Kwanini Rais Samia kamtumbua Ummy Mwalimu?

Kwanini Rais Samia kamtumbua Ummy Mwalimu?

Bima ya Afya - hasa kwa watoto under 18 na mama wajawazito!!
 

Aliyekuwa Waziri wa Afya ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumpa heshima kubwa ya kuwa, Waziri wake kwa kipindi cha miaka mitatu na nusu akiitumikia nafasi ya Waziri wa TAMISEMI na baadaye Wizara ya Afya huku akisema ameyapokea mabadiliko hayo kwa moyo mkunjufu na kwa moyo wa shukrani.

Ummy ametoa shukrani hizo wakati akiongea kwenye mkutano wa ndani katika ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, ambaye ni Mlezi wa kichama katika Mkoa wa Tanga.

Chanzo: ITV Tanzania

Ungeuchuna kama Wenzako akina Makamba na Nape tungekuelewa, ila kwa Kujitetea huku ina maana Umeumia!

PIA SOMA
- Uteuzi: Lukuvi, Kabudi warejeshwa Baraza la Mawaziri, Ummy aondolewa Wizara ya Afya. TTCL, TAKUKURU zapata Mabosi wapya
 
Saikolojia inasema ummy kaumia sana na utenguzi huo, umeshatenguliwa, ofisi umekabidhi unakaa kimya, kwanza kimsingi ukivuliwa uwaziri uzoefu unaonesha hata nguvu jimboni kwako inaisha kabisa na ushawishi kutoweka hivo atulie wasichukue hata ubunge wenyewe
 
Ummy Mwalimu alijiharibia kwa tabia yake ya uswahili kumsengenya boss wako kwa njia ya simu

Ombeni Sefue aliwahi kutimuliwa ikulu usiku wamanane baada ya kudukuliwa akimsimanga JPM kwa JK.saa nane na dk 25 usiku akapigiwa simu na jiwe na kuambiwa YOU ARE FIRED

Ummy Mwalimu hakujifunza akarudia kosala Balozi Sefue.
Pamoja na kuomba msamaha na kumtuma JK ila mama amekaza fuvu hataki kumuona wala kumsikia
 
Back
Top Bottom