Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,220
KWANINI MAHUSIANO / NDOA NYINGI HAZIDUMU?
Unapoingia katika ndoa au mahusiano huwezi kufikiria hata kidogo kwamba asilimia kubwa ya ndoa au mahusiano hayo kufeli.Ndoa au mahusiano yanaweza kufeli kwa sababu nyingi na iwapo ndoa yako ilianguka na kufeli sababu kubwa yaweza kuwa na tofauti nyingine nyingi. Lakini, kuna sababu kadhaa za jumla na za kudumu kwenye ndoa zote zilizofeli.Hebu tazama orodha yangu ya sababu 8 za ndoa nyingi kuanguka na kufeli.
1) Kwa sababu ulitaka harusi badala ya ndoa:
Ni miongoni mwa ada za kijamii kushiriki katika furaha mbalimbali za wenzetu. Miongoni mwa furaha hizo ni shughuli za harusi pindi wahusika wanapoamua kuingia katika taasisi tukufu ya NDOA. Shamshamra zinazoandamana na tukio hilo adhimu hutuhamasisha kuingia katika taasisi hiyo muhimu kabisa katika maisha ya mwanadamu. Mavazi, mapambo ya maharusi na kushangiliwa na wenzetu huwafanya wanandoa wahisi kama nyota. Matukio hayo hukufanya uanze kutamani na hata kupanga namna harusi yako itakavyokuwa. Tazama: hapo umesukumwa na mvuto wa harusi badala ya uhalisia wa NDOA.Ni bahati mbaya kuwa maandalizi ya harusi yanakuwa makubwa kuliko hata maandalizi ya NDOA yenyewe.Nawashauri wazazi kuwashauri watoto wao kwamba: baada ya harusi kuna ndoa. Hivyo nguvu kubwa wazielekeze kwenye suala la pili.
2) Kwa sababu umeoana na mtu usiyeendana naye:
Wakati fulani jambo hili hutokana moja kwa moja na suala la kwanza nililolieleza hapo juu, lakini kuna sababu nyingine ambazo zinaweza kusababisha kufunga ndoa na mtu ambaye hamuendani kabisa. Yumkini ni mtu uliyemzoea; yumkini ni mtu uliyecheza naye tokea utotoni lakini licha ya kutokuwa mtu sahihi unajisemea moyoni na kujipa matumaini “siwezi kuuvunja moyo wake mambo yatabadilika tu”. Yumkini unaona kabisa amekuwa tofauti na ulivyotarajia, lakini umeshaweka ahadi naye. Kabla ya kuingia katika ndoa jitahidi umjue vilivyo mwenza wako wa maisha…. Usiangalie tu kwamba atapendeza ukisimama naye siku ya harusi.
3) Kwa sababu mtu mmoja hawezi kukidhi mahitaji yako yote:
Jambo hili ni miongoni mwa sababu kuu za ndoa nyingi kufeli na hata kuanguka. Tatizo ni kwamba hata kama mwenza wako anakidhi asilimia 75 ya mahitaji yako makubwa kabisa kila siku, asilimia nyingine 25 haitatimizwa moja kwa moja. Hivyo, kwa mfano ukiolewa na mwanaume mchapakazi, mwenye mvuto na anayekupa raha kitandani, lakini hakuiti kwa majina mazuri yenye kukupendeza na hakusikilizi, unatakiwa kujifunza kuridhika na hiyo asilimia 75, kwa sababu hakuna anayeweza kukidhi mahitaji yako kwa asilimia zote. Wengine huwa wanashindwa kiasi kwamba wanafikia hatua ya kutafuta sehemu wanayoweza kujaza hizo asilimia 25 wanazozikosa. Hata huko wanakokwenda hawawezi kupata mtu anayeweza kuwapa furaha kwa asilimia zote na hujikuta wakiingia katika matatizo makubwa zaidi.
