Tunaomba Serikali ipambanie hela za kujikimu kwa Watumishi katika Halmashauri hizi

mkarimani feki

JF-Expert Member
Nov 8, 2023
302
1,136
Najua hii ni platform ambayo ninaweza sikilizwa kilio changu kama Mtumishi wa Umma ambae napitia kipindi kigumu.

Waziri wa TAMISEMI Mchengerwa aliahidi angepambana na Wakurugenzi wa Halmashauri ambao hawatoi hela ya kujikimu kwa watumishi.

Till date mambo sio mambo, maisha ni magumu sana pasipo hela ya kujikimu .

unachukua takehome below 500k

kuna cost ya usafiri, chakula, makazi, afya nk.

Kila ukidai ni spana tu, tumeandika madokezo ya kuidai hiyo hela lakini wapi.

Ileje tafrani, Kishapu tafrani kuna Watumishi wapo Halmashauri ya Kiteto - Manyara ndio kabisa wao nao hali zao afadhali ya kwangu.

Naiomba serikali kuuu itupambanie sisi watumishi wa halmashauri hizi.
 
Back
Top Bottom