Kwanini Mwanza isipate Uwanja mzuri wa mpira?

Kwanini Mwanza isipate Uwanja mzuri wa mpira?

View attachment 3289939View attachment 3289940
KWANINI Mwanza isipatiwe kiwanja cha mpira kizuri kama jiji la Dar, Arusha na Dodoma.

1.Mwanza ni jiji la pili Tanzania kwa watu wengi

2.Mwanza inatoa vipaji vya mpira vingi sanaa kama Aisha masaka,mrisho ngasa na wengine wengi.

3.Mwanza pia ni jiji lenye vivutio vya utalii pia na ni central ya mikoa ya kanda ya ziwa

4.Mwanza pekee ndio jiji lenye stendi mbili za mabasi pia uwepo wa usafiri wa aina zote ndege,bus,Maji na kadhalika.

5.Mwanza ina vibe sana mtupe uwanja msitubainie ata sisi tunataka kiwanja cha mpira hii nchi isijengwe upande mmoja tu.
Sisi atuhitaji gofu la CCM kirumba tu nahitaj kiwanja cha umma.

Capacity ya uwanja watu elfu 70.
🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥
Na iitwe fish stadium 🏟
Ni kwa sababu Mwanza ina wapiga kura wengi sana wa CCM, sehemu yenye wapiga kura wengi huwa haipaswi kupelekewa maendeleo makubwa sanaaaa!!!
 
Tutaomba pesa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2025/2026 ili tuboreshe CCM Kirumba Stadium! Na hili kila mwana Mwanza analiunga mkono. Uwanja upo katikati ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. Jirani kuna Rock City Mall na View nzuri ya Ziwa Victoria. CCM Kirumba Stadium kwakweli inatosha!
Bajeti ya serikali kuboresha uwanja wa chama?
 
Mwambien mkurugenz wa manispaa ajenge.

Huku treusury house balance ni negative trillions, hata toilet paper hatuwez nunua mpaka wahisan watusaidie..!
 
Kwasababu Uchaguzi wa Tanzania ni wa hovyo!

Kataa Uchaguzi bila reforms!
 
Mbeya ndo wanastahil kiwa na uwanja wa kisasa coz kila msimu wana timu mbili au tatu ligi kuu
 
Wanachadema, Wana ACT WAZALENDO, Wana CUF, Wana APPT MAENDELEO na wengineo hawaingiagi CCM Kirumba kuangalia mechi au matamasha ya michezo au muziki?
Comment ya kiwango cha chini sana hii, nisamehe ndg. Kwani zile fremu na maduka mengi ya chama yaliyopo sehemu mbalimbali wanachama wengune hawaendi kununua pale vitu? So tutatengee bajeti ya serikali kuyaboresha?
 
Ndio.
 
Kama uligundua JIWE aliipenda sana Mwanza alianzisha Miradi mingi sana hata SGR bila kufosi isingefika Mwanza...Kwa muhula huu wa Kizimkazi Mwanza itapata tabu sanaa yaani hasa uwaambie swala la Uwanja hawawezi kuelewa zaidi watatoa 100M uwanja upigwe rangi ya bendera za TZ alafu ndio imeisha iyo
Inauma sana sana mwanza yangu jamani
 
Tutaomba pesa kwenye Bajeti ya Serikali ya 2025/2026 ili tuboreshe CCM Kirumba Stadium! Na hili kila mwana Mwanza analiunga mkono. Uwanja upo katikati ya Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela. Jirani kuna Rock City Mall na View nzuri ya Ziwa Victoria. CCM Kirumba Stadium kwakweli inatosha!
Ni faraja kupata watanzania wenye akili kubwa
Hayo mabilioni kujenga uwanja mwingine yanaweza kusaidia sekta nyingine
Viwanja vya arusha na dodoma vilikua vidogo sana na chakavu tofauti na kirumba mkubwa unaowezà kubeba hadi watu 35k
Ikumbukwe viwanja vya arusha na dodoma vyote havitafkisha idadi ya ccm kirumba
Kikubwa kirumba pafanyiwe marekebisho kama amaan zanzibar wafunike juu, waweke taa za usiku na viti patapendeza sana ikichagizwa na location yake itakaa poa sana
 
Ahsante. Na kama CCM Kirumba ingeliboreshwa mapema hata mechi ya Simba na Berkane ingelichezewa hapo na washabiki zaidi ya hamsini elfu wangeliingia!
 
