Ubora wa ndoa Tanzania tunaupimaje, au cha muhimu watu hawajaachana?

Strong ladg

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
691
Reaction score
1,673
Niende moja kwa moja kwenye mada leo asubuhi na mapema.
Katika jamii yetu kwa sasa kumekuwa na mijadala mingi kuhusu ndoa hasa kutokana na idadi ya migogoro na talaka kuongezeka kila mwaka. Wakati wa mijadala hii , vijana wa leo wamekuwa wakitupiwa lawama kwa kutozingatia ndoa zao na kuwa wepesi kuachana huku kukiwa na kauli za " mbona mabibi/ mababu zetu walidumu kwenye ndoa hadi uzeeni?"

Sikatai hiyo mfano maana inabidi tujifunze kwa wazee wetu,lakini je tunaposema walidumu tunamaanisha nini? Walidumu kwa sababu hawakuwa na sababu ya kuachana? Walidumu kwa sababu waliishi kwa amani na upendo? Au walidumu kwa sababu hawakuwa na chaguo lingine?

Tunapozungumzia ndoa imara ambazo huzalisha familia bora,je tunaangalia vigezo gani? Je ni cha muhimu wanandoa wako pamoja au wanandoa wanaishi kwa furaha ,upendo na uaminifu?
Sio kwamba changamoto hazitakuwepo kwenye ndoa, changamoto zipo,lakini watu waliojitoa kwa dhati kwenye ndoa,changamoto zitafunikwa na upendo uliopo baina yao na sio changamoto kukausha ule upendo unaowaunganisha pamoja.

Je jamii yetu inahamasisha nini? Inahamasisha ndoa ambazo ziko imara kwa sababu wanandoa wanakuwa waaminifu kwa viapo vyao vya ndoa au ndo zile za "msiachane kwa sababu mna watoto"?.
 
Zamani ndoa ilikuwa ni jambo la kifamili, yaani linajumuisha familia zote za muoaji na muolewaji. Ni mchakato wenye kuunganisha familia nne (1-familia ya baba wa mume, 2-familia ya mama wa mume, 3- familia ya baba wa mmke na 4-familia ya mama wa mke), na vijana walikuwa wakifundwa kama mambo ya jandoni na unyagoni. Yaani wanandoa walikuwa wakitayarishwa kwa majukumu ya kindoa. Siku hizi tunawatayarisha mainjinia, madakatari, manesi, walimu, wanasheria n.k. lakini hutatayarishi wanandoa ndiyo maana tunapata shida sana na ndoa za vijana wetu, vijana wakikutana manjiani na kwenye viwanja vya starehe mara wanatangaza ndoa, wakizinguana kidogo tu kila mtu anachukua hamsini zake.
 
Kama haupo tayari kusalitiwa usioe wala kuolewa usije kujipiga kamba bure
 
Kwahiyo mkuu wale wanaoogopa kusalitiwa wakiamua kutooa/ kutoolewa, sisi wanajamii tunapaswa kuwaelewa na si kuwahoji unaoa lini maana wameamua kuepusha majanga ya kujitia vitanzi huko mbele?
 
Kilichozilinda ndoa za mababu ni ule uoga wa jamii itanionaje tu. Hapakuwa na maadili wala upendo wowote
Kwahiyo wazee wasitambe mbele ya vijana kwamba ndoa zao zilidumu na kutoa ushauri kama wote😂😂😂
 
Niende moja kwa moja kwenye mada leo asubuhi na mapema.
Katika jamii yetu kwa sasa kumekuwa na mijadala mingi kuhusu ndoa hasa kutokana na idadi ya migogoro na talaka kuongezeka kila mwaka. Wakati wa mijadala hii , vijana wa leo wamekuwa wakitupiwa lawama kwa kutozingatia ndoa zao na kuwa wepesi kuachana huku kukiwa na kauli za " mbona mabibi/ mababu zetu walidumu kwenye ndoa hadi uzeeni?"

Sikatai hiyo mfano maana inabidi tujifunze kwa wazee wetu,lakini je tunaposema walidumu tunamaanisha nini? Walidumu kwa sababu hawakuwa na sababu ya kuachana? Walidumu kwa sababu waliishi kwa amani na upendo? Au walidumu kwa sababu hawakuwa na chaguo lingine?

