Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

Kwanini Mama wa Kambo huwa na Visa?

mama wa kambo wangu ni balaa...alinikuta nina miaka 5 adi leo almost 30 still hanipendi, unizushia mambo kulingana na umri nilipokua shule ya msingi aliniita mchonganishi, sekondary muhuni, chuo akanitabiria kutoolewa, sasaivi nafanya kazi na nimeolewa na nina mtoto anasema mi mchawi naenda kumuwangia..nimepata tabu sana nashukuru mama angu yupo hai na kanisomesha hadi masters... wewe mama Mungu atakulaani kwa ubaya ulionitendea
 
Najua yupo hai mungu amlaani popote alipo, sitaki kukumbuka those bad days.
 
Nataka kuandika maovu ya mama wakambo alivyonifanyia mkono hautaki kuandika.yaani nahisi kama yatajirudia.Siwezi kusema kwamba hakuna hata jema moja alilonifanyia yapo ila mabaya ni mengi na ya kutisha.All in all namuomba mungu ampe maisha marefu na mimi nifanikiwe ili aje ashuhudie mafanikio yangu.
 
naogopa sana kwenda jela ila sitajutia kuspend the rest of my life in jail kutokana na vile naweza fanya kwa yeyote atakayemuabuse mwanangu in any way, B*tch dont try this at home!!
 
superstar1

Wazazi wangu walitengana nikiwa na umri wa miaka minane tu..!!!

Umenikumbusha maisha ya utotoni...!!! Nilala barazani... Nilishinda/Nililala njaa...Nilichapwa viboko (tena uchi wa mnyama..)... Mama wa kambo ni Ibilisi...!
 
Last edited by a moderator:
naogopa sana kwenda jela ila sitajutia kuspend the rest of my life in jail kutokana na vile naweza fanya kwa yeyote atakayemuabuse mwanangu in any way, B*tch dont try this at home!!

Ndo mfunge zipu zenu, kama hauna plan na mtu take precaution usimmimbe, na mkioa mtulie na mvumiliane labda yatokee ya Mungu tu(kufa)
 
mie nimekuzwa na mama wa kambo kwa kweli kanilea vizuri sana mpaka hapa nilipo sasa hivi huwa simsahau kwa mema yake aliyonifanyia, alinifundisha maisha, ila ni wachache kama hawa, asilimia kuwa ni full manyanyaso,
 
Hii chuki nadhani huwa ni ya kumchukia mwanamke mwenzie ambaye hata hivyo anakuwa hayupo muda huo!!!:shocked::shocked::shocked: Ndio maana huwa inasemwa wanawake ni nyoka!

Utamchukiaje mtu ambaye hayupo kwa wakati huo? na hata huyo mtoto ana kosa gani? kama unataka kugombana gombana na mumeo au mke mwenzio na si watoto. mm huwa nawashangaa sana wanaowabagua na kuwatesa watoto wa kambo, mm ninao watoto wawili wa mumewangu nawalea na wala siwabagui na wala siwachukii na wananipenda kiasi mama yao akija hawana habari naye, na hata wakifunga shule ukiwaambia wanaenda kwa mama yao wanakataa, mpk mama yao anasema nimewabrain wash watoto wake. lkn sivyo nilichokifanya ni kuwakumbatia na kuwaonyesha mapenzi na kuwa karibu nao na i sure nitakula vingi kuliko mama yao.
 
Utamchukiaje mtu ambaye hayupo kwa wakati huo? na hata huyo mtoto ana kosa gani? kama unataka kugombana gombana na mumeo au mke mwenzio na si watoto. mm huwa nawashangaa sana wanaowabagua na kuwatesa watoto wa kambo, mm ninao watoto wawili wa mumewangu nawalea na wala siwabagui na wala siwachukii na wananipenda kiasi mama yao akija hawana habari naye, na hata wakifunga shule ukiwaambia wanaenda kwa mama yao wanakataa, mpk mama yao anasema nimewabrain wash watoto wake. lkn sivyo nilichokifanya ni kuwakumbatia na kuwaonyesha mapenzi na kuwa karibu nao na i sure nitakula vingi kuliko mama yao.
Mkuu ngoja mama wa kambo waje kutupa majibu hapa.
 
