Kwanini Mwanza isipate Uwanja mzuri wa mpira?

..badala ya Dodoma wangepeleka mashindano Mwanza.

..pia Mwanza inastahili uwanja wa ndege wenye hadhi ya kimataifa.
Dodoma naelewa, kwamba, ni Capital city kunahitajika ''infrastructure'' isije ikawa yale ya uwanja wa Taifa kabla ya BWM

Zanzibar ipo karibu na DSM , nafasi ingepewa Mwanza. Kupeleka Zanzibar ni '' siasa za Muungano''

Mombasa wana andaa! DSM wana andaa. Hakuna shabiki atakayekwenda Zanzibar
Mwanza, kuna mashabiki wote wa EA kuanzia Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, DRC, Sudan n.k.

Mwanza wamedhulumiwa sana! hata ukiangalia GDP , Mwanza na kanda ya Ziwa wana mchango
 
Hivi viwanja khasa vikubwa kama CCM Kirumba yatakiwa kuuzwa kwa sekta binafsi au kuendeshwa kwa ubia na sekta hiyo kati ya wizara ya michezo na wawekezaji wawe wa ndani au nje.

Pili, timu za soka za mikoa zipewe uwezo wa kumiliki kwa ubia na serikali kupitia Halmashauri ya jiji kwani kupitia ubia huo kiwanja kitaendeshwa kisasa na kwa ufanisi.

Serikali haiwezi kumiliki viwanja vyenye hadhi duni lakini sekta binafsi ikipewa iviendeshe kwa ubia itaweza kufanya hivyo kwani viwanja vitakuwa na vitega Uchumi ndani yake kama hoteli, kumbi za mikutano na maduka makubwa.

Ni wakati umefika kwa serikali kuachana na umiliki wa hivi viwanja kama CCM Kirumba au la iviendeshe kwa ubia ambapo masuala kama Uchumi utakuwa, ajira zitaongezeka na pia serikali itapa kodi.

Umefika wakati wa kufikiri nje ya boksi.
 
View attachment 3289939View attachment 3289940
KWANINI Mwanza isipatiwe kiwanja cha mpira kizuri kama jiji la Dar, Arusha na Dodoma.

1.Mwanza ni jiji la pili Tanzania kwa watu wengi

2.Mwanza inatoa vipaji vya mpira vingi sanaa kama Aisha masaka,mrisho ngasa na wengine wengi.

3.Mwanza pia ni jiji lenye vivutio vya utalii pia na ni central ya mikoa ya kanda ya ziwa

4.Mwanza pekee ndio jiji lenye stendi mbili za mabasi pia uwepo wa usafiri wa aina zote ndege,bus,Maji na kadhalika.

5.Mwanza ina vibe sana mtupe uwanja msitubainie ata sisi tunataka kiwanja cha mpira hii nchi isijengwe upande mmoja tu.
Sisi atuhitaji gofu la CCM kirumba tu nahitaj kiwanja cha umma.

Capacity ya uwanja watu elfu 70.
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Na iitwe fish stadium 🏟
Huo uwanja utasaidia kupunguza umasikini kwa wananchi? tena wa haoo hapo mwanza? Mbona Taifa limejaaa wajinga hivi? kwa hio kwa akili zako unaona viwanja vya mpira ni kipa umbele cha maana sana, Nchi ina pimbi wengi sana
 
Sawa Mkuu. Kwanini tujenge kingine ingali hiki kipo? Kiboreshwe tu!
Ase nyie watu mna mawazo ya kizamani why kukarabati uwanja wa chama cha siasa kwa Fedha za umma.

Location ya kirumba ni mbovu sana kuna eneo tamu la sabasaba Karibu na mbao pale eneo la TBC pawekwe kiwanja good location kabisa ila kwa akili zenu.
 
Kama uligundua JIWE aliipenda sana Mwanza alianzisha Miradi mingi sana hata SGR bila kufosi isingefika Mwanza...Kwa muhula huu wa Kizimkazi Mwanza itapata tabu sanaa yaani hasa uwaambie swala la Uwanja hawawezi kuelewa zaidi watatoa 100M uwanja upigwe rangi ya bendera za TZ alafu ndio imeisha iyo
Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania na hata ukitafuta mbia au mwenza wa biashara ukimwambia kuna jiji kama Mwanza na ina watu wa kutosha atachosema akilini mwake ni fursa na rasilimali watu.

Hivyo Mwanza yahitaji hoteli moja ya Nyota tano, uwanja wa ndege wa kimataifa, uwanja wa kisasa wa michezo na vitega Uchumi vingine vya maana.
 
Huo uwanja utasaidia kupunguza umasikini kwa wananchi? tena wa haoo hapo mwanza? Mbona Taifa limejaaa wajinga hivi? kwa hio kwa akili zako unaona viwanja vya mpira ni kipa umbele cha maana sana, Nchi ina pimbi wengi sana
Mkuu kwa heshima zote nakuomba ujifunze kupanua Mawazo yako.

Fikiria nje ya boksi.

Kuna kitu chaitwa "micro economics" yaani waangalia rasilimali chache utazitumia vipi kuzigeuza kuwa vitega uchumi ambavyo vitaleta faida kwa kila mtu na si mtu mmoja mmoja.

Kwa kuwa sisi watanzania hatujawa na uwezo wa kufikiri "big" ukipata watu ambao watafikiri hii Big watakuambia Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa, ina idadi kubwa ya wananchi na ni fursa kwa biashara za aina Fulani na si biashara zote.

Hivyo hata wawekezaji hufanya kitu chaitwa "PESTLE analysis" tathmini ya kuangalia target markets zilizo nje ya pale walipo kuangalia mambo kama haya.

Moja ya mambo yanowazuia wawekezaji wa nje ni miundombinu bora hivyo akienda Mwanza kwa basi siku inofuata atarudi kwao akiwa mnyonge.
 
View attachment 3289939View attachment 3289940
KWANINI Mwanza isipatiwe kiwanja cha mpira kizuri kama jiji la Dar, Arusha na Dodoma.

1.Mwanza ni jiji la pili Tanzania kwa watu wengi

2.Mwanza inatoa vipaji vya mpira vingi sanaa kama Aisha masaka,mrisho ngasa na wengine wengi.

3.Mwanza pia ni jiji lenye vivutio vya utalii pia na ni central ya mikoa ya kanda ya ziwa

4.Mwanza pekee ndio jiji lenye stendi mbili za mabasi pia uwepo wa usafiri wa aina zote ndege,bus,Maji na kadhalika.

5.Mwanza ina vibe sana mtupe uwanja msitubainie ata sisi tunataka kiwanja cha mpira hii nchi isijengwe upande mmoja tu.
Sisi atuhitaji gofu la CCM kirumba tu nahitaj kiwanja cha umma.

Capacity ya uwanja watu elfu 70.
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Na iitwe fish stadium 🏟
Hoja yako imekaa kitamaa tamaa sana na si kimipango. Serikali Ina watalaamu wa kila aina. Hadi hivyo Viwanja vinajegwa kwenye hayo maeneo si kwa BAHATI mbaya.
Ningekuona una maana kama ungeomba serikali iboreshe pembejeo za kilimo na wavuvi kupatiwa Zana bora za uvuvi kwaajili ya kusaidia maendeleo ya wananchi.Au hata mngeomba vyuo vya veta kuongezewa fedha na kuboresha vilivyopo ili vipokee vijana wengi kutoka vijiji vya kanda ya ziwa na siyo kulilia viwanja kama vile utakula mpira.
 
Ase nyie watu mna mawazo ya kizamani why kukarabati uwanja wa chama cha siasa kwa Fedha za umma.

Location ya kirumba ni mbovu sana kuna eneo tamu la sabasaba Karibu na mbao pale eneo la TBC pawekwe kiwanja good location kabisa ila kwa akili zenu.
Hivi viwanja wapewe sekta binafsi ambayo ina mtaji mkubwa na Mawazo makubwa au viendeshwe kwa ubia kati ya serikali na wawekezaji.

Ingekuwa amri yangu hivyo viwanja wangepewa halmashauri waviendeshe maana viwanja hivyo Kirumba, Sokoine, Jamhuri na vingine vina hali mbaya sana.
 
Mwanza ni jiji la pili kwa ukubwa Tanzania na hata ukitafuta mbia au mwenza wa biashara ukimwambia kuna jiji kama Mwanza na ina watu wa kutosha atachosema akilini mwake ni fursa na rasilimali watu.