5.Mwanza ina vibe sana mtupe uwanja msitubainie ata sisi tunataka kiwanja cha mpira hii nchi isijengwe upande mmoja tu.
Sisi atuhitaji gofu la CCM kirumba tu nahitaj kiwanja cha umma.
Kumbe jibu unalo mwenyewe tayari.

Kijengwe kiwanja na CCM watapeleka wapi hilo "gofu" lao!

Mwanza kuwa na uwanja mzuri wa michezo ni swala la muda tu; na kwa kweli ni bora kusubiri kidogo kuliko kukimbilia ujenzi wa kitu kisichokuwa na hadhi stahiki.

Hakunamtu au kiongozi mwenye uwezo wa kuzuia Mwanza isiwe na uwanja mzuri. Ni wahusika tu wa eneo hilo kujipanga na kuwa tayari kutekeleza ujenzi wa uwanja wa sifa wanaoutaka wao.
Hakuna sababu ya kuletewa toka nje, kama Arusha walivyo lazimishwa wakidhani wamependelewa!
Jipangeni na michoro mnayoitaka wenyewe, halafu anzeni kampeni ya kuujenga uwanja wenu.
 
Ahsante. Na kama CCM Kirumba ingeliboreshwa mapema hata mechi ya Simba na Berkane ingelichezewa hapo na washabiki zaidi ya hamsini elfu wangeliingia!
Ni kama ninakuona hapo, "kwenye kona ya Bwiru".
Sasa nikushauri, kaa kwenye haya haya, achana na ya siasa.

Hapo "CCM kubadilishwa"; hapo hapafai tena, kujengwa uwanja wenye hadhi ya kimataifa.
Tafuteni eneo jingine kungali mapema. Mji unapanuka haraka sana. Mwishowe mtaupeleka uwanja Magu?
 
Kwa hiyo Dodoma na Arusha waweze kuutunza na kupata timu ya kuchezea harafu Mwanza mji mkubwa ukose? Acha utoto!
Kuwa na akili bwana mdogo. Unataka kulinganisha Mwanza na Arusha au Dom?

Arusha ni mji wa kitalii na unawakilisha kanda ya kaskazini.

Dom ni makao makuu ya nchi

Kama ni kugawa kama pipi basi Mbeya, Kigoma na Kagera nao wangelalamika.

Wewe endelea na chaghulagha
 
..badala ya Dodoma wangepeleka mashindano Mwanza.

..pia Mwanza inastahili uwanja wa ndege wenye hadhi ya kimataifa.
Ni swala la muda tu; na kwa kweli kunakosemwa "kuchelewa", ni bora kuliko kukimbizana na kupata kisichokuwa na hadhi stahiki.
Ni swala la viongozi wa Mwanza wenyewe kuchukua jukumu la kuandaa kinachotakiwa kujengwa hapo, na kukisimamia kitokee hapo.
They have leverage.
 
Tatizo nini hapo? Uwanja wa Arsenal wa Emirates umezungukwa na biashara kibao. Umeacha kuwa Uwanja? Kama gereji zinakukera bali unataka Villa Park irudi ili upate madada poa kwa bei poa, sawa tu itarudi. Mteja ni mfalme!
Kwani imeenda wapi
 
Ni kama ninakuona hapo, "kwenye kona ya Bwiru".
Sasa nikushauri, kaa kwenye haya haya, achana na ya siasa.

Hapo "CCM kubadilishwa"; hapo hapafai tena, kujengwa uwanja wenye hadhi ya kimataifa.
Tafuteni eneo jingine kungali mapema. Mji unapanuka haraka sana. Mwishowe mtaupeleka uwanja Magu?
Njoo Diamond hapa unywe Konyagi ukisubiria mechi ya Simba.
 
Back
Top Bottom