Wakuu ni ukweli usiopingika kwamba wa MAMA WA KAMBO huwa wachungu na wakali ajabu kwa watoto wasio wa kuwazaa.

Mfano, Mama wa Kambo ameolewa na mzee ambaye tayari ana watoto wadogo, lazima atawatesa na kuwanyanyasa sana hao watoto. Lakini ni tofauti kidogo kwa baba wa kambo, hawa wababa huwa na mapenzi na upendo wa kweli kwa watoto wanaowakuta.

Jamani kwanini inakua hivi? Kina mama wa kambo hata kama mtoto sio wako sio vizuri kumtesa bila sababu, hii ni dhambi kubwa sana.

Badilikeni mama zangu.
 
unaushahidi gan? na kwawatoto wenye tabia mbaya? au ndio mtu kauma mbwa?
 
Kulea mtoto asiye wako ni kipaji, kuna mengi huwapelekea kuwa hivyo.
 
Mi maza angu wa kufikia ni mshkaji wangu kinoma, ni zaidi ya mama. Matterfact, nipo karibu nae kuliko hata my old man mwenyewe. Abarikiwe sana, na wengine pia kama yeye.
 
nimesikia story ya mama wa kambo aliyemkata mtoto wa mmewe dudu yake nikaona niweke post ya experience yangu na akina mama wa kambo.

Nakumbuka mdingi alimtema mama angu mzazi alikuwa anamzingua sana mimi nikiwa na miaka kama tano hivi, akavuta mama aliyetulea. Mbona tulionja joto ya jiwe? Unadhani mama wa kambo alinifanya mazuri basi? Mdingi alikuwa anasafiri sana.

Yaani home alikuwa anakaa siku moja au mbili anasafiri halafu huko anakaa hata wiki tatu mpaka sita. Alikuwa na wamama wengine huko. Kimaisha hali haikuwa mbaya sana kwani hapo home kulikuwa na lorry tani saba enzi hizo yalikuwa machache sana, kwa hiyo ni full kazi na jumba kuuuubwa ambalo enzi hizo tulikuwa tunaona kama hekalu.

Home store ya misosi ipo full muda wote, mikaa na kuni imejaa kwenye stoo yake kwa sababu kila gari ikisafiri lazima ilete aidha mkaa, kuni, mahindi, mpunga, maharage, kuku, au nyama ya porini. Wakati mwingine vitu kadhaa kati ya hivyo vililetwa kwa pamoja.

Cha ajabu hapo home tulikuwa tunashinda njaa mpaka jioni ndio tunakula! Yaani maskini ya mungu mi sijui hata kosa nililomfanyia huyo mama i was only 5 years old, nashinda na njaa wakati ndani kuna chakula cha kutosha. Wanapewa majirani, vingine vinamwagwa, mi nashinda na njaa mdomo umekaukaaaaa! Siku mshua akirudi ndio napewa kipande cha nyama cha kuzuga.

Akiondoka kesho yake napikiwa maharage ya kula hata siku nne sikumbuki kama hata chumvi yalikuwa yanawekwa yale, na nakula jioni tu, mchana napigishwa pasi ndefu, wakati mdingi ana mahela kibao. Nimepiga hizo since 5 years old mpaka std 7 baada ya kuanza sekondari mateso yalianza kupungua kidogo kidogo.

Acheni utani nyie watu. Kulikuwa na mtoto wa kaka ake hapo home ambaye yeye (maza) ndio alikuwa anasema mwanae, huyo ndio alikuwa anaishi kama mfalme. Akawa anatuonea huruma, akipewa nyama, akipata upenyo anatufichia.

Anajifanya amekula zote baadae tukienda kulala ndio tunakula kitandani huku tumejifunika blanket maza asituone mimi na wenzangu waliokuwapo siku hiyo, hasa ndugu ndugu. mateso makubwa yalikuwa njaa na vipigo. ​kakosa kadogo unatandikwa mpaka unajikojolea halafu no msosi siku hiyo.