Hivyo Mwanza yahitaji hoteli moja ya Nyota tano, uwanja wa ndege wa kimataifa, uwanja wa kisasa wa michezo na vitega Uchumi vingine vya maana.
Hiyo hotel ya nyota tano una fedha za kuingia kupata huduma humo au unataka sehemu ya kupiga picha? Uwanja uliokuwepo unatosha sana mbona? Au una timu yako imekatazwa kutumia uwanja uliokuwepo? Kila mkoa ni muhimu kwahiyo na sisi huku Ruvuma tuseme je?
 
Hivi viwanja wapewe sekta binafsi ambayo ina mtaji mkubwa na Mawazo makubwa au viendeshwe kwa ubia kati ya serikali na wawekezaji.

Ingekuwa amri yangu hivyo viwanja wangepewa halmashauri waviendeshe maan viwanja hivyo Kirumba, Sokoine, Jamhuri na vingine vina hali mbaya sana.
Ndio hilivyo kwa namna nyingine naona kama wanakwamisha ili wapate wao
 
Hiyo hotel ya nyota tano una fedha za kuingia kupata huduma humo au unataka sehemu ya kupiga picha? Uwanja uliokuwepo unatosha sana mbona? Au una timu yako imekatazwa kutumia uwanja uliokuwepo? Kila mkoa ni muhimu kwahiyo na sisi huku Ruvuma tuseme je?
Mwanza tunahitaji football stadium na arena ya matamasha ndio hivyo.
🔥🔥🔥🔥🔥😁
 
Hoja yako imekaa kitamaa tamaa sana na si kimipango. Serikali Ina watalaamu wa kila aina. Hadi hivyo Viwanja vinajegwa kwenye hayo maeneo si kwa BAHATI mbaya.
Ningekuona una maana kama ungeomba serikali iboreshe pembejeo za kilimo na wavuvi kupatiwa Zana bora za uvuvi kwaajili ya kusaidia maendeleo ya wananchi.Au hata mngeomba vyuo vya veta kuongezewa fedha na kuboresha vilivyopo ili vipokee vijana wengi kutoka vijiji vya kanda ya ziwa na siyo kulilia viwanja kama vile utakula mpira.
Mkuu, hao wataalam wako wapi?

Hivi wafahamu kwanini sekta ya michezo kwa mfano sasa hivi imebadilika?

Yaani twaona wasichana, walemavu wakishiriki michezo na wasichana sasa wacheza mpira na ni kama ajira.

Huu ni mkakati kwamba Vijana kupata ajira huwa ni tatizo na ukiliachia laweza kuleta matatizo kwenye jamii iliyopo.

Ndo maana twaona hata wasichana huko Ulaya wacheza mpira mpaka ule wa Champions league kwani unakuza vipaji, kukuza Uchumi na pia kusaidia Vijana na jamii kujikwamua kiuchumi.

Huko ndiko kufikiria nje ya boksi.

Sasa hapa Tanzania Vijana walalamika hawana ajira ni hili ni jeshi hili ambalo sasa lapoteza nguvu nyingi kwenye mambo yaso na maana.

Mtu ajitokeza asema waende VETA lakini asahau, huyu Kijana akimaliza VETA ana uhakika wa kupata ajira?
 
Mkuu, hao wataalam wako wapi?

Hivi wafahamu kwanini sekta ya michezo kwa mfano sasa hivi imebadilika?

Yaani twaona wasichana, walemavu wakishiriki michezo na wasicha sasa wacheza mpira na ni kama ajira.

Waende VETA 😁
 
Ndiyo maana nasema hamasisha vijana hapo kijijini kwenu angalau waende veta kuliko kulilia na kulalama kwa vitu ambayo hata visipo kuwepo haitakuwa na athari kwa wananchi. Bado tunategemea kilimo na Uvuvi kuendesha maisha yetu ya kila siku.
 
Unaacha kusema Mbeya ambayo inaweza pandisha timu tatu ligi kuu kwa msimu mmoja unaisemea pamba jiji.
 
Waende VETA 😁
Yes, wawahimiza Vijana waende VETA lakini VETA ipo tangu ilipoanzishwa ila mtu akifuzu anakuwa hana uhakika wa ajira.

Lakini Waziri wa michezo akiketi na washauri wake wakaja na proposal ya kubadili sekta ya michezo iendeshwe kiufanisi zaidi na kwa faida ya taifa na Uchumi litakuwa jambo jema.

Narudia tena, hivi viwanja vipewe sekta binafsi inojitambua Katika masuala la macro economics ili kunyanyua masuala kama ajira ambayo ni tatizo kubwa kwa sasa ingawa lapigwa pazia.
 
Back
Top Bottom