Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Hoja hii fikiria kwanza uko tayari mwanaume kushare haki yako na mwili wake kwa wanawake kadhaa lakini amekuwekea ukingo wewe kutofanya hivyo, je haki ipo hapo? Maana yake wewe huna haki ya kushare mwili wako kwa mwanaume mwingine isipokuwa mumeo tu wakati mumeo amejihalalishia kushare mwili wake kwa wanawake kadhaa na wewe kukupangia zamu maana yake ukiwa unatamani utabaki kutaabika tu wakati yeye anaserebuka na wake wenza FaizaFoxy.

Sikiliza kwa makini:

[video=youtube_share;IbdaaDMje_8]http://youtu.be/IbdaaDMje_8[/video]
 
Naongea mim kama mim

Ukiolewa n mume ambae n.musilamu na akataka kuongeza mke wa pili bas shart la kwanza akupe taarifa. Na pia ikunbukwe kuoa mke zaidi ya mmoja sio watu wamejiweke bali ni sheria zipo na pia mke wa pili unaoa ikiwa yafuatayo yapo ndani yako
Una uwezo wa kuwalisha wote
Una uwezo wa kuwapa kile wanachostahili na kuwatoshelezea kimahitaji ya kimwili na mengineyo
Na kama huku utaacha elfu tano bas kwa mke mkubwa uache hiyo elfu tano sio huku elfo moja kule msimbazi.
Na kuoa mke wa pili yataka mshauriane ww na mkeo. Sasa mke akikataa mume hilo sio jukumu lako tena bali kalibeba mkeo. Na akikataa akupe sababu hasa za msingi.

Mim binafsi mume anipe mahitaji yangu stahiki anitimizie nitakacho akitaka kuoa mke wa pili akimudu kutugharamia ruksa.

Merehemu Hemed Maneti aliona mbali kwa kutunga "Penzi Haligawanyiki."
 
Nipo kwenye kozi inayoitwa The concept of plural marriage and fair treatment of co-wives na ninatakiwa kufanya presentation mbele ya panel wiki mbili zijazo. So maoni ya wadau hapa ni ya mhimu ili niweze kugraduate, naomba uache wenye michango waje kunisaidia.

Back to the topic, ndugu zanguni Qur'an ni kitabu kitakatifu pekee kinachoruhusu mwanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja yaani mwanaume anaweza akaoa mpaka wanawake wanne so long as anaweza kuwahandle.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanawake wa kiislamu wamekuwa hawataki kuwa mke wa pili, watatu ama hata wa nne. Pia hata yule mwanamke ambae tayari yupo kwenye ndoa akisikia kuwa mume wake ana plan ya kuoa mke wa pili nakuambia nyumbani hapatakalika.

Swali langu ni kwamba, je ina maana wanawake wa kiislamu wameamua kupingana na maandiko yanayoruhusu hicho kitu ama je siku hizi kitabu hicho siyo mwongozo tena?

Ninachoweza kukusaidia ni kuwa iwapo unakusudia muislamu eti kwa kuwa anaitwa Khadija au Sharifa basi mtazamo wako ni kweli . La unazungumzia waislamu walio waislamu basi sio kweli kuwa trend ni kuwa sasa hawataki kuolewa uwili au utatu.
Nikupe mfano halisi, mimi mwenyewe binafsi ninao wawili na nimeona tangu 1990s. Wakati huo ukienda kuposa jambo la mwanzo unaulizwa iwapo una mke au la na ilikuwa tabu kukubaliwa posa iwapo una mke. Trend sasa imebadilika na hakuna mzazi anaeuliza swala hilo kwa kutaka kuweka vikwazo bali huenda akauliza kwa kutaka kujuwa tu.
Wanawake wengi wa kiislamu sasa wanakubali uke wenza kuliko huko nyuma. Hii haina maana kuwa yule aliepo halalamiki lakini wengi hukubaliana na hali.
 
Sikiliza kwa makini:

[video=youtube_share;IbdaaDMje_8]http://youtu.be/IbdaaDMje_8[/video]

Unafikiri nina utashi wa kupoteza muda kwa hizo movie bora niende kuungana na wanajumuiya wenzangu kusali rozari maana huu mwezi oktoba ndo wake haswaaa..!
 
Usomi unaoonekana kuwa nao haulingani na swali la kitoto unaloliuliza. Kama wewe ni mtu unayetegemea kufanya critical analysis ya research unayotakiwa kuandika hukupaswa kuuliza swali linaloweza kuulizwa na muuza dagaa asiyekwenda shule otherwsie kama una nia ya kutaka kudhalilisha dini hiyo. Unawezaje kuuliza kuwa Kitabu chochote kinachoaminika na dini fulani kuwa ni muongozo wao kina ukomo wa kutumika na hasa kwa dini kubwa kama ya Kiislamau Kikristu.
Kilichofanywa au kinachoendelea kufanywa na Wanamama hao ni kuvunja sheria ya dini yao na wanaadhibiwa kama vile wewe kitabu chako kilivyokukataza kuzini na unaendelea kuzini. Kwani mtu akiiba inamaana sheria za nchi hii hazitumika tena, atakamatwa na kuadhibiwa. Mungu ameweka pepo na moto katika imani za dini zote na wamfuatao wataingia peponi na wamkanao wataingia motoni. Usiulize maswali ya kitoto na si dhani majibu haya yatakusaidia vipi katika kuandika paper yako.
 
