Kwanini Mwanza isipate Uwanja mzuri wa mpira?

Kwanini Mwanza isipate Uwanja mzuri wa mpira?

View attachment 3289939View attachment 3289940
KWANINI Mwanza isipatiwe kiwanja cha mpira kizuri kama jiji la Dar, Arusha na Dodoma.

1.Mwanza ni jiji la pili Tanzania kwa watu wengi

2.Mwanza inatoa vipaji vya mpira vingi sanaa kama Aisha masaka,mrisho ngasa na wengine wengi.

3.Mwanza pia ni jiji lenye vivutio vya utalii pia na ni central ya mikoa ya kanda ya ziwa

4.Mwanza pekee ndio jiji lenye stendi mbili za mabasi pia uwepo wa usafiri wa aina zote ndege,bus,Maji na kadhalika.

5.Mwanza ina vibe sana mtupe uwanja msitubainie ata sisi tunataka kiwanja cha mpira hii nchi isijengwe upande mmoja tu.
Sisi atuhitaji gofu la CCM kirumba tu nahitaj kiwanja cha umma.

Capacity ya uwanja watu elfu 70.
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Na iitwe fish stadium 🏟
Kwingine hakuna stendi hata moja nyie mnazo 2
 
..badala ya Dodoma wangepeleka mashindano Mwanza.

..pia Mwanza inastahili uwanja wa ndege wenye hadhi ya kimataifa.
Kwani Dodoma Kuna Afcon?

Harafu ni ujinga kulinganisha Capital City na uswazi city
 
View attachment 3289939View attachment 3289940
KWANINI Mwanza isipatiwe kiwanja cha mpira kizuri kama jiji la Dar, Arusha na Dodoma.

1.Mwanza ni jiji la pili Tanzania kwa watu wengi

2.Mwanza inatoa vipaji vya mpira vingi sanaa kama Aisha masaka,mrisho ngasa na wengine wengi.

3.Mwanza pia ni jiji lenye vivutio vya utalii pia na ni central ya mikoa ya kanda ya ziwa

4.Mwanza pekee ndio jiji lenye stendi mbili za mabasi pia uwepo wa usafiri wa aina zote ndege,bus,Maji na kadhalika.

5.Mwanza ina vibe sana mtupe uwanja msitubainie ata sisi tunataka kiwanja cha mpira hii nchi isijengwe upande mmoja tu.
Sisi atuhitaji gofu la CCM kirumba tu nahitaj kiwanja cha umma.

Capacity ya uwanja watu elfu 70.
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Na iitwe fish stadium 🏟
Sera ya awamu hii inasemaje kuhusu ujenzi wa Kiwanja pande hizo
 
Huo uwanja utasaidia kupunguza umasikini kwa wananchi? tena wa haoo hapo mwanza? Mbona Taifa limejaaa wajinga hivi? kwa hio kwa akili zako unaona viwanja vya mpira ni kipa umbele cha maana sana, Nchi ina pimbi wengi sana
Wewe ndo ujielewi ndo maana haujui kama mpira ni industry ya kibiashara kama utalii.Nakujibu ndio kiwanja kizuri kinaondoa umasikini kama unataka kujua uliza usahidiwe.
 
Kwa hiyo Dodoma na Arusha waweze kuutunza na kupata timu ya kuchezea harafu Mwanza mji mkubwa ukose? Acha utoto!
Arusha umewekwa strategic(utalii), dodoma(makao makuu)

Mwanza ina infulence gani, au strategic vision ya nchi ambayo iko hapo?
 
Kuna hoja hapa
Mashindano ya AFCON , Mwanza ilitakiwa ipewe nafasi
1. Dodoma- Capital na ni njia mojawapo ya kuendeleza Jiji. Inafikika na watu wa kanda zote
2. Dar es Salaam- Hii inaeleweka kwanini! Jiji la Biashara
3. Arusha- Jiji kubwa na makao makuu ya EA. Kuna utalii
4. Zanzibar- Aman inaingiza watu 30,000, imepewa kwasababu ya Muungano! na kwa gharama za Mwanza

Kwanini Mwanza
  • Idadi ya watu wanaoweza kujaza Uwanja hata kufikia 100,000
  • Imekaa vizuri kufikika kutoka Kisumu, Kampala, Bujaumbura, Kigali hata DRC
n.k.

JokaKuu @
Ni swala la muda tu, kwa sababu sifa zote za kuwa na uwanja mkubwa mzuri zipo.
Kwa upande mwingine ni vizuri kutofanya mambo kwa harakaharaka na kufanya kitu kisicho stahili kufanywa.

Wakati utakapo wadia, (si mbali sana na sasa), uwanja huo utajengwa; uwanja unao kidhi vigezo vyote vya kimataifa.
 
Arusha umewekwa strategic(utalii), dodoma(makao makuu)

Mwanza ina infulence gani, au strategic vision ya nchi ambayo iko hapo?
Wewe bado huijui 'strategic location' inayo shikiliwa na Mwanza?
 
