Extrovert
JF-Expert Member
- Feb 29, 2016
- 72,425
- 191,638
Ni kweli ila katika kutafuta suluhu ya tatizo siku zote huwa tunaanza na culprit! Kiini cha mume kuanza kuchepuka ni kipi? Huenda mmeishi vyema miaka miwili ila ghafla unaona mume ameanza kuchepuka.Uko sahihi kabisa sema tu kuna kitu kimoja umekisahau na ambacho ndo kinatesa ndoa nyingi leo
Siku hizi mwanamke unaweza kuwa mtii kwa mumeo,ukamfanyia kila kitu ila atakukosea heshima mno kwa kuwa na michepuko ya kila aina tena bila hofu!
Kwa hali ya kawaida hii huleta maumivu makubwa sana kwa mwanamke mwishoe nae anaona liwalo na liwe ndo hapo unasikia wanaanza kusema mwanamke mjeuri kumbe nyuma kuna chanzo!
Nnachojua wanawake wengi wamejeruhiwa hisia zao na waume zao ndo mana nao mwisho wanaishia kureact negatively,japo wapo wachache ambao their case is different
Cha kwanza ni kuanza udadisi! Kwa upande wangu naweza kukupa experience yangu kwamba kitu cha kwanza ni mabadiliko ya mwanamke na kuanza kupuuza utekelezaji wa yale ambayo yalikuwa yanamfurahisha mme. Hii huanza taratibu ila huwa tunaonekana wabaya ni sie ambao tumetoka nje...wanasema anayeanza haonekanagi ila anayemaliza.
Nilishawahi kuhoji nikapewa jibu hilo...heheh! "kwahio unataka mapenzi yetu yawe kama tulivyoanza mwaka ....... hebu acha mambo ya kitoto"
Katika mazingira hayo nikichepuka ntakuwa na kosa? Kauli laini hakuna tena, unajibiwa ilimradi tu! Lazma utafute faraja nje tu.