Kwanini hakuna usawa Ujenzi wa Majengo ya Shule, Kati ya Tanganyika na Zanzibar?

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,773
21,270
Majuzi kati hapo nilifika kisiwani Unguja nilishangaa sana kupita huku na huko katika pilika pilika za maisha.

MADA; Ukweli Zanzibar pamoja na sensa iliyopita kuonyesha kuwa na watu 1,8mil ambao kwa muktadha wa wingi wa watu na waliopo Tanganyika ni chini ya mkoa wa Manyara yenye watu 1.9mil kiuwiano.

Katika kuangalia maendeleo ya maisha kwa ujumla inaonekana si kwa kiwango kikubwa wananchi wakiwa na kipato kikubwa kutokana na maisha ya kila siku.

Naona Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inafanya uwekezaji mkubwa sana kwenye ujenzi wa shule, ambapo nyingi ya Shule hizi huwezi kuikuta popote nchini Tanganyika landa iwe ya binafsi.

Ujenzi wa hizi shule ni kama hauendani na wingi wa wanafunzi waliopo Zanzibar, tofauti na wingi wa wanafunzi waliopo Tanganyika.

IMG_20230627_111449.jpg

Hiyo juu ni moja ya skuli ya sekondari ambayo kwa sasa ipo asilimia (kwa kukadilia) 90% kukamilika na pembeni yake kuna jengo lingine kubwa kama hilo, hapo naambiwa yapo majengo mengine sehemu nyingine kama hilo yanajengwa.

Ukija hapa Tanganyika, sijui serikali inawaza nini na ndiyo maana hatuwezi kiwa sawa.

IMG_20230627_112720.jpg

Bajeti kubwa ya muungano inaenda Zanzibar na Tanganyika inabaki ukiwa kwenye suala la ujenzi wa majengo ya elimu.
 
Kama ni uwiano wa pesa ya uvico au bajeti ya elimu Tanzania Bara na Zanzibar basi Upande wa bara unaminywa sana hata kama serikali haioni umuhimu wa kuwekeza kwenye majengo mazuri basi tupo nyuma sana.
 
Elimu ya juu ndio ya muungano, hio ya chini sio muungano,
Hizo pesa za ujenz wa shule za ghorofa ni mpango wa Mwinyi,

Mwinyi alikuwa predential material sana, sema ndo hivo hatakuwa raisi wa Tz, but he is good
 
Kama kuna kipindi ambacho wazanzibar tunatafuna vizuri pesa za watanganyika basi ni kipindi hichi. Kama mama yetu akiendelea kukalia kile kiti pale juu kwa miaka kama saba mingine, nina uhakika Zanzibar tutakuwa mbele sana kimiundo mbinu.

Shida ni kuwa watu wenye kuleta mema kama haya ya kupendelea huwa hawadumu sana kukaa kwenye kile kiti, tunaogopa yasije kutukuta ya watu wa Chato, mwamba alipolala na miradi ya upendeleo ya Chato nayo ikafa kifo cha ghafla.
 
Elimu ya juu ndio ya muungano, hio ya chini sio muungano,
Hizo pesa za ujenz wa shule za ghorofa ni mpango wa Mwinyi,

Mwinyi alikuwa predential material sana, sema ndo hivo hatakuwa raisi wa Tz, but he is good
Pesa za Uviko na pesa za bajeti miundo mbinu zimegawiwa nchi nzima pasipo kuangalia uwiano wa watu na eneo, Zanzibar nao wamevuna nyingi, na ndio zinatumika kujenga mashule, hospitali na barabara indirectly na direct.

NOTE:
Afya, Elimu (msingi na seoondari) na miundo mbinu sio mambo ya muungano.
 
dawa yake ni kuunda serikali moja alafu zanzibar iwe wilaya kama bagamoyo tu na iyo itawafanya wazanzibar wapambane kama watu wa mikoa mingine kuliko hii wa kuwapa kila kitu bure tu
Kwa hali halisi iliyopo, hicho kitu kinachoitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umebakia na options mbili tu, naxo ni:-
AIDHA Kuunda Serikali Moja tu ya Shirikisho,
AU Kuuvunja Muungano ili kila upande ubaki na Hamsini zake. BASIIIII!!

Hakuna namna nyingine.
 
Ushasema Zanzibar ni sawa na mkoa wa Manyara Sasa swali lako ni lipi?
Unaelewa kilichoandikwa au labda nikujibu swali lako, maana uelewa wa kila binadamu ni tofauti.

Mfano;
Mgawo wa Uvico kwa mkoa wa Manyara ni shs 50/- lakini zanzibar inapewa shs 170/- unaona kuna usawa hapo?.

WHO walipotoa mkopo wa Uvico hawakusema znz ni nchi ndani ya nchi ilo ni sisi watz ndiyo tunalo.
 
mkuu kwanini unapenda kulialia bila ya hoja za msingi, Sasa Zanzibar na manyara zina usawa gani? Zanzibar ni mshirika wa Muungano na mgao wake upo kisheria kabisa.
 
Kwa hali halisi iliyopo, hicho kitu kinachoitwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umebakia na options mbili tu, naxo ni:-
AIDHA Kuunda Serikali Moja tu ya Shirikisho,
AU Kuuvunja Muungano ili kila upande ubaki na Hamsini zake. BASIIIII!!

Hakuna namna nyingine.

Watanganyika ndio wamekuwa wakiung'ang'ania huu Muungano
 
Pesa za Uviko na pesa za bajeti miundo mbinu zimegawiwa nchi nzima pasipo kuangalia uwiano wa watu na eneo, Zanzibar nao wamevuna nyingi, na ndio zinatumika kujenga mashule, hospitali na barabara indirectly na direct.

NOTE:
Afya, Elimu (msingi na seoondari) na miundo mbinu sio mambo ya muungano.

Zanzibar ni mshirika wa Muungano kwanini mgao wake uwe sawa na mkoa? Mgao wa zanzibar upo kisheria na sio kwa kukadiriwa uwiano wa watu
 
Muungano wa kinyonyaji huu! Imagine Wazanzibari eti wanaruhusiwa kuwa Wabunge, Mwaziri, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, nk kwa upande wa Tanganyika! Lakini Watanganyika hawaruhusiwi kushika wadhifa wowote uke kwenye serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar!!

Yaani tuna Muungano wa chako changu, changu changu. Yaani kuna uwezekano mkubwa hiyo miundomninu yote inajengwa kwa hela za Tanganyika.
 
Ukiachana na Ujamaa, swala la muungano nalo Nyerere alichemka sanaaa
 
Elimu ya juu ndio ya muungano, hio ya chini sio muungano,
Hizo pesa za ujenz wa shule za ghorofa ni mpango wa Mwinyi,

Mwinyi alikuwa predential material sana, sema ndo hivo hatakuwa raisi wa Tz, but he is good
Mbona mtihani wa form 4 ni mmoja?
 
Tanganyika huku tunakimbiza wananchi kuchanga kumi kumi za kujenga madarasa
Tanganyika mnalalamika sana mnasahau kwamba mnaongoza kwa wizi wa pesa za serekali. Ikitengwa pesa ya maendeleo asilimia 60 inaishia kwa viongozi 40 ndo inaenda kutekeleza moradi mnategemea nin?
 
Back
Top Bottom