na roho? Mbona unachekesha! Kama Mungu ni yule yule itakuwaje awaache wengine waoe wake wengi halafu leo nyie mseme hairuhusiwi kuoa wake wengi? kumbuka Mungu aliadhibu watu wangapi kwa sababu ya dhambi katika agano hilo la kale lakini mbona hakumwadhibu Daudi na Solomon na Yakobo kwa kuoa wake wengi kama ilikuwa dhambi. Ina maana Mungu alikuwa anachagua dhambi za kuadhibu na nyingine aliziacha? Au hata kama siyo kuadhibu ni wapi watu hao vipenzi wa Mungu walitubu dhambi ya kuoa wake wengi kama kweli ilikuwa dhambi? Au ni wapi Mungu alipowatumia manabii kuwaonya kuhusu dhambi hiyo? Mbona hamtaki kujibu haya maswali na mnaendelea kupotosha watu kwa tungo zenu? Na kama Yesu alikuja kutimiliza torati ingekuwaje aipinge kwa kukataza yale ambayo tayari yalishakubaliwa na torati hiyo hiyo? Pia hiyo mistari unayoongelea haijasema mtu asioe wake wengi. Hapo mnachapia tu. Nashangaa mnaikomalia wakati haisemi hivyo bali inasema mtu akishaoa asitengane na mke au mume wake. Kwa hiyo haijalishi ni mke wa kwanza au wa ngapi. Kama lengo ingekuwa ni kuweka ukomo wa idadi ya wake lazima kungekuwa na mstari mahsusi unaoongelea jambo hilo. Kumbuka torati ina mistari mingapi ambayo iliorodhesha makatazo yote ambayo Mungu alimwagiza Musa lakini hakuna hata mmoja ambao unaongelea jambo hilo.Kwa hiyo hilo siyo katazo la Mungu na hivyo hilo mnajitungia tu nyie wenyewe wala msimsingizie Mungu.