Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Dah nahisi kama stori yangu inaendana na yako

Kila nikiomba kwa imani yangu huwa namshukuru Mungu alivyonitoa shimoni kwa kumfumbua macho mzee wangu!
Yule Mama hakuwa binadamu wa kawaida! Niliponea tundu la sindano! Mtu unapigwa huwezi kutembea wala kutambaa na hakuna kupewa chakula umefungiwa stoo kisa ni kukutwa na picha ya marehemu mama yangu, picha pekee iliyokuwa na sura yake! Kipimo chake cha kuacha kupiga ilikuwa ni pale unapokuwa huwezi kuMove kabisa au umeFaint!
Mungu ni Mwema, hakuniacha pamoja na mateso yale!
 
Ukatili kwa watoto unatekelezwa sana na wanawake,hii inaonyesha wana roho mbaya.

Ndugu ukisikia ukatili wanaofanyiwa watoto na wanaume utalia sema tu watu wanaona aibu kusema weka mtoto wako mbali na ndugu wa kiume, baba wa kambo na kwa wengine hata baba mzazi ni shetani!
 
Sijui wanawake wana roho gani aiseee, mbona hatusikii issue za baba wa kambo?
 
Yani hata sisemi, Maana bado nipo kwenye huo mnyororo. Najikuta hadi namchukia Baba angu. Maana hasikilizi hataa
 
Nilichomfanya mama wa kambo mpaka leo ananiheshimu kama mtume.......kwani kamwe hawezi kunisahau mpaka anaingia kaburini.........

Mkuu tupe uzoefu huenda ukatusaidia wengine kwenye haya maisha si unajua bado wako wengi huku mitaani.
 
Sijawahi kuishi na mama wa kambo, ila ninavyojijua nahisi angekiona cha mtema kuni, huyo dingi tu wakati nipo la 4 akaanza kunizungua na mambo yasiyoeleweka, siku nikayachoka nilichoanza kufanya mbona alitulia na tangu hapo alikua makini na mimi. Kuna wazazi wanafanya makusudi kabisa kuwachokoza watoto wao, eti we utulie uwe na heshima, aisee mi ilinishinda nikapasua ukweli, na mambo ya kawa shwari.

So who is mama wa Kambo, nashukuru tu sijaishi na hao wa mama, hadi leo ni mtu mzima, na even hata ikitokea now najua hawezi nitesa mimi, na ole nisikie anawatesa wadogo zangu kudadadeki, baba atajua kama amemuoa yeye au nimemuoa mimi. Waende zao huko

Sio rahisi kama unavyodhani. Hivi wewe kwa akili yako mtoto wa miaka 5 atafanya nini? Halafu kumbuka kadri mtoto anavyokuwa anaathirika kisaikolojia hivyo anakuwa na uoga fulani hivi inakuwa vigumu sana kufanya chochote. Of coz mama kambo akikukuta tayari una akili zako ni ngumu kukuletea za kuleta maana unaweza mzibua ukatambaa.
 
....aisee pole sana, huyo mama alikuwa na roho mbaya sana.

Kama unampenda mumeo, itakuaje uchukie mtoto wake? Mie huwa najiuliza sana, sijabahatika tu kuwa mama wa kambo.

Hii chuki nadhani huwa ni ya kumchukia mwanamke mwenzie ambaye hata hivyo anakuwa hayupo muda huo!!!:shocked::shocked::shocked: Ndio maana huwa inasemwa wanawake ni nyoka!
 
Ndugu ukisikia ukatili wanaofanyiwa watoto na wanaume utalia sema tu watu wanaona aibu kusema weka mtoto wako mbali na ndugu wa kiume, baba wa kambo na kwa wengine hata baba mzazi ni shetani!

Mara nyingi ni ngumu baba wa kambo kufanya ukatili kwa kuwa watoto huwa wanakuwa wako karibu na kinamama zaidi. Kama baba wa kambo ni katili basi mwanamke anakuwa anatoa ushirikiano wa kutosha ukiacha kesi za kubaka from no where.
 
Kama hukupata bahati mbaya ya kuishi maafriti hao mshukuru mungu hawafai hao 99% ni washenzi wana roho mbaya wakati yeye ndo kakukuta niishie hapa maneno hayapangiki ila alaaniwe huko alipo
 
Ninachoamini mungu yuko upande wetu sisi tuliolelewa na mama wa kambo kwani asilia kubwa wanafanikiwa katika maisha ulilanganisha na watoto wao wanaowalea kimayai.
 
mama wa kambo msilikilizie kwa mwingine mimi nilikuwa napewa kipondo cha ukweli na chakula nanyimwa hadi maji ya kunywa ilikuwa kasheshe?
 
Mama wa kambo sitomsahau maishani mwangu,kwa mateso aliyonipa mpaka Leo imebakia historia2,ila ameniharibia mambo mengi sana!!but I choose to forgive her!!
 
Kila nikiomba kwa imani yangu huwa namshukuru Mungu alivyonitoa shimoni kwa kumfumbua macho mzee wangu!
Yule Mama hakuwa binadamu wa kawaida! Niliponea tundu la sindano! Mtu unapigwa huwezi kutembea wala kutambaa na hakuna kupewa chakula umefungiwa stoo kisa ni kukutwa na picha ya marehemu mama yangu, picha pekee iliyokuwa na sura yake! Kipimo chake cha kuacha kupiga ilikuwa ni pale unapokuwa huwezi kuMove kabisa au umeFaint!
Mungu ni Mwema, hakuniacha pamoja na mateso yale!
jamani nimehuzunika .. pole mkuu
 
mimi sijawa mama bado natamani angejitokeza mtu aseme shida inakuwa nini kutesa watoto hivi? inahuzunisha sana
 
Back
Top Bottom