4) Kwa sababu ya usaliti:
Baadhi ya watu baada ya kukosa baadhi ya mambo machache kutoka kwa wenzao, kama nilivyosema katika namba 3, hukosa kuridhika na hivyo kuanza kutafuta mahali wanapoweza kukidhi ombwe hilo. Yumkini ukawa na hitajio la jambo dogo lakini kumbe hata huko ukawa huwezi kulipata. Yumkini ulihitaji tendo la ndoa lakini yumkini hitajia lako halisi ni zaidi ya hilo. Usaliti ni jambo la hatari sana kwenye ndoa yoyote, na likishatokea basi mambo hayawezi kuendelea kuwa katika hali ya kawaida. Mara nyingi pigo hilo huipeleka ndoa kwenye maporomoko.
5) Kwa sababu umekata tamaa mapema:
Sio kila tatizo huvunja uhusiano. Ni kawaida kwa wanandoa kukutana na mambo mazito katika maisha yao. Hukutana na matatizo ya kiuchumi, kufiwa na watoto na hata kutukanwa lakini bado huendelea kuwa imara na kuwa pamoja na hakuna anayemkimbia mwenzake. Kuna wengine wanapokutana na matatizo mazito hukata tamaa mapema, huhisi kuwa hawawezi kufanya stahmala hudhani kuwa changamoto hizo hawatozipata wakienda sehemu nyingine.
6) Kwa sababu hakuna fedheha:
Katika miaka ya 1800, kiwango cha talaka kilikuwa kidogo mno. Mwaka 1915 katika baadhi ya maeneo ndoa ilikuwa asilimia 5 ya ndoa zote, na ilikuwa kwa matukio maalumu kama vile unyanyasaji, uzinifu au utelekezaji wa familia.Katika baadhi ya maeneo, ili watu kuachana walihitaji kuidhiniwa na viongozi wa kiroho, wazazi na hata jamii za wahusika. Hata hivyo, wanandoa wengi walipata changamoto kubwa sana kwa sababu walilazimika kuishi katika ndoa zenye machafuko kwa sababu wasingeweza kustahmili “aibu” ya talaka. Suala la talaka lilionekana kama ni fedheha na aibua katika jamii. Lakini leo hii suala la talaka limekuwa jambo la kawaida na ni rahisi kufanywa na kukubaliwa na jamii. Watu wengi hawajali gharama zinazotokana na kuachana.
7) Kwa sababu unadhani kuwa wengine ndio wanaokosea:
Kuna kasumba mbaya sana katika baadhi ya ndoa ambapo mtu mmoja huwa MKAMILIFU na mwingine huwa MKOSEFU. Mwanandoa mmoja anaweza kujiona kuwa yeye hakosei na kumuona kuwa mwenza wake ndiye mkosefu siku zote. Hili ni tatizo ambalo huzigharimu ndoa nyingi. Ni muhimu sana kama wanandoa watakuwa watu SAHIHI badala ya kuwa WAKAMILIFU. Kwa sababu hilo ni jambo lisilowezekana. (Rejea mada yangu ya KANUNI YA SEKUNDE 30).
8) Kwa sababu wewe unataka upendo wakati yeye anahitaji heshima:
Jambo la kawaida, lakini ndoa hufeli pindi wanandoa wanaposhindwa kulielewa. Kwa ujumla mke ana silika ya kuhitaji upendo, ilhali mume anahitaji vipawa vyake vitambuliwe na kuheshimiwa. Tatizo ni kwamba tunajaribu kuwapa wenza wetu mambo ambayo tunayataka sisi, sio yale yanayoendana na silika zao. Angalia kwa mfano mke anamkosoa mume wake mbele ya watoto, mbele ya watu au hata kumuandika vibaya katika mitandao ya kijamii, hakika hilo litamvunjia heshima mume. Angalia pia mume ambaye anayejigamba kwa wengine kuhusu mkewe lakini akiwa nyumbani anampuuza. Ewe mume onesha upendo kwa mkeo, ewe mke mheshimu mumeo, mtaona mabadiliko.