Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Kwanini wanawake wa Kiislamu hawautaki tena ukewenza?

Mungu Alisha tamka kua mke mmoja soma mwanzo sura ya kwanza na ya pili alipewa MSAIDIZI sii wasaidizi

Upo sahihi sana sana;tatizo linakuja unaye mwambia ni muumin gani?Kunw waumin wa allah (wasoma quaran) na waumin wa Mungu wa miungu(wasoma biblia).kamwe hukutakuwa na maafikiano ktk mjadala wowote wa iman za waumini.Kwan hata hao miungu hawaafikian kamwe
 
Ungana na mleta mada kuweka nukuu kwanza za mliyoyaandika kuhusu Qur'an ha pia mtuoneshe hivyo vitabu vingine vinapokataza kuoa zaidi ya mke mmoja.

Halafu pata darsa: [video=youtube_share;IbdaaDMje_8]http://youtu.be/IbdaaDMje_8[/video]
Jibu swali kwanza ,tukuletee mke mwenza? au akifika utaandamana?
 
Mkuu bornagain kilichoandikwa kwenye quran kilizingatia maslahi ya wanaume zaidi kuliko mwanamke kwakuwa walioiandika wote walikuwa wanaume.Nikiweka mbali sababu za dini nitajikita zaidi katika sababu za kiuchumi.Mara nyingi mwanaume anapotaka kuongeza mwanamke anakuwa amefanikiwa kiuchumi then anashindwa kudhibiti tamaa za mwili.Utakuta mwanamke aliye kwenye ndoa kashiriki kwa kiasi kikubwa kufanikisha kupatikana utajiri wa familia ghafla mwanaume anajiangalia mwenyewe kwa kutaka kuongeza mwanamke mwingine hapo ndipo timbwili linapoanza.

Kwani Bible Ilipokuwa inaandikwa walikuwepo nawanawake kuna sehemu inasema mwanamke ha popaswi kuongea kwenye nyumbu za ibada ila akae kimyatu.
 
Last edited by a moderator:
Jibu swali kwanza ,tukuletee mke mwenza? au akifika utaandamana?

Swali la kipuuzi hilo, soma mada. Umeitazama video niliyokuwekea?

Mwanamke anaejiamini haogopi uke wenzza, kumbuka hilo.

Isitoshe, ni bora mume aoe na awe na wake kihalali au awe anazini hivyo nje kama mfanyavyo Wakristo? maana wengi tunawaona kuwa mmoja hawatoshi na wengine wenza wao wagonjwa wao wamebaki kuchepuka tu. Wengiene wengi ndiyo hivyo waliharibiwa makanisani na wamekuwa hawafai tena, sasa na idadi ya wanawake tulivyokuwa wengi unafikiri solution ni nini?

Tazama video hiyo niliyokuwekea juu hapo ujuwe solution ni nini.
 
Suala hapa siyo kuwa mkristo au muislam. Tunachotaka ukiandika kitu kiwe cha kweli kulingana na kitabu unachorejea siyo unalazimisha hoja ya uongo. Hakuna Mungu anayependa uongo. Pili biblia haina dini wala dhehebu. Ndani ya biblia hakuna sehemu yoyote ambapo imeandikwa dini yoyote au dhehebu lolote. Usije ukaleta uongo mwingine hapa. Kwa hiyo mtu yeyote yuko huru kusoma biblia bila kujali ana dini au dhehebu au hana.


Kwanz ww biblia inakuhusu nini.. Kwanini waislam mnakuwa kimbelembele kuhusu biblia.. Moyoni mnakiro kuwa biblia ndo kitabu takatifu.. Ma ipo siku mtakiri kuwa ukristo ndo dini pekee ya kuwasiliana Mungu.. Hzi zingne majanga....

Biblia ndyo inayotoa maneno na maagzo halisi ya mwnyezi Mungu...
 
QURAN ni kitabu kisicho na shaka, hauko sahihi kuwasemea wanawake wa kiislamu kuhusu hilo, kasome bibla 1.mwanzo 25-1
2. hesabu 12;1-2[
3.kutoka 18;1-3 na wafalme 11; 1-2 kisha wasemee na hao wanaokiamini kitabu hicho. QUOTE=bornagain;10896272]Nipo kwenye kozi inayoitwa The concept of plural marriage and fair treatment of co-wives na ninatakiwa kufanya presentation mbele ya panel wiki mbili zijazo. So maoni ya wadau hapa ni ya mhimu ili niweze kugraduate, naomba uache wenye michango waje kunisaidia.

Back to the topic, ndugu zanguni Qur'an ni kitabu kitakatifu pekee kinachoruhusu mwanaume kuwa na wanawake zaidi ya mmoja yaani mwanaume anaweza akaoa mpaka wanawake wanne so long as anaweza kuwahandle.

