Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Nimelelewa na baba wa kambo, na pia nimeishi na mama wa kambo at some point... nna experience zote zote.

mmh we ni mnyiramba nini ha ha ha joke!!!!
haya buana ila ni mara chache sana mwanaume kukaa na mtoto wa kambo
 
Kila nikiomba kwa imani yangu huwa namshukuru Mungu alivyonitoa shimoni kwa kumfumbua macho mzee wangu!
Yule Mama hakuwa binadamu wa kawaida! Niliponea tundu la sindano! Mtu unapigwa huwezi kutembea wala kutambaa na hakuna kupewa chakula umefungiwa stoo kisa ni kukutwa na picha ya marehemu mama yangu, picha pekee iliyokuwa na sura yake! Kipimo chake cha kuacha kupiga ilikuwa ni pale unapokuwa huwezi kuMove kabisa au umeFaint!
Mungu ni Mwema, hakuniacha pamoja na mateso yale!

Yaani machozi yamenitoka pasipo kutarajia. Pole sana aisee. Na hii ilikua ukiwa na umri gani? Dah!
 
Wanawake sisi......!Mungu atuhurumie kwa kweli. Unakuta mtu anafanya juu chini avuruge ndoa ya mtu. Au anafahamu kabisa mtu ana mtoto basi mtoto ataonyeshwa mapenzi yote atapelekwa beach, atafanyiwa shopping. Jamaa anaona dah mke huyuapa Mungu kaniletea anapenda mwanangu (kumbe anapenda ndoa ) Subiri afunge ndoa.....!
 
munisijo kiukweli yule mama ana roho yake kanikuta nasoma primary za st.kayumba ila sekondari kanitafutia shule nzuri sana na alikuwa anahakikisha naenda vizuri shule japo alikuwa anapinga nisipewe hela nyingi na mshua.Mie mshua wangu alikuwa mpole sana na nilikuwa kipenzi chake sasa nilikuwa nikienda shule anachukua either sabuni za kuogea au dawa ya mswaki ananiwekea hela maana yeye ndio alikuwa ananifanyia shopping utasikia ananisisitizia kuwa hakikisha hiyo dawa unaitunza watu wanadhani mshua mbahili kumbe kuna pesa ndani yake

Mshua wako was/is genius
 
Last edited by a moderator:
Wanawake wengi wana roho za Izrael mtoa roho za watu! Mimi sijaishi na mama wa kambo, nimewahi ishi na MAMA MKUBWA, MAMA MDOGO kwa nyakati tofauti! Kwa walichonfanya, bora hata wangenila ......!
 
Nimemsoma page ya kwanza mpaka ya mwishoni, EE MUNGU MUUMBA VITU VYOTE, DUNIANI NA MBINGUNI, NAKUOMBA UNIJALIE PUMZI NA UZIMA WA MWILI NA ROHO, NIWALEE WATOTO WANGU MPAKA. WAFIKE VYUO VIKUU, WATAFUTIE WENZI WEMA WENYE HOFU YAKO BABA MUUMBA WAWEZE KUISHI NAO KWA AMANI, FURAHA NA UPENDO, IKIKUPENDEZA BABA UNIGAWIE NAFASI KUSHUHUDIA WAJUKUU, AMENNNNNNN!

Jamani ni poleni wote mliopata mateso kwa kulelewa NA mashwain, uwiiiiiiii nimesikitikaaaaa
 
Yaani machozi yamenitoka pasipo kutarajia. Pole sana aisee. Na hii ilikua ukiwa na umri gani? Dah!

Asante! Time is the best healer! Nilikuwa na Miaka 10 darasa la tatu wakati huo!
 
Wanawake wengi wana roho za Izrael mtoa roho za watu! Mimi sijaishi na mama wa kambo, nimewahi ishi na MAMA MKUBWA, MAMA MDOGO kwa nyakati tofauti! Kwa walichonfanya, bora hata wangenila ......!

ni nasema nkifa wanangu mara mia waende orphanage
 
Pole. Hata mm nimepitia japokuwa si kama hayo lakn nilikuwa nalia sana halafu baba yangu wala hata hajali, thats y namchukia baba angu hadi leo
 
Poleni sana wahanga wa mateso ya mama wa kambo.
Kuna binadamu wanaroho mbaya na katili kuliko hata wanyama wakali.
 
Mama yangu wa kamba kwakweli ni mwanamke wa pekee,nafikiri mzee wangu ana bahati ya kuwa nae..ana upendo sana.
 
Sijawai ishi na mama wa kambo ila nimekuwa nafanya kaz uku arusha niko na mama fulan hv anaishi na mtt wa mumewe (mtt wa kambo) iko kipigo na kula chakula bila mboga ni maisha ya kila siku....tumejitaidi kila hali kumuambia huyi mama na mumewe ila tatizo wanaume tunapenda vibaya mume no action...baba kipigo mama kipogo mtt hana msaada
Mpende mkeo/mumeo mtt kulelewa na mama wa kambo ni kihama cha duniam
 
Back
Top Bottom