Aisee mimi nikusahidie tu kwa utawala huu wa awamu ya sita kitu kama hicho hakiwezi kufanyika Mwanza labda viongozi wa serikali hii waamue kuokoka.Hakuna siku niyojifeel vibaya kama siku Rais Mama Samia alipokuja kuzindua hotel ya nssf Mwanza akumuuliza mkurugenzi wa nssf kwanini wamejenga hii hotel Mwanza nae mkurugenzi akajitetea pale.Nikahisi huyu mama anaiona Mwanza ni Burundi 🇧🇮 🤣🤣Mfano mwingine ni barabara ya cbd to usagara waziri alikuja akapiga kelele pale buhongwa akasema mama ametoa hela tarehe 15 mwezi 3,2025 mkataba unasaini🤣🤣🤣tar 15 bado mpaka leo zaidi naona pale Mkuyuni naonajJASCO anaangaika kuchafua barabara..Watu wa Mwanza tafuteni hela mjenge majumbani kwenu acheni serikali waangaike na mambo yao.
 
Ndiyo veta watu wachape kazi. We unakuta kijana mzima ana lilia hotel ya nyota tano sijuwi Arena. Unahisi ni kwaajili ya nini hayo ni matoke ya uvivu. Watu wavue na kulima hadi kusafirisha nje ya nchi.
Wewe unamatatizo,watu wanaofanya kazi kwenye hotel za nyota tano hawachapi kazi??Au watu wanoenda veta kusoma hotel management wanasoma ili wawe mamantilie wapigwe virungu na mgambo??Panua ubongo ndugu usipende kila mtu ajui ujinga wako.Au unataka wakimaliza kulima na kuvua waendewapi au kodi wanazolipa zifanye kazi gani,??Ndo maana wazungu wanatuona sisi nyani kwasababu ya kuamini kafanya kazi ni kuangaika tu.Na vitu vizuri ni kwaajili ya watu fulani na ikitokea kitu kizuri tunakinyea kinyesi kukomoa waliokiweka bila kujali anakitumia nani na hadi viongozi wetu waishakuwa wa hivyo ndo maana vitu vizuri vyote viko Dar na Arusha au Dodoma kwasababu wao wako huko na familia zao.
 
MWANZA Pia inahitaji uwanja Mkubwa, Labda tulejee hapo nyuma kidogo kabla Ben Mkapa haijajengwa Baadhi ya Mashindano Makubwa yaliletwa Mwanza CCM kirumba na tuliona ikitapika Sababu ni ilifikika kwa Urahisi Watu kutoka Geita, Shinyanga, Mara,Kagera na hata Tabora waliweza kufika na kuondoka kwa urahisi, Pili Mikoa hii ina idadi kubwa ya watu si chini ya 15 Millioni na wapenda Soka ni wengi, Tatu ni karibu na Kisumu, Kampala, Bujumbura, Kigali na Drc
 
Tutaomba pesa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2025/2026 ili tuboreshe CCM Kirumba Stadium! Na hili kila mwana Mwanza analiunga mkono. Uwanja upo katikati ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. Jirani kuna Rock City Mall na View nzuri ya Ziwa Victoria. CCM Kirumba Stadium kwakweli inatosha!
Huo ni uwanja wa CCM hizo pesa za maboresho kaziombeni CCM

Tunataka uwanja wa UMMA
 
Kwani Dodoma Kuna Afcon?

Harafu ni ujinga kulinganisha Capital City na uswazi city

..mambo ya michezo, mpira wa miguu, ni tofauti na mambo ya kiserikali.

..Dodoma inahitaji ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa kuliko Mwanza.

..wakati Mwanza inahitaji uwanja wa kimataifa wa mpira kuliko Dodoma.

..kupanga ni kuchagua.

Cc Nguruvi3
 
Nimekuuliza hapo, natarajia jibu
Sasa mkuu 'Detective j.', hivi kweli hili nalo unataka liwe ni jambo la kuvutana hapa kati yako na mimi? Huwezi tu kutumia akili yako ya kawaida kupata jibu?

Sasa kama unajuwa 'strategic status' ya huko kwingine, ni kitu gani kinakushinda kujuwa umuhimu wa Jiji la Mwanza hapo lilipo kijiografia?
Kwani kuwa 'strategic', ni mpaka pawepo na nini; wewe unavyo vigezo ambavyo unaona nje ya hivyo vigezo hakuna zaidi ya kufanya mahala pakawa na umuhimu wake?
 
Ni kweli Mwanza kwakua ni jiji la pili kwa ukubwa tz bara wanahitaji kiwanja cha mpira sema ndo hvyo wenzenu wa Arusha wamepata fursa kwa kuwa na hotel nyingi za kisasa. Watu wa mwanza sasa hv mngeomba brt au Tram kurahisisha usafiri kwenye jiji na kufanya jiji lenu liwe la kisasa zaidi.
 
Sasa mkuu 'Detective j.', hivi kweli hili nalo unataka liwe ni jambo la kuvutana hapa kati yako na mimi? Huwezi tu kutumia akili yako ya kawaida kupata jibu?

Sasa kama unajuwa 'strategic status' ya huko kwingine, ni kitu gani kinakushinda kujuwa umuhimu wa Jiji la Mwanza hapo lilipo kijiografia?
Kwani kuwa 'strategic', ni mpaka pawepo na nini; wewe unavyo vigezo ambavyo unaona nje ya hivyo vigezo hakuna zaidi ya kufanya mahala pakawa na umuhimu wake?
Problem with wabongo bwana, swali linajibiwa na swali si jibu. Hii analogy i dont know imetokea wapi haha

Labda nikurahisishie, mwanza ika kipi unique that mikoa mingine haina that wa deserve kujengewa uwanja wa kisasa?
 
Back
Top Bottom