Lakini katika miaka ya hivi karibuni wanawake wa kiislamu wamekuwa hawataki kuwa mke wa pili, watatu ama hata wa nne. Pia hata yule mwanamke ambae tayari yupo kwenye ndoa akisikia kuwa mume wake ana plan ya kuoa mke wa pili nakuambia nyumbani hapatakalika.

Swali langu ni kwamba, je ina maana wanawake wa kiislamu wameamua kupingana na maandiko yanayoruhusu hicho kitu ama je siku hizi kitabu hicho siyo mwongozo tena?

[/QUOTE]
 
Angalia hapo kwenye red. Siyo kweli kwamba Quran pekee ndiyo inaruhusu mwanamme kuoa wake wengi. Hata Biblia inaruhusu - mfalme Daudi alikuwa na wake 100, mfalme solomon alikuwa na wake 1000 (700 + masuria 300), Yakobo (Israel) wake 2 pamoja na kuzaa na wajakazi 2, etc.
Hujasoma bible wewe
 
Inakuwaje wote wanne kila mmoja akihitaji ahudumiwe kimwili na kwa mujibu wa sheria hiyo ni haki yako akuhudumie sawa na wengine. Ni swali tu

Unadhani unalala kitanda kimoja na wake wote? Mwanaume unapanga zamu km siku 2,3,4 au wiki ni wewe ila hakikisha unapokuwa zamu kwa mke mmoja km ni siku 3 basi siku hizo wengine wanapata huduma zao km kawaida hasa chakula kama kila mwanamke anakaa kwake, ingawa wengine wanaishi pamoja nyumba moja na chakula wanakula pamoja.
 
Na ndio maana mwanamme anaweza kuzalisha hata akiwa na miaka 90 km ananguvu....
Huu ni ukweli usiopingika kuwa kuna wanaume ambao mwanamke mmoja hamtoshi...Kutokana na maumbile yao walioumbwa....

Na endapo akiwa na mwanamke mmoja huyo mwanamke hatomuweza...Huko naniiii kutachubuka kwa shughuli...Wanawake ni wakukinai mapenzi...Ila mwanaume hakinai...

umesahau pia kuna wanawake ambao mwanaume mmoja hawawezi kuwatosheleza.
 
kumhandle mmoja tu shughuli nzito halafu leo uniongezee mke mwenza! ntakupasua na chungu.

kuoa wake wengi ni kuongeza nafasi ya kuttombewa na vijana haswa wakati unapoanza kuzeeka.
Wazee wa zamani walikuwa wanajihami na msemo "kitanda hakizai haramu" lakini ukweli walikuwa wanaujua.
 
mnaongelea NDOA na KUACHANA mnasahau UPENDO. HAKUNA BINADAMU CHINI YA JUA ATAKAYESEMA ANAWAPENDA WATU WAWILI SAWASAWA KWA UPENDO ULE ULE, HATA KWA MZAZI KUNA MTOTO ANAKUWA NA MAPENZI NAE ZAIDI YA WENZIE.
KWAHIYO KWA MWANAUME YEYOTE ANAYEKUWA NA WAKE WAWILI, IWE KIDINI, KIKABILA OR WHATEVER....JUA TU NI KWA TAMAA ZAKE MWENYEWE ZA MWILI....NA NDO MAANA AKIJA WA PILI MAPENZI KWA WA KWANZA YANAPUNGUA POLEPOLE.
 
Mimi naomba nimjibu mtoa mada.. Zifuatazo ni sababu zinazopelekea wanawake wengi siku hizi kukataa kuolewa ndoa za mitara

1. Magonjwa siku hizi ni mengi jamani.... HIV klamidia kaswende fangasi.. Yamejaa kwelikweli.. Maana licha ya mwanaume kuoa wake wanne lakin bado anakuwa na michepuko
2. Wanume wajiulize wao wapo tayari kushare mke?? bas kama haiwezekani wajue kuwa wanawake wa siku hzi wanafeel hivyo... Wanajitambua tofauti na zamani
3. Kupunguzwa kwa mfumo dume.... Tunashuhudia siku hizi mwanaume na mwanamke wanashirikiana kutafuta pesa.. Wanawake wana vyeilo.. Wanawake ni wagmfanyabiashara so inakuwa ngumu sana kumpa stori za uke wenza hawez kukuelewa
4. Modernization.... Aiseh siku hizi utandawaz umebadili mambo mengi... Wanaume wengi ni wanaume suruali.. Wengine si riziki.... Wengine hawana uwezo wa kutosheleza hata mke mmoja... Maana ikumbukwe kutosheleza mwanamke ni pamoja na faragha na uchumi..... Sasa wanaume wengi nowdays kumtosheleza mmoja tu inshu then umletee mwanamke stori za kuongeza mke.. Ni dhahiri hawezi kukubali.... Kwa sababu anajua mateso yataongezeka....