Siku ambayo siwezi kusahau ni ile ambayo njaa na tamaa viliponizidia nikadokoa nyama aliyokuwa anamuandalia mwanawe. Weee! Alinipa kichapo mpaka nika-faint. Nilipozinduka (hii ndio itafanya nije niue mwanamke siku moja) akanishika mdomo wangu akaniachamisha kwa nguvu halafu akanitemea mate ya kutosha humo.

Sijui yalikuwa makohozi yale, nakumbuka nilitapika mpaka kidogo niteme maini. Nadhani nilifaint, kwa sababu nilikuja shtukia naamshwa asubuhi niende shule tu wakati kipigo kilikuwa jana yake saa mbili usiku nilikuwa std 3.nakumbuka hata shule sikuenda siku hiyo, nilianza safari ya kwenda kumtafuta mama yangu kwa mguu na hata sijui wapi.

Nilifuata uelekeo flani ambako ndio najua magari ya anakotokea mama angu yanaelekeaga. Nilipoenda kama kilometa tano wasamaria wakaanza kushangaa huyu mtoto anaelekea wapi wakaanza maswali, nilipowaambia nimetoka wapi na ninaenda wapi na kufanya nini wakanikamata wakanirudisha mpaka home.

Sasa pale tunafika karibu na home akatokea mama mmoja kwa kumbukumbu zangu za wakati huo alikuwa anafanana na mama yangu) nilimrukia vibaya mpaka waliokuwa wananirudisha home wakashangaa. Sasa yule mother aliposema mimi sio mwanae wakakomaa nae mpaka wakapaone nyumbani kwake, tukaenda wote mpaka hapo sio mbali na hapo home kwetu.

Alikuwa ndio amehamia mitaa hiyo hiyo siku si nyingi hivyo nilikuwa sijawahi muona) waliporidhika, na mimi baadae nilipokubali kwamba sio mama yangu wakanirudisha kule home kabisa. Ila niliona aibu sana baadae nilipokuja tambua sasa kuwa yule niliyemkumbatia vile wala sio mama yangu. Yule mama alikuja kunipenda
mpaka nakuwa mtu mzima.nadhani huruma ilichangia kwa maisha aliyokuwa anaona naishi.

Ninachotaka kusema ni kwamba muziki wa mama wa kambo mi naujua fresh tu, toka 5 yrs old mpaka form six. Mengine mengi tu inabidi niya-skip kwa sababu story itaboa.


pole sana!hizi story nazisoma mimi ni baba mzima hadi natamani kulia poleni wote mliokelewa na mama wa kambo.ila wapo wengine wazuri.in most cases wanawake wana roho mbaya. Mimi nilishawahi ona mama wa kambo anamgongesha mtoto wa miaka 7 kichwa kwenye ukuta.!!!
 
ila pia mkome uzinzi nakua irresponsible unamlala mtu unamtia mimba alafu humuoi unaoa mtu ambaye kajitunza kweli alafu unamdanganya unamletea mauzauza acheni ujinga wanaume.hapa mnajifanya kunyanyua mdomo bila kujua upumbavu wenu umesababisha haya ungekua responsible haya yote yangetoka wapi? watt wengine washenzi huna pa kushtaki anaakili na anajua anachosema .hata umfanye nini hafurahi anakinyoooongo.inamaana yeye ndio anajua mwanamke anaenfaa baba yake?unajitahidi kuwa mstaarabu kwa mama yake lakini uyo mama yake ndio mshenzi kabisa mwanaume hakulindi wala.anakwambia upo kwako fanya unachotaka.
naamini kama alivyosema mkuu hapo juu kunauwezekano wa step mom kukaa vizuri na steps atakaowakuta kwa mumewe.kweli hawezikutokea wakawawatt wake bt heshima muhim.na wazazi wenza mliokua humu muwe na adabu na ndoa za watu.wewe sio mke mwenza tena hutakiwi kabisa kwenye hiyo ndoa.kama unaakili mbona hukuolewa wewe?kama hujapata bahati subiri wakati wa Mungu acha fujo kwani hakuna mtu alikutuma kuzaa na watu wasiokuoa.
naambao hamjazaa bado mabinti muache kujirahisisha kuepuka migogoro kama hutaki kuolewa ukibeba mimba udiingilie ndoa ya watu.zaa kaa kimya.
 
Back
Top Bottom