Kwanini Rais Samia akienda nje ya nchi hapokelewi na viongozi wenzake wa juu?

kyanyangwe

JF-Expert Member
Oct 31, 2018
1,147
2,746
Kwema jamani?

Hivi mbona Rais wetu akienda nje ya nchi anapokelewa na watu wa ajabu tu?

Mfano alivyoenda USA alipokelewa na mtu mwenye cheo sawa na mtendaji wa kata huku kwetu. Atleast alivyoenda Uganda juzi niliona wamempa mapokezi ya heshima.

Leo kaenda huko Ghana kapokelewa sijui na wakuu wa wilaya wale au sijui ni watu gani.

Mbona Rais wetu hapokelewi kiheshima jamani?

Screenshot_20220523-202945_Instagram.jpg
 
Kwema jamani?
Hivi mbona Rais wetu akienda nje ya nchi anapokelewa na watu wa ajabu tu?
Mfano alivyoenda USA alipokelewa na mtu mwenye cheo sawa na mtendaji wa kata huku kwetu.atleast alivyoenda uganda juzi niliona wamempa mapokezi ya heshima.
Leo kaenda huko Ghana kapokelewa sijui na wakuu wa wilaya wale au sijui ni watu gani.
Mbona Rais wetu hapokelewi kiheshima jamani?

View attachment 2236003
Kwanini ikulu hawakuwataja hao “viongozi mbali mbali” wa huko Ghana? Waziri wa mambo ya nje nk bado wanaweza kuwa viongozi mbali mbali.
 
Hata hivyo sisi ndio huwa tunawatetemekea viongozi wengine. Hiyo ndio njia ya kawaida ya kupokea viongozi. Hapa kwa ajili ya kuendekeza propaganda ndio hujikuta viongozi tunawapokea kwa kuwatetemekea. Huko viongozi wa wenzetu huwa wanaingia madarakani kwa ridhaa ya wananchi wao, hivyo hawana muda wa kuwaonyesha wananchi wao kuwa wamepata wageni.
 
Bila kumtukana mleta hoja,Picha zinaonyesha kabisa.Bora angepokelewa hata kimyakimya.Hayo mapokezi ya wenyeji hayajakaa kidplomasia kabisa.Huyo mmoja kama mpiga debe alochangamka.Hakustahili kabisa kuwa kwenye hiyo foleni.
Labda hiyo safari siyo rasimi kwa serikali ya Ghana. Kama ilivyokua Royal Tour, ile safari haikua rasimi kwa Rais wa Marekani ndiyo maana hakupokelewa na Biden. Hiyo ya Ghana kwa picha hiyo, kama ndiyo yenyewe, mapokezi hayo si ya level ya Rais wa nchi.

Cc kagoshima usitukane watu kwenye ukweli.
 
Back
Top Bottom