Unafikiri nina utashi wa kupoteza muda kwa hizo movie bora niende kuungana na wanajumuiya wenzangu kusali rozari maana huu mwezi oktoba ndo wake haswaaa..!

Naam, hiyo ndiyo Islamophobia.

Usiogope, sikiliza solutin za Uislam, maana hakuna tatizo lisilokuwa na solution katika Uislam.
 
.............lete ushahidi wa Biblia kukataza ndoa ya wake wengi !
Je, Mnabii ambao walioa Mke zaidi ya mmoja, walipotoka !?...........Nabii hupotoka !? instagramboy

Manabii ni binadamu kama mimi na wewe, nao wana mapungufu kama ilivyo kawaida ya kila binadamu. Hata wengine hawakujua nini watatendewa na Muumba wao mara baada ya kutoka hapa duniani.
 
Last edited by a moderator:
Nipo kwenye kozi inayoitwa The concept of plural marriage and fair treatment of co-wives na ninatakiwa kufanya presentation mbele ya panel wiki mbili zijazo. So maoni ya wadau hapa ni ya mhimu ili niweze kugraduate, naomba uache wenye michango waje kunisaidia.

Back to the topic, ndugu zanguni Qur'an ni kitabu kitakatifu pekee kinachoruhusu mwanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja yaani mwanaume anaweza akaoa mpaka wanawake wanne so long as anaweza kuwahandle.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanawake wa kiislamu wamekuwa hawataki kuwa mke wa pili, watatu ama hata wa nne. Pia hata yule mwanamke ambae tayari yupo kwenye ndoa akisikia kuwa mume wake ana plan ya kuoa mke wa pili nakuambia nyumbani hapatakalika.

Swali langu ni kwamba, je ina maana wanawake wa kiislamu wameamua kupingana na maandiko yanayoruhusu hicho kitu ama je siku hizi kitabu hicho siyo mwongozo tena?

Kuoa mke zaidi ya mmoja katika uislamu sio lazima ila ni ruhusa kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo.Ikiwa huna uwezo wakufanya hivyo unaoa mmoja.Kwa waislam wanaooa mke mmoja hawapingani na Qur'an.
Isome aya ya Qur'an vizuri,iliyotoa ruhusa ya kuoa mke zaidi ya mmoja.
 
Ungezama zaidi kwenye mada badala ya kuzungumzia Biblia.

Mifano uliyoitoa haimaanishi ndoa za mitala ni ruksa.

Hayo yote ni ubatili. Hakuna dini ya kikristo inayoruhusu ndoa hizo
Mnaruhusiwa za wanaume kwa wanaume
 
Kwa hiyo unaniambia kuwa kila mwanamke anaeitwa Amina, Zainabu au hata Zinduna huku akiwa amevaa ushingi then anakataa kuolewa ndoa za mitara basi huyo siyo muislam? Unajaribu kuongea politics hapa kama wale wanaosema kuwa wanachama wetu wakiwa kwenye mikutano ni watu wastaarabu sana ukiona wale wanaokuwa wamevaa sare zetu then wakafanya vurugu hao jua ni wahuni tu
Mtu anapokuwa katika la watu fulani,na kukataa makubaliano ya kundi hill,ujuwe huyo si wakundi hilo.
 
Unadhani unalala kitanda kimoja na wake wote? Mwanaume unapanga zamu km siku 2,3,4 au wiki ni wewe ila hakikisha unapokuwa zamu kwa mke mmoja km ni siku 3 basi siku hizo wengine wanapata huduma zao km kawaida hasa chakula kama kila mwanamke anakaa kwake, ingawa wengine wanaishi pamoja nyumba moja na chakula wanakula pamoja.
Hukunielewa swali langu. Siku tatu uko kwa mke wa kwanza, siku zote anataka haki yake ya ndoa. Baada ya hapo unakwenda siku tatu kwa mke wa pili, naye siku zote anataka haki ya ndoa, hivyo hivyo kwa wa tatu na wa nne. Swali, je, mwanaume ataweza kuwahudumia hao wote yeye pekeyake? Maana akiishazunguka kwa wote mpaka anarudimkwa yule wa mwanzo ujue keshakaa siku zaidi ya 9 bila kupata, lkn yeye kila cku yumo tu, si atakufa.
 
Usilolijua....naamini hujanielewa kwa makusudi tu.
 
Back
Top Bottom