Habari za muda ndugu zangu.
Kwanza kabisa niipongeze serikali kwa juhudi za kuajiri hasa mwaka huu wa 2023, imejitahidi sana kuajiri vijana katika kada mbalimbali tofauti na za ualimu na afya sambamba na pongezi hizo naomba serikali kupitia wizara hasa TAMISEMI wawape maelekezo na miongozo watumishi katika halmashauri hizo maana vijana wengi wanakumbana na changamoto ya watu ambao sio wataalamu husika waliokuwa wanakaimu baadhi ya nafasi kuzing'ang'ania na kuona vijana hao wapya hawajui chochote kitu ambacho ni kuchelewesha maendelea ambayo serikali imekusudia (wengi wa ajira mpya katika halmashauri wamekumbana na hii)
Kama uzi unavyoeleza juu pamoja na maagizo ya Mhe. Waziri Mchengerwa juu ya malipo ya kujikimu kwa wakati kwa ajira mpya ila changamoto imekuwa kufanya malipo hayo kwani yamekuwa ni kama hisani tu waajiriwa hao hali inayopelekea kuishi katika hali ngumu.
Ikumbukwe ajira mpya wengi wanatoka mbali na maeneo yao ya kazi hivyo hutegemea pesa hiyo kwa ajili ya kujikimu na kuanzia maisha.
Naomba wahusika kupitia TAMISEMI wafatilie hili jambo waone kwa nini kumekuwa na ugumu ilihali Mhe. Waziri alishaagiza.