Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Dah jamani pole sana ila wengine tunaijua miziki yote ya mama wa kambo na mashangazi aiseeh acha kabisa yaani hii unaambiwa weka mbali na watoto aiseeh!!!!

Aisee acha tu. Miye maza wa kambo ilikuwa vipigo bila kosa. Majirani wakaingilia kati nikapelekwa kwa bibi kijijini. Huko nimekaa wakanambia (miaka hiyo) kuwa kwa mazingira haya huyu hawezi kufaulu, so nikahamishiwa kwa aunt. Hapo ndo niliona mziki. Unaamka saa kumi na moja unafanya kazi zoote za ndani (leo naona ilikuwa sawa tu maana leo hivyo vitu havinisumbui), aunt akiamka akukute hujaondoka shule hata kama ulikuwa na kazi nyingi anakutimua bila chai. Mchana unarudi msosi bado unaogopa fimbo za kuchelewa unaosha. Acheni Mungu aitwe Mungu, kwani kati kati ya njaa kali unakuta rafiki anakupa andazi. Usiku unafanya kazi mpaka karibu saa sita.
The thing ambayo sitasahau ni baada ya mama yangu kufariki nikiwa kwa aunt mkoa mwingine. Wiki moja baada ya aunt kupewa taarifa aliniuliza 'eti ukisikia mama yako amekufa utafanyaje?'. Nikamwambia sijui, akasema basi mama yako amekufa, at that time nikiwa darasa la nne. Niliingia chumbani nikalia sana. Alivoona nalia alinivurumushia matusi na sikuruhusiwa kwenda hata kuliona kaburi la mama yangu. From that day niliapa sitazaa mtoto nje ya ndoa Mungu anisaidie katika hili. Wanawake huwezi kuwaelezea, huwezi jua rangi zao. Utakapofikiri ni nyeupe kumbe ni nyekundu.
Ila good thing mama wa kambo alibadilika sana though nilikuwa namuogopa she was so nice to me nikiwa form two hadi leo. Aunt alikuwa tia maji tia maji hivyo hivyo ila leo mimi ndo nimekuwa msaada mkubwa kwao, na sina kinyongo now! I really love them maana pamoja na yote nilipata fursa ya shule.
 
Mimi ni mama wa kambo lakini mtoto wa kambo ndio alinitesa .....nililetewa bint wa miaka 14 yani full visa mi nimempita miaka 11...analala mpaka saa6 akiamka ndio. Aoge aje jikoni anywe chai akimaliza kwenye tv anasubiri mchana chakula ..mimi ajabu sikua nikimsemesha naona akawa anastaajabu naona alikua akinitafuta
 
dah naelewa situation yako...

ingawa inahitaji roho na moyo aisee

Mungu atakubariki kwahilo

ameen
hv anaekupenda anaweza akataarifu majirani ndoa ya mdogo wangu jmos trh 20 siku moja b4?i mean alhamis binti kwao wana send off ndo anagawa kadi za mchango
nililia sana that day sitosahau kamwe
thnx to my uncles na ndugu wa mama mzazi
hili ni dogo sana ktk aliyofanya ila nafsi sasa inamsuta mno
 
Kila nikiomba kwa imani yangu huwa namshukuru Mungu alivyonitoa shimoni kwa kumfumbua macho mzee wangu!
Yule Mama hakuwa binadamu wa kawaida! Niliponea tundu la sindano! Mtu unapigwa huwezi kutembea wala kutambaa na hakuna kupewa chakula umefungiwa stoo kisa ni kukutwa na picha ya marehemu mama yangu, picha pekee iliyokuwa na sura yake! Kipimo chake cha kuacha kupiga ilikuwa ni pale unapokuwa huwezi kuMove kabisa au umeFaint!
Mungu ni Mwema, hakuniacha pamoja na mateso yale!
Unyama wa hali ya juu.
 
Mara nyingi ni ngumu baba wa kambo kufanya ukatili kwa kuwa watoto huwa wanakuwa wako karibu na kinamama zaidi. Kama baba wa kambo ni katili basi mwanamke anakuwa anatoa ushirikiano wa kutosha ukiacha kesi za kubaka from no where.

