Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

" je ina maana wanawake wa kiislamu wameamua kupingana na maandiko yanayoruhusu hicho kitu ama je siku hizi kitabu hicho siyo mwongozo tena?"

Mkuu nahisi imekaa kidini zaidi kuliko MMU. Kwa maana hiyo, jukwaa muafaka lingekuwa ni la Dini.
Mimi sijakaa kidini natafuta michango ya watu walio serious nikajifanyie paper langu
 
bornagain
Hizo ni dhana, Hakuna utafiti wa kuthibitisha madai haya.
Pili, Kwa alieshiba dini hasa uke wenza haiwezi kuwa tatito kwake.

Tatizo lililopo ni kuamini iuwa kila mwenye jina la kiislamau au anaejivika Shungi basi ni Mwislam.
USHAURI WA BURE, Tafiti kwanza kujua kuwa je, ni kweli Waislam hasa wanazipinga hizo ndoa za uke-wenza ama lah?
Ukishakugundua kuwa ni kweli sasa unaweza kutafuta chanzo na sababu ya kutokuzitaka, na si ku-generalize kama ufanyavyo sasa.

Kwa hiyo unaniambia kuwa kila mwanamke anaeitwa Amina, Zainabu au hata Zinduna huku akiwa amevaa ushingi then anakataa kuolewa ndoa za mitara basi huyo siyo muislam? Unajaribu kuongea politics hapa kama wale wanaosema kuwa wanachama wetu wakiwa kwenye mikutano ni watu wastaarabu sana ukiona wale wanaokuwa wamevaa sare zetu then wakafanya vurugu hao jua ni wahuni tu
 
Angalia hapo kwenye red. Siyo kweli kwamba Quran pekee ndiyo inaruhusu mwanamme kuoa wake wengi. Hata Biblia inaruhusu - mfalme Daudi alikuwa na wake 100, mfalme solomon alikuwa na wake 1000 (700 + masuria 300), Yakobo (Israel) wake 2 pamoja na kuzaa na wajakazi 2, etc.

mathayo 19:

7 Lakini wao wakamwuliza, "Kwa
nini basi, Musa alituagiza
mwanamke apewe hati ya talaka
na kuachwa?"
8 Yesu akawajibu, "Musa
aliwaruhusu kuwaacha wake zenu
kwa sababu ya ugumu wa mioyo
yenu.
9 Lakini haikuwa hivyo tangu
mwanzo. Basi nawaambieni,
yeyote atakayemwacha mke wake
isipokuwa kwa sababu ya uzinzi,
akaoa mke mwingine, anazini."
 
Kama hairuhusiwi kwa nini imeandikwa kwenye Biblia? Na wapi kwenye Biblia mfalme Daudi au Solomon au Yakobo (Baba wa kabila 12 za Israel) aliwahi kukatazwa au hata kukemewa kwa kuoa wake wengi? Kama hawa watumishi wakubwa wa Mungu kutokana na Biblia hawakukatazwa ina maana inaruhusiwa. Kwa hiyo wewe usilete mambo yako yasiyo ya kibiblia. Au wewe ni mkristo ambaye husomi na kuamini Biblia? Pia mtoa mada amezungumzia vitabu vitakatifu vinavyoruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja na Biblia kama nilivyosema inaruhusu, labda kama hukuisoma mada vizuri na labda kama wewe una Biblia yako ambayo haina mfalme Daudi (Mtumishi wa Mungu) wala mfalme Solomon. Ilete hapa tuione.


Ungezama zaidi kwenye mada badala ya kuzungumzia Biblia.

Mifano uliyoitoa haimaanishi ndoa za mitala ni ruksa.

Hayo yote ni ubatili. Hakuna dini ya kikristo inayoruhusu ndoa hizo
 
Kama hairuhusiwi kwa nini imeandikwa kwenye Biblia? Na wapi kwenye Biblia mfalme Daudi au Solomon au Yakobo (Baba wa kabila 12 za Israel) aliwahi kukatazwa au hata kukemewa kwa kuoa wake wengi? Kama hawa watumishi wakubwa wa Mungu kutokana na Biblia hawakukatazwa ina maana inaruhusiwa. Kwa hiyo wewe usilete mambo yako yasiyo ya kibiblia. Au wewe ni mkristo ambaye husomi na kuamini Biblia? Pia mtoa mada amezungumzia vitabu vitakatifu vinavyoruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja na Biblia kama nilivyosema inaruhusu, labda kama hukuisoma mada vizuri na labda kama wewe una Biblia yako ambayo haina mfalme Daudi (Mtumishi wa Mungu) wala mfalme Solomon. Ilete hapa tuione.

mathayo 19

7 Lakini wao wakamwuliza, "Kwa
nini basi, Mose alituagiza
mwanamke apewe hati ya talaka
na kuachwa?"
8 Yesu akawajibu, "Mose
aliwaruhusu kuwaacha wake zenu
kwa sababu ya ugumu wa mioyo
yenu.
9 Lakini haikuwa hivyo tangu
mwanzo. Basi nawaambieni,
yeyote atakayemwacha mke wake
isipokuwa kwa sababu ya uzinzi,
akaoa mke mwingine, anazini."
 