Tunapozungumzia ndoa imara ambazo huzalisha familia bora,je tunaangalia vigezo gani? Je ni cha muhimu wanandoa wako pamoja au wanandoa wanaishi kwa furaha ,upendo na uaminifu?
Sio kwamba changamoto hazitakuwepo kwenye ndoa, changamoto zipo,lakini watu waliojitoa kwa dhati kwenye ndoa,changamoto zitafunikwa na upendo uliopo baina yao na sio changamoto kukausha ule upendo unaowaunganisha pamoja.

Je jamii yetu inahamasisha nini? Inahamasisha ndoa ambazo ziko imara kwa sababu wanandoa wanakuwa waaminifu kwa viapo vyao vya ndoa au ndo zile za "msiachane kwa sababu mna watoto"?.
Angalia ndoa ya rais samia na mume wake. Fikiria kuna mke wa kwanza ambaye sio rais, kwa hiyo jamaa anamheshimu zaidi mke wa kwanza kuliko hata rais wa nchi na bado ndoa yao ipo hai hadi sasa.
 
Kwahiyo mkuu wale wanaoogopa kusalitiwa wakiamua kutooa/ kutoolewa, sisi wanajamii tunapaswa kuwaelewa na si kuwahoji unaoa lini maana wameamua kuepusha majanga ya kujitia vitanzi huko mbele?
Yes hiyo ndio point uamuzi wa mtu uheshimiwe
 
Ubora wa ndoa unapiwa kwa upendo na utii ( balance ya hivyo ). Heka heka sio kipimo cha ubora wa ndoa, na kwanza ukiona ndoa ina heka heka ujue ipo kwenye ambulance inaelekea ICU kujifia (Ukianza kuona kuvumiliana kunakuwa kwingi kuliko upendo, ilhali mioyo ina makovu na majeraha ujie pamechacha hapo) mgonjwa anasubiri kukata pumzi ya mwisho
 
Kwahiyo wazee wasitambe mbele ya vijana kwamba ndoa zao zilidumu na kutoa ushauri kama wote😂😂😂
Kama hao wazee bado wako katika ndoa, pengine haitakuwa busara kutowasikiliza. Jifunze kutoka kwao.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada leo asubuhi na mapema.
Katika jamii yetu kwa sasa kumekuwa na mijadala mingi kuhusu ndoa hasa kutokana na idadi ya migogoro na talaka kuongezeka kila mwaka. Wakati wa mijadala hii , vijana wa leo wamekuwa wakitupiwa lawama kwa kutozingatia ndoa zao na kuwa wepesi kuachana huku kukiwa na kauli za " mbona mabibi/ mababu zetu walidumu kwenye ndoa hadi uzeeni?"

Sikatai hiyo mfano maana inabidi tujifunze kwa wazee wetu,lakini je tunaposema walidumu tunamaanisha nini? Walidumu kwa sababu hawakuwa na sababu ya kuachana? Walidumu kwa sababu waliishi kwa amani na upendo? Au walidumu kwa sababu hawakuwa na chaguo lingine?

Tunapozungumzia ndoa imara ambazo huzalisha familia bora,je tunaangalia vigezo gani? Je ni cha muhimu wanandoa wako pamoja au wanandoa wanaishi kwa furaha ,upendo na uaminifu?
Sio kwamba changamoto hazitakuwepo kwenye ndoa, changamoto zipo,lakini watu waliojitoa kwa dhati kwenye ndoa,changamoto zitafunikwa na upendo uliopo baina yao na sio changamoto kukausha ule upendo unaowaunganisha pamoja.

Je jamii yetu inahamasisha nini? Inahamasisha ndoa ambazo ziko imara kwa sababu wanandoa wanakuwa waaminifu kwa viapo vyao vya ndoa au ndo zile za "msiachane kwa sababu mna watoto"?.
Ndoa haitaki watu wanaojua vitu vingi
 
Ndoa za siku hizi zimekuwa na sarakasi nyingi, kuachana ni sekunde tu. Hakuna haja ya kutoa mahari na kuchangisha watu michango ya harusi kama ushenzi wa kuachana upo
 
Single mother wamekuwa wengi kutokana na kutokuwepo ndoa imara, watu hawaheshimu ndoa zao
 
Back
Top Bottom