Mmiliki wa shule ya sekondari Elly's iliyopo Halmashauri ya Mji wa Bunda baadhi ya majengo yako yanahifadhi wanafunzi watukutu wa shule jirani

Mjukuu wa kigogo

JF-Expert Member
Sep 19, 2023
201
437
Salaam zangu zikufikie mmiliki wa shule ya Sekondari ELLY'S ILIYOPO halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.

Inafahamika wazi shule yako Ina wanafunzi wachache sana huku ikiwa na majengo mengi yasiyotumika. Majengo haya yasiyotumika imekuwa hifadhi kuu Kwa wanafunzi watukutu wa shule za Sekondari ziliko karibu na eneo husika.Majengo haya yanahifadhi wanafunzi wakorofi toka shule za Sekondari.

Dkt. Nchimbi, Manyamanyama, Nyiendo, Bunda stoo, na hata kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi zilizo jirani mfano Nyasura na Miembeni. Ukweli unawapa shida sana walimu wa shule tajwa hapo juu katika kupambana na utoro sugu pamoja na vita ya tokomeza ziro na inavyoonekana ulishapewa taarifa kuhusu kero hii ila hujaamua kuchukua hatua stahiki.

Mbaya zaidi ndani ya majengo hayo wanafunzi wamefikia hatua mpaka ya kupikia chakula hapohapo, kufanyia zinaa, kuvutia sigara, na bangi kujifunza judo, kuchezea kamari, kunywea pombe, kupanga mikakati ya kudhuru wenzao na hata kufundishana mbinu za uhalifu.

Vikao vya WDC na vikao vya wazazi katika shule zilizoathirika washajadili sana hili kwa kina suala na mara nyingi lawama zinaelekezwa kwako kwamba taarifa unazo ila umeamua kuziba masikio.

Ushauri wetu sasa;Ipo wazi suala la kuendesha shule ni gharama,sasa kama uendeshaji umekuelemea, binafsisha au uza Kwa watu binafsi wanaoweza kuimudu kuendesha.

Hatuombei mabaya ila fikiria likitokea la kutokea mfano mtoto aumizwe na wenzake na hata kupoteza maisha ndani ya majengo yako utaweza kweli kuukwepa mkono wa Sheria? Fikiria Kwa kina kuhusu hili.

Kumbuka usipoziba ufa, utajenga ukuta! Usije kusema hujaambiwa
 
Mbaya zaidi ndani ya majengo hayo wanafunzi wamefikia hatua mpaka ya kupikia chakula hapohapo, kufanyia zinaa, kuvutia sigara, na bangi kujifunza judo, kuchezea kamari, kunywea pombe, kupanga mikakati ya kudhuru wenzao na hata kufundishana mbinu za uhalifu
 
Salaam zangu zikufikie mmiliki wa shule ya Sekondari ELLY'S ILIYOPO halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.

Inafahamika wazi shule yako Ina wanafunzi wachache sana huku ikiwa na majengo mengi yasiyotumika. Majengo haya yasiyotumika imekuwa hifadhi kuu Kwa wanafunzi watukutu wa shule za Sekondari ziliko karibu na eneo husika.Majengo haya yanahifadhi wanafunzi wakorofi toka shule za Sekondari.

Dkt. Nchimbi, Manyamanyama, Nyiendo, Bunda stoo, na hata kwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi zilizo jirani mfano Nyasura na Miembeni. Ukweli unawapa shida sana walimu wa shule tajwa hapo juu katika kupambana na utoro sugu pamoja na vita ya tokomeza ziro na inavyoonekana ulishapewa taarifa kuhusu kero hii ila hujaamua kuchukua hatua stahiki.

Mbaya zaidi ndani ya majengo hayo wanafunzi wamefikia hatua mpaka ya kupikia chakula hapohapo, kufanyia zinaa, kuvutia sigara, na bangi kujifunza judo, kuchezea kamari, kunywea pombe, kupanga mikakati ya kudhuru wenzao na hata kufundishana mbinu za uhalifu.

Vikao vya WDC na vikao vya wazazi katika shule zilizoathirika washajadili sana hili kwa kina suala na mara nyingi lawama zinaelekezwa kwako kwamba taarifa unazo ila umeamua kuziba masikio.

Ushauri wetu sasa;Ipo wazi suala la kuendesha shule ni gharama,sasa kama uendeshaji umekuelemea, binafsisha au uza Kwa watu binafsi wanaoweza kuimudu kuendesha.

Hatuombei mabaya ila fikiria likitokea la kutokea mfano mtoto aumizwe na wenzake na hata kupoteza maisha ndani ya majengo yako utaweza kweli kuukwepa mkono wa Sheria? Fikiria Kwa kina kuhusu hili.

Kumbuka usipoziba ufa, utajenga ukuta! Usije kusema hujaambiwa
Hiyo shule naijua aisee. Ina majengo mengi sana lkn hayatumiki tena muda mrefu sana. Pia shule iko jirani sana na sekondari ya Dkt Nchimbi at the same time wanafunzi wa Manyamanyama wanapita nyuma ya shule hiyo. Kwa jinsi ilivyojengwa ni rahisi kuingia kwenye majengo hayo bila watu/wahusika kuona maana administration iko mbali sana na hayo majengo.

Sidhani kama mwenyewe anaweza hata kujenga uzio.
 
Back
Top Bottom