Kwanini Rais Samia akienda nje ya nchi hapokelewi na viongozi wenzake wa juu?

Kwema jamani?

Hivi mbona Rais wetu akienda nje ya nchi anapokelewa na watu wa ajabu tu?

Mfano alivyoenda USA alipokelewa na mtu mwenye cheo sawa na mtendaji wa kata huku kwetu. Atleast alivyoenda Uganda juzi niliona wamempa mapokezi ya heshima.

Leo kaenda huko Ghana kapokelewa sijui na wakuu wa wilaya wale au sijui ni watu gani.

Mbona Rais wetu hapokelewi kiheshima jamani?

Hii ndio heshima aliyostahili, unataka heshima gani tena. Nonsense
 
simkubali mama ila kwenye hili GHANA wametukosea adabu.

kuna watu wanajenga hoja kwamba itakuwa haikuwa ziara rasmi,sawa.
lakini ndio watuwekee wapokeaji wasio rasmi!!!!watu walikuwa na mishe zao wakapigiwa simu oyaaa kuna mgeni airport mkampokee mumpeleke hoterini.
kama tunadharauliana wenyewe kwa wenyewe hakuna mtu mweupe atajipa muda na sisi.
 
Kwema jamani?

Hivi mbona Rais wetu akienda nje ya nchi anapokelewa na watu wa ajabu tu?

Mfano alivyoenda USA alipokelewa na mtu mwenye cheo sawa na mtendaji wa kata huku kwetu. Atleast alivyoenda Uganda juzi niliona wamempa mapokezi ya heshima.

Leo kaenda huko Ghana kapokelewa sijui na wakuu wa wilaya wale au sijui ni watu gani.

Mbona Rais wetu hapokelewi kiheshima jamani?

daaaah
 
Hv wanawezaje kuja kumpokea mtu anazurura waache kufanya kazi za kusimamia viwanda vikubwa,Wazungu na mataifa mengine yenye akili hawanaga ujinga wa kiafrika ambao bado umekumbatiwa na viongozi wengi wa kiafrika.
 
Kwani lazima Rais Mwenyeji aje akupokee yeye personal?

Subiria Activities zinazojiri ndio utajua
wengi hamjui protocal ni kitu gani.

hiyo tafsiri yake rais mwenyeji yuko busy,basi atume maofisa waandamizi.
makamu,spiker,au jaji sio huyo jamaa na maraba yake ya cossovo.
 
apunguze safari za nje. kitu adimu hutakwa na wengi. she has become too common, mfano alikwenda rwanda, lakini kagame alituma messenger tu. Kenya vile vile hata DRC.....someone should tell her to recheck her trips
 
Hapa TZ kwani huo uzi umeletwa na mtu kutoka Ghana?? Mtu anasema mavazi ya waliompokea sio mazuri vipi MUSEVENI anavaa vizuri??
Tanzania mama hachukiwi ndiyo maana akirudi nchini anapokelewa vizuri. Labda huko Ghana ndo wanamchukia ndo mapokezi yale, labda lakini.
 
S I J A P E N D A

Kuna heshima alitakiwa aitengeneze kwanza ndipo aanze kuzurura..

JPM alikuwa anapokelewa kama Rais kwasababu hakuwa anazurura sana
 
Ndugu, hao sio kwamba wanampokea bali anatambulishwa kwao. Kama inavyoonekana, Mhe. Rais tayari keshapokelewa, kinachoendelea hapo ni utambulisho kwa viongozi mbali mbali waliojitokeza katika mapokezi hayo.
 
Asiseme ukweli???
Kwan hiyo picha si imejieleza, angalia hata wearing style ya waliompokea, huoni kama wametoka kwenye vikoba??
Alaf kweli hivi raisi anakuja kupokelewa na watu wamevaa raba au huko wanajua wametembelewa na moja ya watendaji wa mtaa wa huku tanzania
 
Back
Top Bottom