Ukatili wa baba wa kambo upo sana na mara nyingi ni ubakaji ambao hata mama anaamua kunyamaza either kuficha aibu au ni tegemezi
 
ameen
hv anaekupenda anaweza akataarifu majirani ndoa ya mdogo wangu jmos trh 20 siku moja b4?i mean alhamis binti kwao wana send off ndo anagawa kadi za mchango
nililia sana that day sitosahau kamwe
thnx to my uncles na ndugu wa mama mzazi
hili ni dogo sana ktk aliyofanya ila nafsi sasa inamsuta mno

Daah kweli tumetoka mbali then nimegundua sipo peke yangu....Mungu huwa hatutupi aisee though huwa nawasiwasi kuwa wadogo zangu hawanipendi kama niwapendavyo....Sina jinsi ndio msaada wao kwasasa nawahudumia.
 
tuko wengi sana wahanga nna mengi sana bas tu
 
Kila nikiomba kwa imani yangu huwa namshukuru Mungu alivyonitoa shimoni kwa kumfumbua macho mzee wangu!
Yule Mama hakuwa binadamu wa kawaida! Niliponea tundu la sindano! Mtu unapigwa huwezi kutembea wala kutambaa na hakuna kupewa chakula umefungiwa stoo kisa ni kukutwa na picha ya marehemu mama yangu, picha pekee iliyokuwa na sura yake! Kipimo chake cha kuacha kupiga ilikuwa ni pale unapokuwa huwezi kuMove kabisa au umeFaint!
Mungu ni Mwema, hakuniacha pamoja na mateso yale!

dah mi sikufikia huko pole sana
 
Ukatili wa baba wa kambo upo sana na mara nyingi ni ubakaji ambao hata mama anaamua kunyamaza either kuficha aibu au ni tegemezi
Mkuu fanya utusaidie kwenye hili eneo kwa kufanya utafiti rasmi. Vinginevyo inakuwa ngumu kukubaliana na wewe kuwa upo sana tu. hata hivyo kama umenisoma vizuri nimesema kama baba wa kambo anafanya ukatili basi utakuta mama anajua tofauti na mama wa kambo ambapo mara nyingi kina baba wanakuwa hawajui.
 
Kila nikiomba kwa imani yangu huwa namshukuru Mungu alivyonitoa shimoni kwa kumfumbua macho mzee wangu!
Yule Mama hakuwa binadamu wa kawaida! Niliponea tundu la sindano! Mtu unapigwa huwezi kutembea wala kutambaa na hakuna kupewa chakula umefungiwa stoo kisa ni kukutwa na picha ya marehemu mama yangu, picha pekee iliyokuwa na sura yake! Kipimo chake cha kuacha kupiga ilikuwa ni pale unapokuwa huwezi kuMove kabisa au umeFaint!
Mungu ni Mwema, hakuniacha pamoja na mateso yale!

Pole mkuu.
 
Mkuu fanya utusaidie kwenye hili eneo kwa kufanya utafiti rasmi. Vinginevyo inakuwa ngumu kukubaliana na wewe kuwa upo sana tu. hata hivyo kama umenisoma vizuri nimesema kama baba wa kambo anafanya ukatili basi utakuta mama anajua tofauti na mama wa kambo ambapo mara nyingi kina baba wanakuwa hawajui.

nimefanya utafiti sana wa ukatili wa watoto si tanzania tu hata nje ya nchi infact unyama kwa watoto unatisha nashangaa watu wanaotetea baba wa kambo. ukatili kwa mama wa kambo mi huwa namlaumu baba it means wakina baba wengi hawako karibu na watoto wao. ukiwa karibu na rafiki kwa watoto wako huu ujinga hatutaushuhudia lakini mna kazi ya kuacha pesa mkifikiri watoto wanahitaji pesa peke yake. the need your love and attention.
 
mimi nilikuwa nalazwa kwenye meza ndio kitanda change..siruhusiwi kulala kitandani hasa baba anaposafiri..motto wake ndio alikuwa analala kitandani

katika maisha yangu sikumbuki kufuliwa nguo,tangu nipo la kwanza nafua mwenyewe..huyu mtt wake amefuliwa hadi la saba...

kuna wkati baba alisafiri muda mrefu ikawa huyu mama hatupi chakula kabisa ikabidi niache shule nifanye vibarua vya kubeba mchanga ili npate hela ya kula..mzee aiporudi ndio akanirudisha shule

iliikia sehemu akaninunia akawa haongei na mimi hata nikimsalimia haitikii..hapo nilikuwa nimefaulu kwenda form 1 na mwanae kafeli

mimi nasema simwachi mwanangu kwa mama wa kambo labda niwe nimekufa!!!!!!!!!!
 
Jamani poleni sana mliokutana na mikasa ya mama wa kambo kiukweli inasikitisha sana
Nakumbuka mama yangu kabla hajafariki alikuwa anasema katika jambo analomshukuru Mungu sana ni kumjalia uhai hadi watoto wake wote wamekuwa wakubwa
 
nimefanya utafiti sana wa ukatili wa watoto si tanzania tu hata nje ya nchi infact unyama kwa watoto unatisha nashangaa watu wanaotetea baba wa kambo. ukatili kwa mama wa kambo mi huwa namlaumu baba it means wakina baba wengi hawako karibu na watoto wao. ukiwa karibu na rafiki kwa watoto wako huu ujinga hatutaushuhudia lakini mna kazi ya kuacha pesa mkifikiri watoto wanahitaji pesa peke yake. the need your love and attention.

Yaani unataka kuja hapa useme umefanya utafiti sana halafu tukuamini bila ushahidi wowote? Pili watu hawatetei au niseme mimi kwa upande wangu sitetei baba wa kambo ila tunazungumzia hali halisi. Wewe kama misheni yako ni kuonesha kuwa baba wa kambo ni wabaya sana haya umeshinda haina haja ya kubishana sana.

Pili tuna kazi ya kuacha pesa kina nani? Mbona una jazba sana. Hebu tulia na upangilie hoja zako maana inakuwa kama unafanya mashindano hivi.
 
soma journals na articles za research majibu utayapata yote huko. kuhusu kuacha pesa unamwachia mkeo lakini kukaa na watoto wako kujua hali halisi unafikiri nani anatakiwa kufanya hivyo? ni baba wa jirani au wewe baba mzazi? kuhusu kupendelea sipendelei upande wowote nimewaona wababa na wamama wa kambo wenye roho mbaya na si kwa binadamu tu hagta kwa wanyama kama unafuga wanyama angalia tu kifaranga cha kuku kipotee njia kiende kwa mama mwingine utaona kitakavyofukuzwa. so kwa bnadamu ni hivyo hivyo ila naona watu wengi wanalaumu sana mama wa kambo! ila ukweli wote wanaroho mbaya jitahidi uzae mtoto wako na mtu utakayeishi nae mpk siku ya kifo.
 
Daah Mungu nashukuru kwa neema uliyonipa ya kulelewa na wazazi wangu wote wawili, hadi sasa nimekuwa binti/ mdada mkubwa kabisa. Ukazidi kuwapa wazazi wangu maisha marefu pamoja na yenye ukamilifu ili angalau siku moja waje wafaidi matunda yangu.
Poleni wote mliokutwa na mikasa mibaya na mama zenu wa kambo, wao Ni binadamu tu, watakuzuia mafanikio yako kwa muda, but kwa neema ya Mungu utafika tu pale yeye Mungu anapotaka ufike. Mmmh wanawake Mungu atuhurumie tu
 
pole kwa lililokukuta.mimi ni mama wa kambo.sitetei ubaya ila baba zenu ni waongo sana.unaloambiwa sio kabisa na kuishi na mtoto wa mtu inataka neema ya Mungu hasa akiwa mtata.mimi mtt wangu hakua anatakakuishi nasisi kwa alichoelezwa na mama yake baadae akawa anawaambia wanangu kua mama yake ni mzuri sana kuliko mimi alitakiwa akaepale.mtt huyo ambae nimempenda mpaka watu hawajui tofauti ndio anafanya hivyo.mama mtu nimkorofi wala hatumi nguo wala mafuta.nimekata bima kwa mshahara wangu bado anatukana hovyo.guys kama uliwaiteswa pole sana .ila watoto wa kambo ni tanzi
 
mmesema kuhusu mama lakini kunawatoto wa kambo ambao ni washenzi sana.kazi ulizofanya mamako akiwepo ukiambiwa saa hizi unateswa.unakuja na motive ya kumrudisha mama yako kwa baba yako kwani baba yako hakumuona mamayako? kwanin asimuoe waishi?mama wazazi wengine kashaachika ila anatafuta sababu zakukaa pamoja anamtuma mtoto kufanya vitu vya ajabu.unadhani nirahisi kumpenda?unajitahidi kumpenda anakujibu fyongo.mama wakambo ni binadamu anadamu na nyama hakuna mtu ambaye hapendikuishi kwa raha kama mama wa kambo hajakufanyia ubaya usimzulie baya.Mungu anaishi hatawewe unawezakua alafu utajua jinsi ilivyongumu
 
Nikisema nifunguke hapa naweza kujaza pages kibao but poleni sana watu mliopitia life hilo, I am among of them. Nooma sana
 
Back
Top Bottom