Waziri Mchengerwa njoo Halmashari ya Ngara Watumishi Wapya hatujalipwa Fedha za Kujikimu

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Sisi watu wa ajira mpya kada mbalimbali tofauti na Elimu na Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara Mkoani Kagera hatujalipwa fedha za kujikimu.

Mfano Kada ya Maliasili na Mazingira, hatujalipwa fedha za kujikimu na tunazungushwa sana, fedha zikiingia Halmashauri wanazipangia vipaumbele vyao huku sisi Watumishi tunabaki na madeni ya watu.

Nayasema haya kwa kuwa licha ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa alitoa tangazo la kumuagiza Naibu Waziri, Deogratius Ndejembi kufuatilia Wakurugenzi ambao bado hawawalipa fedha za kujikimu watumishi wapya ili aone hatua za kuchukua dhidi yao.

Pia kuna wenzetu ambao hawajalipwa malimbikizo ya madeni ya kupandishwa Vyeo na Likizo kwa upande wa Walimu na Maafisa elimu kata, hapahapa Ngara.
Pia soma:
 
Back
Top Bottom