GE2025 Ummy Mwalimu: Siwezi kususa, naipambania CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,765
Reaction score
2,878
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga, Ummy Mwalimu, amehudhuria uzinduzi wa kampeni za kumnadi na kumuombea kura ya ndiyo Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge wa CCM katika Jimbo la Tanga, Kassim Amar M’baraka (Makubel), katika mkutano uliofanyika katika Viwanja vya Majengo, Jijini Tanga.

Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo, Ummy Mwalimu amesema hana sababu ya kususa baada ya kutopitishwa tena kuwania ubunge, kwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemheshimu na kumpa nafasi za juu katika uongozi kwa muda mrefu.

Soma pia

Ameeleza kuwa amehudumu kama Mbunge kwa miaka 15 na pia ameshika nyadhifa mbalimbali za Uwaziri kwa kipindi cha miaka 14, hivyo hana sababu ya kuwa na hasira au kukasirika, kwani kufanya hivyo ni sawa na kumkosea Mungu

“Siwezi kususa, nimsusie nani? CCM imeniheshimu sana mimi mtoto wa Kidogo. Nimehudumu kama Mbunge kwa miaka 15 na nimepewa dhamana ya kuwa Waziri kwa miaka 14. Nikikasirika, nitakuwa namkosea Mungu,” amesema Ummy Mwalimu kwa msisitizo.

Aidha, alisifu uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, akisema umetekeleza mambo makubwa na ya kihistoria yanayostahili kuendelezwa kwa maslahi ya Taifa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Jiji la Tanga waliokusanyika kusikiliza sera na mikakati ya wagombea wa CCM kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Source: Clouds
 
Asisuse anaweza kukumbukwa maana rais ana nafasi nyingi mno.
 
Screenshot_20250906-195521.png
 
View attachment 3467336
Source: Clouds
huyo ummi tatizo lake ndiyo ilo
 
Kuficha mtu Kama ummy ghafla ni kuvua bikini beach
 
Ukisusa Abdul anapita na wewe mazima
 
K

Kwa sababu unajua uko guilty, leo hii watanzania wasingejua kuwa bimkubwa ni chapombe ni sababu ya kamdomo kako lazima uwe mdogo kama Pirton.
 
Back
Top Bottom