Hapa biblia inazungumzia kuhusu talaka na haijasema mtu asioe wake wengi. La sivyo itakuwa inajipinga yenyewe kama sehemu moja iruhusu wake wengi halafu ije tena ikataze, ina maana Mungu atakuwa kigeugeu? Pia mfalme Daudi hakuoa na kuacha bali alioa na kuishi nao wote. Mfalme Solomon na Baba Yakobo vivyo hivyo.



mathayo 19:

7 Lakini wao wakamwuliza, "Kwa
nini basi, Musa alituagiza
mwanamke apewe hati ya talaka
na kuachwa?"
8 Yesu akawajibu, "Musa
aliwaruhusu kuwaacha wake zenu
kwa sababu ya ugumu wa mioyo
yenu.
9 Lakini haikuwa hivyo tangu
mwanzo. Basi nawaambieni,
yeyote atakayemwacha mke wake
isipokuwa kwa sababu ya uzinzi,
akaoa mke mwingine, anazini."
 
tusikilize mawaidha kuhusu hii kitu:
 
Last edited by a moderator:
Nadhani maandiko ya vitabu vitakatifu yalikuwa/yana malengo mazuri kabisa, tatizo hao watekelezaji ndio ngoma a.k.a ishu.......ni kama ilivyoandikwa msiibe na bado mafisadi wamevaa miwani za mbao.....hawajali.

Nakumbuka hata Marehemu Marijani alikuwa na wimbo...."uke weza mimi sitaki..jama sitaki...tena nimekoma hata kulisikia hilo neno sipendi.....ukeweza ni ufahari kwa wanaume kwetu(wanawake) ni tabu".............
 
Hapa biblia inazungumzia kuhusu talaka na haijasema mtu asioe wake wengi. La sivyo itakuwa inajipinga yenyewe kama sehemu moja iruhusu wake wengi halafu ije tena ikataze, ina maana Mungu atakuwa kigeugeu? Pia mfalme Daudi hakuoa na kuacha bali alioa na kuishi nao wote. Mfalme Solomon na Baba Yakobo vivyo hivyo.

mathayo 19

4 Yesu akawajibu, "Je,
hamkusoma katika Maandiko
Matakatifu kwamba Mungu
aliyemuumba mtu tangu mwanzo
alimfanya mwanamume na
mwanamke,
5 na akasema: `Kwa sababu hiyo
mwanamume atamwacha baba
yake na mama yake, ataungana na
mke wake, nao wawili watakuwa
mwili mmoja?`
6 Kwa hiyo wao si wawili tena,
bali mwili mmoja. Basi,
alichounganisha Mungu, binadamu
asikitenganishe."
 
mkuu bornagain kinachofanya wanawake wa kiislamu kuchukia uke wenza ni tabia za wengi wa wanaume wetu. kwanza wengi wao dini wameiweka kando,kutekeleza swala tano za fardhi zimewashinda, sunna ya kuongeza mke wataiweza? watu kama hawa wakioa wanaishia kuwabyanyasa wana wa wenzao,haya mambo yanatakiwa yaende sambamba na taqwa.

jambo lengine ni wanaume wa zama hizi kukosa uadilifu,akishaoa mke mwingine bi mkubwa anakuwa kama bablish iliyokwisha utamu,wengine wanadiriki kusema"kipya kinyemi ingawa kidonda" japo mambo yanakwenda kwa zamu lakini wengi wanaegemea upande mmoja wa bi mdogo.

jambo jengine ni sisi wanawake wenyewe,tukiolewa bi wadogo tunaanza kuwafanyia visa wale tunaowakuta hata kwa ndumba mpaka wanaachwa,kwa hiyo wengi wanaogopea kuvunjika ndoa zao,
 
Last edited by a moderator:
WENGINE HAWATAKI......
INDONESIA_-_POLIGAMIA_CONTRO.jpg
 
Back
Top Bottom