UTAMADUNI HUJ KWA SASA UNAPOKELEWA ZAIDI KWA MIKOA YA PWANI.. ILA IPO SIKU UTATOKOMEA
HOJA ZAKO HAZINA MASHIKO
​
wizi,uzinzi,dhulma ,ufisadi,ulevi nk.hivi vyote vimekatazwa lakini watu wanafanya kutokana na kutojitambua ,hulka ya mtu au kupotea lakini kwa mungu kiimani kuna adhabu kubwa kwa anayefanya yalokatazwa.
mpaka mtu anaamua kuoa mke wa pili kwanza lazima awe na uwezo wa kiafya na kihali.Na hata mwanamke akikataa anakuwa anapingana na mungu kama alvyokataza mambo mengine.
- Pia hoja ya kupunguzwa mfumo dume tangu zamani wanawake walikuwa wanafanya biashara hata mtume muhammad swa kamuoa bi khadija na walikuwa wanafanya biashara ni maamuzi ya wana ndoa..
- swala la kusema wanaume wajiulize kuwa wapo tayari kushea mwanamke mmoja MIMI NI MWAUME NITAKUWA TAYARI PALE
ENDAPO MWANMKE ATAWEZA KUBEBA MIMBA MBILI ZA WANAUME WAWILI KWA WAKATI MMOJA
-Mwisho naomba nieleze moja ya faida ya kuoa wanawake wengi.
mfano mimi mungu kanijaalia afya nzuri nimeoa mke kwanza lakini ni TASA(mgumba) ,kumwaacha tasa na kutafuta mwingine au kuoa wa pili ambaye ni mzazi nikawa na wawili kipi ni bora.??
au kuna mwanamke mtaani kafiwa na mumewe na hali inamruhusu kuwa na mume kumstiri na kumwacha atange kupi ni bora??


 
Jibu ni kwamba wanawake wa kiislam wameanza kuelimika. Walikuwa wanaburuzwa saiv hawakotayari. Period
 
umekosea katika kuelezea kwenye swali lako hapo juu uliposema Qurain ndio kitabu pekee kilichoruhusu mke zaidi ya mmoja,,,nadhan sio kweli..kwani kuna sehemu kwenye biblia au kitabu kingine kimeelezea mke mmoja? kwa kusahihisha ni kwamba Qurain ndio kitabu pekee kilichotoa idadi kamili vingine havijatoa idadi kwahiyo hata dini nyingine unaweza kuoa zaidi ya mmoja..hakuna sehemu imeelezea idadi ktk biblia au maandiko mengine
 
Jamii ya kizazi hiki tunakurupuka kuvamia neno na kudaka kamstari kamoja na kuondoka nako bila kuelewa aya yote inataka nini...kwangu mie kama mie hua naangalia sana aya yote na hata vitabu vilivyosema oa kama una uwezo wa kuwahudumia ipasavyo..angalizo hapo pia ikumbukwe hata Mtume alielemea upande mmoja kwa mke anaempenda sn na ndio maana neno halikumuacha likamsema pia ila yeye exceptional sasa tuje kwetu sie tutaweza kutokuegemea pande yoyote...kwangu ni mtego yapaswa tuuangalie maana unaweza ukaoa wengi lakini kujificha tuu ili usijulikane ukawa uko kwa mmoja kutwa kucha ndio neno linataka hivyo??? Kwangu mie neno limeweka mtego kwa mwenye akili mmoja anamtosha hasa kizazi hiki kisicho na lolote kichwani....OVER
 
Jamii ya kizazi hiki tunakurupuka kuvamia neno na kudaka kamstari kamoja na kuondoka nako bila kuelewa aya yote inataka nini...kwangu mie kama mie hua naangalia sana aya yote na hata vitabu vilivyosema oa kama una uwezo wa kuwahudumia ipasavyo..angalizo hapo pia ikumbukwe hata Mtume alielemea upande mmoja kwa mke anaempenda sn na ndio maana neno halikumuacha likamsema pia ila yeye exceptional sasa tuje kwetu sie tutaweza kutokuegemea pande yoyote...kwangu ni mtego yapaswa tuuangalie maana unaweza ukaoa wengi lakini kujificha tuu ili usijulikane ukawa uko kwa mmoja kutwa kucha ndio neno linataka hivyo??? Kwangu mie neno limeweka mtego kwa mwenye akili mmoja anamtosha hasa kizazi hiki kisicho na lolote kichwani....OVER

Na ktk mapenzi huwezi mpenda mwenza zaidi ya mmoja.. Tunadanganyana tu... Moyo humpenda mmoja tu wengine unawatamani.. Ambapo kwa tafsiri yangu mi naona ni uzinzi
 
Back
Top Bottom