Mchengerwa ataka majina ya Wakurugenzi wasiolipa Fedha za Kujikimu za Watumishi Wapya

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amemuagiza Naibu Waziri, Mhe. Deogratius Ndejembi kufuatilia Wakurugenzi ambao bado hawawalipa fedha za kujikimu watumishi wapya ili aone hatua za kuchukua dhidi yao.

Watumishi hao ni wale walioajiriwa katika sekta za afya Julai mwaka huu.

Mchengerwa ametoa agizo hilo hayo jijini Dodoma kwenye mkutano Mkuu wa Umoja wa Walimu wa Shule za Msingi nchini (TAPSHA) uliofanyika tarehe 10.11.1023.

"Natambua kuna halmashauri Wakurugenzi wake bado hawajalipa stahiki za Watumishi wa Ajira mpya na nikitoa deadline ni mwezi wa kumi kama mpaka sasa kuna ambaye hajalipa nileteeni majina ya wakurugenzi hao. Tunachotaka kila mmoja wetu afanyekazi kwa kwa amani."

"Niwaombe watumishi hawa wa ajira mpya mchape kazi tangulizenk maslahi ya taifa letu mbele, msiruhusu hata kidogo kukiuka maadili ya taifa letu niwaombe sana maskahi yenu mimi nitayashughulikia."

Mchengerwa alisisitiza kuwa: "Nimekwisha kusema na nina rudia tena nitawalinda, nitalinda maslahi yenu ya walimu kote nchi nzima, sitakubali kuona uonevu wa walimu na nitayasimamia maslahi yenu."

Pia soma
 
Pasua kichwa ni hili la watumishi wenye kada na umri wa kazi unaofanana kulipwa tofauti tofauti toka halmashauri moja hadi nyingine. Kwa mfano MWALIMU aliyeko Tandahimba ;aliyeajiriwa mwaka 2004; ambaye kwa sasa ana digrii na muundo umemtambua ,hujikuta akilipwa kiwango/ daraja la chini akilinganishwa na MWALIMU mwenye viwango sawa na hivyo aliyeko hapa Arusha manispaa . Kimsingi hawa wawili wote wangestahili KUWA katika kiwango Cha TGTS I. Na hili zoezi litaipunguzia pakubwa SERIKALI hizi promotion za @ mwaka Kwa watumishi. Maana watafika ukomo weeengi.
 
Mhe mchengerwa anafanya kazi sana,( anachapa kazi sana lkn) changamoto huko kwenye halmashairi kuna changamoto hata maelekezo ya wazi toka TAMISEMI yanapuuzwa tu.
 
Pasua kichwa ni hili la watumishi wenye kada na umri wa kazi unaofanana kulipwa tofauti tofauti toka halmashauri moja hadi nyingine. Kwa mfano MWALIMU aliyeko Tandahimba ;aliyeajiriwa mwaka 2004; ambaye kwa sasa ana digrii na muundo umemtambua ,hujikuta akilipwa kiwango/ daraja la chini akilinganishwa na MWALIMU mwenye viwango sawa na hivyo aliyeko hapa Arusha manispaa . Kimsingi hawa wawili wote wangestahili KUWA katika kiwango Cha TGTS I. Na hili zoezi litaipunguzia pakubwa SERIKALI hizi promotion za @ mwaka Kwa watumishi. Maana watafika ukomo weeengi.
Hilo ni tatizo kubwa kwa watumishi na kwa kiwango kikubwa linasababishwa na maafisa wanaohusika na upandishaji wa madaraja kwa baadhi ya halmashauri,
Unakuta halmashauri nyengine watumishi wanapanda kwa wakati lakini kwengine utasikia amesahaulika, kwani rasilimali watu kwenye ofisi Kama tsc zinatakiwa kuwa na watu active na siyo watu wasiojua computer, na ni watu waliochoka.
 
Achana na ushabiki, Mchngerwa Yuko vizuri hata kipindi amepelekwa Tamisemi alifanya vizuri sana
 
Hii wizara ni ngumu na ina changamoto nyingi, waakirugenzi wengi wa hizi halmashauri wanajiona Miungu watu. Agizo lake sijui kama linatekelezeka.
 
Mtumishi yoyote aliyehamishwa na Serikali au ajira mpya ana haki ya kulipwa posho ya kujikimu naona Waziri amebase kwenye ajira mpya tu wakati haohao TAMISEMI wanahamisha watumishi na kuwatupia jukumu la malipo Wakurugenzi bila kujali pesa ipo au haipo hivyo kuongeza madeni Kwa Serikali

Sent from my TECNO BF7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom